STD VII KISWAHILI NECTA ONLINE SELF TESTS(2005-2018)
STD VII KISWAHILI NECTA EXAM OF YEAR 2021 Try This  |  


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI

01 KISWAHILI

 Muda: Saa 1:40 Mwaka: 2021

Maelekezo

l . Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali arobaini na tano (45).

2. Jibu maswali yote katika kila sehemu.

3. Soma maelekezo yote yaliyoko katika fomu maalum ya kujibia (OMR).

4. Jaza taarifa zote katika fomu ya OMR.

5. Andika Namba yako ya Mtihani kisha weka kivuli kwenye tarakimu za namba hiyo mahali panapohusika kwenye karatasi yako ya kujibia.

6. Weka kivuli kwenye herufi ya jibu lililo sahihi kwa swali 1 — 40. Kwa mfano, kama jibu sahihi ni A weka kivuli kama ifuatavyo:

7. Ukigundua kuwa herufi uliyowekea kivuli si jibu sahihi futa kivuli hicho kwa umakini kwa kutumia kifutio safi kabla ya kuweka kivuli katika herufi mpya.

8. Tumia penseli ya HB tu katika kujibu swali la 1— 40; na kalamu ya Wino wa bluu au mweusi kwa swali la 41 hadi 45.

9. Simu za mkononi na Vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi ndani ya chumba cha mtihani.

SEHEMU A (Alama 35)

Sikiliza kwa makini hadithi utakayosomewa na msimamizi, kisha jibu swali la 1 - 5, kwa kuweka katika herufi ya jibu lililo sahihi katika fomu yako ya kujibia.

Bofya Hapa Kusikiliza Hadithi

Maswali

1. Malkia wa nyuki alikuwa analindwa na nani?

  1. Vibaraka
  2. Askari hodari
  3. Wanakijiji
  4. Nyuki Hohehahe
  5. Wafanyakazi.


2. Ni kitu gani ambacho malkia wa nyuki hakukipenda?

  1. Wanakijiji hohehahe
  2. Mafundi wa masega
  3. Ushirikiano wa nyuki
  4. Vibaraka wa malkia
  5. Kuwalipa vibarua


3. Nani alijishughulisha kutafuta nekta kwenye maua?

  1. Nyaki wote
  2. Vibarua
  3. Wafanyakazi
  4. Vibaraka
  5. Wanakijiji


4. Utajiri katika kijiji cha nyuki ulitokana na nini?

  1. Kuuza asali
  2. Kuuza nta
  3. Kuuza masega
  4. Kuuza maua
  5. Kuuza mizinga


5. Nani walitumika kupeleka habari mbalimbali katika vijiji vya jirani?

  1. Vibarua
  2. Wafanyakazi
  3. Vibaraka
  4. Wanakijiji
  5. Nyuki


Katika swali la 6 - 35, weka kivuli katika herufi ya jibu lililo sahihi katika fomu yako ya kujibia.

6. Wanakijiji walifanya juu Chini ili kuleta maendeleo katika kijiji Chao. Nahau "fanya juu chini" inafafanuliwa na kifungu kipi cha maneno kati ya vifuatavyo?

  1. Walijitahidi kwa kila njia.
  2. Walishirikiana kwa pamoja.
  3. Walijituma kwa ujasiri.
  4. Walijituma kwa uzalendo.
  5. Walitumia nguvu.


7. Nahau ipi yenye maana ya "kunywa pombe?"

  1. Piga mbizi
  2. Piga chenga
  3. Piga yowe
  4. Piga soga
  5. Piga maji


8. Katika sentensi "Dada alimwambia kuwa atakapopata muda atakuja nyumbani ," mzungumzaji ametumia nafsi gani kati ya hizi?

  1. Nafsi ya pili wingi
  2. Nafsi ya tatu wingi
  3. Nafsi ya tatu umoja
  4. Nafsi ya pili umoja
  5. Nafsi ya kwanza wingi


6. "Sisi ni wanafunzi hodari wa somo la kiswahili". Kauli hiyo inawakilisha nafsi ipi kati ya hizi zifuatazo?

  1. Nafsi ya kwanza umoja
  2. Nafsi ya tatu wingi
  3. Nafsi ya tatu umoja
  4. Nafsi ya kwanza wingi
  5. Nafsi ya pili wingi


10. Daktati alisema kwamba mgojwa wetu amepata ahueni" Hiyo ni aina gani ya kauli kati ya zifuatazo?

  1. Tata
  2. Mazoea
  3. Halisi
  4. Taarifa
  5. Kutenda


11. Masumbuko aliwaambia kuwa, hataingia darasani tena. Kauli halisi ya sentesi hii ni ipi kati ya zifuatazo??

  1. Masumbuko aliwaambia kuwa. "haingii darasani tena."
  2. Masumbuko aliwaambia. "hataingia darasani tena".
  3. Masumbuko aliwaambia. "sitaingia darasani tena."
  4. Masumbuko aliwaambia. "hakuingia darasani tena.'
  5. Masumbuko aliwaambia "kamwe haingii darasani i'


12. "Nyamante alikata shauri na kuwaambia wenzake, kweli elimu ndiyo mkombozi wa mtoto wa kike." Nahau "kata shauri" katika sentensi hii ina maana ipi kati ya zifuatazo?

  1. Kuamua
  2. Kuwatahadharisha
  3. Kuwaasa
  4. Kuonya
  5. Kufundisha


13. Chekacheka anapenda watoto wake wawe na tabia njema hadi ukubwani. Methali ipi kati ya zifuatazo inahimiza tabia ya aina hiyo?

  1. Zimwi likujualo halikuli likakwisha.
  2. Asiyesikia la mkuu huvujika guu.
  3. Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.
  4. Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu.
  5. Tabia hupamba kuliko libasi.


14. "Nikitembea walio wafu huamka na walio hai hukaa kimya." Jibu la kitendawili hiki ni lipi kati ya yafuatayo?

  1. Nyuki ndani na nje ya mzinga
  2. Yai na kifaranga chake
  3. Majani makavu na mabichi
  4. Kulala usingizi na kuamka
  5. Tumbo na chakula


15, Ni methali ipi kati ya zifuatazo inamaana sawa na methali "akufaaye kwa dhiki ndio rafiki"?

  1. Baniani mbaya kiatu chake dawa,
  2. Damu nzito kuliko maji,
  3. Undugu kufaana si kufanana,
  4. Shukrnni ya punda njateke,
  5. Sikio la kufa halisikii dawa,


16. Neno lipi kati ya yafuatayo ni jumuishi kwa maneno haya "nyanya, vitunguu, pilipili na tangawizi'?"

  1. Nafaka
  2. Matunda
  3. Vinywaji
  4. Vitoweo
  5. Viungo


17. Mwaka 1985 Mwalimu Julius Kambaragc Nyerere aliamua kung'atuka madarakaní na kumwachia Mheshimiwa, Ali Hassan Mwinyi, Kitcndo cha Mwalimu Julias Kambarage Nyerere kung'atuka kinamaanisha nini?

  1. Kuaga wafanyakazi
  2. Kuwaachia wafanyakazí
  3. Kustaafu kazi
  4. Kujiuzulu madaraka
  5. Kupumzika kazi kidogo


18. Neno lipi kati ya yafuatayo ni jumuishi kwa maneno haya "almasí, dhahabu, Tanzanaiti na lulu" ?

  1. Shaba
  2. Vyuma
  3. Marumaru
  4. Mgodi
  5. Madini


19. Katika neno "ninakula" kiambishi cha wakati uliopo ni kipi kati ya vifuatavyo?

  1. -ni-
  2. -ku-
  3. -na-
  4. -la-
  5. -kul-


20. "Muda ulipowadia wanafunzi wote tulisimama foleni.' Neno "wadia" linashabihiana na neno lipi kati ya yafuatayo?

  1. fika
  2. kwisha
  3. patikana
  4. pungua
  5. ongezeka


21. Katika sentensi "Wimbo wa Taifa umeimbwa kwa ustadi." Neno lipi kati ya yafuatayo limesimama kama kitenzi?

  1. wimbo
  2. ustadi
  3. taifa
  4. kwa
  5. umeimbwa


22. Neno lipi halilandani na mengine kati ya maneno yafuatayo?

  1. Kuku
  2. Bata
  3. Kaa
  4. Mwewe
  5. Kunguru


23. "Mtoto mzuri anajua kupangilia ratiba." Katika sentensi hii, neno lipi kati ya yafuatayo limetumika kama kivumishi?

  1. mzuri
  2. mtoto
  3. kupangilia
  4. ratiba
  5. anajua


24. "Hawa ndio wapole darasani mwetu." Katika sentensi hii, neno lipi kati ya yafuatayo limetumika kama kiwakilishi?

  1. ndio
  2. hawa
  3. wapole
  4. darasani
  5. mwetu


25 Ni neno lipi kati ya yafuatayo linakamilisha sentensi hii kwa usahihi? "Nikisoma kwa bidii . . . . . . . mtihani wangu."

  1. ningefaulu
  2. nitafaulu
  3. ningalifaulu
  4. ningelifaulu
  5. ninafaulu


26. "Nitakula uji wangu kesho asubuhi." Sentensi hii imekosewa. Sentensi sahihi ni ipi kati ya zifuatazo?

  1. Nitamung'unya uji wangu kesho asubuhi.
  2. Nitatafuna uji wangu kesho asubuhi.
  3. Nitakunywa uji wangu kesho asubuhi.
  4. Nitameza uji wangu kesho asubuhi.
  5. Nitabugia uji wangu kesho asubuhi.


27. "Kijiji Chetu kina maendeleo duni lakini mwaka ujao itakua kinyume chake." Je, mwaka ujao kijiji Chetu kitakuwa na maendeleo gani?

  1. Imara
  2. Dhaifu
  3. Mabaya
  4. Hafifu
  5. Dhahili


28. Maneno yapi kati ya yafuatayo yapo katika mpangilio sahihi kwa kuzingatia matumizi ya kamusi?

  1. fana, fani, faraja, farasi
  2. fana, faraja, farasi, fani
  3. fana, farasi, faraja, fani
  4. fani, fana, faraja, farasi
  5. fana, farasi, fani, faraja


29. Kitenzi kipi kati ya vifuatavyo kinatokana na nomino "mchemsho?"

  1. Mchemshaji
  2. Chemsha
  3. Chemshika
  4. Chemshana
  5. Chemshiana


30. Ni nomino ipi inaundwa kutokana na neno "chunga'?"

  1. Chungana
  2. Chungiana
  3. Mchungaji
  4. Chungika
  5. Chungisha


31. "Polepole ndio mwendo." Methali hii inahusiana na methali ipi kati ya hizi zifuatazo?

  1. Maneno mengi hula matendo.
  2. Chembe na chembe mkate huwa.
  3. Chanda chema huvikwa pete.
  4. Shukrani ya punda ni mateke.
  5. Dua la kuku halimpati mwewe.


32. Charubuma alionywa na wazazi wake kuacha tabia ya wizi, lakini hakuwasikiliza hatimaye alifungwa jela. Methali gani kati ya zifuatazo inakemea tabia hiyo isiyofaa katika jamii'?

  1. Asiye na mwana aeleke jiwe.
  2. Asiye na lake hafungi safari mapema.
  3. Asiyesikia la mkuu huvunjika guu.
  4. Asiye na bahati habahatishi.
  5. Asiye na mengi ana machache.


33. ”Hakuna msiba . . . . . . . . . . . . . . ". Kifungu kipi cha maneno kati ya vifuatavyo kinakamilisha methali hii?

  1. usiokuwa na vilio
  2. usiokuwa na mwenziwe
  3. usiokuwa na chakula
  4. usiokuwa na matanga
  5. usiokuwa na watu


34. Kirefu cha neno BAKITA ni kipi kati ya maneno yafuatayo?

  1. Baraza la Sanaa la Taifa
  2. Baraza la Mitihani la Tanzania
  3. Baraza la Michezo Tanzania
  4. Baraza la Kiswahili Tanzania
  5. Baraza la Kiswahili la Zanzibar

35. Katika uandishi wa kumbukumbu za mkutano saini ya mwenyekiti hukaa sehemu gani?



  1. Mwanzoni mwa kichwa cha kumbukumbu
  2. Katikati ya kumbukumbu kwenye ajenda za mkutano
  3. Mwishoni mwa kumbukumbu upande wa kulia
  4. Mwishoni mwa kumbukumbu upande wa kushoto
  5. Baada ya majina ya waliohudhuria na wasiohudhuria


11. Mahali panapochimbwa madini ya chumvi. makaa ya mawe, dhahabu na almasi panaitwaje?

  1. Mgodi
  2. Handaki
  3. Mtoni
  4. Bondeni
  5. Shimoni.


12. Neno lipi kati ya yafuatayo ni kinyume cha neno 'kinai" ?

  1. Tosheka
  2. Ridhika
  3. Shibe
  4. Ridhia
  5. Tamani.


13. Neno lipi linakosekana katika sentensi ifuatayo? "Humo . . . . . . . . . . . alimopita mbunge wakati wa kuomba kura".

  1. ndipo
  2. ndio
  3. ndiko
  4. ndie
  5. ndimo.


14. Abdi . . . . . . . . . . mtoto wa jirani yangu. Neno linalokamilisha sentensi hii ni lipi?

  1. siye
  2. Siyo
  3. sie
  4. si
  5. sio.


15. Hawa . . . . . . . . . . walioalikwa katika sherehe hii. Neno lipi linakamilisha sentensi hii kwa usahihi?

  1. ndio
  2. ndiyo
  3. ndiye
  4. ndiwo
  5. ndilo.


16. "Baba atam kanya mjomba ili aache ulevi.” Sentensi hii ipo katika wakati gani?

  1. Timilifu
  2. Ujao
  3. Uliopo
  4. Mazoea
  5. Uliopita.


17. 'Sitakubafi kuonewa”. Neno "sitakubali” liko katika hali gani?

  1. Endelevu
  2. Mazoea
  3. Timilifu
  4. Ukanushi
  5. Uyakinishi.


18. Mti unakatwa na Ali. Neno "unakakatwa" liko katika kauli ipi?

  1. Kutenda
  2. Kutendeka
  3. Kutendea
  4. Kutendwa
  5. Kutendewa


19. "Mtoto alinunuliwa zawadi."Kitenzi 'alinunuliwa” kipo katika kauli gani?

  1. Kutendana
  2. Kutendewa
  3. Kutendesha
  4. Kutenda
  5. Kutendeka


20. "Ndizi yake imeliwa na Ngedere” . Wingi wa sentensi hii ni upi?

  1. Ndizi yake imeliwa na mangedere.
  2. Ndizi zao zimeliwa na ngedere.
  3. Ndizi zake zimeliwa na mangedere.
  4. Mandizi yake yameliwa na mangedere.
  5. Ndizi zao zimeliwa na mangedere.


STD VII KISWAHILI NECTA EXAM OF YEAR 2020 Try This  |  

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA

MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI

01 KISWAHILI

Muda: Saa 1:30 Mwaka: 2020

Maelekezo

l. Karatasi hii ina sehemu A, B, C, D na E zenye maswali arobaini na tano (45).

2. Jibu maswali yote katika kila sehemu.

3. Soma maelekezo yote yaliyoko katika fomu maalum ya kujibia (OMR).

4. Jaza taarifa zote katika fomu ya OMR na katika ukurasa wenye swali Ia 41 hadi 45 kwenye karatasi ya maswali.

5. Andika Namba yako ya Mtihani kisha weka kivuli kwenye tarakimu za namba hiyo mahali panapohusika kwenye karatasi yako ya kujibia.

6. Weka kivuli kwenye herufi yajibu lililo sahihi kwa swali I - 40. Kwa mfano, kamajibu sahihi ni A weka kivuli kama ifuatavyo:

7. Ukigundua kuwa herufi uliyowekea kivuli si jibu sahihi futa kivuli hicho kwa umakini kwa kutumia kifutio safi kabla ya kuweka kivuli katika herufi mpya.

8. Tumia penseli ya HB tu katika kujibu swali Ia 1 — 40; na kalamu ya wino wa bluu au mweusi kwa swali Ia 41 hadi 45.

9. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi ndani ya chumba cha mtihani.

SEHEMU A (Alama 20)

SARUFI

Katika swali la 1 - 20, weka kivuli katika herufi ya jibu lililo sahihi katika fomu yako ya kujibia.

l . "Amevaa kichina mimi nimevaa kihindi." Maneno "Kichina na Kihindi" ni aina gani za maneno?

  1. Vielezi
  2. Vivumishi
  3. Viwakilishi
  4. Vihusishi
  5. Nomino.


2. "Wewe ni mtoto mzuri sana." Neno lililotumika kama kiwakilishi ni lipi?

  1. mtoto
  2. ni
  3. mzuri
  4. sana
  5. wewe.


3. "Walimu wanafundisha lakini wanafunzi hawajisomei." Neno "lakini" ni aina gani ya neno?

  1. Kivumishi
  2. Kiunganishi
  3. Kitenzi
  4. Kielezi
  5. Kihisishi.


4. "Amenunua bidhaa kadhaa na kuzipeleka nyumbani."Neno 'kadhaa" ni aina gani ya neno?

  1. Kielezi
  2. Kitenzi
  3. Nomino
  4. Kiwakilishi
  5. Kivumishi.


5. "Madaktari walifanya kila njia ili kunusuru maisha yake." Neno "ili" ni aina gani ya neno?

  1. kihisishi
  2. kihusishi
  3. kiunganishi
  4. kielezi
  5. kiwakilishi


6. "Watoto wawili waliimba wimbo vizuri sana." Neno "wawili" ni aina gani ya neno?

  1. Kiunganishi
  2. Kiwakilishi
  3. Kivumishi
  4. Kielezi
  5. Kitenzi.


7. Neno lipi halihusiani na maneno mengine kati ya haya yafuatayo?

  1. Wali
  2. Ugali
  3. Ndizi
  4. Viazi
  5. Mchicha.


8. Kuku, bata, mwewe. kunguru na kanga kwa neno moja wanaitwaje?

  1. Wanyama
  2. Ndege
  3. Wadudu
  4. Wanyamapori
  5. Ndegepori.


9. Neno lipi halilandani na mengine kati ya yafuatayo?

  1. Mchungwa
  2. Embe
  3. Ndizi
  4. Papai
  5. Pera.


10. Mtu hodari asiyeogopa huitwaje?

  1. Jambazi
  2. Jangili
  3. Jasiri
  4. Jeuri
  5. Njemba.


SEHEMU B (Alama 10)

LUGHA YA K?FASIHI

Katika swali la 21 - 30, weka kivuli katika herufi ya jibu lililo sahihi katika fomu yako ya kujibia.

21 . Kamilisha methali hii, "Udongo upate . . . . . . . . . . . ."

  1. ungali mfinyanzi
  2. ungali kichanga
  3. ungali maji
  4. ingali mapema
  5. ukiwa na mbolea


22. . . . . . . . . . . . . . ila siku ya idi.” Kifingu kipi cha maneno kinakamilisha methali hii?

  1. Anafunga mchana
  2. Hatasali
  3. Hatafaidi pilau
  4. Mkaidi hafaidi
  5. Hapati zawadi


23. 'Mia nawe hafi nawe ila mzaliwa nawe.” Methali hii inahusiana na ipi kati ya zifuatazo?

  1. Jembe halimtupi mtu
  2. Baada ya dhiki faraja
  3. Damu ni nzito kuliko maji
  4. Penye urembo ndipo penye ulimbo
  5. Kila mtoto na koja lake


24. Hana adabu wala staha kwa watu.” Jibu la kitendawili hiki ni lipi?

  1. Kinyesi
  2. Kamasi
  3. Jasho
  4. Utelezi
  5. Pombe


25. 'Mwavuli 'tva nyikani haukingi mvua." Jibu la kitendawili hiki ni lipi?

  1. Mgomba
  2. Mpapai
  3. Uyoga
  4. Mnyonyo
  5. Mfenesi


26. "Akibeba watoto wake hawezi kuwashusha." Jibu la kitendawili hiki ni lipi?

  1. Mzaituni
  2. Mhindi
  3. Mchundwa
  4. Mwembe
  5. Mpera


27. "Babu huanika sembe usiku,asubuhi huiondoa."Jibu la kitendawili hiki ni lipi?

  1. Mvua
  2. Giza
  3. Mwezi
  4. Umande
  5. Mawingu


28. "Unga mkono." Maana ya nahau hii ni ipi?

  1. Kushikana mkono
  2. Ongozana
  3. Kubaliana
  4. Fuatana
  5. Tembeleana


29. Ni nahau ipi kati ya zifuatazo inadhihirisha hali ya kumsema mtu kwa mafumbo ili asitambue?

  1. Kumpiga vijembe
  2. Kumpiga kinagaubaga
  3. Kumsema kimasomaso
  4. Kumsema kisiasa
  5. Kumsema kwa kumjuza


30. 'Nikipata wasaa nitajitahidi kukutupia jicho."Usemi "kukutupia jicho" una maana gani?

  1. Kukusikiliza
  2. Kukuletea fedha
  3. Kukupa miwani
  4. Kukuona
  5. Kukupima macho.


SEHEMU C ( Alama 06)

USHAIRI

Soma kwa makini shairi lifuatalo kisha jibu swali la 31 - 36 kwa kuweka kivuli katika herufi ya jibu lililo sahihi katika fomu yako ya kujibia.

Kuwaza na kuwazua, matukio mbalimbali,

Ndivyo akili yakua, pungufu kuwa kamili,

Asojua akajua, kwa lile ama kwa hili,

Lau ukipuuzia, katu hutofika mbali.

Kusoma na kuchambua, vitabu na mafaili,

Mambo ukapambanua, ya uwongo na ukweli,

Hapo hatokusumbua, kila aliye jahili,

Lau ukipuuzia, katu hutofika mbali.

Kupanga na kupangua, mikakati ya halali,

Utaweza kubagua, lilo jema na batili,

Jema utalichukua, baya utaweka mbali,

Lau ukipuuzia, katu hutofika mbali.

31. Kichwa kinachofaa kwa shairi hili ni kipi?

  1. Umuhimu wa Elimu
  2. Kusoma na kuchambua
  3. Kupanga na kupangua
  4. Katu hutofika mbali
  5. Asojua akajua


32. Vina vya kati na vya mwisho katika mistari ya ubeti wa tatu ni vipi?

  1. u na li
  2. ku na li
  3. ana li
  4. ku na u
  5. ta na we


33. Jumla ya silabi kumi na sita katika kila mstari wa shairi huitwaje?

  1. Ubeti
  2. Mizani
  3. Vina
  4. Silabi
  5. Mshororo


34. Shairi hili lina mizani ngapi?

  1. Nane
  2. Kumi
  3. Nne
  4. Kumi na mbili
  5. Kumi na sita


35. Kituo kilichotumika katika shairi hili ni kipi?

  1. Jema utalichukua, baya utaweka mbali,
  2. Kuwaza na kuwazua, matukio mbalimbali,
  3. Hapo hatokusumbua, kila aliye jahili,
  4. Lau ukipuuzia, katu hutofika •mbali
  5. Kupanga na kupangua, mikakati ya halali,


36. Neno "jahili" kama lilivyotumika katika ubeti wa pili lina maana gani?

  1. Mjanja
  2. Mpole
  3. Mjinga
  4. Mwizi
  5. Hasidi


STD VII KISWAHILI NECTA EXAM OF YEAR 2018 Try This  |  

1. Neno lipi kati ya haya lina maaana sawa na shari?

  1.  Ubunifu
  2. Umaarufu
  3. Uzembe
  4. Ugomvi
  5. Uzushi


2.      Shida alivaa nguo za kijeshi wakati wa mkutano.Neno "za kijeshi" ni aina gani ya neno?

  1. Kivumishi
  2. Kielezi
  3. Kitenzi
  4. Kiwakilishi 
  5.  Nomino


3.      Hicho ulichopata sikupata lakini nimepata hiki" katika sentensi hii, maneno "hicho na hiki"ni aina gani ya maneno?

  1. Vivumishi 
  2. Viwakilishi
  3. Vielezi    
  4. Vitenzi
  5. Nomino


4.      Ni sentensi ipi iliyo sahihi kimuundo  kati ya zifuatazo?

  1.  Amenunua gari mashaka
  2. Mashaka gari amenunua 
  3. Amenunua mashaka gari 
  4. Mashaka amenunua gari
  5.  Gari amenunua mashaka.


5.      Maana ya neno "faraghani" ni ipi kati ya hizi?

  1. Wazi wazi
  2. Kivulini
  3. Pembejeo
  4. Mafichoni
  5. Hadharani


6.      Wingi wa sentensi "Mbuzi wamepotea" ni upi?

  1. Mbuzi zetu zimepotea
  2. Mbuzi yetu zimepotea
  3. Mbuzi wetu wamepotea 
  4.  Mbuzi zetu wamepotea
  5. Mbuzi yetu wamepotea.


7.      "Wanafunzi kenda walikwenda ziara nchini Kenya".neno wa ni aina gani ya neno?

  1. Kivumishi
  2. Kiwakilishi
  3. Kielezi 
  4.  Kitenzi
  5. Nomino.


8.      Ashura anacheza mpira wa miguu vizuri.katika sentensi hii,neno lipi limetumika kama kielezi?

  1. Anacheza
  2.  Mpira
  3. Vizuri
  4. Ashura
  5. Wa mguu.


9. Mtu anayetafsiri ana kwa ana katika lugha moja kwenda lungha huitwaje?

  1. Msuluhishi
  2. Mpatanishi
  3. Mkalimani
  4.  Mfafanuzi
  5. Mhubiri


10. "Sote tunafanya mtihani darasani". "darasani" limetumika kama aina gani ya neno?

  1. Kielezi
  2. Kivumishi
  3. Kitenzi
  4. Kiwakilishi 
  5.  Nomino


I l. Baraka aliona --------- kuwa miongoni mwa waliofaulu. Ni neno i:zn linakamilisha sentensi hii kwa usahihi  ya maneno yafuatayo?

  1. Fadhili
  2. Fahari
  3. Fahiri
  4. Fadhaa
  5. Fadhila


12. Mwanamke yule alikaa baada ya kufiwa na mume wake. Ni neno lipi linakamilisha sentensi hii kati ya maneno yafuatayo?

  1. eda 
  2.  heda 
  3. arobaini 
  4.  fungate 
  5. edaha.


13. Kitenzi "piga"kikiwa katika kauli ya kutendeka kitakuwa neno lipi kati ya maneno yafuatayo?

A  Pigia             

B  Pigwa

C  Pigika

D  Pigiwa

E   Pigana.



14. Wewe unasoma kwa bidii"wingi wa sentensi hii ni upi?

  1.  Sisi tunasoma kwa bidii 
  2.  Wale wanasoma kwa bidii
  3. Nyinyi mnasoma kwa bidii 
  4.  Ninyi tunasoma kwa bidii 
  5. Wao wanasoma kwa bidii


15."Wanafunzi wale ni hodari sana" neno "wale" ni aina gani ya neno?

  1. Kitenzi 
  2.  Kivumishi 
  3. Nomino 
  4.  Kielezi
  5. Kiwakilishi


16. "Wasichana saba wamechaguliwa kujiunga na kozi ya uhandisi." Neno na ni aina gani ya neno?

  1. Kitenzi
  2. Nomino
  3. Kiwakilishi 
  4.  Kielezi
  5.  Kiunganishi.


17. Ni neno lipi lina maana sawa na neno kumzonga mtu kwa maneno makali kwa lengo la kumkasirisha?

  1. Kumhukumu
  2. Kumwinda
  3.  Kumwadhibu 
  4.  Kumaskama
  5. Kumzoea.


18. Katika vitenzi "sitafyeka" na "hupendi" ni silabi zipi zinazoonesha ukanushi?

  1. ta na hu
  2. ta na pe
  3. ka na ndi 
  4.  si na hu
  5. fye na pe.


19. Neno lipi kati ya haya halilandani na mengine?

  1. Cheka
  2. Tabasamu
  3. Furaha 
  4.  Sherehe 
  5.  Shere.


20. Mnyama huyu anafanana na ngombe. Wingi wa sentensi hii ni ipi?

  1. Wanyama anayefanan na ngoombe 
  2.  Mnyama anayefanana na ngombe
  3. Wanyama wanaofanana na ngombe 
  4. Wanyama wanaofanana na mango mbe 
  5. Mnyama wanaofanana na ngombe.


21.   Ni methali ipi kati ya zifuatazo inahimiza ushirikiano katika jamii?

  1. Chanda chema huvikwa pete
  2. Mchumajanga hula na wa kwao
  3. Umoja ni nguvu utengano ni dhaifu
  4. Mwenda pole hajikwai
  5.  Wapishi wengi huharibu mchuzi


22.   "Watoto wa mfalme ni rahisi kujificha" Jibu la kitendawili hiki ni kipi?

  1.  Macho
  2.  Vifaranga
  3. Siafu
  4. Mvi
  5. Sungura


23.   "Uzururaji umepigwa marufuku".Nahau umepigwa marufuku ina maaña gani?

  1. Umezoeleka
  2. Umepigwa winda
  3. Umepigwa konde
  4. Umekithifi
  5. Umekatazwa


24.   "Amenisahau kwa moyo mweupe" Nahau"moyo mweupe" ina maana ipi"?

  1. Bila kinyongo
  2. Kwa lazima
  3.  Kwa shingo upande
  4. Kwa kusita sita 
  5. Kwa kusua sua


25.   "Mwenye nguvu Neno linakamilisha methali hii?

  1. mfunge
  2. usimkamate
  3. mkimbie
  4. usimpigie 
  5.  mpishe


26.   "Asiyefunzwa na mamaye hufunzwa ulimwengu." Ni methali ipi inafanana na methali hii?


  1. Asiyesikia la mkuu huvunjika guu
  2. Asiye na mwana aelekee jiwe 
  3. Asiye na bahati habahatishi
  4. Asiyejua kufa atazame kaburi
  5. Asiyekubali kushindwa si mshindani.


27.   "Haba na haba hujaza kibaba" Methali hii inatoa funzo gani?

  1. Umuhimu wa kupima vitu
  2. Tunajiwekea akiba
  3. Vitu hupimwa na kibaba tu 
  4. Tunapawa kupima vibaba 
  5.  Kibaba hujaza vitu.


28.   "Heri kufa macho kuliko "Methali hii UKAMILISHWA na kifungu kipi cha maneno?

  1. kujikwaa ulimi
  2. kuumia moyo
  3. kuzama majini
  4. kufa moyo
  5. kufa jicho moja


29.   "Maji yakimwagika hayazoolekl hii ina maana gani kati ya zifuatayo?

  1. Ukitaka usizoe maji,usimwage
  2. Tuwe waangalifu katika kutenda jambo
  3. Tuwe waangalifu tunapobeba maji
  4. Maji yakimwagika hugeuka matope
  5. Jambo lililoharibika halitengenezeki


30.   "Amani haiji kifung•z cha maneno kinakamilisha methali usahihi?

  1. ila kwa mzozo mkubwa
  2. ila kwa malumbano makali
  3.  bila kuwa na imani 
  4. ila kwa ncha ya upanga 
  5. bila makubaliano.


USHAIRI Soma kwa makini shairi lifuatalo kisha jibu maswali 31-36 kwa kuweka kivuli katika herufi ya jibu sahihi katika fomu yako ya kujibia

Kazi ifanye kwa nia,itakupatia

Ifanye kwa kupania,iwe kwako ni daraja

Kazi ni kuibobea, ili ilete faraja.

Juhudi katika kazi,ni zawadi maridhawa

Ni zawadi maridhawa juhudi katika kazi

Ifanye uwe mzawa,uonekane wazi,

Uoneshe uelewa,nchini mwako azizi

Tufanye kazi kwa dhati,itatupa manufaa

Itatupa manufaa ,tufanye kazi kwa dhati,

Tuoneshe yanofaa,kwa moyo ulo thabiti

Kazi ndiyo mhimili,popote utapokuwa.

Popote utapokuwa,kazi ndio mhimili, Kama gari huendeshwa,vile inastahili, Mafunzo uliyopewa,vile inastahili,

Mafuzo uliyopewa iwe kwako ni kivuli,

Kwako ni muhimu maisha kuendelea,

31. Kichwa kinachofaa kwa shahiri hili ni

  1. Juhudi katika kazi
  2. Mafunzo ya kazi
  3. Kazi inayostahili 
  4. Kazi inayofaa
  5. Changamoto za kazi .


32. Mwandishi "anasema kazi ni kuibobea" ana maana gani?

  1. Kuipenda na kuithamini
  2. Kuleta faraja
  3. Kuijua na kuifanya ipasavyo
  4. Kuifanya kwa kutumia nguvu
  5. Kazi ndiyo mhiniili


33. Vina vya kati na mwisho katika ubeti wa pili ni vipi?

  1. wa naju
  2. wa na hu
  3. tin na i
  4. ti na a
  5. wa na zi


34. Shairi hili linatoa funzo gani?

  1. Ni vyema kuithibitisha kazi
  2. Kazi ni muhimu katika maisha
  3. Ni bora kuajiriwa
  4. Ni muhumu kupewa mafunzo
  5. Yawe ya mafanikio.


35. Neno "thabiti" katika shairi hili lina maana gani?

  1. Mkunjufu
  2. Mnyenyekevu
  3. Mweupe
  4. Madhubuti
  5. Mwepesi


UTUNGAJI

Umepewa habari yenye sentensi nne(4)zilizoandikwa bila mtiririko wa mawazo katika swali la 37-40 zipange sentensi hizi ili ziwe na mtiririko wenye mantiki kwa kuzipa herufi weka kivuli katika herufi ya jibu sahihi katika fomu yako ya kujibia.

37. Kwa mfano,wavulana walipofikia umri wa kuoa iliwalazimu kujijengea nyumba ya kuishi na kuwa na mazao ya chakula.



38. Elimu hiyo ilitolewa na walimu maalum wa jadi na ilihusisha na vitendo.



39. Wakati wa ukoloni elimu hiyo ilipigwa vita na kuonekana kuwa haifai hivyo uliletwa mfumo mpya wa Elimu.



40. Kabla ya kuja kwa wakoloni Waafrika walikuwa na mfumo wao wa elimu ya jadi.



STD VII KISWAHILI NECTA EXAM OF YEAR 2017 Try This  |  

SEHEMU A: SARUFI Katika swali la 1 — 20, weka kivuli katika herufl ya jibu lililo sahihi katika karatasi yako ya kujibia

1. Neno lipi ni tofauti na maneno mengine kati ya haya

  1. Chungwa
  2.  Embe
  3. Ndizi
  4. Nanasi
  5.  Mgomba


2.  Mto Ruvu umefurika mwaka huu. Katika sentensi hii, maneno "mwaka huu" ni ya aina gani?

  1. Nomino
  2.  Vitenzi
  3. Vivumishi
  4. Vielezi
  5. Viwakilishi


3."Mimi sitakuja" Sentensi hii iko katika kauli gani?

  1. Kanushi
  2. Ombi
  3. Swali 
  4.  Taarifa 
  5. Halisi


4.Mama mdogo amepika ugali mwingi". Maneno gani ni vivumishia sentensi hii?

  1. Mdogo na mwingi
  2. Mama na mdogo
  3. Uglai na mwingi 
  4. Mdogo na amepika 
  5. Amepika na ugali


5.       "Wakulima wamehamisha mizinga ya nyuki kutoka mashambani mwao. "Umoja wa sentensi hii ni upi?

  1.  Mkulima amehamisha mizinga ya nyuki kutoka shambani mwao. 
  2.  Mkulima amehamisha mzinga wa nyuki kutoka shambani mwake
  3. Mkulima amehamisha mizinga ya nyuki kutoka shambani mwake.
  4. Mkulima amehamisha mzinga wa nyuki kutoka shambani mwao.
  5.  Mkulima amehamisha mzinga ya nyuki kutoka shambani mwake.


6.       "Mwajuma amemwibia Mwanahamisi kalamu yake". Katika sentensi hii. "Mwajuma ni nani?

  1. Mtendewa 
  2.  Mtendana
  3.  Mtendeka 
  4.  Mtenda
  5. Mtendwa


7.   Kinyume cha neno "duwaa" ni kipi?

  1. Shangaa
  2. Staajabu
  3.  Bashasha
  4. Pumbaa
  5.  Butwaa


8.       "Uvumilivu ulimfanya Pendo apate zawadi. "Uvumilivu ni aina gani ya neno?

  1. Nomino
  2.  Kitenzi
  3. Kivumishi
  4. Kihisishi
  5. Kiwakilishi


9.       Yupi kati ya wafuatao ni lazima awe mwanaume?

  1. Mjomba 
  2. Binamu
  3. Mjukuu
  4.  Ndugu 
  5. Mzee


IO. "Walimu watafundisha masomo yao vizuri". Sentensi hii ipo katika wakati gani?

  1. Uliopita 
  2.  Ujao
  3. Uliopo
  4. Mazoea
  5. Timilifu


11.  "Wanafunzi wenzake walimnyanyapaa. Neno walimnyanyapaa lina maana gani kati ya hizi zifuatazo?

  1. Walimpenda
  2. Walimhurumia
  3. Walimtenga
  4. Walimhusudu
  5. Walimchekesha


12.    Neno nimerudi lipo katika nafsi ipi?

  1. Pili umoja
  2. Kwanza umoja
  3. Kwanza wingi
  4. Tatu umoja E. 
  5. Tatu wingi


13. Kiwanda hutoa ajira kwa wananchi "kiwanda" ni aina gani ya neno?

  1. Kivumishi
  2. Kiwakilishi
  3. Nomino
  4.  Kielezi
  5. Kitenzi


14. Mashine nyingi hupatikana" kiwandani" ni aina gani ya neno

  1. Kivumishi.
  2. Kiwakilishi
  3. Nomino 
  4. Kielezi
  5. Kitenzi.


15.Kisawe cha neno "ndovu" ni kipi kati ya maneno yafuatayo?

  1. Nyati
  2. Faru
  3. Nyumbu 
  4. Tembo
  5. Mbogo.


16, "Mlima meru unafuka moshi" Ukanusha wa sentensi hii ni upi?

  1. Mlima meru unawaka moshi
  2. Mlima meru unatoa moshi.
  3. Mlima meru unafukiza moshi D. 
  4. Mlima meru haufuki moshi 
  5. Mlima meru hauwaki moshi.


17.       Panga maneno yafuatayo kwa kuanzia na neno ambalo katika familia hiyo linaonesha aliyetangulia kuzaliwa hadi wa mwisho kuzaliwa: Baba, kitukuu, babu, kilembwe,

mjukuu, kilembwekeza.

  1. Babu, Baba, Mjukuu, Kitukuu,Kilembwe, Kilembwekeza
  2.  Baba, mjukuu, kitukuu, kilembwe,  kilembwekeza, babu
  3. Kilembwekeza, kitukuu, mjukuu, bab babu, kilembwe
  4. Babu, mjukuu, kitukuu, kilembwe,  kilembwekeza, baba
  5. Mjukuu, kitukuu, baba, babu, kilembwe, kilembwekeza


18.       Kisawe cha neno ”kinyinginya” ni kipi katika maneno yafuatayo?

  1. Mjukuu  
  2. Kitukuu
  3. Kijukuu
  4. Kilembwe
  5.  Kilembwekeza


19.Kisawe cha neno ”mviringo” ni kipi?

  1. bapa
  2. duara
  3. mstatili
  4. pembe tatu
  5. pembe nne


20.Mtu anayechonga vinyago anaitwaje?akaokota,

  1.  Mnajimu
  2. Boharia
  3.  Msanii
  4. Mwashi
  5. Seremala


21. Alipomwona Yule Chui, Juma akapiga moyo konde na kuanza kumshambulia kwa mpini wa jembe. Maana ya msemo kupiga moyo konde ni ipi?

  1.  Kujikaza
  2.  Kuamua
  3. Kutetemeka
  4.    Kutahan?ki
  5.   Kuruka


22. Nimeugua kwa kipindi kirefu sana, lakini sasa ni wa afya. Neno lipi linakamilisha sentensi hii?

  1.  Hoi
  2.  Buheri 
  3.  Buheli
  4. Mzuri
  5.  Mwingi.


23. Wakikua mama yao huwatupa mbali kwa kishindo.Jibula kitendawili hiki ni lipi?

  1. Mbalika
  2. Nzi            
  3. Mhindi 
  4.  Embe 
  5. Mtama.


24.Kati ya methali zifuatazo ni ipi haitoi  msisitizo wa kufanya juhudi katika jambo?

  1.  Maji ukiyavulia nguo sharti uyaoge,
  2.  Bandu bandu humaliza gogo,
  3. Mwenda bure si mkaa bure huenda akaokota
  4. panapofuka moshi hapakosi moto
  5. ukupigao ndio ukufunzao


 25. Kutoa ni moyo usambe ni utajiri”maana  ya methali hii ni ipi?
  1. Matajiri ndio wenye moyo wa kutoa,
  2. masikini ndio wenye moyo wa kusaidia
  3. Kuonyesha moyo wa ukarimu hakuhitaji utajiri,
  4. Utajiri na umaskini havitangamani,
  5. Mwenye nacho ni tajiri.


26 sihimili kishindo"kifungu kipi cha maneno kinakamilisha methali hii?

  1. Mimi nyumba ya nyasi,
  2. Mimi nyumba ya miti,
  3. Mimi nyumba ya vioo, 
  4.  Mimi nyumba ya udongo,
  5. Mimi nyumba ya zamani.


27. "Asiyeuliza" maneno yapi yanakamilisha methali hii kwa usahihi

  1. Kaa naye mbali
  2. Hana budi kujua
  3. Usimwambie kitu
  4. Usimwambie lolote
  5. Hana ajifunzalo


28." Gari langu halitumii mafuta jibu la kitendawili hiki ni lipi?

  1. Macho
  2. Miguu
  3. Mikono 
  4. Tumbo
  5. Masikio.


29. "Anatengeneza mchuzi mtamu sana lakini hapiki jikoni" kitendawili hiki jibu lake ni lipi?

  1.  Ngombe
  2.  Nyuki 
  3.  Mbuzi 
  4.  Muwa
  5.  Mbuzi.


30. "Ukiona vyaelea vimeundwa" methali hii ina maana gani?

  1. Ubora wa kitu hautegemei upya wake,
  2. Vitu vinavyoelea baharini ni meli, 
  3. Vitu vya thamani hupatikana kwa jasho,
  4. Vitu vimeumbwa ili vielee,
  5. Vitu vya thamani vimeundwa.


UFAHAMU.

Soma kwa makini habari ifuatayo kisha jibu maswali 31-40 kwa kuweka kivuli katika herufi ya jibu lililo sahihi katika karatasi yako ya kujibia.

Jua lilikuwa linaunguza mithili ya moto. Hapakuwa na nyasi wala miti iliyokuwa na majani ya rangi ya kijani.Kila uoto ulikuwa wa rangi ya kahawia kavu! Aidha kupata tone la maji ya kunywa ilikuwa ndoto kwani mito na visima vyote vilikauka kau.Baada kuhangaika kwa njaa na kiu, ndipo wanyama waliamua waitishe mkutano ili wajadili hatua ya kuchukua. Makundi • ya wanyama wa aina mbalimbali walikutana chini ya mbuyu. Swala, nyani, mbawa na tembo wote walikuwepo.

"Kama mjuavyo mimi ndimi mfalme wa wanyama wote.Niungurumapo hapana achezae kwa hiyo bila shaka mtakubali kuwa mimi ndiye mwenyekiti wa mkutano huu."alitangaza simba.Wanyama wote walitazamana na kutikisa vichwa kwa ishara ya kuafiki. Kisha alisimama na kusema "Mheshimiwa mwenyekiú, jana nilisikia mlindimo toka upande wa magharibi. Hivyo ninashauri sote tuhame na kuelekea upande huo ili tuokoe maisha yetu kwani huko kuna dalili ya mvua."Wanyama wote waliunga mkono hoja hiyo,isipokuwa kobe ambaye alisema, "mheshimiwa mwenyekiti, endapo kweli tumeazimia kuhama, sisi akina kobe tunaomba mtubebe kwani kasi yetu ya kutembea ni ndogo mno."

Baada ya kila mnyama kutoa rai yake ,Mwenyekiti alisimama na kusema, "Nimesikia yote mliyosema, kabla ya kuanza kuhama nakutuma wewe ngombe upeleke ujumbe wetu kwa binadamu ili waache kuharibu mazingira, kwani hicho ndicho kiini cha matatizo yanayotusibu.Wewe ni kiungo baina yetu na binadamu." ngombe alikubali.

Baada ya kufika ujumbe ule, binadamu alijibu kuwa alikwishaelewa tatizo Ia mazingira na tayari alikuwa na mpango kabambe wa kuchinja mifugo yote ili kutekeleza ushauri wa wataalamu wa mazingira wa kuiokoa dunia na janga Ia jangwa. Kusikia hivyo ngombe alichanja mbuga kuelekea kwa wanyama wengine.

31.  Kwa mujibu wa habari uliyo soma, mkutano wa wanyama ulifanyika wapi?

  1. Kwa mfalme
  2.  Kisimani
  3. Chini ya mbuyu D. 
  4. Kwenye majani
  5. Jangwani.


32.  Mwenyekiti wa mkutano wa wanyama alikuwa nani?

  1. Ng ombe
  2.  Kobe
  3. Nyati
  4. Simba
  5. Nyani


33. Hali ya kukauka kwa mito,visima nyasi na miti kunakutokana na ukosefu wa mvua inaitwaje?

  1. Ukame
  2. Uoto
  3.  Kahawia
  4.  loto
  5. Janga.


34. Jina lingine Ia mnyama aliye washauri wanyama wote kuhamia upande ambako kulikuwa na dalili ya mvua ni lipi kati ya yafuatayo.

  1.  Ndovu B.
  2.  Ngwena
  3. Mbega 
  4.  Kima
  5. Mbogo.


35.Katika habari uliyo soma sababu iliyomfanya kobe kutoafiki moja kwa moja hoja ya kuhama ni ipi?

  1. alikuwa mpinzani wa mwenyekiti ,
  2. aliogopa kuachwa nyuma,
  3. kulikuwa na jua kali
  4. wanyama wengine wangeweza kumla,
  5. kobe ni mvivu kutembea.


36. kwa mujibu wa habari hii ,uharibifu mkubwa wa mazingira hufanywa na nani?

  1. tembo
  2.  mbawala
  3.  swala
  4. binadamu
  5.  nyani.


37. Neno lipi kati ya yafuatayo lina maana sawa na neno janga?

  1. Maafa 
  2.  Kiu
  3. Ukame D. J
  4. angwa 
  5. Joto.


38.  Kifungu cha maneno "alichanjambuga"kinamaana gani?

  1. Alijirudi
  2. Alitembea
  3. Alikimbia
  4. Alirudi
  5. Aliruka


39.  Binadamu alikusudia kuchinja wanyama wa aina gani

  1. Wanyama pori wote
  2. Ngombe na simba 
  3. Wanyama wadogo wote
  4. Wanyama wakubwa wote
  5. Wanyama wote wanaofugwa


40.  Kichwa cha somo uliyosoma kingefaa kiwe kipi?

  1. Kiangazi na jangwa
  2. Matatizo ya binadamu
  3. Jua kali
  4.  Uhamisho wa wanyama
  5. Uharibifu wa mazingira


41.   Kituo cha shairi hili ni kipi?

  1. Kuku kapewa uwezo, kutaga na kuangua
  2. Yai wewe ni mtoto
  3.  Ungegeuka uozo, kuku angekuziria
  4. Kuku kwkao ndiye mama
  5.  Yai wewe ni mtoto, Kuku kwako ndiye mama


42.   Katika shairi hili vina vya kati na mwisho ni vipi? 

  1. zo na ku 
  2.  Zonaa
  3. To na ku
  4. U na ku
  5.  Ya na ku


43.   Shairi hili lina mizani ngapi?

  1. Kumi na sita
  2. Minne
  3.  Nane
  4. Ishirini na tatu 
  5. Sita


44.   Shairi hili lina beti ngapi?

  1. Nne
  2.  Nane
  3. Moja
  4.  Mbili
  5.  Kumi na sita


45.   Neno "kuangua" kama lilivyotumika katika shairi hili lina maana ipi?

  1.  Kuvunja mayai
  2. Kula mayai
  3. Kukwangua mayai
  4.  Kutoa vifaranga katika mayai
  5. Kulalia mayai


46.   Neno "Mizozo" kama lilivyotumika katika shairi hili lina maana gani?

  1. Ghasia
  2. Udadisi
  3.  woga
  4. Majigambo 
  5. Utafiti


SEHEMU E:

UTUNGAJI

Panga sentensi nne (4) zifuatazo ili ziwe na mtiririko wenye mantiki kwa kuzipa herufi

A, B, C na D.

47.   Zizi hilo limegawanywa katika sehemu mbili



48.     Baba yangu anafuga ngombe, mbuzi na kondoo.



49.   Nje ya nyumba yetu kuna zizi kubwa.



50.   Sehemu moja ni ya ngombe na nyingine ni ya mbuzi na kondoo.



STD VII KISWAHILI NECTA EXAM OF YEAR 2016 Try This  |  

Katika swali la 1 — 20, weka kivuli katika herufiyajibu lililo sahihi.

1.  "Wachache wamehamia Boro". Katika sentensi hiyo "Wachache" limetumika kama aina gani ya neno?

  1. Kivumishi
  2. Kielezi     
  3. Kiwakilishi
  4. Kitenzi 
  5.  Kiunganishi


2.         Alimwita nyumbani kwake kwa dhamira ya kumpa karo ya shule. Neno "dhamira" lina maana ipi?

  1. Dhamana 
  2. Madhumuni
  3. Thumuni  
  4.  Dhumuni 
  5. Dhamini


3.         Kauli ipi inaonesha hali ya kutendewa?

  1. Tumechimba visima vyetu. 
  2.  Tunachimbisha kisima chetu. 
  3. Tulichimbiwa kisima chetu. 
  4. Tumechimba kisima chetu.
  5. Tutachimba kisima chetu.


4.         Katika vifungu vya maneno vifuatavyo, kifungu kipi kipo katika kauli taarifa?

  1. Unataka kuondoka lini? 
  2. Alitaka kukuuliza unaondoka lini. 
  3. Ni lini wewe utaondoka? 
  4.  Aliuliza, utaondoka lini?
  5. Aliuliza kuwa ataondoka lini?


5.         Mwenyekiti hakufika mkutanoni leo. Kitenzi "hakufika" kipo katika hali gani?

  1. Mazoea  
  2. Kuendelea  
  3. Timilifu
  4. Matarajio 
  5.  Kanushi


6.         "Wapiganaji wetu walipowasili visiwa vya Comoro walishangiliwa kwa   Ni neno lipi linakamilisha sentensi hiyo?

  1. hofu   
  2.  mzaha  
  3. shangwe
  4. mayowe
  5. dhihaka


7.         Mawaziri wote wa Baraza la Mapinduzi waliapishwa. Neno "wote" limetumika kama aina gani ya neno?

  1. Nomino  
  2.  Kiwakilishi 
  3. Kitenzi
  4. Kivumishi   
  5. Kiunganishi


8.         Babu amemhamishia yule mbuguma kwenye zizi kubwa. Neno "mbuguma" lina maana

  1. Mbuzi dume anayelima  
  2. Ngombe dume anayelima
  3. Kondoo jike aliyezaa 
  4. BWombe jike anayelima
  5. Ngombe jike anayeendelea kuzaa


9.         "Chama kimeteka nyara sera ya serikali." Wingi wa sentensi hiyo ni upi?

  1. Vyama vimeteka nyara masera ya serikali. 
  2.  Vyama vimeteka nyara sera ya serikali. 
  3. Vyama vimeteka nyara serikali.
  4.  Vyama vimeteka sera za serikali.
  5. Vyama vimeteka nyara visera vya serikali.


10.     Nyumba ya ndege huitwaje?

  1. Mzinga 
  2. Kiota 
  3. Korongo
  4.  Banda 
  5.  Shimo


11.     "Wanafunzi hodari watapewa zawadi". Sentensi hiyo ipo katika wakati gani?

  1. Ujao 
  2.  Timilifu 
  3. Uliopita   
  4.  Mazoea 
  5. Uliopo


12.     Maji yamejaa "pomoni" Neno "pomoni" ni aina ipi ya neno?

  1. Nomino  
  2.  Kiwakilishi   
  3. Kielezi
  4. Kihisishi  
  5. Kivumishi


13.     Kati ya maneno "Sherehi, Sherehe, Shamrashamra, Hafla, Tafrija" neno lipi halihusiani na mengine?

  1. Sherehi  
  2. Sherehe 
  3.  Shamrashamra 
  4. Hafia 
  5. Tafrija


14.     Neno lipi kati ya maneno yafuatayo lina maana sawa na "thubutu"?

  1. Ufidhuli  
  2. Ujasiri 
  3. Umahiri 
  4. Ukakamavu 
  5. Utashi


15."Kuzua kizaazaa" ni msemo wenye maana gani?

  1. Ushabiki   
  2. Upendeleo
  3. Malumbano
  4. Masikitiko  
  5. Majungu 


16. Mtu anayetafuta kujua jambo fulani kwa kuuliza maswali huitwaje?

  1. Mawazo
  2. Mbeya
  3. Mfitini
  4. Mdadisi
  5. Mjuaji 


17. Neno Mchakato lina maana ya mfululizo wa................

  1. Mawazo
  2. maoni
  3. shughuli
  4. safari
  5. fikra


18. Neno lipi kati ya yafuatayo lina maana sawa na neno shehena

  1. roda
  2. furushi
  3. mizigo
  4. bidhaa
  5. robota


19. Mtu aliyezaliwa na wazazi wa rangi mbalimbali huitwaje?

  1. Albino
  2. Mkimbizi
  3. mhamiaji
  4. chotara
  5. mzawa


20.      Baada ya miaka minne Kalunde ... ...... mafunzo yake ya udaktari. Ni neno lipi linakamilisha sentensi hiyo?

  1. aliitimu 
  2.  alihimidi
  3.  aliitimisha
  4. alihitimu 
  5.  halihitimu


Katika swali la 21 — 30, weka kivuli katika herufiyajibu lililo sahihi.

21.      Methali isemayo, "Katika msafara wa mamba na kenge wamo" iko sawa na methali ipi kati ya zifuatazo?

  1. Akutukanaye hakuchagulii tusi. 
  2.  Kila kiboko na kivuko chake.
  3. Amulikaye nyoka huanzia miguuni mwake. 
  4. Tajiri na mali yake maskini na mwanawe. 
  5.  Hakuna masiki yasiyo na mbu.


22.      Diengi anapenda kuwarairai watu. "l<urairai watu" ni msemo wenye maana ipi?

  1. Kuwasihi watu ili apate cheo anachokipenda
  2. Kusema na watu kwa maneno mazuri
  3. Kusema na watu ili uwape chochote
  4.  Kusema kwa watu kwajili ya kuwatapeli
  5. Kuwabembeleza watu ili wasimpangie kazi


23.      Msemo "kubarizi" maana yake ni kukusanyika kwa ajili ya .

  1. Sherehe 
  2.  mkutano 
  3.  mazungumzo ya kawaida 
  4. burudani 
  5.  chakula cha pamoja


24.      Methali isemayo "Kila mtoto na koja lake" ina maana gani? 

  1. Kila binadamu ana mapungufu yake.
  2.  Kila mtoto ana matatizo yake.  
  3. Kila mtoto ana mapungufu yake. 
  4.  Kila mtoto ana wazazi wake.  
  5. Kila binadamu ana tabia yake.


25.      Nahau isemayo "kuvishwa kilemba cha ukoka" ina maana gani?

  1. Kupewa sifa unazostahili 
  2.  Kupewa sifa mbaya 
  3.  Kupewa sifa nyingi 
  4.  Kupewa sifa chache
  5. Kupewa sifa usizostahili


26.      Tegua kitendawili kifuatacho: "Nyumbani kwangu kuna jini mnywa maji."

  1. Kikombe 
  2.  Kata 
  3. Kinywa 
  4.  Kibatari  
  5. Mtungi


27.      "Wakulima wa kahawa wa wilaya ya Mbinga wamepewa heko kwa kuzalisha kahawa bora".

Msemo "wamepewa heko" hufanana na msemo gani kati ya ifuatayo?

  1.  kupewa tunzo 
  2. kupewa pongezi   
  3.  kupewa heri 
  4.  kupewa zawadi  
  5. kupewa hawala


28.      Methali isemayo, "Mwenda pole hajikwai" inafanana na methali ipi kati ya zifuatazo?

  1. Haba na haba hujaza kibaba. 
  2.  Fuata nyuki ule asali. 
  3.  Mchumia juani hulia kivulini.
  4. Awali ni awali hakuna awali mbovu.
  5. Baada ya dhiki faraja.


29.     Methali ipi kati ya hizi zifuatazo haifanani na zingine?

  1. Mtegemea nundu haachi kunona. 
  2. Nazi haishindani na jiwe. 
  3. Mlinzi wa kisima hafi kiu. 
  4.  Mchumia juani hulia kivulini.
  5. Baada ya dhiki faraja.


30.     Mwamba ngoma    .. Kifungu kipi cha maneno kinakamilisha methali hiyo?

  1. hualika watu wengi   
  2. hufanya maandalizi mengi
  3. huimba nyimbo nyingi
  4. ngozi huvutia kwake
  5.  hucheza na jamaa zake


SEHEMU C

UFAHAMU

Soma kwa makini habari ifuatayo kisha jibu maswali 31 — 40 kwa kuweka kivuli katika herufi ya jibu lililo sahihi.

Mpendwa kaka Yohana,

Natumani hujambo na unaendelea vizuri na masomo yako. Nimefurahi kusikia kwamba umechaguliwa kujiunga na masomo ya Sekondari. Ndugu wote wanakupongeza na kukutakia kila la kheri katika masomo yako. Soma kwa bidii zaidi kwani elimu ni bahari na haina mwisho.

Baba na mama walifurahi sana baada ya kupata taarifa za kuchaguliwa kwako kwa-njia ya simu kutoka kwa shangazi. Wanamshukuru sana shangazi kwa kukuwezesha na misaada yake mingi kwako ya hali na mali. Baba ameahidi kumtembelea shangazi tarehe ishirini mwezi wa kumi na moja mwaka huu ili kumkabidhi zawadi aliyomwandalia kutokana na ukarimu wake kwako.

Rafiki yako Juma alifika hapa nyumbani akasema kwamba ataniletea picha nikutumie. Hamisi amekuandalia zawadi ambayo atakukabidhi utakapokuja nyumbani wakati wa likizo yako ya mwisho wa muhula. Tunu amesema atakutembelea, lakini uwe mwangalifu unapoongea naye asije akakuchezea shere. Siku hizi ni msanii.

Nisalimie sana shangazi na wanae wote, yaani Amani, Anasitazia na Asia. Sisi sote tunakutakia kila la kheri katika masomo yako.

Akupendaye daima, Mdogo wako, Tumaini.

31.     Neno "ukarimu” lina maana sawa na lipi kati ya maneno yafuatayo?

  1. Fadhila  
  2. Fadhaa  
  3.  Fedheha 
  4.  Faraja 
  5. Fanaka


32.     Mwandishi wa barua hii ametumia msemo "kuchezea shere” Msemo huo una maana ipi?

  1. Fujo   
  2.  Mzaha
  3. Sheria
  4. Shindano
  5. Wivu


33.     Ushindi wa Yohana na mafanikio yake katika masomo umetokana na nini? 

  1. Kuwahi shuleni asubuhi na mapema
  2. Kuhimizwa na wazazi wake
  3. Msukumo kutoka kwa shangazi
  4. Masomo ya ziada kutoka kwa walimu wake  
  5. Kuiga maendeleo aliyonayo Tunu


34.     Wazazi na ndugu zake Yohana walipata taarifa ya kufaulu kwake kwa njia gani?

  1. Kwa njia ya barua
  2. Kwa njia ya simu
  3.  Kutoka kwa walimu
  4. Kupitia matangazo
  5. Vyombo vya habari


35.     Uhusiano wa Yohana na watoto wa shangazi yake ni upi?

  1. Binamu zake 
  2.  Wapwa zake 
  3. Wadogo zake 
  4. Wakubwa zake 
  5.  Ami zake


36.     Katika barua hii mwandishi anafananisha elimu na nini?

  1. Ufunguo wa maisha   
  2. Bahari isiyo na mwisho
  3. Njia ndefu 
  4.  Njia ya maisha 
  5. Marefu yasiyo na ncha


37.     Unafikiri ni sababu ipi ilimfanya baba yake Yohana kumwandalia dada yake zawadi?

  1. Kumpongeza kwa kumsaidia Yohana. 
  2.  Kwa kuwa hajaonana naye muda mrefu. 
  3. Dada yake hupenda sana kupata zawadi.
  4. Alitaka asimchukie Yohana.
  5.  Alipata ushauri kutoka kwa mkewe.


38.     Lengo la Tumaini kumwandikia kaka yake barua lilikuwa lipi?

  1. Kumshauri 
  2.  Kumshawishi 
  3. kumzawadia
  4.  Kumsalimia 
  5.  Kumpongeza


39. Kifungu hiki cha habari ni aina gani ya barua?

  1. Barua ys kirafiki
  2. barua ya wito
  3. barua rasmi
  4. barua ya shukrani
  5. barua ya pongezi


40. Ni methali ipi inatoa fundisho kutokana na ushindi wa Yohana?

  1. Asiyejua maana haambiwi maana. 
  2. Mtumaini cha ndugu hufa masikini. 
  3. Mtoto wa nyoka ni nyoka. 
  4.  Mchuma janga hula na wa kwao.
  5. Mcheza kwao hutuzwa.


   

Soma kwa makini shairi lifuatalo kisha jibu maswali 41 - 46 kwa kuweka kivuli katika herufiya jibu.

Nimekwisha peleleza, karibu kila mahali,

Mule wanamotangaza, matangazo lugha mbili, Juu kuwa Kingereza, Chini kuwa Kiswahili, Juu kiwe Kiswahili, Chini kiwe Kingereza.

Kitangazwe Kingereza, baada ya Kiswahili

Hivi tutapotimiza, lugha itakuwa ghali,

Hivi mnavyofanyiza, sana mnaidhalili,

Juu kiwe Kiswahili, Chini kiwe Kingereza

Serikali bembeleza, tafakari tafadhali,

Jambo hili kueleza, kwa zingine serikali Kiswahili kutangaza, kuwa Chini twakidhili Juu kiwe Kiswahili, Chini kiwe Kingereza.

Tuache kukipumbaza, kwa andiko au kauli, Kwa nyuma kukisogeza, kukipa kisulisuli,

Lazima kuyafukuza, yawezayo kikatili,

Juu kiwe Kiswahili, Chini kiwe Kingereza

Na wenyewe kujikaza, kwa bidii za kimwili kiswahili kutukuza, tukivalie bangili,

Ngomani kutumbuiza, waume na wanawali Juu kiwe Kiswahili, Chini kiwe Kingereza.

41. Katika shairi hilo mstari wa pili katika ubeti wa pili una mizani mingapi?

  1. Tano
  2. mbili
  3. kumi na sita
  4. nane
  5. thelathini na tatu


42. Katika ubeti wa nne, vina ni vipi?

  1. Za na li
  2. La na li
  3. La na ya
  4. Ju na za
  5. Tu na li


43.      Kituo ni kipi katika shairi hili?

  1. Nimekwisha peleleza, karibu kila mahali
  2.  Kitangazwe Kingereza, badala ya Kiswahili 
  3. Serikali bembeleza, tafakari tafadhali
  4. Tuache kukipumbaza, kwa andiko na kauli
  5. Juu kiwe Kiswahili, Chini kiwe Kingereza


44.      Shairi hili linahimiza kuhusu nini?

  1. Kudumisha na kuendeleza mila
  2. Kudumisha na kuendeleza jadi zetu
  3. Kudumisha lugha ya Kingereza
  4.  Kudumisha na kuendeleza Kiswahili 
  5.  Kudumisha na kuendeleza lugha


45.      Ujumbe unaopatokana katika shairi hili unafanana na methali ipi?

  1. Asiyesikia la mkuu huvunjika guu. 
  2.  Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu.
  3. Mkono usioweza kuukata ubusu. 
  4.  Ukitaka cha uvunguni sharti uiname.
  5. Ukipata chungu kipya usitupe cha zamani.


46.      Kutokana na shairi ulilosoma neno "kutukuza” lina maana ipi?

  1. Shutumu 
  2.  Laumu
  3. Heshimu 
  4. Fadhaisha
  5. Kasirisha


SEHEMU E

UTUNGAJI

Umepewa habari yenye sentensi nne(4) zilizoandikwa bila mtiririko sahihi wa mawazo katika swali 47 — 50. Zipange sentensi hizo ili ziwe na mtiririko wenye mantiki kwa kuzipa herufi A, B, C, na D. Weka kivuli katika herufi yajibu sahihi.

47. Hivyo mazoezi huleta afya, kwa hiyo ni muhimu kwa kila mmoja wetu kufanya mazoezi.



48. Mtu asiyefanya mazoezi anapata maradhi ya moyo; atanenepa kupita kiasi, kwa hiyo atapata ugonjwa wa kuumwa mgongo na magoti.



49. Mazoezi ya viungo yanachangamsha misuli ya mwili, mifupa na ubongo.



50. Lakini mtu anayefanya mazoezi anaepuka magonjwa ya moyo na msukumo wa damu.



STD VII KISWAHILI NECTA EXAM OF YEAR 2015 Try This  |  

Katika swali la 1 — 20, weka kivuli katika herufiyajibu lililo sahihi.

1.  "Ramadhani anacheza mpira uwanjani." Sentensi hii ikiwa katika hali ya mazoea itakuwa ipi kati ya hizi zifuatazo?.....

  1. Ramadhani hucheza mpira uwanjani.
  2. Ramadhani atacheza mpira uwanjani. 
  3. Ramadhani alicheza mpira uwanjani. 
  4. Ramadhani amecheza mpira uwanjani 
  5. Ramadhani anacheza mpira uwanjani.


2.          "Bura yangu sibadili na rehani." Kitenzi "sibadili" kipo katika hali ipi?.......

  1. Mazoea 
  2. Timilifu 
  3. Ukanushi 
  4. Kuendelea
  5.  Shurutia


3.          "Babu alikuwa analima shambani." Neno "alikuwa" ni aina ipi ya kitenzi? .

  1. Kitenzi kikuu 
  2.  Kitenzi kitegemezi 
  3. Kitenzi jina
  4. Kitenzi kishirikishi 
  5. Kitenzi kisaidizi


4.          Katika sentensi zifuatazo ipi ina maana sahihi?..

  1. Sikuwa najua Halima ni dada yako.
  2. Sikujua kuwa Halima ni dada yako. 
  3. Sikuwa ninajua Halima ni dada yako.
  4. Sikuwa ninajua kwamba Halima ni dada yako.


5.          Ni neno lipi kati ya yafuatayo ni kisawe cha neno "hifadhi"? .

  1. Weka 
  2.  Panga    
  3. Tunza 
  4.  Ficha  E.
  5.  Funga


6.          Lahaula! Loo! La hasha! Masalale! Ni maneno ya aina gani? 

  1. Vitenzi 
  2. Vihisishi 
  3. Viwakilishi
  4.  Vivumishi 
  5.  Viunganishi


7.          "Ingawa walipata matatizo mengi safarini walifika salama." Neno lipi linakamilisha sentensi hiyo kwa usahihi?

  1. vilevile
  2. kwa hiyo
  3.  halikadhalika D. 
  4. hivyo 
  5. hatimaye


8.          "Mjukuu wangu hupenda kuniamkia kila mara." Sentensi hiyo ipo katika kauli gani? 

  1. Kutendwa  
  2. Kutenda  
  3. Kutendeka
  4. Kutendana  
  5.  Kutendewa


9.          "Wawili wameshindwa kupanda mlima Kilimanjaro." Kiwakilishi katika sentensi hiyo ni kipi? 

  1. Mlima 
  2.  Kupanda 
  3.  Wameshindwa
  4. Kilimanjaro 
  5. Wawili


10.      ”Vita ilipoanza nchini Kenya watu wote . . Kitenzi kipi kinakamilisha sentens hiyo?

  1. walitweta 
  2.  walitaharuki 
  3. walitunukiwa 
  4. walinusurika  
  5.  walitahamaki


11.      "Tulicheza ngoma na kuimba usiku kucha.” Katika sentensi hii watenda ni nafsi ipi?

  1. Ya tatu wingi 
  2. Ya pili wingi
  3.  Yapili umoja
  4. Ya tatu umoja 
  5. Ya kwanza wingi.


12.      ”Utundu wake ulimfanya ajulikane shuleni.” Neno "Utundu” limetumika kama aina gani

neno? 

  1. Kivumishi  
  2.  Nomino
  3.  Kiwakilishi
  4.  Kitenzi  
  5. Kielezi.


13.      "Mwanamuziki hodari aliimba nyimbo vizuri.” Kielezi katika sentensi hii ni kipi? ........

  1. Hodari 
  2.  Aliimba 
  3. Mwanamuziki
  4. Nyimbo  
  5. Vizuri


14.      "Mgeni aliondoka alikofikia.............kuaga.” Kifungu kipi cha maneno kinachokamilishE sentensi hiyo kwa usahihi?

  1. licha ya 
  2. pasi ya 
  3. bila kwa 
  4.  bila ya   
  5.  bila na


15.      Neno moja linalojumuisha herufi "a, e, i, o na u” ni lipi? 

  1. Silabi   
  2.  Konsonanti   
  3. Mwambatano
  4.  Kiambishi 
  5. Irabu.


16.      "Kaka anapenda kujisomea chumbani mwake.” Katika sentensi hiyo kitenzi kisaidizi ni kipi? ........

  1. Anapenda   
  2. . Chumbani 
  3.  Kujisomea
  4. Kaka  
  5.  Kwake.


17.      ”Mchezo mkali ni ule tuliocheza ......... ya Timu ya Majengo.” Neno lipi linakamilisha tungc hiyo kwa usahihi?

  1. zidi
  2. zaidi
  3. kabla
  4. thidi
  5. dhidi


18.      Mama Ntilie akiondoka, uondoke naye. Sentensi hii ipo katika wakati gani? ........

  1. Ujao 
  2.  Timilifu 
  3.  Shurutia 
  4.  Uliopo 
  5.  Mazoea.


19.      Mpira umegonga mwamba nusura goli liingie. Neno lipi linaonesha kitendwa? ........

  1. Nusura 
  2.  Goli C. 
  3. Mpira D.
  4.  Mwamba 
  5. Liingie.


20.      Ni neno lipi kati ya haya yafuatayo ni tofauti na mengine? ........

  1. Sahibu 
  2.  Ajuza 
  3. Msiri
  4. Mwandani 
  5.  Mwenzi


Katika swali la 21 — 30, weka kivuli katika herufiya jibu lililo sahihi.

21.      Nahau isemayo, "Mtu mwenye ndimi mbili" ina maana ipi kati ya zifutazo? ...... .

  1. Mropokaji 
  2.  Mwongo  
  3. Kilimilimi
  4. Kigeugeu
  5. Mfitini


22.      Wanafunzi walipotoka safari walilala usingizi wa pono. Msemo usemao, "Usingizi wa pono" una maana gani?

  1. Usingizi wa mangamungamu
  2. Usingizi wa maruweruwe 
  3. Usingizi mzito mno
  4. Usingizi wa kustukastuka  
  5. Usingizi wa njozi


23.      Kitendawili kisemacho: "Kamba yangu ndefu lakini haiwezi kufunga kuni," kina maana ipi kati ya hizi zifuatazo? 

  1. Mkufu  
  2.  Nyoka 
  3. vvaya 
  4. Treni  
  5.  Njia


24.      Methali isemayo: "Mgaagaa na upwa hali wali mkavu," inatoa funzo gani

  1. Bidii huleta mafanikio 
  2. Mafanikio ni matokeo ya kazi
  3.  Bidii huleta faraja
  4. Bidii ni kazi ya kuhangaika
  5. Mafanikio ni ya lazima


25.      Usingelitia chumvi kwenye kile kikao wajumbe wasingeligombana. "Kutia chumvi" ni usemi wenye maana gani?

  1. Kuongeza maneno yenye maudhi
  2. Kuongeza maneno ya kushtusha 
  3. Kuongeza maneno ya utani
  4. Kuongeza maneno yenye ukweli
  5. Kuongeza maneno yasiyo na ukweli


26 "........... hufa maskini." Kifungu kipi hukamilisha methali hiyo kwa usahihi? .

  1. Anayeiba cha nduguye
  2.  Anayekula cha nduguye
  3. Mtegemea cha nduguye 
  4.  Mkimbilia cha nduguye 
  5.  Asiyethamini cha nduguye


27.      Nahau ipi kati ya hizi zifuatazo hutumika kwa watu ambao matendo yao si ya kupendana?

  1. Kumkubali mtu kwa ulimi tu. B.
  2.  Hawapikiki katika chungu kimoja.
  3. Kupaka mafuta kwa mgongo wa chupa. 
  4. Mkaidi hafaidi mpaka siku ya idi.
  5. Panya huuma huku akipuliza.


28.      Methali ipi kati ya hizi zifuatazo inapingana na hii, "Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu." 

  1. Asiyesikia la mkuu huvunjika guu. 
  2.  Kiburi si maungwana.
  3. Mtoto mkaidi mngoje siku ya ngoma. 
  4.  Mkaidi hafaidi mpaka siku ya idi. 
  5.  Mtoto mwerevu hafunzwi adabu.


29.      Methali ipi kati ya hizi zifuatazo inapingana na hii, "Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu”.

  1. Panya wengi hawachimbi shimo
  2. Kidole kimoja hakivunji chawa
  3. Polipo na wengi hapaharibiki neno 
  4. Mkono mmoja hauchinji ngombe 
  5. Jifya moja haliinjiki chungu.


30. "Mchelea mwana kulia hulia yeye mwenyewe”. Methali hii inatoa funzo gani? 

  1.  Bora kulea kuliko kulelewa.
  2.  Kuhofia kulea si malezi bora.
  3. Mtoto asipofunzwa vema huaibisha.
  4. Kulea mtoto ni kazi kubwa.
  5. Malezi ya mtoto husababisha hofu.


SEHEMU C

UFAHAMU

Soma kwa makini habari ifuatayo kisha jibu maswali 31 — 40 kwa kuweka kivuli katika herufi ya jibu lililo sahihi.

Matunda kama yalivyo mazao mengine ya kilimo yanatokana na mimea mbalimbali. Kwa mfano fenesi ni tunda litokanalo na mfenesi na chungwa hutokana na mchungwa. Maembe, mapapai, mananasi na mapera ni matunda matamu. Ubuyu, ukwaju na limau ni matunda machachu. Hata hivyo, karibu matunda mengi huwa machachu yakiwa mabichi, yakiiva huwa matamu.

Miaka ya hivi karibuni watu wengi wamepanda mimea ya matunda kwenye maeneo ya nyumba zao, hivyo kujipatia matunda kwa njia rahisi. Baadhi ya watu wanaoishi katika mikoa kama vile Tanga na Morogoro wamelima mashamba ya matunda na wameshaona faida ya kilimo hicho na kupanua mashamba yao. Licha ya watu hao kujipatia chakula bora, wameuza na kuwa na pato kubwa.

Matunda yana umuhimu mkubwa sana katika miili yetu. Matunda tunayokula yanaikinga miili yetu isipatwe na maradhi. Pia matunda yanaongeza damu mwilini, husaidia kuponyesha vidonda haraka na macho kuona vizuri katika mwanga hafifu. Watu wasiokula matunda hupata udhaifu wa fizi ambao husababisha fizi kutoa damu.

Aidha matunda ni kiburudisho wakati wa joto. Watu wengi wamekuwa wakisindika matunda ili kupata juisi kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na biashara.

MASWALI

31.      Kichwa cha habari hii kinachofaa zaidi ni kipi?

  1. Matunda kwa afya
  2. Umuhimu wa matunda
  3.  Matunda chanzo cha pato 
  4.  Matunda na ulinzi wa mwili 
  5. Matunda hujenga mwili.


32.      "Watu wanaokula matunda huepuka magonjwa mengi,” ni methali ipi inaendana na kauli hii?

  1. Heri kufa macho kuliko kufa moyo 
  2. Usiache mbachao kwa msala upitao 
  3.  Kinga ni bora kuliko tiba.
  4.  Lisemwalo lipo na kama halipo laja. 
  5.  Mwenye kovu usidhani kapoa.


33.      Maji ya matunda yaliyokamuliwa huitwaje? .

  1. Mvinyo
  2. Juisi
  3. Jusi
  4. Rozera
  5. Zabibu


34.

"Matunda yaliyoiva” ina maana sawa na ipi kati ya zifuatazo? ........

  1. yenye ukakasi
  2. machachu
  3. matamu
  4. mabichi
  5. mabivu


35."Kilimo cha matunda kimekuwa cha faida kubwa kwao.” Methali ipi ambayo inaendana na maelezo hayo?

  1. Jembe halimtupi mtu
  2. Mla ni mla leo, mla jana kala nini?
  3. Jisaidie Mungu Akusaidie
  4. Mchumia juani hulia kivulini
  5. Kula nanasi kwahitaji nafasi


36. Ni kwanini wakulima wa matunda hupanua mashamba yao? 

  1. Kupata chakula  
  2. Kupata kiburudisho
  3. Kuongeza pato D. 
  4. Kupata sifa 
  5.  Kupata mikopo


37.      Matunda ya ubuyu na ukwaju yakiwa yameiva huwa na ladha gani? 

  1. Chumvi  
  2. Uchungu 
  3. Ukakasi 
  4.  Ukali 
  5. Uchachu


38.      Kazi kubwa ya matunda mwilini ni ipi? 

  1. Kuponyesha macho 
  2. Kuburudisha
  3.  Kujenga mwili 
  4.  Kuponyesha vidonda
  5.  Kulinda mwilli


39.      "Kusindika matunda” ina maana sawa na kifungu kipi kati ya vifuatavyo? 

  1. Kusaga na kukamua matunda
  2. Kukamua matunda na kuyahifadhi
  3. Kukamua na kuchuja matunda
  4.   Kuyasaga matunda yaliyoiva
  5. Kuyaivisha matunda na kuyasaga


40.      Umepata funzo gani kutokana na kifungu hiki cha habari?

  1. Matunda hukuza akili. 
  2.  Matunda huongeza unene.
  3.  Matunda hukuza akili na mwili.
  4. Matunda hulinda mwili na huongeza damu.
  5.  Matunda hujenga mwili na huongeza joto.


SEHEMU D

USHAIRI

Soma kwa makini shairi lifuatalo kisha jibu maswali 41 - 46 kwa Kuweka kivuli katika herufi ya jibu.

Mtu kujitegemea, huwajambo Ia lazima,

Usipende subiria, kusaidiwa daima,

Huwezi kuendelea, ndugu usipojituma,

Kamwe hupati heshima, usipojitegemea.

Kama Mungu kakuumba, mzima huna kilema, Fedheha kuombaomba, takuwa mtu wa nyuma, Hutakuja kujigamba, ukikudharau umma. Kamwe hupati heshima, usipojitegemea.

Kazi mtu usidhani, sharti niya kusoma,

Ya kuleta ofisini, na kuhesabu ndarama,

Waweza kwenda shambani, ushikejembe kulima, Kamwe hupati heshima, usipojitegemea.

Utaambiwa doezi, mtu uso taadhima,

Pengine uitwe mwizi, umezoea dhuluma, Wajapo wapelelezi, ndiwe watakuandama, Kamwe hupati heshima, usipojitegemea.

41.      Katika shairi ulilosoma neno "ndarama" lina maana ipi? 

  1. Mali
  2. Pesa
  3.  Gharama
  4. Amana
  5. Thamani


42.      Kisawe cha neno "taadhima" ni kipi? 

  1. Heshima
  2. Taashira
  3. Dhamiri
  4. Dhima
  5. Dhamana


43.      Ujumbe unaopatikana katika shairi hili unaweza kuwasilishwa kwa methali ipi kati ya zifutazo? ........

  1. Mkulima ni mmoja walaji ni wengi 
  2. Mchagua jembe si mkulima
  3. Mkulima hasahau jembe kiserema 
  4.  Mkulima halaumu jembe lake
  5. Kilimia kikizama kwa jua huibuka


44.      Katika shairi ulilosoma kituo bahari ni kipi? 

  1. Mtu kujitegemea, huwa jambo la lazima. 
  2.  Kama Mungu kakuumba, mzima huna kilema.
  3. Utaambiwa doezi, mtu uso taadhima.
  4. Waweza kwenda shambani, ushike jembe kulima 
  5.  Kamwe hupati heshima, usipojitegemea.


45.      Katika shairi ulilosoma nusu mstari una mizani ngapi? 

  1. Nane
  2. Mbili
  3. Tatu
  4.  Nne
  5. Kumi na tano


46.      Neno "fedheha" kama lilivyotumika katika shairi hili lina maana gani?

  1.  Maudhui
  2. Lawama
  3. Adibu
  4.  Adhibu 
  5.  Aibu


Umepewa habari yenye sentensi nne(4) zilizoandikwa bila mtiririko sahihi wa mawazo katika swali 47 — 50. Zipange sentensi hizo ili ziwe na mtiririko wenye mantiki kwa kuzipa herufi A, B, C, na D weka kivuli katika herufi ya jibu sahihi.

47.      Ukataji wa miti kwa wingi kwa ajili ya ujenzi na shughuli zingine huweza kuisababisha nchi yetu ya Tanzania kuwa jangwa.



48.      Kutokana na miti watu hujenga nyumba nzuri za kila namna, zinazopendeza na za kudumu.



49.      Hivyo ni muhimu kwa kila mtu kupanda mti kila anapokata mti kwani nchi isiyo na miti ni sawa na mtu ambaye amevuliwa nguo.



50.      Miti ina faida nyingi sana kwa binadamu.



STD VII KISWAHILI NECTA EXAM OF YEAR 2014 Try This  |  

2014: KISWAHILI

 SEHEMU A: SARUFI

 Katika swali la 1 - 20, andika herufi ya jibu lililo sahihi katika karatasi yaka ya kujibia.

 1. "Yeye amefaulu mitihani yake vizuri." katika sentensi hii neno lipi limetumika kama kielezi? 

  1.  amefaulu
  2.  yeye
  3.  vizuri 
  4.  mitihani
  5.  yake 


2. "Dada ameandika barua kwa baba." Sentensi hii iko katika kauli gani? 

  1.  kutendea
  2.  kutenda
  3.  kutendwa 
  4.  kutendeana
  5.  kutendeka


3. Katika sentensi zifuatazo ipi ni sahihi?

  1. Nimekuja hapa tangia asubuhi 
  2. Nimekuja hapa tangiapo asubuhi 
  3. Nimekuja hapa tanguapo asubuhi 
  4. Nimekuja hapa tangu asubuhi 
  5. Nimekuja hapa tangiepo asubuhi 


4. Neno lipi ni tofauti na maneno mengine kati ya maneno yafuatayo?

  1.  viwakilishi
  2.  vivumishi
  3.  vielezi 
  4. vitenzi
  5. visaidizi 


5. "Tunu angalisoma ..... mtihani wake." Neno lipi linakamilisha sentensi hiyo kwa usahihi? 

  1.  angefaulu
  2.  angalifaulu
  3. asingefeli 
  4.  angelifaulu
  5. asingalifaulu 


6. "Mnyama mkali amekamatwa leo." Katika sentensi hii neno "mkali" limetumika kama aina gani ya neno? 

  1. kielezi
  2. kiwakilishi
  3. kitenzi 
  4. kivumishi
  5. kiunganishi 


7. "juma amefika na hatacheza mpira" Kitenzi "hatacheza" kipo katika half gani? 

  1.  Ukanushi
  2.  Titnilifu
  3.  Mazoea 
  4.  Ujao
  5.  Shurutia 


8. "Alisema hanywi dawa tena." Kauli halisi ya sentensi hii ni ipi? 

  1. "Hanywi dawa"
  2. "Hatakunywa dawa" 
  3. "Sinywi dawa" 
  4.  "Sitakunywa tena dawa"
  5. ."Sinywi tena" 


9. "Walikotoka kuna mvua." Sentensi hii ipo katika wakati gani? 

  1. Mazoea
  2. Shurutia
  3. Uliopo 
  4. UliopitaE.Ujao


10. "Hamisa na Hanifa ni mapacha walioungana." Katika sentensi hii neno "na" limetumikakama aina gani ya neno?

  1. Kihisishi
  2. Kiunganishi 
  3. Kimilikishi
  4. Kivumishi 
  5. Kiwakilishi


11. Panya huyu anakula unga wangu. Wingi wa sentensi hii ni upi?

  1. Panya hawa wanakula unga wangu.
  2. Mapanya hawa wanakula unga wetu.
  3. Panya hizi zinakula unga wangu.
  4. Panya hizi zinakula unga wetu.
  5. Panya hawa wanakula unga wetu.


12. Siku ile ya maandamano kulikuwa na...........wa pikipiki. Ni neno lipi linakamilisha sentensi hii?

  1.  msururu 
  2.  msuluru 
  3.  msurulu
  4.  Msululu 
  5.  musururu


13. "Mpira wetu umechanika vibaya" Sentensi hii ipo katika kauli gani?

  1.  Kutenda 
  2.  Kutendeka 
  3.  Kutendeana
  4.  Kutendwa 
  5.  Kutendewa


14. Neno mchwa lina silabi ngapi?

  1.  Mbili 
  2.  Tana 
  3.  Moja
  4.  Nne 
  5.  Tatu


15. "Hapa ...............alipoishi chifu Mirambo." Ni neno lipi linakamilisha sentensi hii kwa usahihi?

  1.  ndiko 
  2.  ndimo 
  3.  ndiyo
  4.  ndipo 
  5.  ndio


16. Atakapomnyonyoa yule hata ......... kwenye moto. Kitenzi kipi kinakamilisha tungo hii?

  1.  atambanika 
  2.  anambanika 
  3.  humbanika
  4.  amembanika 
  5.  alimbanika


17. "Kitabu changu ni cheusi, chako ni cheupe." Neno "chako" ni aina gani ya neno?

  1.  Kivumishi 
  2.  Kiwakilishi 
  3.  Kielezi
  4.  Kihusishi 
  5.  Kiunganishi


18. Yeye ni kijana mdogo. Neno "yeye" lipo katika nafsi gani?

  1.  Ya kwanza umoja 
  2.  Ya tatu umoja 
  3.  Ya pill umoja
  4.  Ya tatu wingi 
  5.  Ya pill wingi


19. Kinyume cha kitenzi "paa" ni kipi?

  1.  Toweka 
  2.  Potea 
  3.  Elea
  4.  Shuka 
  5.  Tua


20. Mwalimu J. K. Nyerere ni mwasisi wa chama cha TANU. Neno "ni" limetumika kama ainaipi ya kitenzi?

  1.  Kitenzi kikuu 
  2.  Kitenzi kisaidizi
  3.  Kitenzi kishirikishi 
  4. Kitenzi kikamilifu
  5.  Kitenzi kitegemezi


SEHEMU B

 LUGHA YA KIFASIHI 
Katika swali la 21- 30 chagua herufi ya jibu lililo sahihi kisha andika kwenye karatasiya majibu.

21. "Ulichokitupa pwani ................" Kifungu kipi cha maneno hukamilisha methali hiyo?

  1.  kakingoje ufuoni
  2.  kisubiri bandarini
  3.  utakipata bara 
  4.  hukomea kivukoni
  5.  hutokomea baharini


22. "Mkiweza..............katika kazi hiyo, hatimaye mtafanikiwa." Nahau ipi inakamilisha tungo hii?

  1.  kuuma na kupulizia 
  2.  kujikaza kisabuni
  3.  kuwa chuma 
  4.  kuwa na sauti
  5.  kuwa na nafasi


23. Methali isemayo, "Ngoma ikilia sana hupasuka" hulingana kimaana na methali ipi kati yahizi zifuatazo?

  1.  Mgema akisifiwa tembo hulitia maji.
  2.  Debe tupu haliachi kutika. 
  3.  Tamaa mbele mauti nyuma.
  4.  Mpanda ovyo ndiye mla ovyo. 
  5.  Mshindo mkuu huvuma mbali.


24. "Ukukuu wa kamba si upya wa ukambaa." Methali hii ina maana sawa na methali ipi?

  1. Heri nusu shari kuliko shari kamili.
  2. Ukipata chungu kipya usitupe cha zamani.
  3. Kamba hukatikia pabovu.
  4. Nazi mbovu harabu ya nzima.
  5. Badiliko kwa mjukuu huanza na babu.


25. "Hamadi kibindoni." Kati ya tafsiri zifuatazo ni ipi inayotoa maana sahihi ya msemo huo?

  1. Akiba ni ile iliyo nyingi
  2. Weka akiba yako vizuri
  3. Kizuri hakinabudi kuhifadhiwa
  4. Kikufaacho ni kile ulicho nacho
  5. Akiba iliyohifadhika hunusurika


26. "Samaki mkunje angali mbichi." Methali ipi kati ya zifuatazo ina maana sawa na hii?

  1. Samaki huanza kuoza kichwani.
  2. Ukitaka riba sikio ziba.
  3. Jino la pembeni si dawa ya pengo.
  4. Sikio la kufa halisikii dawa.
  5. Ngozi ivute ill maji.


27. Methali isemayo. "Chanda chema huvikwa pete" inatoa funzo gani?

  1. Dhahabu hupewa aliyeshinda.
  2. Jambo zuri huzawadiwa.
  3. Inapobidi jamii hupewa zawadi.
  4. Mtu mzuri husifiwa.
  5. Mshindi hupokea Baraka.


28. "Ukitaka kuruka agana na nyonga" Methali hii inaasa kuhusu jambo gani?

  1. Tekeleza jambo kwa kufuata maelekezo
  2. Tafakari kwa kina kabla ya kutenda
  3. Fuatilia kwa haraka, ndipo utende
  4. Kuuliza ni muhimu kabla ya kutenda
  5. Tenda jambo kwa kufanya maamuzi


29. Methali isemayo. "Mpofuka ukongweni.................. " hukamilishwa na kifungu kipi cha maneno kati ya hivi vifuatavyo?

  1. huzuni yake ni kubwa
  2. hakumbuki zamani
  3. hupotea njia 
  4. hukumbuka ujanani
  5. hapotewi na njia


30. Nikikutana na adui yangu nanyongea. Jibu la kitendawili hiki ni lipi?

  1. Askari
  2. Ugonjwa 
  3. Mbwa
  4. Ujinga
  5. Umaskini


SEHEMU C  

  UFAHAMU  

Soma kwa makini habari ifuatayo kisha jibu maswali 31 - 40 kwa kuandika herufi ya jibu lililo sahihi katika karatasi ya majibu.

Mabadiliko ya hali ya hewa yamekuwa makubwa kiasi cha kutisha. Zamani mababu wetu walitabiri mvua wao wenyewe pasi na kuwa na vyombo vya kisasa. Suala linalozungumziwa sana siku hizi ni mabadiliko ya hali ya hewa na athari zake kwa jamii nzima. Kila mtu ana wasiwasi kuhusu mvua ambazo huchukua muda mrefu bila kunyesha.

Ukosefu wa mvua ambao mwishowe huleta ukame na njaa umechangiwa kwa kiasi kikubwa na shughuli za binadamu ambazo zinaongezeka kwa haraka siku hadi siku. Shughuli hizo mbalimbali ambazo kwa upande mmoja zimeonekana kama za kimaendeleo ni kuongezeka kwa matumizi ya maliasili. Mifano mbalimbali ambayo inaonesha matumizi hayo ni pamoja na ujenzi wa nyumba nyingi zaidi, kupata nishati ya kutosha kwa ajili ya kupikia na upatikanaji wa mbao na magogo kwa wingi kwa matumizi ya ndani na hata ya nje ya nchi.

Hata hivyo, iii maendeleo hayo yawe na mwelekeo chanya jamii inalazimika kupanda miti kwa wingi iii kukidhi mahitaji hayo. Aidha ni vema kuzingatia kuwa ukataji miti ni chanzo kikubwa cha mito na vijito kuwa na maji haba au kukauka kabisa.

MASWALI

31. Kichwa cha habari kinachofaa habari hii ni kipi?

  1. Mabadiliko ya hali ya hewa 
  2. Ukosefu wa chakula
  3. Kuongezeka kwa joto
  4. Kuongezeka kwa ukame
  5. Mabadiliko na athari zake


32. Tatizo kubwa zaidi ambalo husababishwa na ukosefu wa mvua kwa muda mrefu ni lipi kati ya haya yafuatayo?

  1. Kukatika kwa umeme
  2. Ujenzi pungufu
  3. Kukosekana nishati
  4. Kukosekana kwa miti
  5. Kuwepo kwa baa la njaa


33. Mwandishi anayaelezea mabadiliko ya hali ya hewa kuwa yalikuwa.

  1.  hayakadiriki
  2.  ya hali ya juu 
  3.  ya kutisha
  4.  ya kukadirika 
  5.  hayatabiriki


34. Neno "haba" kama lilivyotumika katika kifungu cha habari lina maana gani?

  1.  Kidogo 
  2.  Kiasi
  3.  Kadiri
  4.  Wastani 
  5.  Rasharasha


35. Dalili mojawapo kubwa ya maendeleo ni ipi kama ilivyoelezwa katika kifungu cha habari?

  1.  Kupata nishati ya kupikia
  2.  Ongezeko la miti ya kujengea 
  3.  Ongezeko la utumiaji wa maliasili
  4.  Upatikanaji wa mbao na magogo 
  5.  Ongezeko la ujenzi wa nyumba


36. Mabadiliko ya hali ya hewa yana maana sawa na ipi kati ya hizi zifuatazo?

  1.  Uoto
  2.  jotoridi
  3.  Mazingira ya nchi 
  4.  Sura ya nchi 
  5.  Tabia nchi


37. Kisawe cha neno "mwishowe" kama kilivyotumika katika habari hii ni kipi?

  1.  Tamati 
  2.  Hatima 
  3.  Baadaye
  4.  Hatimaye
  5.  Hitimisho


38. Watu wa zamani waliweza kutabiri mvua kwa kutumia:

  1.  vyombo vya kisasa 
  2.  kipaji chao wenyewe
  3.  vyombo vya zamani 
  4.  kipima mvua cha kienyeji
  5.  ubunifu waliorithi


39. Mito na vijito huwa na maji haba au kukauka kutokana na nini?

  1.  Kukata miti kwa wingi 
  2.  Kuchoma majani karibu na mito
  3.  Kukata majani kwa wingi
  4.  kuchoma miti iliyozunguka mito
  5.  Kukata miti iliyozunguka vijito


40. Nishati ni neno lenye maana sawa na lipi?

  1.  Kawa
  2.  Kivo
  3.  Kiwi 
  4.  Kivi 
  5.  Kawi


SEHEMU D

USHAIRI

Soma kwa makini shairi lifuatalo kisha jibu maswali 41 - 46 kwa kuandika herufi ya jibulililosahihi kwenye karatasi ya majibu.

Msituni nikakuta, nyuki wamo mzingani,Kwa juhudi wanakita, mara nje mara ndani,Husuda wameikata, hata hawasengenyani,

Nyuki ni wadudu duni, wanashinda kwa umoja,

Mchwa nao nikaona, wamejenga maskani,Wafanya bidii sana, uvivu hawatamani, Wao husaidiana, tena hawadanganyani,

Mchwa wadudu wa chini, wanaishi kwa umoja.

Nalojeshi la siafu, hutandawaa njiani, Laenda bila ya hofu, maana lajiamini,Silaha zao dhaifu, menu tena hawaoni,Wa kuwatania nani, kwani wanao umoja

Nao chungu wachukuzi, nyamarima wa njiani,Maskani wapagazi, mizi,go yao kichwani,Ingawa si wachokozi, wakali ukiwahini,

Katu hawafarakani, wanadumu kwa umoja

41. Mwandishi wa shairi hili anasisitiza kuhusu nini?

  1. Uzalishaji 
  2.  Maarifa
  3. Ushirikiano
  4. Urafiki 
  5. Undugu


42. Shairi hili lina mizani mingapi kwa kila mstari?

  1.  Sita 
  2. Kumi na sita
  3. Tano
  4.  Saba 
  5. Thelathini na moja


43. Neno "husuda" kama lilivyotumika katika shairi hili lina maana gani?

  1. Uhasama
  2. Hisani
  3. Hiana
  4. Wivu 
  5. Huzuni


44. Kisawe cha neno "Tadi" ni kipi?

  1. Uchokozi 
  2.  Tishio 
  3. Kemea 
  4. Ukombozi
  5. Umbua


45. Kina cha kati katika ubeti wa pili ni kipi?

  1. Wa 
  2. Na
  3.  la 
  4. U
  5. Ni


46. Kichwa cha habari kinachofaa kwa shairi hill ni kipi?

  1. Upekee wa wadudu 
  2. Umuhimu wa wadudu
  3. Uhatari wa wadudu 
  4. Uchunguzi wa wadudu
  5. Umoja wa wadudu


SEHEMU E

UTUNGAJI

Umepewa habari yenye sentensi nne (4) zilizoandikwa bila mtiririko sahihi wa mawazo katikaswali la 47 - 50. Zipange sentensi hizo iii ziwe na mtiririko wenye mantiki kwa kuzipa herufi A,B,C na D. Andika herufi ya jibu sahihi katika karatasi ya kujibia.

47. Kwa njia hii, vizazi vilivyofuata viliweza kujua uvumbuzi uliofanywa kabla yao.



48. Jambo muhimu lililofanywa na mababu zetu ni kuhifadhi kumbukumbu za uvumbuzi waokwa kuchora kila kifaa walichovumbua.



49. Kwa kutumia vizazi vilivyotangulia nasi pia tunaweza kuvumbua vitu vipya ambavyovitaweza kutuletea maendeleo zaidi.


50. Hivyo maisha ya binadamu yakaendelea kuwa bora na yenye manufaa kila siku.



STD VII KISWAHILI NECTA EXAM OF YEAR 2013 Try This  |  

11. Sentensi ipi kati ya hizi ipo katika hali timilifu?

  1.  Mheshimiwa Rais anahutubia mkutano
  2.  Mheshimiwa Rais alihutubia mkutano
  3.  Mheshimiwa Rais atahutubia mkutamo 
  4. Mheshimiwa Rais amehutubua mkutano
  5.  Mheshimiwa Rais alikuwa anahutubia mkutano.


12. Neno lipi ni tofauti na maneno mengine kati ya yafuatayo?

  1.  Maji 
  2.  Maziwa 
  3.  Soda 
  4.  Juisi 
  5.  Samli


13. "Kitabu chako ni kizuri, ukienda dukani nami uninunulie ... ......” Ni kifungu kipi cha maneno hukamilisha sentensi hiyo?

  1.  kama hivyo 
  2.  kama hiko 
  3.  kama icho
  4.  mfano wa iko 
  5.  kama hicho


14. Tunda huachwa mpaka likauke." Setensi hiyo ikiwa katika hali ya ukanushi itakuwa ipi kati ya zifuatazo?
  1.  Tunda haliachwi mpaka likauke
  2.  Tunda haliachi mpaka likauke
  3.  Tunda halikuachwa mpaka likauke
  4.  Tunda halitaachwa mpaka likauke
  5.  Tunda halijaachwa mpaka likauke


15. Mkutano haukufanyika kwa sababu mwenyekiti na katibu hawakufika. Kifungu kipi cha maneno kati ya vifuatavyo kinasadifu sentensi hiyo?

  1.  Mkutano uliairisha 
  2.  Mkutano uliahirishwa
  3.  Mkutano ulihairishwa 
  4.  Mkutano uliharishwa 
  5.  Mkutano ulihairisha


16. Mlinzi wa mlangoni huitwaje?

  1.  Boharia 
  2. Baharia 
  3. Bawaba
  4.  Banati 
  5.  Bawabu


17. Joshua yuko jikoni anapaa samaki. Neno "anapaa” kama lilivyotumika katika sentensi hii lina maana ipi?

  1.  Kuwapaka samaki chumvi 
  2.  Kuondoa magamba ya samaki 
  3.  Kuondoa mifupa katika samaki 
  4.  Kukausha samaki kwa moto 
  5. .Kuwakata samaki vipande vipande.


18. "Mtoto wa ngombe anaitwa ndama, watoto wa kuku, bata, kanga wanaitwa vifaranga, kimatu ni mtoto wa nani?

  1. Nzige
  2. Nyuki
  3. Inzi
  4. Kipepeo
  5. Buibi


19. Kisawe cha neno ”eupe” ni kipi?

  1. Chokaa
  2. Angavu
  3. Theluji
  4. Ukungu
  5. Angaza


20. Siku ya nne baada ya leo huitwaje?

  1. Mtondo
  2. Mtondo kutwa
  3. Mtondogoo
  4. Kesho kutwa
  5. Mtondogoo kutwa


SEHEMU C

UFAHAMU

Soma kifungu cha habari na kishajibu maswaliyanayofuata:

Maji ni moja kati ya vitu vitatu muhimu sana vinavyotuwezesha kuishi. Vitu vingine ni hewa na chakula. Hewa ndiyo yenye umuhimu wa kwanza, ikifuatiwa na chakula. Kusingelikuwa na maji maisha ya binadamu na ya viumbe wengine yasingewezekana. Kila mtu anaelewa umuhimu wa maji katika maisha. Maji yanatawala maisha kwa kiasi kikubwa sana. Baadhi ya viumbe kama vile samaki, mamba, kasa, konokono, nyangumi na wengineo maskani yao ni majini, hivyo maji yakikosekana viumbe hao huweza kuaga dunia.

Binadamu anatumia maji kwa shughuli mbalimbali. Shughuli hizo ni pamoja na kupikia, kufulia, kusafishia vyombo, kuoga na kunywa. Katika sehemu nyingi za nchi yetu watu hutumia maji kwa kumwagilia bustani za mboga, maua na miti. Katika maeneo yenye mito mikubwa na maziwa maji yake hutumika kwa kumwagilia mashamba kama yale ya mpunga na mahindi. Kilimo cha umwagiliaji kinafaa kwa sababu mkulima anakuwa na uhakika wa kuvuna.

Maji ya mvua huwezesha watu kulima na kupanda mazao ya chakula na ya biashara. Hivyo zipo sehemu ambazo wakulima hulima kilimo cha umwagiliaji lakini sehemu kubwa ya wakulima hutegemea kilimo cha mvua.

Kwa ujumla maji yawe ya mvua au yanayotokana na mito au maziwa yana umuhimu mkubwa mno kwa binadamu kama walivyosema wahenga maji ni uhai, hivyo inashauriwa kwamba ni muhimu kwa kila mtu kunyvva maji safi na salama ili kulinda siha zetu.

MASWALI

31.Vitu vitatu muhimu vinavyomwezesha binadamu kuishi ni vipi?

  1. Hewa, chakula na nyumba 
  2. Hewa, maji ma chakula
  3.  Maji ushauri na hewa 
  4. Maji, hewa na mvua
  5. Chakula, mvua na hewa


32.Wakulima wengi kama ilivyoelezwa katika habari hii hulima kilimo kinachotegemea nini?

  1.  Mito 
  2.  Umwagiliaji 
  3. Mvua
  4. Mabwawa 
  5.  Maziwa


33. Kiumbe yupi kati ya wafuatao halandani na wenzie?

  1.  Kima 
  2.  Mamba
  3. Nyangumi
  4. Kasa
  5. Samaki


34.Kilimo cha umwagiliaji kina sifa gani kubwa?

  1.  Uvunaji upo dhahiri 
  2. Kinatumia maji ya maziwa makubwa
  3. Kinatumia maji yaliyohifadhiwa 
  4. Mazao hayapati magonjwa 
  5. Kinalimika majira yoyote


35.Neno "siha" kama lilivyotumika katika kifungu hiki cha habari lina maana gani?

  1. Afya njeme
  2. Sifa njema
  3. Maisha mema
  4. Tabia njema
  5. Kinywa safi


36. "Kuaga dunia" ni msemo wenye maana gani?

  1. Kuzirai 
  2. Kuzimu
  3. Kulala fofofo
  4. Kufariki 
  5. Kufia mbali


37. Ni kwanini mtunzi wa habari hii anashauri watu kunywa maji safi na salama?

  1.  Ili kuondokana na kiu 
  2.  Ili kulinda vinywa vyetu
  3.  Ili kuburudisha mwili 
  4.  Ili kuondokana na kichocho 
  5.  Ili kulinda afya zetu


38.Neno "maskani" kama lilivyotumika katika kifungu cha habari lina maana gani?

  1.  Nyumba 
  2.  Makao 
  3.  Maisha 
  4.  Mahitaji 
  5.  Shughuli


39.Kichwa cha habari kinachofaa kwa kifungu hiki ni kipi?

  1.  Hewa ni muhimu 
  2.  Maji ni uhai
  3.  Maji salama 
  4.  Hewa na chakula
  5.  Siha bora


SEHEMU D

USHAIRI

Soma shairi lifuatalo kisha jibu maswali yanayofuata

Nyumbani kwako kuzuri,japokuwa ni pangoni,

Nyumba yako nijohari,ya mwenzako sitamani, Hata pawe pa tajiri, hapafai maishani,

Nyumbani kwakojohari, kwingine usitamani. 

Kwingine usitamani, nyumbani kwakojohari,

Unaishi kwa amani, na pia kwa ujasiri,

Hiyo kweli abadani, nyumbani kunasetiri,

Nyumbani kwakojohari, kwingine usitamani,

Uipende nyumbayako, utaona raha yake,

Kisha penda nduguyako, kwako apaone kwake, Dunia mahangaiko, usipende pekepeke,

Nyumbani kwakojohari, kwingine usitamani.

Usichaguejirani, bali chagua rafiki,

Usitenge asilani, shauri pia afiki,

Palipo na burudani, kaa nao marafiki,

Nyumbani kwakojohari, kwingine usitamani

MASWALI

41. Kichwa cha shairi kinachofaa ni kipi?

  1.  Johari ni nyumba 
  2.  Nyumbani si pangoni
  3.  Tuthamini kwetu
  4.  Tupende majirani
  5.  Tupende marafiki


42. Kituo katika shairi hili ni kipi?

  1.  Nyumbani kwako johari, kwingine usitamani 
  2.  Usichague jirani, bali chagua rafiki
  3.  Kwingine usitamani, nyumbani kwako johari
  4.  Nyumbani kwako kuzuri, japokuwa ni pangoni
  5.  Uipende nyumba yako, utaona raha yake


43. Neno "johari" kama lilivyotumiwa na mtunzi lina maana gani?

  1.  Kitu licho dhahiri
  2.  Kitu chenye dhamana
  3.  Kitu cha thamani
  4.  Kitu cha matamanio
  5. Kitu cha kujivunia


44. Neno "pekepeke" kama lilivyotumiwa na mshairi lina maama gani?

  1.  Ukatili
  2.  Ufitini
  3.  Uonevu
  4.  Uchoyo
  5. Uwongo


44. Neno "pekepeke" kama lilivyotumiwa na mshairi lina maama gani?

  1.  Ukatili
  2.  Ufitini
  3.  Uonevu
  4.  Uchoyo
  5. Uwongo

45. Vina vya kati na vya mwisho katika ubeti wa tatu ni vipi?

  1.  Ko na Ke 
  2.  U na Ke
  3.  Du na Ke
  4.  Ri na Ni
  5. Ki na Ke


46. Funzo linalopatikana katika shairi hilo linawakilishwa na methali ipi kati ya zifuatazo?

  1.  Raha haiji ila baada ya tabu. 
  2. Mkataa pema pabaya panamwita. 
  3. Ukikosa shukuru kupata kuna Mungu. 
  4. Fimbo ya mbali haiui nyoka.
  5.  Usiache mbachao kwa msala upitao.


SEHEMU E

UTUNCAJI

Katika Sehemu hii kuna habariyenye sentensi nne (4) zilizoandikwa bila mtiririko sahihi unatakiwa kuzipanga sentensi hizo ili ziwe na mtiririko wenye mantiki kwa kuzipa herufi A, B, C, na D

47. Vile vile matunda huongeza damu mwilini



48. Hivyo matunda yana umuhimu mkubwa katika miili yetu.



49. Lakini watu wasiokula matunda hupata maradhi kama vile ugonjwa wa fizi, macho na ngozi.



50. Kula matunda kunasaidia kuponyesha magonjwa na vidonda haraka, pia husaidia macho kuona vizuri katika mwanga hafifu.



SEHEMU B

Jibu swali la 6 - 10 kwa kuchagua herufi ya jibu sahihi na kuiandika katika kisanduku pembeni ya kilo swali.

6. Mtu anayeongoza meli huitwa

  1. rubani
  2. dereva
  3. nahodha
  4. utingo


7. Nimepatwa na. . . . . . . . . . . kutokana na msiba wa mjomba.

  1. majonzi
  2. furaha
  3. njaa
  4. homa


8. Usipoziba . . . . . . . . . . . utajenga ukuta

  1. mwanya
  2. ufa
  3. nafasi
  4. upenyo


9. Mkoa wa Iringa ni mojawapo ya mikoa iliyoko nyanda za juu ......

  1. Kaskazini
  2. Mashariki
  3. Magha ri hi
  4. Kusini


10. Ili kupika ugali unahitaji maji na

  1. maziwa
  2. sukari
  3. unga
  4. chumvi


STD VII KISWAHILI NECTA EXAM OF YEAR 2012 Try This  |  

 KISWAHILI-2012

SEHEMU A

SARUFI

Chagua herufiyajibu lililo sahihi kisha andika katika karatasiyakoya kujibia.

1. Katika maneno yafuatayo ni lipi ambalo ni nomino dhahania?

  1. Unakuja
  2. Umeenea
  3. Utalima
  4. Uelewa
  5. Ulisoma


2. Wingi wa neno "paka" ni upi?

  1. Mipaka
  2. Paka
  3. Mapaka
  4. Vipaka
  5. Wapaka


3."Akiondoka Sulubu kazi zote zitalala." Neno "sulubu" ni la aina ipi?

  1.  Kielezi 
  2.  Kivumishi 
  3.  Kiwakilishi 
  4.  Nomino 
  5.  Kiunganishi


4."Ili tuendelee.... ..... kufanya kazi kvva bidii." Neno lipi limekosekana kukamilisha sentensi hiyo?

  1.  ni budi 
  2.  hatuna budi 
  3.  tuna budi 
  4.  kuna budi 
  5.  Hapana budi


5."Mvua ilinyesha jana usiku kucha. " Katika sentensi hiyo kikundi kielezi ni kipi?

  1.  Mvua ilinyesha jana 
  2. Usiku kucha 
  3.  Ilinyesha jana 
  4. Mvua ilinyesha 
  5. Jana usiku kucha


6."Baba alilimiwa shamba." Sentensi hii ipo katika kauli gani?

  1.  Kutenda 
  2. Kutendewa 
  3.  Kutendwa
  4. Kutendeka E. Kutendea


7."Adili alikuwa anaimba tangu ujana wake." Neno "alikuwa" ni aina gani ya kitenzi? 

  1.  Kisaidizi 
  2.  Jina 
  3.  Kishirikishi
  4. Kitegemezi 
  5. Kikuu


8."Mchungaji alivaa suti maridadi sana."Katika sentensi hii neno lipi limetumika kama kivumishi?

  1.  Suti 
  2. Alivaa 
  3.  Maridadi 
  4. Mchungaji 
  5. Sana


9.Kitenzi " anapigwa" kipo katika kauli gani?

  1.  Kutenda 
  2. Kutendewa 
  3. Kutendwa 
  4. Kutendeka 
  5. Kutendesha


10.Kisawe cha neno "bahati" ni kipi kati ya maneno yafuatayo?

  1.  Tunu 
  2. Sudi 
  3.  Shani
  4. Hiba 
  5. Hidaya


11."Maandishi yanasomeka vizuri." Sentensi hii ipo katika wakati gani?

  1.  Ujao 
  2. Uliopita 
  3. Mazoea 
  4. Uliopo 
  5. Timilifu


12. "Makubi ni mtoto wa mjukuu wangu." Makubi ni nani kwangu?

  1.  Kilembwekeza 
  2. Kijukuu 
  3. Kilembwe 
  4. Kitukuu 
  5. Mtukuu


13."Sipendi uongo." Sentensi hii ipo katika nafsi ipi?

  1.  Nafsi ya kwanza wingi 
  2. Nafsi ya tatu umoja 
  3. Nafsi ya kwanza umoja 
  4. Nafsi ya tatu wingi
  5. Nafsi ya pili umoja.


14.Neno "poni" lina maana sawa na neno lipi kati ya maneno?

  1.  Posho 
  2. Rahani 
  3. Mali 
  4. Mkopo 
  5. Pesa


15. "Shuleni kwetu kuna upungufuwa . Ni neno lipi hukamilisha tungo hiyo kwa usahihi?

  1.  thamani 
  2. thamini 
  3. dhamini
  4. zamani 
  5. samani


16. "Mtoto ametengeneza toroli Ia mti." Wingi wa sentensi hii ni upi?

  1.  Watoto wametengeneza toroli za miti
  2.  Watoto wametengeneza matoroli ya mti
  3.  Watoto ametengeneza matoroli ya miti
  4.  Watoto wametengeneza toroli za mti
  5.  Watoto wametengeneza matoroli ya miti


17. "Muda mfupi atakuwa anaingia uwanjani." Sentensi hii ipo katika wakati gani?

  1. Uliopo
  2. Uliopita
  3. Wa mazoea
  4. Ujao
  5. Timilifu


18.

Ni neno lipi kati ya haya yafuatayo halilandani na mengine?

  1. Fikiria
  2. Dodosa
  3. Uliza
  4. Hoji
  5. Saili


19. Juma aliondoka hivi punde. Maneno "hivi punde" yana maana ipi?

  1. Haraka
  2. Muda mrefu
  3. Karibuni
  4. Kwa pupa
  5. Kwa haraka


20. Neno lipi ni kisawe cha neno adili?

  1. Ujinga
  2. Wema
  3. Uovu
  4. Ujasiri
  5. Ukatili


SEHEMU B

LUCHA YA KIFASIHI

Katika swali la 21 — 30 andika katika herufiyajibu lililo sahihi katika karatasiyakoya kujibia.

21. "Mwanzo wa ngoma ni lele.” Methali inayofanana na hii kati ya hizi zifutazo ni ipi?

  1.  Dawa ya moto ni moto 
  2. Dalili ya mvua ni mawingu
  3.  Dira ya binadamu ni kichwa 
  4.  Dawa ya jibu ni kulipasua 
  5.  Mtoto wa nyoka ni nyoka


22. "Akutendaye mtende usimche akutendaye.” Methali hii inatoa funzo gani?

  1.  Mwovu akomeshwe kwa adhabu kali
  2.  Akufanyiae maovu usimche 
  3. Mwovu akwepwe kwa kutenda.
  4. Anayekutendea usilipize kisasi 
  5. Mwovu akwepwe kwa kutendwa


23. "Uzuri wa mkakasi ndani .........” Ni kifungu kipi kati ya vifuatavyo kinakamilisha methali hiyo?

  1. kuna mti laini 
  2. kipande cha mdalasini
  3. kipande cha mti 
  4. ni mti mkavu 
  5. kipande laini.


24. Msemo upi kati ya ifuatayo unakamilisha sentensi, "Kinjekitile alijaribu lakini baadaye hakuitekeleza.”

  1. Kuweka hadhari 
  2. kuweka nadhiri
  3. kuweka hadhira 
  4. kuweka nadharia
  5. kuweka nadhari


25. Tegua kitendawili kisemacho, " Atembeapo kila mara huringa hata kama kuna adui.”

  1.  Bata 
  2. Konokono 
  3.  Kobe
  4.  Kanga 
  5.  Kinyonga


26. "Siku hizi siri za mafisadi zimeanikwa juani.” Usemi "kuanikwa juani” una maana ipi kati ya hizi zifuatazo?

  1. Kuelezwa waziwazi
  2. Kusemwa hadharani
  3. Kusemwa nje ya kikao
  4. Kuelezwa hadharani
  5. Kusemwa jukwaani


27. Methali ipi kati ya zifuatazo ina maana sawa na hii isemayo "Meno ya mbwa hayaumani.”

  1.  Mwana kidonda, mjukuu kovu 
  2. Akipenda chongo, huita kengeza 
  3. Damu nzito kuliko maji 
  4. Heri mrama, kuliko kuzama 
  5. Maneno matupu hayavunji mfupa.


28. "Tatizo la ufisadi limeota mizizi katika nchi yetu.” Usemi "kuota mizizi” una maana gani?

  1.  Kuibuka 
  2.  Kuchipuka 
  3.  Kushamiri
  4.  Kuongezeka 
  5.  Kuenea


29. Tegua kitendawili kifuatacho "Kondoo wangu kachafua njia nzima.”

  1. Konokono
  2. Jingoo
  3. Tandu
  4. Mjusi
  5. Kinyonga


30. "Ntandu alikuwa na kichwa cha panzi." Msemo "kichwa cha panzi" una maana gani?

  1. Msikivu sana 
  2. Msahaulifu sana
  3. Ana utambuzi 
  4. Ana kumbukumbu
  5. Mtiifu sana


SEHEMU C

UFAHAMU

Soma kwa makini habari ifuatayo kishajibu maswali 31 - 40 kwa kuchagua herufiyajibu sahihi na kuandika katika karatasi yakoya kujibia.

Uuzaji wa mazao ni tendo la kubadilisha mazao kwa fedha. Mkulima anampa mtu mwingine mazao yake ili yeye apewe fedha. Uuzaji huu unaweza kufanywa na mkulima mwenyewe au dalali. Kituo kibubwa cha kuuzia mazao haya ni soko au gulio. Serikali huwa inawashauri wakulima kuanzisha vyama vya ushirika. Vyama hivi vitakuwa na kazi ya kununua mazao ya wakulima na kuyauza ndani na nje ya nchi. Tatizo kubwa la vyama vya ushirika ni ile tabia ya kukopa mazao kwa wakulima halafu kuyauza ndipo ipatikane fedha ya kuwalipa wakulima. Mfumo huu unatakiwa uwe unaratibiwa vizuri na wakulima, kwani mali bila daftari hupotea bila habari.

Siku hizi kuna soko huria. Watu binafsi hujitokeza kununua mazao kwa bei nzuri na hulipa fedha kwa wakati huo huo. Kwa njia hii huwasaidia wakulima kupata soko ka mazao yao. Hata hivyo, wakulima wanapaswa kuwa makini kwa kuwa wanunuzi wengine ni matapeli. Mashambega hawa hufanya hila kwa kutumia mizani zisizo sahihi na hivyo wakulima huambulia fedha kichele tu. Hali hii huwaletea simanzi wakulima, lakini pamoja na masononeko hayo kwa kuwa walanguzi hutoa pesa papo kwa papo, wakulima wengi huona bora kuwauzia walanguzi kuliko kuikopesha serikali. Wahenga walisema heri kenda kisha kuliko kumi nenda uje.

MASWALI

31. Kichwa cha habari kinachofaa kwa habari uliyosoma ni kipi?

  1.  Soko la mazao
  2.  Mazao na walanguzi
  3.  Biashara isiyolipa 
  4. Biashara ya mazao
  5.  Kubadilisha mazao


32. Neno "simanzi" kama lilivyotumika katika habari hii lina maana tofauti na lipi?

  1.  Masononeko 
  2. Mawazo 
  3. Majonzi 
  4. Masikitiko 
  5. Huzuni


33. Vyama vya ushirika vinahitaji kuwa na nini?

  1. Pesa taslimu
  2. Utaratibu mzuri
  3. Utunzi kumbukumbu
  4. Kuondoa matapeli
  5. Udhibiti mzuri


34.

"Fedha kichele." Nahau hii ina maana ipi?

  1. Fedha kidogo
  2. Fedha kiasi
  3. Fedha ndogondgogo
  4. Fedha taslimu
  5. Fedha wazi wazi


35.Kisawe cha neno tapeli ni kipi?

  1.  Mlanguzi 
  2.  Mhujumu 
  3.  Fisadi 
  4.  Mlaghai 
  5.  Mnyonyaji


36.Methali "Heri kenda shika kuliko kumi nenda uje" inatoa funzo gani?

  1.  Tuone umuhimu wa kuwa nacho
  2.  Kidogo tulichonacho kitatufaa zaidi
  3.  Kuthamini kidogo tunachopata 
  4. Turidhike na chetu si cha jirani 
  5. Kuthamini mali tuliyonayo.


37.Katika habari uliyoisoma jamii inaaswa kuhusu nini?

  1.  Umuhimu wa kuorodhesha mali
  2.  Umuhimu wa kumbukukmbu katika biashara
  3.  Umuhimu wa kutunza biashara ndani ya daftari
  4. Umuhimu wa biashara kuorodheshwa wazi
  5. Umuhimu kwa mfanyabiashara kuwa na daftari.


38.Neno lipi kati ya yafuatayo ni kinyume cha neno "hili?"

  1. Udanganyifu 
  2. Ughilibu 
  3. Uungwana 
  4. Ujanja 
  5. Unadhifu


39.Neno "dalali" kama lilivyotumika katika habari hii lina maana gani?

  1.  Wakili 
  2. Mnadi
  3. Mkopeshaji 
  4. Muuzaji 
  5. Mnunuzi


40.Funzo muhimu zaidi ulilolipata katika habari uliyosoma linawakilishwa na methali ipi?

  1.  Mali bila daftari hupotea bila habari
  2.  Biashara haigombi
  3.  Baniani mbaya kiatu chake dawa
  4. Banda likikushinda jenga kibanda. 
  5. Haba na haba, hujaza kibaba.


SEHEMU D

USHAIRI

Soma kwa makini shairi lifuatalo kishajibu maswali 41 - 46 kwa herufiyajibu lililo sahihi katika karatasiya kujibia.

Wanafunzi sikiliza, nawapa huu wasia,

Nataka kuwaeleza, mambo muhimu sikia, Kwanza ninawapongeza, hapa mlipofikia,

Hongereni hongereni, hongereni kuhitimu.

Hapa mlipofikia, kamwe msije bweteka,

Malenga kuyafikia, huu ni mwanzo hakika, Usije kuvizikia, vitabuvyo kwenye taka,

Hongereni hongereni, hongereni kuhitimu.

Shuleni mmejifunza, masomo kwa uhakika,

Kiswahili ni cha kwanza, lugha hamkuichoka,

Kwa ari mkijifunza, mbele kitawapeleka, Hongereni hongereni, hongereni kuhitimu.

Safari miaka saba,yenye raha na karaha,

Mlichopata si haba, mwende nacho kwa furaha,

Hicho kidogo kibaba, kisilete majeraha,

Hongereni hongereni, hongereni kuhitimu.

MASWALI

41. Mshairi anaposema "mlichokipata si haba" ana maana gani?

  1. Mlichokipata si kilele
  2. Mlichokipata si kidogo
  3. Mlichokipata si duni
  4. Mlichokipata si dhaifu
  5. Mlichokipata si kibaya


42. Vina katika ubeti wa pili ni vipi?

  1.  ha na ka 
  2.  a na ka 
  3. ho na ho 
  4. ni na mu 
  5. u na vi


43. Wazo kuu katika shairi hili ni lipi?

  1. Kuhitimu ni jambo muhimu
  2. Elimu ya msingi ni bora zaidi
  3. Kujiendeleza kielimu ni muhimu
  4. Kiswahili ni somo la muhimu
  5. Kuhitimu ni lazima


44. Kichwa kinachofaa kwa shairi hili ni kipi?

  1.  Ushauri kwa wahitimu 
  2. Kuhitimu ni fahari 
  3. Elimu ya msingi 
  4. Wanafunzi wahitimu
  5. Fahari ya kuhitimu.


45. Kinyume cha neno "karaha" ni kipi?

  1.  Kero 
  2.  Adabu 
  3. Furaha 
  4.  Adhabu 
  5. Amani



46. Neno "bweteka" kama lilivyotumika kwenye shairi hilo lina maana ipi?

  1. Kuridhika 
  2. Kudhihaki 
  3. Kudhoofika
  4. Kudhalilika 
  5. Kudhihirika


SEHEMU E

UTUNGAJI

Umepewa habari yenye sentensi nne (4) zilizoandikwa bila mtiririko sahihi wa mawazo katika swali la 47 - 50. Zipange sentensi hizo ili ziwe na mtiririko wenye mantiki kwa kuzipa herufi A, B, C na D. Weka kivuli katika herufiyajibu sahihi katika karatasiyakoya kujibia.

47.Dakika chache baadaye, tuliona msafara wa magari ukiingia.



48.Gari hilo lilifuatwa na gari lingine lililojaa askari wa kuzuia fujo, kisha lilifuata gari la Rais.



49.Mnamo saa saba hivi tuliona pikipiki ya askari wa usalama barabarani ikija mbio kama mshale.



50.Mbele ya msafara huo kulikuwa na pikipiki nne zilizofuatiwa na gari la polisi lenye kingora.



KISWAHILI 2013

SEHEMU A

SARUFI

1. Sweta langu limeshonwa na fundi mzoefu? "Mzoefu" ni aina gani ya neno?

  1.  Kielezi 
  2.  Kivumishi 
  3.  Kiunganishi 
  4.  Nomino 
  5.  Kitenzi


2. "Ningejua ukweli wa mambo kabla ......... hapa bure saa hizi." Neno gani Iinakamilisha sentensi hiyo?

  1.  nisingalikuja 
  2.  ningekuja 
  3. singelikuja 
  4. nisingelikuja 
  5. nisingekuja


3. "UKIMWI unaua." Mbunge alisema. Ipi ni kauli taarifa ya sentensi hiyo kati ya hizi zifuatazo?

  1.  Mbunge aliwaambia UKIMWI unaua
  2.  Mbunge alisema UKIMWI unaua
  3.  UKIMWI unaua mbunge alisema
  4.  Mbunge alisema kwamba UKIMWI unaua 
  5.  Mbunge alieleza UKIMWI unaua.


4. "Anna anatembea polepole twiga." Kifungu kipi cha maneno kinakamilisha sentensi hiyo?

  1.  mithili ya 
  2.  mathalani ya
  3.  mahadhi ya 
  4.  maridhawa ya 
  5.  madhali ya


5. Neno lipi halilandani na maneno yafuatayo?

  1.  Msonge 
  2.  Tembe
  3. . Daraja 
  4.  Kibanda 
  5.  Ghorofa


6. Sentensi ipi kati ya hizi zifuatazo ni kauli ya kutendea?

  1.  Watoto wanacheza mpira. 
  2.  Mpira unachezwa na watoto. 
  3.  Watoto wanachezeana mpira.
  4.  Watoto wanachezea mpira.
  5.  Mpira unachezewa na watoto.


7. "Tumejifunza . kujikinga na VVU na UKIMWI." Kifungu kipi cha maneno kati ya vifuatavyo kinakamilisha sentensi hiyo?

  1.  ibara ya 
  2.  jinsi ya
  3.  jinsia ya 
  4.  ilhali ya 
  5.  aina ya


8. Sehemu ambayo ngombe huogeshwa ili kuwaepusha na magonjwa huitwaje?

  1.  Mto 
  2.  Bwawa
  3.  Ziwani 
  4.  Josho 
  5.  Joshi


9. ”Mboga haina chumvi ya kutosha.” Wingi wa sentensi hiyo ni upi?

  1.  Mboga hazina chumvi ya kutosha
  2.  Mboga haina machumvi ya kutosha
  3.  Mamboga hayana chumvi ya kutosha
  4.  Mamboga hayana chumvi za kutosha 
  5.  Mboga haina chumvi za kutosha


10. Nywele zinazoota kuanzia karibu na masikio mpaka kwenye mashavu huitwaje?

  1.  Mvi 
  2. Sharafa 
  3. Ndevu 
  4. Sharubu 
  5. Kope


SEHEMU B

LUCHA YA KIFASIHI

21. Tegua kitendawili kisemacho: "Mwenye kuitwa amefika lakini mjumbe bado hajarudi.”

  1.  Nazi na mkwezi 
  2.  Yai na kifaranga 
  3.  Birika na Chai 
  4.  Nyama na ngozi
  5.  Chupa na mfuniko


22. Wakoloni walitunyanyasa lakini hatimaye unyanyasaji huo ulifika ukingoni kwani .........” Ni methali ipi kati ya zifuatazo inakamilisha sentensi hiyo?

  1.  hakuna marefu yasiyokuwa na ncha
  2.  mchumia juani hulia kivulini
  3.  ukiona vyaelea vimeundwa
  4.  umoja ni nguvu utengano ni udhaifu E. bandu bandu humaliza gogo


23. ”Kidagaa kimemwozea.” Msemo huu una maana gani?

  1.  Kukwepa kulipa deni 
  2.  Kutowajibika kulipa
  3.  Kuelemewa na jambo 
  4.  Kupoteza tumaini 
  5.  Kulipa deni maradufu


24. "Kukubali kwa ulimi” ni msemo wenye maana ipi?

  1.  Kukubali kwa dhati
  2.  Kukubali kwa maneno
  3.  Kukubali bila kusema neon 
  4.  Kukubali kimoyomoyo
  5.  Kukubali kwa moyo mmoja


25. Nahau isemayo, "amevimba kichwa” ina maana ipi?

  1.  Kupata mafanikio makubwa
  2.  Kukabidhiwa madaraka ya juu
  3.  Kuwa na hali ya hasira
  4.  Kuwa na hali ya huzuni
  5.  Kuwa na tabia ya majivuno


26. "Kitanda usichokilalia hujui kunguni wake." Methali ipi kati ya zifuatazo ina maana save na hiyo?

  1.  Pema usipopema ukipema si pema tena
  2.  Kizuri hakikosi ila
  3.  Mtu siri kusema na moyo wake
  4.  Nyumba usiyoilalia ndani hujui ila yake
  5. Pilipili usiyoila yakuwashia nini


27. "Nina mwanangu mweupe nikimtia maji hufa." Kitendawili hicho kina maana ipi?

  1.  Maziwa 
  2.  Tui la nazi 
  3.  Majivu 
  4.  Barafu 
  5. E. Karatasi


28 Bwana mkubwa amelala ndani lakini ndevu zipo nje zapepea." Jibu sahihi la kitendawili hiki ni lipi?

  1. . Ulezi 
  2. . Mpunga 
  3. . Ngano 
  4. . Mahindi 
  5. . Mtama


29. "Kazi mbaya si mchezo mwema." Methali inayofanana na methali hiyo ni ipi?

  1.  Hewala haigombi.
  2.  Mchezea tope humrukia.
  3.  Heri kuwa mbichi kuliko kuungua. 
  4. Hucheka kovu asiyekuwa na jeraha.
  5. Hukunyima tonge, hakunyimi neno.


30. Msemo usemao, "kushikwa sikio" una maana ipi?

  1.  Kusemwa 
  2. Kunongonezwa 
  3.  Kuelezwa
  4. Kusengenywa 
  5. Kuonywa


STD VII KISWAHILI NECTA EXAM OF YEAR 2011 Try This  |  

KISWAHILI 2011

SEHEMU A

SARUFI

Katika swali la (1 - 20) andika herufi ya jibu sahihi katika karatasi yako ya kujibia.

1. Neno "jenga" likinyumbulishwa katika kauli ya kutendeka litakuwa neno lipi?

  1. Jengwa
  2. Jengea
  3. Jengeka
  4. Jengesha
  5. Jengewa


2. Neno "wamewalisha" linadokeza hali gani ya kitenzi?

  1. Kuendelea
  2. Mazoea
  3. Masharti
  4. Matarajio
  5. Timilisho


3. "Yeye hupenda sana kusoma Kiswahili". Katika sentensi hii ni neno lipi limetumika kama kiwakilishi?

  1. Hupenda
  2. Kiswahili
  3. Sana
  4. Yeye
  5. Kusoma


4. Katika sentensi zifuatazo ni ipi ipo katika hali ya mazoea

  1. Roda alisoma gazeti la Mtanzania.
  2. Roda atasoma gazeti la Mtanzania.
  3. Roda husoma gazeti la Mtanzania.
  4. Roda amesoma gazeti la Mtanzania.
  5. Roda anasoma gazeti la Mtanzania.


3. Sara alimwambia Heri kwamba hakusafiri bali alikuwepo pale pale. Kauli halisi itakuwa ipi?

  1. Sara alimwambia Heri, "Sikusafiri nipo hapa hapa".
  2. Sara alimwambia Heri, "Sitasafiri nipo hapa hapa".
  3. Sara alimwambia Heri, "Sisafirinipo hapa hapa".
  4. Sara alimwambia Heri, "Hajasafiri yupo hapa hapa".
  5. Sara alimwambia Heri, "hakusafiri yupo hapa hapa".


6. "Alikuwa anajibu kihuni". Neno "kihuni" limetumika kama aina gani ya neno?

  1. Kielezi
  2. Kiwakilishi
  3. Kivumishi
  4. Kitenzi
  5. Kihisishi


7. "Mtu anayetaka msaada wa aina nitampa". Neno linalofaa kukamilisha tungo hiyo ni lipi?

  1. wowote
  2. yoyote
  3. yeyote
  4. vyovyote
  5. lolote


8. "Wanafunzi wanaendelea kusoma Kiswahili ingawa hawana mwalimu". Neno "wanaendelea" limetumika kama aina gani ya kitenzi?

  1. Kikuu
  2. Kishirikishi
  3. Jina
  4. Kisaidizi
  5. Kitegemezi


9. Mahali pale panatisha. Neno "pale" ni aina gani ya neno

  1. Kivumishi
  2. Kiwakilishi
  3. Kiunganishi
  4. kihisishi
  5. Kielezi


10. "Kinyonga anatembea". Ukanushi wa sentensi hii ni upi?

  1. Kinyonga hakitembei
  2. Kinyonga hakutembea
  3. Kinyonga hajatembea
  4. Kinyonga haternbei
  5. Kinyonga hatatembea


11. "Mama anapika lakini baba abapangamawe". Neno lakini limetumika kama aina gani ya neno?

  1. Kivumishi
  2. Kiwakilishi
  3. Kielezi
  4. Kitenzi
  5. Kiunganishi


12. "Kiburi si maungwana". Neno "si" limetumika kama aina gani ya kitenzi

  1. Kikuu
  2. Kishirikishi
  3. Jina
  4. Kisaidizi
  5. Kitegemezi


13. "Baba yangu ni mwenyekiti wa lopp". Neno "mwenyekiti ni nomino ya aina gani?

  1. Dhahania
  2. Kawaida
  3. Pekee
  4. Jumla
  5. Mguso


14. Wingi wa neno chuma ni upi kati ya maneno yafuatayo?

  1. Machuma
  2. Mavyuma
  3. Vichuma
  4. Vyuma
  5. Michuma


15. "Wanafunzi walitumiana salamu". Sentensi hii ipo katika kauli gani?

  1. Kutendeana
  2. Kutendana
  3. Kutendewa
  4. Kutendea
  5. Kutendeka


16. Kinyume cha neno "elea" ni kipi?

  1. [buka
  2. Ibukia
  3. Zamia
  4. Zama
  5. Zamisha


17. "Huyu mwanangu mpendwa". Neno lipi ni sahihi iii kukamilisha sentensi hiyo.

  1. ndiye
  2. ndio
  3. ndiyo
  4. ndie
  5. ndiwe


18. "Mbwa ameonekana". Neno lipi ni sahihi kukamilisha tungo hiyo?

  1. aliyepotea
  2. aliopotea
  3. alipotea
  4. amepotea
  5. alivyopotea


19. Hall ya kuwa na fedha au mall nyingi huitwaje?

  1. Ukachero
  2. Ukapa
  3. Ukata
  4. Ubahili
  5. Ukwasi


20. Ni sentensi ipi inawakilisha kauli ya kutendwa?

  1. Nyumba imeharibiwa na mvua.
  2. Nyumba imeharibishwa na mvua.
  3. Nyumba imeharibika na mvua.
  4. Nyumba imeharibika kwa mvua.
  5. Nyumba imeharibiwa kwa mvua.


SEHEMU B

LUGHA VA KIFASIH1

21. "Uzi mwembamba unafunga dume kubwa". Kitendawili hiki kina maana gani?

  1. Mawingu
  2. Usingizi
  3. Ndoto
  4. Mvua
  5. Ugonjwa


22. "Usisahau ubaharia kwa sababu ya unahodha". Methali ambayo ina uhusiano na hii ni ipi kati ya hizi zifuatazo?

  1. Ufalme kama mvua, hupiga na kupita.
  2. Ujana ni tembo la nazi, halikawii kupita.
  3. Usiache mbachao, kwa mswala upitao.
  4. Usishindane na kari, kari ni mja wa Mungu.
  5. Ukiwa na lako, usitizame la mwenzio.


23. "Watoto wangu wote wamevaa hirizi nyeupe" Kitendawili hiki kina maana gani

  1. Mwewe
  2. Kunguru
  3. Njiwa
  4. Kasuku
  5. Chiriku


24. Hali ya kumfanya mtu atii kila analoambiwa ina maana sawa na nahau ipi kati ya zifuatazo?

  1. Kutia akili
  2. Mkalia kitako
  3. Kumweka kiganjani
  4. Kumkalia kichwani
  5. Kumkalia kooni


25. Ni muhimu kwa kila mtu kuwa mwangalifu kwa wanaojitangazia kutibu kisukari. Ni usemi upi kati ya ifuatayo ina maana sawa na "kuwa mwangalifu"?

  1. Kuwa macho
  2. Kuwa hima
  3. Kuwa mweledi
  4. Kuwa hadhiri
  5. Kuwa shupavu


26. "Mambo mema na mabaya hayafungamani", kifungu hiki cha maneno kinatoa maana ya methali ipi kati ya zifuatazo?

  1. Gongo la mbuyu si la mvule.
  2. Liwapo lako ni jema, la mwenzako ni baya.
  3. Lila na fila havitengamani.
  4. Lako ni lako, likikufika lina mwenzako.
  5. Padogo pako si pakubwa pa mwenzako.


27. Tegua kitendawili kisemacho "Gari langu halitumii mafuta ya waarabu"

  1. Nywele
  2. Ngozi
  3. Miguu
  4. Mikono
  5. Macho


28. "Umejuaje kuwa mimi ni mgeni hapa?" methali ipi kati ya zifuatazo inawajibu swali hilo?

  1. Jogoo wa shamba hawiki mjini.
  2. Waarabu wa Pemba hujuana kwa vilemba.
  3. Mtoto wa nyoka ni nyoka.
  4. Kuku mgeni hakosi kamba mguuni.
  5. Aibu ya maiti aijuaye mwosha.


29. Juma alipumzika chini ya mti, alipoulizwa anafanya nini pale alijibu kuwa, "Navinjari to mwalimu". Jibu sahihi alilotakiwa kutoa ni lipi?

  1. Napiga domo.
  2. Napunga upepo.
  3. Nimepigwa na butwaa.
  4. Napiga kambi.
  5. Nazunguka mbuyu.


30. "Babu kafa kaniachia pete". Kitendawili hiki kina maana gani?

  1. Mjusi
  2. Tandu
  3. Nyoka
  4. Konokono
  5. Jongoo


SEHEMU C

UFAHAMU

Soma kwa makini habari ifuatayo kisha jibu maswali 31 - 40 kwa kuchagua herufi ya jibu lililo sahihi na kuandika katika karatasiyakoya kujibia.

Umewahi kusikia viumbe wanaoitwa dinozo? Hawa ni wanyama ambao walikuwepo duniani zaidi ya miaka milioni 65 iliyopita. Wanasayansi wamegundua mabaki ya mafuvu na mifupa yao ardhini. Wanasayansi wamechunguza sana sababu za kutokomea kwa dinozo. Mpaka leo hii haijapatikana sababu rasmi ya tukio hilo. Hata hivyo, bado uchunguzi unaendelea kufanywa katika kutafuta sababu za kupotea kwa wanyama hao.

Tanzania ni miongoni mwa nchi chache duniani zenye wanyama wa aina nyingi. Watalii wengi kutoka kila pembe ya dunia huja kuwaangalia wanyama hawa. Hali hiyo huongeza pato Ia taifa.

Aidha, vitendo mbalimbali vinahatarisha usalama wa viumbe hao; kwa mfano makazi ya wanyama yanaharibiwa kwa kuchomwa misitu na kukata miti ovyo. Hali hii husababisha misitu kubaki vichaka tu, hivyo wanyama hukosa makazi na mwishowe hupotea. Vile vile binadamu huwinda wanyama kama tembo kwa ajili ya pembe zao.

Sasa umefika wakati kwa kila mmoja wetu kukemea vitendo hivi. Wanyama na mimea ni urithi wa taifa letu. Ni fahari iliyoje kwetu kuwa navyo. Tusipokuwa waangalifu wanyama hao na mimea adimu kama mianzi vitatoweka kabisa. Vizazi vijavyo vitabaki kusimuliwa kama tunavyosikia kuhusu dinozo.

MASWALI

31. Dinozo ni wanyama wenye sifa ipi kati ya hizi zifuatazo?

  1. Waliotoweka duniani
  2. Wanaovutia watalii
  3. Walioishi duniani miaka mingi
  4. Wanaoishi duniani
  5. Wenye mifupa na Mafuvu


32. Kwa kuzingatia habari uliyosoma mambo mawili yanayoathiri ustawi wa wanyama ni yepi?

  1. Uoto wa maji
  2. Mvua na utalii
  3. Uwindaji na ujangili
  4. Vichaka na uwindaji


33. Sababu kubwa ya watu kuwinda na kuwaua ndovu ni ipi?

  1. Kupata kitoweo
  2. Kupata pembe
  3. Kupata ngozi
  4. Kupata mkonga
  5. Kupata malighafi


34. Kutokana na habari hii ni sababu ipi inayowafanya watalii kuja Tanzania?

  1. Kuwinda wanyama
  2. Kuongeza pato Ia taifa
  3. Kupata malighafi
  4. Kupata pembe
  5. Kuwaangalia wanyama


35. Tanzania hupata faida gani kubwa kutokana na sekta ya utalii?

  1. Kupata fedha za kigeni
  2. Kupata wageni mbalimbali
  3. Kuuza bidhaa nyingi
  4. Kuongeza pato la taifa
  5. Kujulikana nchi za nje


36. Mwandishi anatoa wito gani kwa jamii kuhusiana na usalama wa viumbe hai?

  1. Kukemea vitendo vinavyohatarisha usalama wa viumbe hai
  2. Kulinda mianzi iliyopo iii isitoweke kabisa
  3. Kuhudumia na kuvitunza viumbe hai kwa umakini zaidi
  4. Kuthamini na kutambua kuwa viumbe hai ni urithi wa taifa
  5. Kulinda na kutunza tembo wallop iii wasitoweke


37. Athari zipi zinapatikana kutokana na kuchoma misitu?

  1. Kuwepo kwa jua kali na uoto wa asili
  2. Kuwepo kwa vichaka na ukame wa kutisha
  3. Makazi na malisho ya wanyama kuharibika
  4. Mimea na mianzi kutoweka kwa haraka
  5. Tembo na mimea kutoweka kwa kasi


38. Mwandishi anadai kuwa fahari ya taifa letu bi kuwa na vitu gani?

  1. Mimea na mianzi
  2. Maji na misitu
  3. Wanyama na mimea
  4. Mimea na maji
  5. Wanyama na utalii


39. Kuna tofauti gani kati ya msitu na kichaka?

  1. Msitu ni nyasi na kichaka ni miti.
  2. Msitu ni miti na kichaka ni nyasi.
  3. Misitu ni miti mirefu na kichaka ni miti midogo.
  4. Misitu ni miti mikubwa na kichaka ni miti mifupi.
  5. Misitu ni nyasi ndefu na kichaka ni nyasi fupi.


40. Kwa ujumla habari hii inahusu nini?

  1. Viumbe hai
  2. Manzingira
  3. Dinozo
  4. Usalama wa viumbe
  5. Tembo


SEHEMU D

USHAIRI

Soma shairi lifuatalo kisha jibu maswali 41 - 46 kwa kuandika herufi ya jibu lililo sahihi katika karatasi ya kujibia.

Kasimama kizimbani, popo anatetemeka,

Kuitwa mahakamani, popo kujibu shitaka,

Atakiwa abaini, kwa ulimi kutamka,

Ajitetee bayana, ni mnyama au ndege.


Hakimu nashukuru, shitaka kunisomea,

Sina jadi na kunguru, ila na Pundamilia,

Mimi ni mnyama huru, amini ninakwambia,

Tukidaiwa ushuru, kwa wanyama nalipia.


Ni kweli popo napaa, na mabawa nimepata,

Lakini mimi nazaa, hilo halina utata

Kuwa ndege nakataa, sina undugu na bata

Nakataa katakata, mimi si ndege nasema.


Hakimu nathibitisha, kwa moyo wangu thabiti,

Nazaa na kunyonyesha, vipi niwe msaliti,

Wale wanaopotosha, niwaonyeshe matiti,

Hakimu simama kati, nipatie kaki.

MASWALI

41. Popo anakataa kuwa si ndege kwa sababu gani?

  1. Anataga
  2. Ana mabawa
  3. Anazaa
  4. Anapaa
  5. Ana manyoya


42. Katika ubeti wa pill popo anasema "sina jadi na kunguru", usemi "sina jadi" una maana gani?

  1. Hana uhusiano
  2. Hana ushirikiano
  3. Hana nasaba
  4. Hana urafiki
  5. Hana muafaka


43. Popo alitakiwa kujitetea bayana. Usemi "Kujitetea bayana" una maana gani?

  1. Kujiteta waziwazi
  2. Kujitetea hadharani
  3. Kujitetea kwa hadhari
  4. Kujitetea kwa kificho
  5. Kujitetea kwa hadhira


44. Mstari wa mwisho katika kila ubeti wa shairi hill huitwaje?

  1. Kituo vina
  2. Kituo kimalio
  3. Kituo bahari
  4. Kituo kitoshelevu
  5. Kituo kikamilifu


45. "Kitendo cha kuzaa na kunyonyesha hufanywa na viumbe ambao ni " Neno linalokamilisha sentensi hiyo ni lipi?

  1. Bata
  2. Wadudu
  3. Samaki
  4. Kunguru
  5. Wanyama


46. Kichwa cha shairi hill chafaa kiwe kipi?

  1. Hakimu
  2. Popo
  3. Popo mahakamani
  4. Hakimu mahakamani
  5. Wanyama


SEHEMU E

UTUNGAJI

Umepewa habari yenye sentensi nne (4) zilizoaandikwa bila mtiririko sahihi wa mawazo katika swali la 47 - 50. Zipange sentensi hizo iii ziwe na mtiririko wenye mantiki kwa kuzipa herufi A, B, C, na D.

47. Alipomaliza kusema hayo Mzee komba akauliza, "Tupande miti wakati inaota kwa uwezo wa Mungu?"



48. Mkutano ulipomalizika kila mtu alirejea nyumbani kwake akiwa na dhamira ya kupanda miti.



49. Bwana miti akasema "Yapasa kupanda miti kwa sababu matumizi yake yameongezeka sana siku hizi".



50. "Tusipopanda miti mipya tutaishiwa miti kabisa". Bwana miti alijibu.



STD VII KISWAHILI NECTA EXAM OF YEAR 2010 Try This  |  

KISWAHILI 2010

SEHEMU A

SARUFI

Katika swali la 1-5 andika herufiya jibu lililo sahihi katika karatasiyakoya kujibia.

1. "Ukitaka cha mvunguni inama". Hii ni sentensi ya aina gani?

  1. ambatano 
  2. changamano 
  3. shurutia 
  4. nyofu 
  5. sahili


2. Katika neno "hatutakamilisha", kiambishi kinachoonesha nafsi ni kipi?

  1. -ka- 
  2. -ta- 
  3. -ha- 
  4. -sha- 
  5. -tu-


3. "Kampeni ya upandaji miti wilayani Kishapu ilifanikiwa sana na wananchi." Sentensi hii ipo katika kauli gani?

  1. kutendwa
  2. kutendewa
  3. kutenda
  4. kutendana
  5. kutendeka


4. Kisawe cha neno "beseni" ni kipi?

  1. debe 
  2. karai
  3. ndoo 
  4. pipa
  5. chupa


5. Wingi wa sentensi isemayo, "Ubao umetumika" ni ipi?

  1. Mbao itatumika
  2. mbao umetumika
  3. mbao zitatumika 
  4. mbao imetumika
  5. mbao zimetumika


6. Katika sentensi ifuatayo, ni neno lipi limetumika kama kiwakilishi? "Huu ni wa maziwa."

  1. ziwa 
  2. huu 
  3. Ni 
  4. Wa 
  5. Maziwa


7. Ubegete ameshinda kondeni akiamia ndege. Kielezi katika sentensi hii ni kipi?

  1. Kondeni 
  2. Akiamia 
  3. Ameshinda 
  4. Ndege 
  5. Kondeni akiamia


8. Mwalimu alikuwa anatunga mtihani. N eno "anatunga" limetumika kama aina ipi ya kitenzi?

  1. Kishirikishi 
  2. Kitenzi Kikuu 
  3. Kisaidizi 
  4. Kitenzi kipungufu 
  5. Kitenzi jina


9. Alfajiri na mapema tuliondoka ukumbini. Mzizi katika neno lililopigiwa mstari ni upi?

  1. -ondo-
  2. -iondoka
  3. -ondok-
  4. ondoka
  5. -iondok-


10. Kinyume cha neno "Tandika" ni kipi?

  1. Tandaza
  2. Tandua
  3. Tanzua
  4. Tanzia
  5. Tandiko


11. Umoja wa sentensi "Machungwa mabichi yana ladha ya uchachu” ni...

  1. Chungwa bichi lina ladha ya uchachu
  2. Chungwa bichi lina ladha yake
  3. Chungwa bichi lina kaladha ka uchachu
  4. Chungwa bichi lina ladha kali
  5. Vichungwa vibichi vina ladha ya uchachu.


12. Fundi atengenezaye herein, pete an mikufu huitwaje?

  1. Sofara 
  2. Mfuaji 
  3. Sonara 
  4. Mnajimu 
  5. Fundi


13. "Zena amemnunulia mwanae kizibao” limetumika kwa maana ipi?

  1. Suti yenye mikono mirefu
  2. Jaketi kubwa
  3. Shati la mikono mifupi
  4. Koti fupi lisilo na mikono
  5. Koti lenye mikono mirefu


14. Neno "kindumbwendumbwe” lina silabi ngapi?

  1. Saba
  2. Nne 
  3. Tano
  4. Mbili 
  5. Tisa


15. Watalii wengi hufika Tanzania ili .mlima Kilimanjaro. Ni neno lipi linalokosekana kukamilisha sentensi hiyo?

  1. kuzuru 
  2. kuthuru 
  3. kudhuru
  4. kufuru 
  5. kudhulu


SEHEMU B

MSAMIATI

Katika swali la 16 - 25 andika herufiyajibu lililo sahihi katika karatasiyakoya kujibia.

16. Baada ya mshenga kutoa wageni waliondoka na kurudi makwao. Chagua neno sahihi kati ya maneno yafuatayo ili ukamilishe sentensi hiyo.

  1. fahari
  2. posa
  3. barua
  4. mahali
  5. mali


17. Neno "msimu” lina maana gani?

  1. Majira
  2. Muda
  3. Mvua
  4. Kipupwe
  5. Masika


18. Yule bwana amelima kwa bidii na amevuna . . mwingi sana.

  1. mipunga
  2. mchele
  3. mpunga 
  4. wali 
  5. michele


19. Kisawe cha neno ”hitimisho” ni kipi?

  1. Hitima
  2. Tamati
  3. Mwanzo
  4. Katikati 
  5. Tanguliza


20. Katika vifungu vya maneno vifuatavyo ni kifungu kipi chenye maneno yanayoshabihiana?

  1. Kuku, chiriku, njiwa, mwewe.
  2. Almasi, dhahabu, kitok, chui
  3. Maembe, mapera, shaba, matopetope
  4. Shati, kiwiko, ukucha, kidole
  5. Tembo, nyani, kondoo, mtende


21. Kinyume cha neno "shaibu" ni kipi?

  1. Barubaru 
  2. Ngariba 
  3. Banati
  4. Ajuza 
  5. Kijana


22. Ng'ombe dume aliyeachishwa ambaye hutumika kwa kufanya kazi kama vile kuvuta mkokoteni au plau huitwaje?

  1. Fahali 
  2. Maksai 
  3. Dume
  4. Beberu 
  5. Fahari


23. "Mfanyabiashara alipatwa na nuksi kubwa baada ya bidhaa zake kuungua moto". Ni neno lipi linalandana na neno "nuksi" kati ya yafuatayo?

  1. Ghasia
  2. Balaa 
  3. Dhahama
  4. Mkasa  
  5. Tashititi


24. Kisawe cha neno "runinga" ni kipi?

  1. Mninga 
  2. Ninga
  3. Televisheni
  4.  Tovuti
  5. Kinakilishi


25. Kinyume cha neno "kunyanyapaa" ni kipi?

  1. Kutunza 
  2. Kusifia
  3. Kuhifadhi
  4. Kubembeleza 
  5. Kustahi



SEHEMU C

METHALI, NAHAU NA VITENDAWILI

Katika swali la 26 - 30 Andika herufiyajibu lililo sahihi katika karatasi yakoya kujibia.

26. Wanafunzi wa darasa la tano wanafanya kazi zote bega kwa bega. Neno lililopigiwa mstari lina maana gani?

  1. Kuwasilishana 
  2. Kuegemeana 
  3. Kutegeana
  4. Kushirikiana 
  5. Mabega mawili


27. Kifungu cha maneno kisemacho, "Anayefanya juhudi katika masomo au jambo Iolote hufanikiwa" kinashabihiana na methali ipi kati ya zifuatazo?

  1. Nazi haishindani na jiwe
  2. Mwenye nguvu mpishe
  3. Mgaagaa na upwa hali wali mkavu
  4. Ukitaja nyoka shika fimbo mkononi
  5. Uzuri wa mkakasi ndani kipande cha mti


28. Baada ya John kupanda cheo, alimtilia Sara kitumbua chake mchanga. Maana ya msemo "kutilia kitumbua mchanga" ni upi?

  1. Kumsifia mtu asiye na sifa
  2. Kumharibia mtu sifa zake au mambo yake mazuri
  3. Kumharibia jina wakati hana jina
  4. Kumtangaza maovu wakati hana
  5. Kumtangazia mtu sifa asizokuwa nazo


29. Wanafunzi wa darasa Ia saba wamesoma kwa makini hadi wamehitimu masomo yao. Ni methali ipi kati ya zifuatazo inasadifu sentensi hiyo?

  1. Ngoja ngoja yaumiza matumbo 
  2. Kuuliza si ujinga
  3. Ahadi ni deni 
  4. Mwenda pole hajikwai
  5. Mvumilivu hula mbivu


30. "Mwana wa ndugu kirungu, mjukuu mwanangwa." Methali ambayo haifanani na mehtali hii kati ya hizi zifuatazo ni ipi?

  1. Ndugu chungu jirani mkungu
  2. Damu nzito kuliko maji
  3. Ndugu bora kuliko rafiki
  4. Adui aangukapo mnyanyue
  5. Mwana kidonda mjukuu kovu


31. Kifungu kipi cha maneno kinakamilisha methali ifuatayo? "Ikiwa kilemba kimelowa..."

  1. kanzu nayo imeloa 
  2. na mkuti uhali gani?
  3. uhali gani mkuti? 
  4. na mkuti umeloa
  5. mwili wote umeloa


32. Aisatu hujulikana sana kwa "majina ya lakabu". "Majina ya lakabu" maana yake ni ipi?

  1. Majina ya kujipa au ya watu wengine
  2. Majina ya kupanga au kuchekesha
  3. Majina ya kujipa au ya ukoo
  4. Jina Ia kupanga au kupewa na watu 
  5. Majina ya wazazi na ya ukoo


33. Binetuu anawachukua wazazi wake. "Kuwachukua" lina maana gani?

  1. Huwatunza wazazi wake
  2. Huwakaribisha wazazi wake
  3. Huwakidhi haja za maisha 
  4. Huwabeba kila wachokapo 
  5. Huwagomboa wazazi wake.


34. Mama Chakupewa alipotokeza tu sebuleni, wapangaji wenzake wote yyaliangua-kichelo Msemo uliopigiwa mstari una maana gani?

  1. Kucheka hadi mtu anatokwa na machozi
  2. Kucheka sana 
  3. Kucheka sana kwa sauti
  4. Kucheka bila sababu 
  5. Kucheka kwa muda mrefu


35. Kasanga alitegewa kitendawili na babu yake na akakitegua kwa kusema "Mwangwi". Kitendawili hicho ni kipi?

  1. Huko ng'o na kule ng'o
  2. Jinamizi laniita lakini silioni
  3. Huku pi na kule pi
  4. Kaa hapa nikae pale tumfinye mchawi
  5. Kila niendako ananifuata


SEHEMU D

UFAHAMU

Soma kwa makini kifungu cha habari kifuatacho kashajibu swali la 36 - 45 kwa kuandika herufi yajibu lililo sahihi katika karatasiyakoya kujibia.

Hapo kale watu walikuwa wakila vyakula vibichi. Kadri miaka ilivyokwenda mbele watu igundua matumizi ya moto kwa njia ya kupekecha vijiti. Ugunduzi huu uliwasaidia kuanza kuchoma nyama na kupika vyakula.

Kadri miaka ilivyoendelea ndivyo maendeleo yalivyopatikana. Baada ya watu kupata moto kwa kupekecha vijiti, waligundua pia njia nyingine. Njia iliyotumiwa na watu wengi ni ile ya kutumia viberiti. Hivyo waliweza kutumia majiko ya aina mbalimbali kama jiko la mafuta ya taa, jiko la mkaa, jiko la gesi na waliweza kupika kwa kutumia kuni.

Kazi ya kupika ilikuwa rahisi baada ya ugunduzi huu, walianza kula vyakula vya mchanganyiko. Walitambua kwamba vyakula vinavyopikwa kwa mchanganyiko kama mseto na vinginevyo vina manufaa makubwa. Vyakula hivi hujulikana kama mlo kamili. MIO kamili huimarisha siha ya mlaji.

Matumizi ya viberiti hayakuishia katika kuwasha majiko. Viberiti hadi leo vinatumika kuwashia kandili, karabai, vibatari na mishumaa ili kuweza kupata mwanga katika nyumba zetu. Tunatumia viberiti kupata moto tunaoutumia kuchoma mabiwi na takataka nyingine ili kuondoa uchafu katika mazingira yetu.

Moto pia huweza kupatikana kwa njia ya umeme ambao aghalabu hutumika katika sehemu za miji. Ugunduzi wa umeme umesaidia katika shughuli za upishi. Huwawezesha akina mama kupika vyakula kwa kutumia majiko ya umeme. Hupika vyakula vingi kwa urahisi na kwa haraka zaidi. Hali hii imeleta uwezekano wa kupika vyakula vya mchanganyiko yaani mlo kamili. Vyakula hivi huwa na mchanganyiko wote, yaani vyakula vinavyotia nguvu na joto mwilini, vyakula vya kulinda mwili na kujenga mwili. Watu walao mlo kamili kwa nadra huwa goigoi.

Moto pia huweza kupatikana kwa kutumia lensi, kwani lensi ikielekezwa kwenye mwanga wa jua kwa muda mrefu basi karatasi itakayowekwa chini yake hushika moto.

Faida za moto ni nyingi. Hutupa mwanga wakati wa usiku, hutumika katika kuendesha mashine na mitambo mbalimbali. Kama moto usingegunduliwa, maisha ya watu yangekuwa duni.

Aidha, moto una madhara mbalimbali usipotumika vema. Madhara haya hutukumbusha kwamba "uzuri wa mkakasi, ndani kipande cha mti". Athari zake ni kama kuunguza majengo na mitambo, majengo yanapoungua wakati mwingine husababisha maafa ya watu kuungulia ndani ya majengo na mali zao.

Kuepuka madhara na hasara zitokanazo na moto hatuna budi kuwa waangalifu. Tuweke viberiti, mishumaa na taa mbali na watoto; tuunganishe nyaya za umeme kwa kutumia wataalamu, warina asali kufuata njia za kisasa kwa kutumia mavazi ya kitaalamu, kulima kwa kuepuka kuchoma mapori na mashamba. Tusipochukua tahadhari hiyo tutajuta, kwani "Hamna! Hamna! Ndimo mliwamo".

MASWALI

36. Kichwa cha habari hapo juu ni kipi?

  1. Moto 
  2. Umeme
  3. Viberiti 
  4. Taa 
  5. Mkaa


37. Neno "Mseto" lina maana sawa na kifungu kipi cha maneno kati ya vifuatavyo?

  1. Mchanganyiko wa matunda na mboga
  2. Mlo kamili wenye virutubisho
  3. Mlo uliotengenezwa kwa mboga mbichi
  4. Kachumbari na wali
  5. Mchanganyiko wa mchele na choroko


38. "Watu walao mlo kamili kwa nadra huwa goigoi". Sentensi hii ina maana ipi?

  1. Watu walao mlo kamili maridhawa huonekana goigoi 
  2. Watu walao mlo kamili maridhawa huonekana wanyonge
  3. Watu walao mlo kamili mara chache huonekana dhaifu na wanyonge.
  4. Watu walao mlo kamili mara nyingi huonekana wenyenguvu 
  5. Watu walao mlo kamili mara moja moja huwa si wasikivu


39. "Hamna! Hamna! Ndimo mliwamo". Methali hii ina maana gani?

  1. Ni hatari kutegemea mashine na mitambo kwani huleta madhara
  2. Ni vizuri kuchukua tahadhari kabla ya janga kutokea
  3. Tusizoee kusema hamna! Hamna! Mara kwa mara ili tusipate madhara.
  4. Heri kusubiri tatizo ili upambane nalo kuliko kubashiri mambo yajayo 
  5. Ni vizuri kuepuka madhara ya moto


40. Neno "siha" kama lilivyotumika katika kifungu cha habari Ilina maana gani?

  1. Afya njema 
  2. Sifa njema
  3. Maisha mema
  4. Tabia njema 
  5. Bora afya


41. Kwanini watu wa kale walikula vyakula vibichi?

  1. Moto ulikuwa na nguvu hafifu
  2. Moto ulitumika kidogo
  3. Moto ulikuwa haujagunduliwa
  4. moto ulikolea polepole
  5. Hawakuwa na vyakula vya kupika


42. MIO kamili huwa na mchanganyiko wa vyakula vyenye virutubisho mwilini. Vyakula hivyo ni vipi?

  1. Vyakula vya kutia nguvu na joto, vya kujenga na kulinda mwili.
  2. Vyakula vya protini, vinavyojenga mwili na hamirojo
  3. Vyakula vinavyotia nguvu, joto na vitamin na vinavyolinda mwili
  4. Vyakula vinavyojenga miili, hamirojo, vinavyotia nguvu na joto mwilini
  5. Vyakula vinavyolinda mwili, hamirojo na vitamin.


43. Moto una faida nyingi katika maisha ya kila siku. Taja faida tatu za moto.

  1. kupasulia miamba, kuota na mwanga
  2. kupikia, kuota na kuzuia umande
  3. kupikia, mwanga na kuteketeza uchafu
  4. mwanga, kupasulia miamba na kulimia mashambani
  5. kupasulia miamba, kupikia na kujenga


44. kama ilivyotumiwa na mwandishi, methali inayosema "Uzuri wa mkakasi ndani kipande cha mti" ina maana gani?

  1. Hakuana marefu yasiyokuwa na ncha
  2. Kitu kizuri lazima kitengenezwe kwa kutumia kipande cha mti
  3. Usipochukua tahadhari mapema utapata mdhara
  4. Kila chenye mwanzo kina mwisho
  5. Hakuna kizuri kisicho na kasoro


45. Madhara yasababishwayo na moto kama yalivyoelezwa kwenye kifungu cha habari ni yapi?

  1. Huleta uharibifu wa rasilimali na mazingira
  2. Huteketeza nyumba na mitambo na husababisha vifo
  3. Huleta maafa kwa viumbe hai, mali na huharibu mazingira
  4. Husababisha vifo, uharibifu wa migodi na mabwawa ya samaki
  5. Huteketeza nyumba, mali na huharibu miundo mbinu.


SEHEMU E

UTUNGAJI

Umepewa insha yenye sentesi tano (5) zilizoandikwa bila mtiririko sahihi wa mawazo. Zipange sentensi hizi ili ziwe na mtiririko wenye mantiki kwa kuzipa herufi A, B, C, D na E ili ujibu maswali 46 - 50.

46. Ili mpate kuyajua ni lazima mjifunze kwa bidii na maarifa muweze kufaulu mitihani yenu.



47. Ninyi ni vijana wadogo bado wenye matumaini ya kupata maendeleo katika maisha yenu ya baadaye.



48. Endeleeni kusoma na kujifunza kwa bidii kwani Elimu ni bahari, haina mwisho.



49. Elimu ndiyo itakayoweza kuwafungulia njia za kupata maendeleo hayo, katika safari hii ya kuelimika zaidi.



50. Katika safari hiyo ya kuelimika zaidi, utagundua kuwa yapo mambo mengi muhimu ambayo hamyajui.



STD VII KISWAHILI NECTA EXAM OF YEAR 2009 Try This  |  

KISWAHILI 2009

SEHEMU A

SARUFI

Etika swali la 1 - 15 andika herufi yajibu lililo sahihi katika karatasiyakoya kujibia.

1. Angeliamka mapema asingeliachwa na ndege. Kiambishi cha masharti katika sentensi hiyo ni kipi?

  1. -a- 
  2. -nge- 
  3. -ngeli- 
  4. angeli- 
  5. -ili-


2. Neno lipi kati ya haya yafuatayo halina uhusiano na mengine?

  1. Masika 
  2. Mavunde 
  3. Kipupwe
  4. Kiangazi 
  5. Kifuku


3. Alisema hajisikii vizuri. Kauli halisi ya sentensi hii ni ipi?

  1. "Hajisikii vizuri” 
  2. "Anajisikia vizuri”
  3. "Najisikia vizuri”
  4. "Nilijisikia vizuri” 
  5. "Sijisikii vizuri”


4. Neno lipi linakamilisha sentensi ifuatayo:

Kama kazi hii ingalifanywa na mtu mmoJa ... ... ... kumaliza.

  1. asingeweza 
  2. asingaliweza
  3. angaliweza
  4. asingeliweza 
  5. asingeweza


5. Chakula hiki si kibayahakina viungo. Neno linalokosekana katika sentensi hii ni lipi?

  1. kama 
  2. ila
  3. wala
  4. alimurudia 
  5. kwa kuwa


6. "Shule imefunguliwa” ukanushi wa sentensi hii ni ipi?

  1. Shule haitafunguliwa 
  2. Shule aijafunguliwa
  3. Shule haijafunguliwa 
  4. Shule haikufunguliwa
  5. Shule aikufunguliwa


7. Kiranja mkuu wa shule . . . . . . . . mawazo ya wanafunzi wenzake katika kikao cha uongozi wa shule. Neno lipi linakamilisha sentensi hiyo?

  1. aliwakilisha
  2. ariwasilisha
  3. aliwasirisha
  4. aliwasilisha
  5. ariwasirisha


8. Wingi wa neno "kuku” ni upi?

  1. Kuku
  2. Vikuku
  3. Makuku
  4. Makuku 
  5. Vijikuku


9. Kayumba na Neema wanaosha vyombo. Neno "vyombo” limetumika kama aina gani ya neno?

  1. Kitenzi 
  2. Nomino 
  3. Kivumishi
  4. Kielezi 
  5. Kiwakilishi


10. "Padri Joni anapenda sana kucheza mpira wa kikapu." Sentensi hii ipo katika nafasi ipi?

  1. Nafsi ya kwanza - umoja
  2. Nafsi ya tatu - wingi
  3. Nafsi ya pili - umoja 
  4. Nafsi ya tatu - umoja 
  5. Nafsi ya kwanza — wingi


11. Sentensi ipi kati ya zifuatazo ipo katika kauli taarifa?

  1. Anakwenda mjini, Joti alisema
  2. Joti alisema, ninakwenda mjini
  3. Joti alisema, nitakwenda mjini
  4. Joti alitaka kujua kama atakwenda mjini
  5. Joti alisema kuwa amekwenda mjini


12. Buibui, inzi, mbu, papasi na tandu kwa neno moja huwa wanaitwaje?

  1. Wanyama 
  2. Warukao 
  3. Wadudu 
  4. Ndege 
  5. Viroboto


13. "Mzee Masanja amempa binti yake mume." Sentensi hii ina maana ipi?

  1. Mzee Masanja amemwolesha binti yake
  2. Mzee Masanja ameozesheana na binti yake
  3. Mzee Masanja amemwozesha binti yake
  4. Mzee Masanja amemwoza binti yake
  5. Mzee Masanja amemchukua mume na kumpa binti yake


14. Katika sentensi zifuatazo ni ipi iliyo sahihi kimuundo?

  1. Nilikwenda kituo cha afya nilimkuta daktari hayupo
  2. Nilikwenda kituo cha afya lakini nilimkuta daftari hayupo
  3. Nilikwenda kituo cha afya lakini sikumkuta daktari
  4. Nilipokwenda kituo cha afya nikamkuta daktari hayupo
  5. Nilipokwenda nikamkuta hayupo


15. Ni kipi kinyume cha neno "kaditama?"

  1. Kati 
  2. Mwanzo
  3. China
  4. Juu 
  5. Mwisho


SEHEMU B

MSAMIATI

Katika swali la 16 - 25 andika herufiyajibu lililo sahihi latika karatasiyakoya kujibia.

16. Wakati akiendesha baiskeli yake, magurudumu yalimrushia tope kwa kuwa hayajakuwz na . . . . . . la kuzuia. Sentensi hii inakamilishwa na neno lipi?

  1. mbago 
  2. zuio
  3. bati
  4. jiwe 
  5. bano


17. Mtu mwenye elimu ya mienendo ya nyota anaitwaje?

  1. Mnadhimu 
  2. Mnajimu
  3. Mnandi
  4. Mwananyota 
  5. Shauku


18. "Mnyamavu" ni neno lenye maana sawa na kifungu kipi cha maneno kati ya vifuatavyo?

  1. Mwenye kupenda wanyama
  2. Mwenye kuchukia wanyama
  3. Mwenye tabia ya kuongea sana
  4. Mwenye tabia ya kukaa kimya
  5. Mwenye tabia ya ucheshi


19. Kifungu cha maneno chenye maana sawa na neno "mwafaka" ni kipi?

  1. Mapatano baina ya watu
  2. Mafarakano baina ya watu
  3. Utengano baina ya watu
  4. Matatizo baina ya watu
  5. Ushirikiano baina ya watu


20. Wanakijiji wa Songambele walifanya kazi zao kikoa. Neno "kikoa" lina maana gani?

  1. Kiukoo 
  2. Kwa ushirika
  3. Kwa ubinafsi 
  4. Kwa bidii 
  5. Kwa utengano


21. Siku hizi bei ya mafuta imekithiri. Neno "kithiri" limetumika kwa maana ipi?

  1. Kushuka
  2. Kupungua
  3. Iko kawaida 
  4. Aghali sana 
  5. Ni ndogo


22. Mtu anayefanya kazi ya kuhifadhi vitabu katika maktaba na kuviazimisha kwa wasomaji anaitwaje?

  1. Mhudumu
  2. Mkutubi
  3. Mhariri
  4. Karani
  5. Mchambuzi


23. Alionesha ......... kuwa Diengi ndiye aliyehusika na uuzaji wa madawa ya kulevya. Neno linalokamilisha sentensi hii kwa usahihi ni lipi?

  1. dahiri
  2. dhamiri
  3. dhamira 
  4. zahiri 
  5. dhahiri


24. Kifungu cha maneno kati ya vifuatavyo chenye maana sawa na neno "nishati" ni kipi?

  1. Kuni, umeme, mafuta na moto
  2. Mafuta, joto, miti na gesi
  3. Kuni, umeme, viwanda na mimea
  4. Mafuta, kuni, gesi na umeme
  5. Joto, viwanda,kuni na miti


25. Neno "kuengua" lina maana gani?

  1. Kuondoa tunda juu ya mti
  2. Kuondoa utando juu ya kitu kilichoganda
  3. Kutikisa polepole mti wa matunda
  4. Kuondoa buibui
  5. Kutenganisha vitu vilivyoganda


SEHEMU C

METHALI, NARAU NA VITENDAWILI

Katika swali la 26 - 35 andika herufi ya jibu sahihi katika karatasiyakoya kujibia.

26. Methali isemayo, "Mti hawendi ila kwa nyenzo” iko sawa na methali ipi kati ya hizi zifuatazo?

  1. Mwenda tezi na Omo marejeo ngamani
  2. Ngozi ivute ingali maji
  3. Penye kuku wengi usimwage mtama
  4. Kaa akiinua gando, mambo yamekatika
  5. Mkono mtupu haulambwi


27. Wanakijiji walimtaka yule mwizi asalimu amri.” Kusalimu amri” ni usemi wenye maana ipi?

  1. Ahame kijijini 
  2. Akubali na kutubu
  3. Asikubali kabisa
  4. Hawapatani kamwe 
  5. Akubali kwenda jela


28. Kitendawili kisemacho. "Mbwa mwitu wamezunguka kumlinda” hutenguliwa kwa jibu lipi?

  1. Ulimi na meno 
  2. Mdomo na meno
  3. Kichwa na nywele 
  4. Mkono na vidole 
  5. Kucha na vidole


29. Methali inayopingana na methali isemayo, "Haraka haraka haina Baraka” ni ipi?

  1. Mcheza kwao hutuzwa
  2. Mbio za sakafuni huishia ukingoni
  3. Ngoja ngoja yaumiza matumbo 
  4. Mwenda pole hajikwai
  5. Mgaagaa na upwa hali wali mkavu


30. Wanafunzi wengi wamepigwa na butwaa baada ya kuyaona matokeo yao ya mtihani wa Darasa la Saba. "Kupigwa butwaa” ni msemo wenye maana ipi?

  1. Kushangaa 
  2. Kustuka 
  3. Kukimbia
  4. Kutoweka 
  5. Kupata ahueni


31. Mwita anataka mtoto wake awe na "maadili mema” hadi ukubwani. Methali ipi ataitumia kuhimiza tabia hiyo?

  1. Mcheza kwao hutunzwa. 
  2. Panapofuka moshi pana moto.
  3. Mvumilivu hula mbivu. 
  4. Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.
  5. Adhabu ya kaburi aijuaye maiti.


32. Kiangazi chote hulala usingizi; yakija masika nakesha. Maana ya kitendawili hiki ni ipi?

  1. Nyota
  2. Kaa 
  3. Samaki
  4. Ndege 
  5. Chura


33. Moto alioniachia babu yangu huzima ninapokwenda kulala na huwaka tena mara ninapoamka. Kitendawili hiki kina maana gani?

  1. Mshumaa 
  2. Taa 
  3. Mwezi
  4. Jua 
  5. Nyota


34. ”Chemsha bongo.” Usemi huu una maana gani?

  1. Tafakari kimya kimya
  2. Uutulize ubongo 
  3. Fikiria kwa haraka
  4. Tulia kwao kituo 
  5. Fikiria kwa makini


35. Methali isemayo, "Avumaye baharini papa kumbe wengine wapo”, ina onyo gani?

  1. Kila avumaye avume na wenzake
  2. Tupendane kama papa 
  3. Hakuna anayevuma pekee
  4. Kuna samaki wengi baharini
  5. Wapo papa wengi baharini


SEHEMU D

UFAHAMU

Soma kwa makini shairi lifuatalo kisha jibu maswali (36 - 45) kwa kuandika herufi ya jibu lililo sahihi katika karatasiyakoya kujibia.

Leo ninawasilisha, haya utakayosikia,

Wazazi mmetuchosha, haki zetu mwafukia, Kwa kweliyametuchosha, tumekwisha shitukia, Twaomba mtukidhie, haki hizi za watoto.

Asubuhi twaondoka, shuleni kujisomea,

Na shuleni tukifika, usafi ni mazoea,

Vinywa vyetu vinanuka, njaa kwetu mazoea, 

Twaomba mtukidhie, haki hizi za watoto.

Mtazame mama yangu, anang'ara kwa mapambo,

Tazama mavaziyangu, maduaraya matobo,

Kupendeza baba yangu, utadhani ni mgambo,

Twaomba mtukidhie, haki hizi za watoto,

Amanda wa kijijji, sareya shule hadithi,

Matekenya miguuni, elimu kwake hadithi,

Baadayeya kilabuni,jana njaa kalalia,

Hana mbele wala nyuma, haki atapata lini?

Walimu nao shuieni, sare wasisitizia, 

Usafi nao mwilini, kwa hakika wakazia, 

Tupate wapi sabuni,jana njaa kalalia,

Wazazi muwajibike, haki zetu tupatiwe.

Shuleni nako kifika, elimu wapulizia,

Viboko navyo kulika, matakoni vyatulia, 

Nyumbani nako kufika, mama hataki tulia, 

Twaomba kupumzika, hakiyetu ya msingi.

Mwalimu acha viboko, nikanye takusikia,

Adhabu bila viboko, ukijali takufaa,

Vifaa liwe tamko, shuleni kujisomea,

Elimu ni haki kwetu, tupate iliyo bora.


Haki kwa wote sikia, wakubwa nao watoto,

Chakula bora sikia, afya zetu kuwa moto, 

Ubaguzi kususia, wasichana ni watoto,

Haki msizitoweshe, kwetu taifa la kesho.

Njaa inatusumbua, ajira twazitafuta,

Waajiri wasumbua, kwao utu wamefuta, 

Jamani watuumbua, kwa nini kututafuta, 

Chungulia kwajirani, haki zetu hatupati.

Mwishoni nimefikia, badoo ninawakumbusha,

Heri ninawatakia, huduma kuimarisha, 

Unapopata rupia, umgawie na ngosha, 

Ukijalifamilia, mungu atakubariki.

MASWALI

36. Kichwa kinachofaa kwa shairi hili ni kipi?

  1. Mavazi yanayofaa kwa watoto
  2. Usafi kwa watoto wetu
  3. Adhabu kwa watoto
  4. Haki za watoto
  5. Watoto watukutu


37. Neno "kizingiti" kama lilivyotumiwa na mshairi lina maana sawa na neno lipi kati ya yafuatayo?

  1. Kizuizi
  2. Kibao
  3. Mlango
  4. Kufuli
  5. Kitasa


38. Vina katika ubeti wa Sita ni:

  1. ka na ngi 
  2. Shu na e 
  3. via na a
  4. ko na tu 
  5. a na ka


39. Haki wanazozidai watoto katika shairi hili ni zipi?

  1. Mapambo, kinywaji, sare, miswaki na viatu
  2. Elimu, mavazi kuthaminiwa, chakula na kutunzwa
  3. Usafi, elimu, viboko, viatu na kuthaminiwa
  4. Sabuni, ajira, chakula bora, mapambano na viatu
  5. Miswaki, viatu, mavazi na kuthaminiwa


40. Neno "kuwasilisha" kama lilivyotumiwa na mwandishi lina maana gani?

  1. Kwenda mahali kwa niaba ya wengine
  2. Kusema jambo bila woga
  3. Kufikisha kitu mahali kinakohitajika
  4. Kudai haki za msingi
  5. Kuwapa ukweli watu wasiotimiza wajibu wao


41. Mshairi anaposema, "elimu kwake hadithi" ana maana gani?

  1. Walimu hawafundishi 
  2. Hapendi kwenda shule
  3. Hawajawahi kwenda shule 
  4. Husimulia habari za shule
  5. Hupenda kwenda shule


42. Mtunzi anaposema "hana mbele wala nyuma”, msemo huo una maana ipi?

  1. Mjinga
  2. Mkaidi 
  3. Mzembe 
  4. Fukara 
  5. Mvivu


43. Katika ubeti wa nane, mwandishi anashauri nini kuhusu elimu kwa jinsia zote?

  1. Wazazi wasiwasuse watoto wao
  2. Wazazi na walimu wasiwabague watoto kwa jinsia zao
  3. Watoto wawasikilize wazazi wao
  4. Walimu wasiwabague wanafunzi wakati wa kufundisha 
  5. Wanafunzi wasikaidi wanapotumwa na walimu wao


44. Kuna mizani mingapi katika kila mstari wa shairi?

  1. Mizani minne (4)
  2. Mizani kumi (10)
  3. Mizani kumi na nane (18)
  4. Mizani kumi na sita (16) 
  5. Mizani (6)


45. Kwa ujumla shairi hili linamshauri kila mtu afanye nini?

  1.  Atambue haki za wakubwa
  2. Atambue haki zake za msingi
  3. Afanye kazi na starehe
  4. Afanye usafi wa mwili
  5. Adai haki bila wajibu


SEHEMU E

UTUNCAJI

Umepewa insha yenye sentensi tano (5) zilizoandikwa bila mtiririko sahihi wa mawazo. Zipange sentensi hizo ziwe na mtiririko wenye mantiki kwa kuzipa herufi A, B, C, D na E ili kujibu swali 46 - 50.

46. Baadhi ya mambo yanayochangia kuenea kwa gonjwa hatari la UKIMWI ni kuchangia vifaa vya kutogea masikio, vifaa vya kutahiri, ngono isiyo salama na kutoka kwa mama mjamzito kwenda kwa mtoto wakati wa kujifungua na kunyonyesha.



47. Dalili za gonjwa hili ni homa za mara kwa mara, kupungua uzito, upungufu wa damu mwilini, ukurutu, kuvimba matezi na kuharisha.



48. Ili kuzuia gonjwa hili la hatari lisienee hatuna budi kuepuka kuchoma sindano za mitaani zisizochemshwa, kutochangia vifaa vya kutogea masikio na kutahiria, kuwa mwaminifu na kusubiri, hivyo Tanzania bila UKIMWI itawezekana.



49. UKIMWI ni ugonjwa hatari usiokuwa na tiba wala kinga.



50. Madhara yatokanayo na ugonjwa huu ni kudidimia kwa uchumi kwa sababu ya kupoteza nguvu kazi ya taifa, umasikini na kuongezeka kwa watoto yatima.



STD VII KISWAHILI NECTA EXAM OF YEAR 2008 Try This  |  

KISWAHILI 2008 

SEHEMU A

SARUFI

Katika swali la 1 - 15 andika herufiyajibu lililo sahihi katika karatasiyakoya kujibia.

1. Neno lipi linakamilisha sentensi isemayo, "Humu . . alimoingia yule nyoka"

  1. ndiye
  2. ndio 
  3. ndiyo 
  4. ndimo 
  5. ndiko


2. Badala ya kusema, "mimi sijambo". Ninaweza kusema, "mimi .. kamilisha sentensi hiyo kwa neno sahihi.

  1. wa afya 
  2. ahueni 
  3. heri
  4. buheri 
  5. mzima


3. Ala kumbe! Kihisishi ni kipi kati ya yafuaatayo?

  1. Ameondoka 
  2. Leo 
  3. Ala kumbe
  4. Ala 
  5. Kumbe


4. Kisawe cha neno kati ya yafuatayo?

  1. Hadharani 
  2. Mafichoni 
  3. Pembezoni
  4. Waziwazi 
  5. Kivulini


5. Mtoto aliyepotea amepatikana. Hii ni aina ipi ya sentensi?

  1. Sahili
  2. Tegemezi
  3. Changamano
  4. Changamano
  5. Shurutia


6. Yule msichana anaimba vizuri. Neno lililopigiwa mstari limetumika kama aina ipi ya maneno?

  1. Nomino 
  2. Kielezi 
  3. Kitenzi
  4. Kivumishi 
  5. Kiwakilishi


7. Sentensi ipi kati ya zifuatazo ipo katika kauli halisi?

  1. Mimi siendi 
  2. Alisema haendi 
  3. Ameenda 
  4. Alisema hataenda
  5. Alisema anaenda


8. Nomino inayotokana na kitenzi "Vaa" ni ipi?

  1. Nguo
  2. Valisha
  3. Kivalo 
  4. Kivazi 
  5. Vazi


9. Neno lipi linakamilisha sentensi isemayo, Timu ya Taifa ingalicheza vizuri . mchezo

A. ingelishinda B. ingeshinda C. ingashinda

D. ingalishinda E. itashinda



10. Siku ya Mei Mosi wafanyakazi walipita mbele ya Waziri Mkuu wakishikilia ......... yenye maneno ya kuhimiza kazi. Neno lipi linakamilisha sentensi hiyo?

  1. mabango 
  2. libango 
  3. kibango
  4. vibango
  5. bango


11- "Nguo yangu imechafuka sana.” Wingi wa sentensi hii ni upi?

  1. Nguo yangu imechafuka sana 
  2. Nguo zetu zimechafuka sana
  3. Nguo yetu zimechafuka sana 
  4. Nguo zao zimechafuka sana 
  5. Nguo yetu zimechafuka sana


12. Lipi kati ya maneno yafuatayo halina uhusiano na mengine?

  1. Ng'ombe 
  2. Mbuzi
  3. Simba 
  4. Chiriku
  5. Nyani


13. Samaki, dagaa na nyama. Kwa neno moja huitwaje?

  1. Kitoweo 
  2. Mboga 
  3. Mchuzi
  4. Mlo 
  5. Chakula


14. Sentensi isemayo, ”ltakapofika mchana .... kuondoka” inakamilishwa kwa usahihi na neno lipi kati ya yafuatayo?

  1. tuliruhusiwa
  2. tataruhusiwa
  3. tumeruhusiwa
  4. hurusiwa 
  5. tunaruhusiwa


15. Kinyume cha neno "duni” ni kipi?

  1. Thamani
  2. Kidogo
  3. Hafifu
  4. Kikubwa 
  5. ?mara


SEHEMU B

MSAMIATI

Katika swali la 16 - 25 andika herufiyajibu lililo sahihi katika karatasi yakoya kujibia.

16. Mzee Jumbe aliwapa wanae mavvaidha juu ya maisha yao. Neno lilipogiwa mstari lina maana gani?

  1. Mawazo 
  2. Urithi
  3. Maonyo
  4. Mahubiri
  5. Hotuba


17. Mtu anayesimamia kazi za shambani huitwaje?

  1. Nokoa 
  2. Mnyapara 
  3. Msimamizi
  4. Kiongozi 
  5. Kiranja


18. Pondamali ni kijana mwenye hila sana. Kisawe cha neno ”hila l'ni kipi?

  1. Hasira 
  2. Ulafi 
  3. Udanganyifu
  4. Ukorofi 
  5. Ukabila


19. "Jioni bahari ilikuwa . kwa hiyo wavivu walivua samaki bila wasiwasi. Neno lipi linakamilisha sentensi hiyo kwa usahihi?

  1. kupwa 
  2. shwari 
  3. kavu
  4. Baridi
  5. joto


20. Mama alijifunza kuendesha gari lakini bado hajafuzu. Neno "Hajafuzu” lina maana ipi kati ya zifuatazo?

  1. Hajajua kuendesha 
  2. Hajamaliza mafunzo hayo 
  3. Hajapata leseni 
  4. Hajahitimu mafunzo hayo
  5. Hatamaliza mafunzo haya


21. Mchanganyiko wa mboga au matunda unaoliwa bila kupikwa huitwaje?

  1. Mchicha 
  2. Kabichi
  3. Nyanya
  4. Matango 
  5. Saladi


22. Kabwela alimsihi baba yake ampe nauli akatembelee mbuga za wanyama. Neno sihi kama lilivyotumika katika sentensi hiyo lina maana gani?

  1. Kubembeleza 
  2. Kumtaka 
  3. Kulazimisha 
  4. Kumshauri 
  5. Kumdanganya


23. Neno lipi linakamilisha sentensi isemayo, "Anapenda kukaa bure ... ...... ana nguvu nyingi”.

  1. pamoja 
  2. iwapo
  3. angalau
  4. japokuwa
  5. isipokuwa


24. Kijana yule anafanya kazi zake kwa makini. Badala ya kutumia neno "makini” ungeweza kutumia neno lipi kati ya yafuatayo?

  1. Busara 
  2. Hekima 
  3. Ujasiri
  4. Wasiwasi 
  5. Uangalifu


25. "Timu ya mieleka ya mkoa wa Rukwa ilikuwa na pambano ......... ya timu ya mieleka ya mkoa wa Mtwara”. Kamilisha sentensi hiyo kwa neno mojawapo kati ya yafuatayo:

  1. zidi 
  2. zaidi 
  3. dhidi
  4. kuzidi
  5. miongoni


SEHEMU C

METHALI, NAHAU NA VITENDAWILI

26. "Kidole kimoja hakivunji chawa”. Methali hii ina maana sawa na methali ipi kati ya zifuatazo?

  1. Mchagua jembe si mkulima
  2. Kilema si ugonjwa
  3. Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu
  4. Kuvuja kwa pakacha nafuu kwa mchukuzi
  5. Kulia kwake ni kicheko kwetu


27. Kifungu kipi cha maneno hukamilisha kitendawili kifuatacho kwa usahihi? 'Watoto wa binadamu  . . . . . .

  1. huondoka na kurudi 
  2. wakiondoka hawarudi
  3. hutangulia kuondoka 
  4. huchelewa kuondoka
  5. huondoka pamoja na binadamu


28. "Sina hali”. Nahau hii ina maana gani?

  1. Sina pesa 
  2. Ninaumwa
  3. Sina ahueni
  4. Sijambo
  5. Sijiwezi


29. "Udongo uwahi ungali maji". Methali hii ina maana gani?

  1. Udongo ukikauka unakuwa mgumu
  2. Kuchukua tahadhari kabla ya hatari
  3. Usitatue tatizo kabla ya hatari
  4. Udongo wenye maji usiuwahi 
  5. Kukimbilia tatizo si kulitatua


30. Tatizo la ufisadi limeota mizizi katika nchi yetu. "Kuota mizizi" ni usemi wenye maana gani?

  1. Kuibuka
  2. Kutoweka
  3. Kufifia
  4. Kuanza
  5. Kushamiri


31. "Mgonjwa aendapo hospitalini na kutopata matibabu hadi atoe chochote kwa mhudumu wa afya." Nahau ipi inasaidia hali hiyo?

  1. Kutia mkono kizani
  2. Kuzunguka mbuyu
  3. Kuua tembo kwa ubua
  4. Kujikaza kisabuni 
  5. Kutoa ni moyo


32. Katika methali zifuatazo ni methali ipi ambayo haifanani na zingine?

  1. Mlilala handingwandingwa mwenye macho haambiwi tule
  2. Usimuamshe aliyelala
  3. Mwenye uchungu hambiwi liwa
  4. Asiyeuliza hanalo ajifunzalo
  5. Mtaka cha mvunguni sharti ainame


33. Neno lipi linakamilisha methali isemayo: Ndugu chungu jirani ?

  1. ndugu
  2. rafiki
  3. jamaa
  4. mkungu
  5. kinu


34. Tegua kitendawili kisemacho "Ajihami bila silaha" kwa kuchagua neno sahihi kati ya yafuatayo:

  1. Nyoka
  2. Mbwa
  3. Kinyonga
  4. Paka
  5. Mjusi


35. Tegua kitendawili kisemachö "Maskini huyu hata umchangie namna gani haridhiki", kwa kuchagua neno moja kati ya yafuatayo:

  1. Tumbo 
  2. Macho
  3. Pua
  4. Masikio
  5. Mdomo


SEHEMU D

UFAHAMU

Soma habari ifuatayo halafu jibu maswali (36 - 45) kwa kuandika herufi sahihi katika karatasi yakoya kujibia.

Kijana Makubwa alikuja juu katika kushikilia tabia yake ya ufedhuli na maringo. Kwa kuwa alikuwa msomi, hakudiriki kufumbata jembe na kulima shambani pamoja na wazazi wake. Yeye katika mawazo yake aliona kuwa alihusika na kwenda mjini kutafuta kazi ya ukarani. Aidha Makubwa alikuwa akiwaudhi wengi kijijini, alipozungumza nao aliwamung'unyia Kiswahili kwa majivuno na ukaidi sana. Matendo na mwenendo wake vilionesha kuwa alijiona mtu wa maana sana kuliko wengine na alijawa na mawazo kemkem ya ukubwa wa madaraka.

Shuleni kwake, kama kijijini, Makubwa alipenda maisha ya huria, kutenda Iolote alilotaka akilini mwake. Mara nyingi alikuwa kiguu na njia, hakupenda kutulia mahali pamoja. Alikuwa hajali sheria, aliamka, alisomea alipopataka na kujivalia alivyotaka. Yeye kila wakati alipenda starehe. Kazi alikuwa hafanyi, hata akazoea kusingizia mvua kwa kila wajibu ambao hakuutimiza. Lakini siku zake arobaini ziliwadia, shule haikuweza kuvumilia tena kijana Mkubwa aliyependa huria kuliko nidhamu iliyokubalika na wengi. Shuleni kwake alipigwa kalamu nyekundu. Bila shaka kijijini walianza kusema. "Aliye juu mngoje chini". Wengine walisema "msiba wa kujitakia hauna kilio".

MASWALI

36.Makubwa hakuweza shughuli za kilimo kwa sababu

  1. alishindwa kushika jembe 
  2. hakuwa na muda wa kufanya kazi
  3. ya maringo kujiona msomi 
  4. alieendelea na tabia ile ile
  5. wazazi wake walimruhusu


37.Makubwa alikuwa na tabia gani ambayo haikupendeza huko shuleni?

  1. Maisha ya kutenda alilotaka
  2. Kupenda ukarani
  3. Kushirikiana na wazazi wake
  4. Kutulia sehemu moja
  5. Kuzungumza lugha ya Kiswahili


38. Mwandishi anasema, "alijawa na mawazo kemkem ya ukubwa wa madaraka." Maana ya neno kemkem ni ipi?

  1. Finyu 
  2. Kidogo 
  3. Kinyume
  4. Mengi
  5. Kuonekana


39.Kutenda mambo kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa. Neno gani kati ya yafuatayo linasadifu sentensi hiyo?

  1. Unyenyekevu 
  2. Nidhamu 
  3. Uadilifu 
  4. Kanuni 
  5. Wajibu


40. Ni kipi kilichomsibu Makubwa baada ya shule kushindwa kuvumilia tabia yake?

  1. Alionywa 
  2. Alifukuzwa shule
  3. Wazazi waliitwa shuleni 
  4. Alisimamishwa masomo
  5. Hakupewa uhuru


41. Mwandishi anazungumzia nini juu ya wanafunzi kutimiza wajibu wao?

  1. Kujali sheria, kusoma na kutenda yote yanayohitajiwa
  2. Kusoma, kuthamini starehe na michezo
  3. Kuwa na nguvu za kutosha, mahitaji muhimu na kucheza
  4. Kucheza, matayarisho muhimu na kusoma 
  5. Kutulia mahali, starehe na kusoma


42. Kwa maoni yako kichwa cha habari hii kinaweza kuwa kipi?

  1. Wanafunzi wa Makubwa 
  2. Tabia ya shule
  3. Tabia ya Makubwa 
  4. Maisha ya shule 
  5. Mambo ya wanafunzi


43. 'Msiba wa kujitakia hauna kilio". Usemi huu una maana gani? 

  1. Matatizo hayaepukiki
  2. Matatizo hayana masikitiko
  3. Matatizo na msiba yana masikitiko 
  4. Matatizo ni ya kujilaumu
  5. Ukijitafutia matatizo usisikitike


44. Fundisho unalolipata katika habari hii ni "wanafunzi tuwe na: 

  1. utii na uvumilivu 
  2. uhuru na uwazi
  3. subira na kujiamiani 
  4. kiasi na bidii
  5. uaminifu


45. Kifungu kipi cha habari hukamilisha sentensi isemayo "Makosa ya kutotimiza wajibu shuleni yakijitokeza mara nyingi ... ... ... "

  1. hupata majibu mchache 
  2. huachwa bila wajibu
  3. hupata visingizio vingi
  4. hayana ufumbuzi 
  5. hupatiwa ufumbuzi


SEHEMU E

UTUNGAJI

Umepewa insha yenye sentensi tano (5) zilizoandikwa bila mtiririko sahihi wa mawazo. Zipange sentensi hizo ili ziwe na mtiririko wenye mantiki kwa kuzipa A, B, C, D na E ili kujibu maswali 46 - 50.

46. Tutaendelea kusaidiana na kushirikiana katika mambo mbalimbali hasa katika shughuli za kiuchumi, kielimu na kijamii.



47. Kumekuwa na mwingiliano wa tamaduni za kigeni katika nchi zetu mfano mavazi, lugha, ngoma, nyimbo, mila, na desturi.



48. Lakini katika kijiji chetu cha Tupendane tumeamua kudumisha upendo na ushirikiano miongoni mwetu.



49. Baadhi ya misingi mizuri ya maisha imevurugwa.



50. Mambo mengi yaliyotokea na yanayoendelea kutokea yameathiri sehemu ya utamaduni wetu.



STD VII KISWAHILI NECTA EXAM OF YEAR 2007 Try This  |  

KISWAHILI 2007

SEHEMU A

SARUFI

Katika swali Ia 1-15 andika herufiyajibu lililo sahihi katika karatasiyakoya kujibia.

1. Mvutano kati ya wanakijiji na viongozi wao ulikuwa haujapatiwa neno lipi linakamilisha sentensi hii?

  1. Ugunduzi 
  2. Ufunguzi 
  3. Ufumbuzi
  4. Uvumbuzi 
  5. Uchunguzi


2. Maneno "mrefu, mweusi, mwerevu na mpole" yakitumika pamoja na majina hufanya kazi gani?

  1. Kivumishi 
  2. Kielezi 
  3. Kitenzi
  4. Nomino 
  5. Kiswahili


3. Sentensi ipi kati ya zifuatazo ni umoja wa sentensi "Bakari amehamisha mizinga ya nyuki kutoka shambani mwake"?

  1. Bakari amehamisha mizinga ya nyuki shambani
  2. Bakari amehamisha mzinga wa nyuki shambani mwake
  3. Alihamisha kimzinga cha nyuki shambani mwake
  4. Amehamisha kamzinga ka shambani mwake
  5. Bakari ameamishia mzinga wa nyuki shambani mwake


4. Katika sentensi ifuatayo ni neno lipi limetumika kama kiwakilishi "Yule ni mnene kupita kiasi".

  1. Yule
  2. Ni
  3. Mnene 
  4. Kupita 
  5. Kiasi


5. Kinyume cha neno ughaibuni ni kipi?

  1. Nchi jirani 
  2. Magharibi
  3. Nchi za mbali 
  4. Mashariki
  5. Nyumbani


6. Sentensi ipi kati ya hizi zifuatazo ipo katika kauli taarifa?

  1. Rafiki yetu yule kachoka kusubiri
  2. Amechoka kusubiri rafiki yetu yule
  3. Rafiki yetu amesema kwamba amechoka kusubiri
  4. Rafiki yetu vipi, umesema umechoka kusubiri? 
  5. Amesema hajachoka kusubiri


7. Kipi ni kinyume cha neno gwiji?

  1. Mwerevu 
  2. Asiye hodari
  3. Mwanamuziki 
  4. Mwimbaji 
  5. Hodari


8. Katika neno "sitakuwepo" kiambishi kinachoonyesha ni kipi?

  1. -ta- 
  2. -we- 
  3. -ku- 
  4. -po- 
  5. -si-


9. "Mvvanafunzi aliyefaulu vizuri atapewa tuzo". Kishazi tegemezi katika sentensi hii ni kipi?

  1. Atapewa tunzo
  2. Aliyefaulu tunzo
  3. Mwanafunzi aliyefaulu vizuri
  4. Mwanafunzi vizuri atapewa
  5. Aliyefaulu vizuri atapewa


10. Neno lipi limekosekana kuikamilisha sentensi ifuatayo kwa usahihi? "Mtoto haandiki . . . . . . . . . . . hasomi".

  1. Ila
  2. bali
  3. kama 
  4. wala 
  5. hata


11. "Ukifanya vizuri utapongezwa". Sentensi hii ni ya aina gani?

  1. Sahili 
  2. Shurutia 
  3. Changamano 
  4. Tegemezi 
  5. Ambatano


12. "Nyumba ya Amini imejengeka vizuri". Sentensi hiyo ipo katika kauli gani?

  1. Kutenda 
  2. Shurutia
  3. Kutendeka
  4. Kutendeana 
  5. Kutendwa


13. Unaponyumbulisha neno apiza unapata nomino ipi?

  1. Apizo 
  2. Pizo
  3. Apizika
  4. Waapizo 
  5. Apizana


14. Neno lipi ni tofauti na maneno mengine kati ya yafuatayo?

  1. Senge'nge 
  2. Wigo
  3. Barabara
  4. Ukuta 
  5. Ukingo


15. "Uji huu una sukari na maziwa". Ukanushi wa kauli hii ni upi?

  1. Uji huo hauna sukari ila maziwa
  2. Uji huu hauna sukari wala maziwa
  3. Uji huo hauna sukari bila maziwa
  4. Uji huu sukari bila maziwa
  5. Uji huu hauna lakini una maziwa


SEHEMU B

MSAMIATI

Katika swali 16 - 25, andika herufiya jibu lililo sahihi katika karatasiyakoya kujibia.

16. Neno lenye maana sawa na neno "mawio" ni lipi kati ya yafuatayo?

  1. Macheo 
  2. Magharibi 
  3. Mchana
  4. Jioni 
  5. Machweo


17. Watu waliokusanyika kwa pamoja ili kuabudu huitwaje?

  1. Wafuasi 
  2. Waabudu
  3. Waumini
  4. Waswalishwa 
  5. Wakereketwa


18. Selina alitumwa sokoni kununua mbuzi ya kukuna nazi. Neno "mbuzi" limetumika kwa maana ipi?

  1. Mnyama anayekuna nazi
  2. Kinu cha kutwangia nazi
  3. Kibao chenye kipande cha chuma cha kukunia nazi
  4. Kitu cha kukalia ambacho hutumika kukunia nazi 
  5. Kitu chenye kibao cha kukunia nazi


19. Neno lipi kati ya maneno yafuatayo lina maana sawa na neno "shaghalabaghala"?

  1. Mpangilio
  2. Ovyo ovyo 
  3. Vizuri
  4. Viovu
  5. Faragha


20. Neno lipi kati ya maneno yafuatayo halilandani na mengine?

  1. Kuona 
  2. Kunusa
  3. Kuonja
  4. Kusikia 
  5. Kutoa jasho


21. "Elimu maalumu inayohusiana na matukio na mambo yaliyopita". Neno lipi kati ya maneno yafuatayo lina maana sawa na kauli hii?

  1. Historia 
  2. Jiografia 
  3. Jiolojia
  4. Mageuzi 
  5. Unajimu


22. Mtu anayeacha kazi ya ajira baada ya kutimiza umri uliowekwa kutokana na kanuni anaitwaje?

  1. Mstaarabu
  2. Mstaafu
  3. Mchapakazi
  4. Mzee
  5. Mchovu


23. Ni kipi kinyume cha neno "barubaru"?

  1. Banati
  2. Kijana
  3. Ajuza
  4. Mrembo 
  5. Mtoto


24. Neno lipi kati ya maneno yafuatayo lina maana sawa na neno "zuzu"?

  1. Mjanja 
  2. Mpole 
  3. Mjinga
  4. Mzubafu 
  5. Mzururaji


25. Mahindi, maharage, ufuta, michungwa, migomba na mihogo. kwa neno moja ni

  1. Mimea 
  2. Vyakula 
  3. Matunda
  4. Mboga
  5. Miche


SEHEMU C

METHALI, NAHAU NA VITENDAWILI

26. Maneno yapi yanakamilisha methali ifuatayo kwa usahihi? Tamu ya sukari  . . . . . . . . .

  1. ikizidi inakuwa chungu 
  2. kailie kivulini
  3. si tamu ya chumvi 
  4. ajuaye mwonja
  5. ina madhara


27. Methali isemayo "kila mwamba ngoma, ngozi huvutia kwake" ina maana gani?

  1. Ngoma ikilia sana hupasuka
  2. Ngoma huwambwa kwa kutumia ngozi
  3. Bandubandu humaliza gogo
  4. Mtaka cha mvunguni sharti ainame
  5. Kila cha mtenda jambo, huvutia upande wake


28. Kibarua chake kimeota nyasi. Maana ya maneno "kuota nyasi" ni ipi?

  1. Kazi anayoifanya sasa haifai tena
  2. Wamewahamishia sehemu nyingine ya kazi
  3. Wamemtoa ofisini, sasa anafyeka majani
  4. Ameachishwa kazi
  5. Ameonewa kazini


29. Babu huanika sembe usiku, asubuhi huiondoa. Kitendawili hiki kina maana ipi?

  1. Mawingu
  2. Mwezi 
  3. Nyota
  4. Giza 
  5. Umande


30. Mtoto huyu anamlanda baba yake. "Anamlanda baba yake" ni usemi wenye maana gani?

  1. Anamkasirisha baba yake 
  2. Anamfuata baba yake
  3. Anampenda baba yake
  4. Anaongozana na baba yake
  5. Anafanana na baba yake


31. Ni kifungu kipi cha maneno hukamilisha methali ifuatayo kwa usahihi? Mtafunwa na nyoka akiona . . . . . . .

  1. jani anatimua
  2. nyasi huchomoka
  3. ung'ongo hushituka 
  4. nyoka hushtuka
  5. mtafunwa hukimbia


32. Mtoto umleavyo, ndivyo akuavyo". Methali hii ina maana sawa na methali ipi kati ya zifuatazo?

  1. Gogo halianguki mara mbili
  2. Samaki mkunje angali mbichi
  3. Mtoto akililia wembe mpe 
  4. Mtoto kwa mama hakui
  5. Mchelea mwana kulia, hulia yeye


33. Wageni walipofika nyumbani kwake aliwapokea kwa mikono miwili. "Kupokea kwa mikono miwili" ni usemi wenye maana gani?

  1. Ukarimu 
  2. Uchoyo 
  3. Upole 
  4. Kuwanyoshea mikono
  5. Kuwashika mikono


34. Akitembea huringa hata akiwa hatarini. Kitendawili hiki kina maana gani?

  1. Nyoka 
  2. Mbwa 
  3. Mbuzi 
  4. Kinyonga 
  5. Kondoo


35. Kitendawili kisemacho "wana wa mfalme ni wepesi sana kujificha" kina maana gani?

  1. Ulimi 
  2. Masikio
  3. Macho
  4. Figo 
  5. Pua


SEHEMU D

UFAHAMU

Soma kwa makini kifungu cha habari kishajibu maswali 36 — 45 kwa kuandika herufiyajibu lililo sahihi katika karatasi yakoya kujibia.

Lugha iwe ya mazungumzo au ya maandishi ni chombo cha mawasiliano. Katika mawasiliano kuna pande mbili. Chanzo na kikomo. Chanzo niyule anayeandika na kusema pamoja nayote atakayoandika au atakayosema. Kikomo ni msemaji au msikilizaji, mtu ambaye anaandikiwa au kusemeshwa. Kwa msomaji au msikilizaji inatakiwa apate maana na ujumbe muda mfupi iwezekanavyo, achague, azingatie na hatimaye aweze kuitumia katika kuyajadili maisha yanayomzunguka. Hivyo katika uwanja wa uandishi, ni wajibu wa kila mwandishi kuwafikiria wale awaandikiao.

Ni vema kuelewa kuwa tunawaandikia binadamu. Kila binadamu amezaliwa pekee na kujaliwa kukubaliana na mazingira tofauti. Katika kuwatambua wasomaji wa vitabu tutakavyoandika ni lazima kufikiria mazingira waliyo nayo, yaani vitabu vyetu vya kiada vioneshe uhalisi wa maisha ya wasomaji. Kwa maneno mengine vitabu hivyo vifikirie mahitaji na matakwa ya wasomaji wake. Ingawaje katika somo Iolote lile, maarifa na stadi zaweza kuwa zilezile kwa aina moja ya wanafunzi. Lakini kiwango na Nyanja za kutolea maudhui hayo, misimamo na tathimini zake zitatofautiana kufuatana na hali ya kisiasa, kijamii na kiuchumi ya nchi ambazo mwanafunzi huyo anaishi.

Kwa hiyo mwandishi, lazima afikirie hayo yote wakati anapotarajia kuandika kitabu cha kiada.

MASWALI

36. Pande kuu za mawasialiano ni

  1. mazungumzo na msikilizaji
  2. chanzo na kikomo
  3. anayeandika na msomaji
  4. mwandishi na msomaji
  5. waandishi na wachapishaji


37. Msomaji asomapo kitabu cha kiada azingatie nini?

  1. Kusoma kwa haraka na kukimaliza chote
  2. Kupata ujumbe na kuutafakari 
  3. Kusoma kwa muda mfupi
  4. Jina Ia kitabu na michoro 
  5. Kusoma kwa muda mrefu, apate habari yote


38. Neno "hatimae" kama lilivyotumika katika kifungu hiki lina maana sawa na neno lipi kati ya yafuatayo?

  1. Hakika 
  2. Kisha c
  3. Ili 
  4. Lakini
  5. Mwishoe


39. Katika kifungu cha habari ulichosoma maneno "uwanja wa mwandishi" yametumika kwa maana ipi?

  1. Huo ulikuwa uwanja wa mwandishi
  2. Sehemu aishiyo mwandishi
  3. Nyanja ya uandishi
  4. Eneo lililojaa vitabu
  5. Vitabu vya mwandishi


40. Wajibu mkubwa wa mwandishi ni upi?

  1. Kuandika ajuacho
  2. Kuandika jambo lenye maudhui
  3. Msomaji apate maana
  4. Kutumia taaluma yake
  5. Kuwafikiria wale awaandikiao


41. Madhumuni ya kitabu cha kiada ni muhimu kwa msomaji kwa sababu gani?

  1. Yatamsaidia kupa?a maisha mbadala
  2. Binadamu ni kiumbe mwenye ubinafsi
  3. Kwa kawaida binadamu hapendi kusoma
  4. Kila binadamu anayo mazingira yake
  5. Anachohitaji mwandishi ni maarifa na maudhui


42. Vitabu vinatakiwa vioneshe uhalisi wa msomaji. Sentensi hii ina maana gani?

  1. Vitabu viandikwe kuonesha maisha ya vijiji
  2. Vitabu viandikwe tu vile vinavyopendwa na wanafunzi
  3. Vitabu vifikirie mahitaji na matakwa ya wasomaji 
  4. Vitabu vioneshe maudhui ya wahusika wakuu
  5. Mwandishi atumie lugha inayozungumzwa kijijini


43. Mambo ambayo ni muhimu kuzingatia katika uandishi ni yapi?

  1. Hali ya siasa, uchumi na maisha ya kijamii
  2. Mila, siasa na utamaduni
  3. Hali ya kijamii
  4. Hali ya kiuchumi ya mahali husika 
  5. Desturi za wa?u na siasa


44. Kitabu cha kiada. Hiki ni kitabu gani?

  1. Kitabu cha hadithi
  2. Kitabu cha hiyari
  3. Kitabu cha msingi
  4. Kitabu chenye maudhui
  5. Kitabu cha msomaji


45. Kichwa cha habari hii kinachofaa ni kipi?

  1. Kazi ya uandishi
  2. Msomaji na mwandishi na umuhimu wao
  3. Msemaji na msikilizaji wapewe kipaumbele
  4. Uandishi wa vitabu vya hiyari E. Uandishi wa vitabu vya kiada


SEHEMU E

UTUNGAJI

Umepewa insha yenye sentensi tano (5) zilizoandikwa bila mtiririko sahihi wa mawazo. Zipange sentensi hizo ili ziwe na mtiririko wenye mantiki kwa kuzipa herufi A, B, C, D na E ili ujibu maswali 46 - 50.

46. Baada ya kusubiri kwa nusu saa, basi liliwasili na nikapanda kwenda Bunda.



47. Abiria wo?e walishuka kutoka kwenye gari moshi.



48. Lilipowasili mjini Mwaza, gari moshi lilisimama taratibu na kutangaza kuwa hapo ndipo ulikuwa mwisho wa safari yake.



49. Nami nilishuka na kwenda moja kwa moja hadi kwenye kituo cha mabasi.



50. Mimi na abiria wenzangu tulisafiri kwa amani na kufika Bunda salama jioni.



STD VII KISWAHILI NECTA EXAM OF YEAR 2006 Try This  |  

KISWAHILI 2006

SEHEMU A

SARUFI

Katika swali la 1-15 andika herufi yajibu lililo sahihi katika karatasiya kujibia.

1. Huyu ......... mtoto aliyekuwa amepotea.

  1. ndio 
  2. ndiyo 
  3. ndiye
  4. ndiyo
  5. ndivyo


2. Neno lipi ni kinyume cha neno 'Adili"? .

  1. wema 
  2. uovu 
  3. ujasiri
  4. ujanja
  5. ujinga


3. "Ala kumbe! Ameondoka leo asubuhi”. Kihisishi ni kipi kati ya maneno haya?

  1. Ala kumbe
  2. leo
  3. Ala
  4. kumbe
  5. ameondoka


4. Kisawe cha neno shaibu ni .

  1. barabara
  2. baneti
  3. buda 
  4. ajuza 
  5. kigori


5. Neno "MBWA” lina silabi ngapi?

  1. nne
  2. mbili
  3. moja 
  4. tatu 
  5. sifuri


6. Kipi kinyume cha neno aghalabu? ......

  1. mara nyingi
  2. mara kwa mara
  3. nadra
  4. muda wote
  5. kila wakati


7. Kitoto hiki kinacheza kitQtQ. Neno lililopigiwa mstari limetumika kama ...

  1. Nomino 
  2. Kitenzi 
  3. Kielezi 
  4. Kivumishi 
  5. Kielelezi


8. Shule ile imeendelea ingawa haina umeme. Sentensi hii iko katika aina ipi ya tungo?

  1. Tungo tegemezi 
  2. Tungo sahihi
  3. Tungo shurutia 
  4. Tungo ambatano 
  5. Tungo huria


9. Sikuweza kutambua ni nani amelala kitandani kwa sababu alijifunika shuka  . . . . . . .

  1. Lote 
  2. Gubigubi
  3. Zima
  4. Nzima 
  5. Zama


10.Neno "Vibaya” katika sentensi isemayo "Vibaya pia vinanunuliwa” limetumika kama aina ipi ya maneno?

  1. Kivumishi 
  2. Kiwakilishi 
  3. Kielezi
  4. Kisifa 
  5. Nomino


11. Mkutano kati ya Viongozi wa DECI na Serikali ulikuwa haujapatiwaNeno lipi linalokamilisha sentensi hii?

  1. Uchunguzi 
  2. Ufumbuzi 
  3. Ufunguzi
  4. Kutendwa
  5. Kutendea


12. 'Salama na Samina wanapendana sana". Sentensi hii ipo katika kauli ipi?

  1. Kutendwa 
  2. Kutendana 
  3. Kutenda
  4. Kutendwa 
  5. Kutendea


13. Katika neno "tutakuja” kiambishi cha wakati ni .........

  1. tu- 
  2. -ku 
  3. -ja-
  4. u
  5. -ta-


14. Neno ”MWALIMU” lipo katika upatanisho wa ngeli ya aina gani?

  1. A-WA
  2. I-ZI
  3. LI-YA 
  4. U-YA
  5. U-ZI


15. Wingi wa sentensi ifuatayo ni ipi? mti huu unaharibu mazingira

  1. Miti hizi zinaharibu mazingira
  2. Miti hiyo inaharibu mazingira
  3. Miti hii itaharibu mazingira
  4. Miti hii inaharibu mazingira
  5. Miti hii imeharibu mazingira


SEHEMU B

MSAMIATI

16. Mzee Mwendapole aliwapa wanaemawaidha juu ya maisha ya baadaye. Neno lililopigiwa mstari lina maana gani?

  1. Hotuba 
  2. Maonyo 
  3. Urithi
  4. Mawazo 
  5. Mahubiri


17. Neno lenye maana sawa na "mawio” ni lipi kati ya yafuatayo?

  1. Asubuhi 
  2. Maonyo
  3. Mawazo
  4. Urithi
  5. Mahubiri


18. Mwl. Juma alinunua shati dukani. Neno lililopigiwa mstari lilmetumika kama aina gani ya maneno?

  1. Kivumishi 
  2. Kiwakilishi
  3. Kielezi 
  4. Kihisishi


19. Mtu anayesimamia kazi za shambani anaitwaje?

  1. Kiongozi 
  2. Msimamizi
  3. Mkuu
  4. Nokoa 
  5. Mnyapara


20. Jina analotumia mjomba kumwita mtoto wa dada yake ni:

  1. Mtoto 
  2. Mjomba
  3. Binamu
  4. Shangazi 
  5. Mpwa


21. Kipindi cha muda wa mika mia huitwaje? .

  1. Milenia
  2. Karne
  3. Muongo
  4. Jubilei


22. Kutembea kwa matao ni kutembea kwa .........

  1. Kukimbia
  2. Kejeli
  3. Maringo
  4. Kurukaruka
  5. Kutambaa


23. Nimetumwa ujumbe lakini sijapata mwitiko wowote. Neno mwitiko lina maana sawa na

  1. utata 
  2. mwaliko
  3. mwangwi 
  4. mwito 
  5. jibu


24. Maelezo gani kati ya haya yanatoa maana ya neno "Mseja .

  1. Mwanaume aliyefiwa 
  2. Mtu anayetunza vitabu
  3. Mtu anayewinda Wanyama 
  4. Mwanamke aliyefiwa 
  5. Mtu ambaye hajaoa au kuolewa


25. Neno lipi linakamilisha sentensi isemayo, "Anapenda kukaa bure ......... ana nguvu nyingi?".

  1. Pamoja 
  2. Japokuwa 
  3. Ujasiri
  4. Hekima 
  5. Uangalifu


SEHEMU C

METHALI, NARAU NA VITENDAWILI

26. Moja kati ya Methali zifuatazo haihimizi watu kujiendeleza kielimu. Methali hiyo ni ipi?

  1. Kuuliza si ujinga
  2. Kuishi kwingi kuona mengi
  3. Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki
  4. Elimu ni bahari
  5. Penye nia pana njia


27. Kinyume cha nahau "Kata tamaa ni

  1. Pata chungu
  2. Ona fahari
  3. Kufa moyo
  4. Kata maini 
  5. Tia moyo


28. Ana mkono wa birika

  1. mchoyo
  2. ameshika birika
  3. kaumia
  4. mwizi
  5. kujikunja


29. Kitendawili kipi kati ya hivi jibu lake siyo kinyonga?

  1. Huuawa na uzazi wake
  2. Tajiri wa rangi
  3. Tajiri wa macho
  4. Napigwa faini kosa silijui
  5. Ajihami bila silaha


30. ”Chungu cha mwitu hakipikiwi wapishi wake wakaiva” jibu la kitendawili hiki ni ... ... ...

  1. Mafuta na chungu 
  2. Moshi na moto
  3. Mzinga wa nyuki 
  4. Tumbo na njaa
  5. Meno na ulimi


31. "Mtu akifanya kazi yake bila umakini mambo hayatakuwa mazuri, itamlazimu apokee matokeo mabaya ya mambo hayo". Maelezo hayo ni sawa na maana ya methali isemayo

  1. Lila na fila havitantagamani 
  2. Akiba haiozi
  3. Dunia tambara bovu 
  4. Mpanda ovyo hula ovyo 
  5. Mganga hajigangi


32. Kifungu kipi kinafaa kumalizia methali? Jina jema .........

  1. Hutambulika toka mwanzo 
  2. Hupumbaza watu
  3. Hung'aa gizani 
  4. Hupendwa na watu wengi
  5. Wengi huwa matajiri


33. Nini maanaya Nahau "Ku iga chuku"

  1. Kujivuna 
  2. Kupiga moyo
  3. Kurandaranda 
  4. Kuanguka 
  5. Kutia chumvi


34. Tegua kitendawiYhiki. Nina kitand changu cha Mkangashale mwana wa halali aende akalale:

  1. Mvua 
  2. Maji 
  3. Bahari 
  4. Nyumba 
  5. Jua


35. Walipofika mahakami kusikiliza kesi-ya ufisadi walitulia sana ili wasikie vizuri na kuelewa zaidi. Maneno yaliyopogiwa mstari yanawakilisha nahau isemayo:

  1. Unga mkono 
  2. Kodoa macho 
  3. Tia fora
  4. Tega sikio 
  5. Pigwa na butwaa


37. Mstari wa pili katika kila ubeti wa kwanza una jumla ya mizani

  1. 8
  2. 14
  3. 16
  4. 17
  5. 19


38. Mstari wa nne katika kila ubeti wa shairi huitwa:

  1. Mizani 
  2. Vina 
  3. Silabi 
  4. Urari
  5. Kituo


39. Katika ubeti.wa pili Msanii anasema "Waliosoma vyuoni, hawachoki kuuliza." Maneno haya yanatuaSä kuwa .

  1. Tusihangaike kujifunza yale tusiyoyajua
  2. Waliosoma vyuoni wanauliza maswali mengi
  3.  Wanaotakiwa kujifunza ni wale wasiosoma vyuoni
  4. Tujifunze yale tusiyoyajua
  5. Kujifunza vyuoni inatosheleza kuliko kuuliza maswali


40. Neno "adhiri" kama lilivyotumiwa na mtunzi lina maana ya .

  1. Kuolewa
  2. Aibishi
  3. Ugonjwa wa Figo
  4. Ujuzi
  5. Thamini


41. Neno "Misuli" katika ubeti wa tatu lina maana ya:

  1. Nguo zivaliwazo na wanaume
  2. Mishipa midogo ndani ya mwili
  3. Nyuzi za nyama ndani ya mwili
  4. Nyuzi za upasuaji watumiazo madaktari 
  5. Masomo ya udaktari


42. Katika ubeti wa tatu tunajifunza kuwa ni aibu ..

  1. Mtu kushindwa kufanya jambo fulani
  2. Nahodha ndani ya mwili
  3. Nahodha kushidwa kuendesha ndege
  4. Kufikiria kuwa anajua kila kitu
  5. Walioko vyuoni kuuliza maswali


43. Jambo muhimu linalozungumzwa na msanii katika shairi hili ni:

  1. Udaktari
  2. Elimu
  3. Kazi ya Urubani
  4. Aibu kujifunza unajua
  5. Aibu kujifanya unajua


44. "EIimu pana ajabu” maneno haya yana maana kuwa elimu

  1. Ina maajabu
  2. Ina mwisho wa maajabu
  3. Ina upana lakini haina urefu
  4. Haina mwisho
  5. Haina maana kama aliyesoma haajiriwi


45. Pendekeza kichwa cha habari cha shairi kutoka katika nahau hizi:

  1. Elimu kwa wote
  2. Elimu na bahari
  3. Elimu ndio uti wa mgongo
  4. Elimu ni ufunguo wa maisha
  5. Elimu ni usiasa


SEHEMU E

UTUNGAJI

Panga sentensi hizi Ili ziwe na mtiririko wenye mantiki kwa kuzipa herufi A, B, C, D na E ili ujibu maswali 46 - 50.

46. Anko alikuwa ndiye aliyetawala ukoo ule kwa muda mrefu kuliko viongozi wengine waliopita. [   ]



47. Ukoo huo ulikuwa na mjamii wapatao elfu moja na mia tano hivi wote wakiongozwa na mjamii Mzee aliyeitwa Anko. [   ]



48. Kutokana na uongozi wake mzuri. mara tatu alipotaka kujiuzulu, mjamii wenzake walimkatalia ?sijiuzulu. [   ]



49. Ukoo mkubwa wa mjamii ulikuwa ukiishi katika msitu mmoja karibu na kijiji cha Namtumbo mkoani Ruvuma. [   ]



50. Anko alikuwa Mzee kuliko mjamii wote wa ukoo wake. [   ]



STD VII KISWAHILI NECTA EXAM OF YEAR 2005 Try This  |  

KISWAHILI 2005

SEHEMU A

SARUFI

Katika swali 1 - 15 andika herufiyajibu lililo sahihi katika karatasiyakoya kujibia

1. Sudi na Celina "wanapigana". Neno lililopigiwa mstari liko katika kauli ipi?

  1. Kutendwa 
  2. Kutendana 
  3. Kutendewa
  4. Kutendea 
  5. Kutendeana


2. Kamilisha sentensi ifuatayo kwa kutumia neno moja kati ya uliyopewa: "Ingawa walipata shida nyingi njiani . walifika salama

  1. hatimaye 
  2. ingawa
  3. ingawaje
  4. hivyo 
  5. hatima


3. Sentensi isemayo, . Jumatatu tulipoanza mtihani" inakamilishwa kwa usahihi na neno lipi kati ya yafuatayo?

  1. Itakuwa 
  2. Ilikuwa
  3. Ifikapo
  4. Ifikiapo 
  5. Ilikuwepo


4. Neno haiba lina maana sawa na neno lipi kati ya haya yafuatayo?

  1. Urembo wa mavazi 
  2. Urembo wa sura
  3. Mwenendo mwema 
  4. Amani na utulivu
  5. Uzuri na majivuno


5. Tumia neno mojawapo kati ya haya yafuatayo ili ukamilishe sentensi isemayo "Tukitaka kupata mazao mengi ......... tutumie mbolea".

  1. ni budi 
  2. si budi 
  3. tuna budi
  4. budi. 
  5. hatuna budi


6. Ni neno lipi linalokamilisha sentensi isemayo "Kiranja wetu wa darasa alikwenda dukani  . . . . . . . alikatazwa na mwalimu"?

  1. ila
  2. lakini 
  3. ingawa
  4. iwapo 
  5. isipokuwa


7. "Kitabu ulichonipa kina kurasa chache". Katika sentensi hii maneno yaliyokolezwa wino yanawakilisha nini?

  1. Kishazi kitegemezi
  2. Kishazi huru
  3. Kishazi ambatano
  4. Kirai
  5. Kielezi


8. "Kobe anatembea taratibu". Neno "taratibu" ni aina ipi ya maneno?

  1. Kivumishi 
  2. Nomino
  3. Kishazi ambatano 
  4. Kielezi
  5. Kihusishi


9. Neno "vibaya" katika sentensi isemayo "vibaya pia vimenunuliwa" limetumika kama aina ipi ya maneno?

  1. Kivumishi 
  2. Nomino 
  3. Kiwakilishi
  4. Kielezi 
  5. Kisifa


10. Katika sentensi: "Mama anaendesha gari," herufi a-katika neno anaendesha inawakilisha kiambishi cha aina ipi?

  1. Tendo 
  2. Rejeshi 
  3. Tamati
  4. Wakati 
  5. Nafsi


11. Neno shule limetolewa kutoka katika lugha ipi?

  1. Kijerumani 
  2. Kihindi
  3. Kireno
  4. Kiingereza 
  5. Kiarabu


12. Sentensi isemayo "Shangazi mkubwa alikuwa analima shambani" ni aina ipi ya sentensi?

  1. Ambatano 
  2. Sahili 
  3. Shurutia 
  4. Changamano 
  5. Ambatano — sahili


13. Kinyume cha neno adimu ni kipi?

  1. haba 
  2. ghali 
  3. tele 
  4. rahisi 
  5. potea


14. Sentensi isemayo "Ukinisaidia nitakusadia" ni aina ipi ya sentesi?

  1. Changamano
  2. Sahili
  3. Ambatano
  4. Shurutia
  5. Mseto


15. "Huyu si ndugu yangu". Katika sentensi hii, neno si ni aina ipi ya maneno?

  1. Kitenzi kikuu 
  2. Kielezi jinsi 
  3. Kitenzi kisaidizi
  4. Kitenzi jina 
  5. Kielezi kivumishi


SEHEMU B

MSAMIATI

Katika swali 16 — 25 andika herufi yajibu lililo sahihi katika karatasi yakoya kujibia.

16. Mahali panapochimbwa madini panaitwaje?

  1. Mgodini 
  2. Shimoni 
  3. Mererani
  4. Porini 
  5. Madinini


17. "Furaha alishikwa na fadhaa alipobaini ameuziwa mali ya wizi" Neno ' fadhaa" katika sentensi hii lina maana ipi?

  1. Aibu 
  2. Mshangao 
  3. Hofu
  4. Ghadhabu 
  5. Chuki


18. Ni kiumbe kipi kisichokuwa na uhusiano baina ya hivi vifuatavyo?

  1. Ngamia 
  2. Ng'ombe 
  3. Punda
  4. Mbuzi 
  5. Nyumbu


19. Neno "tamati" lina maana sawa na neno lipi?

  1. Pembeni
  2. Katikati
  3. Mwisho
  4. Mwanzo
  5. Chanzo


20. Kinyume cha neno tapanya ni kipi?

  1. Sambaza
  2. Tawanya
  3. Kusanya
  4. Eneza 
  5. Ongeza


21. "Seremala alinihadaa aliponiambia angenipa kabati juzi". Neno alinihadaa limetumika kwa maana ipi?

  1. Alinisingizia
  2. Alinidanganya
  3. Aliniahidi 
  4. Alinizawadia
  5. Alinikejeli


22, "Matona alioa msichana wa hirimu yake." Neno "hirimu" lina maana ipi katika sentensi hii?

  1. Nasaba
  2. Rika
  3. Kabila 
  4. Jinsi 
  5. Dini


23.Kinyume cha nuka ni kipi?

  1. Nukia
  2. Nukanuka
  3. Harufu
  4. Uozo
  5. Fukiza


24. Kifungu cha maneno chenye maana sawa na samani ni kipi?

  1. Kabati, saa, kiti, radio
  2. Meza, kisu, kiti, kiatu
  3. Kigoda, kisu, kitu, kiatu
  4. Kapu, kiti, kabati, kasha
  5. Kiti, meza, kitanda, kabati.


25. Kinyume cha neno okota ni kipi?

  1. Dokoa
  2. Gusa 
  3. Dondosha
  4. Nyakua
  5. Daka


SEHEMU C

METHALI, NAHAU NA VITENDAWILI

Katika maswali 26 - 35 chaguajibu lililo sahihi kwa kuandika herufiyake katika karatasiyakoya kujibia. Kwa swali la 35 andikajibu kwa NENO moja tu.

26. Methali isemayo "jifya moja haliinjiki chungu" ina maana ipi?

  1. Joka likujualo halikuli likakwisha
  2. Watu huzaliwa wawili wawili
  3. Wingi sio hoja
  4. Kibaya chajitembeza; chema chajiuza 
  5. Umoja ni nguvu; utengano ni udhaifu


28.Methali isemayo "Ukipewa shubiri usichukue pima" ina maana ipi?

  1. Mpishi 
  2. Mgema 
  3. Muuza
  4. Mkwezi 
  5. Mlevi


29.Methali inayofanana na methali isemayo "Ajali haina kinga” ni ipi?

  1. Tahadhari kabla ya hatari 
  2. Maji ya kifuu bahari ya chungu
  3. Furaha mbele mauti nyuma 
  4. La kuvunda halina ubani 
  5. Mwenda tezi na omo marejeo ni mgamani


30."Mzigo wa mwenzio ni ... ... ...” ni methali inayokamilishwa na sehemu ipi kati hizi zifuatazo?

  1. Kanda la sufi 
  2. Kasha la sufi 
  3. Ganda la sufi 
  4. Godoro la sufi 
  5. Gunia la sufi


31."Kazi ya Daudi ni ya kijungujiko”. Kazi ya kijungujiko ni kazi ya aina ipi?

  1. Kazi ya kutengeneza meko
  2. Kazi ya upishi 
  3. Kazi ya kutosha mahitaji ya m?o tu 
  4. Kazi ya sulubu 
  5. Kazi rahisi


32.M?u asemapo 'Ashakum si matusi” ana maana ipi?

  1. Nayatamka haya na wala si matusi
  2. Yafuatayo ndiyo matusi kwangu
  3. Yafuatayo siyo matusi kwangu
  4. Niwie radhi kwa haya ninayotamka 
  5. Nakutukana lakini usikasirike


33.Katika kilimo cha pareto mkoa wetu umetia fora. "Umetia fora" maana yake ni ipi?

  1. Umefurahi sana 
  2. Umefanikiwa kiasi kikubwa
  3. Umeanguka mno 
  4. Umetia aibu
  5. Umekuwa wa nyuma sana


34.Kitendawili kisemacho "Babu apiga mbizi; akiibuka ndevu zimekuwa nyeupe” huteguliwa kwa jibu lipi?

  1. Mwiba 
  2. Mwiko 
  3. Mkono 
  4. Taa 
  5. Nyota


SEHEMU D

UFAHAMU

Soma kwa makini kifungu cha habari kifuatacho kishajibu maswali 36 - 45 kwa kuandika herufi ya jibu lililo sahihi katika karatasiyakoya kujibia.

Mpendwa Shangazi, 

Shikamoo.

Asante sana kwa kututhibitishia kwamba ndugu Yangu, binti yako Sekelo, ataolewa tarehe 10 Oktoba 2005 huko mjini. Tarehe hiyo, hasa kwa mimi, ni nzuri sana kwani sitakuwa na pingamizi la kuhudhuria kwani nitakuwa nimemaliza kufanya mtihani wangu. Naingoja siku hiyo kwa shauku kubwa ili nimwone Sekero akiwa amevaa shela kama ishara ya kuingia katika hatua ya utu-uzima.

Shangazi, baba anasikitika sana kwa kukosa kuhudhuria kwenye harusi ya mpwawe. Hivi sasa mzee Musa hajiwezi kutokana na nyonda ya shinikizo la damu tangu pale alipoibiwa ng'ombe wake sita wa maziwa. Hata hivyo, mimi na mama tutakuja. Kwa vile tutakuwa na mizigo mingi, tunaomba watu watatu waje kwenye kituo cha mabasi watupokee siku tatu kabla ya tarehe harusi.

Huku nyumbani mwaka huu hakukuwa na masika ya kutosha, mazao mengi yamenyauka mashambani. Watu wengi wameanza kukata tamaa kwa jinsi njaa inavyonyemelea bila kuikaribisha. Kwa upande mwingine, ukame umeleta neema kwa baadhi ya watu. Huwezi kuamini shangazi, mbuzi sasa anauzwa kwa shilingi elfu tatu! Watu wanafanya hivyo ili wapate pesa za kununulia chakula. Sisi tumepata bahati ya kuwa na shamba la bonde. Ndiyo maana tuna chakula cha kutosha hata cha watu watakaokuwa harusini.

Shangazi, nisalimie sana Sekelo na mdogo Wake, Rehema. Mungu akipenda tutaonana ili nije niwape visa vya Tongoni ya sasa; siyo ile waliyoiacha miaka saba iliyopita. Tongoni sasa kumekucha!

Wasalaam,

Mwanao,

Hawa

MASWALI

36. Barua uliyoisoma hapo juu ni:

  1. taarifa ya harusi ya Sekelo
  2. jibu la taarifa ya harusi ya Sekelo
  3. ya mwaliko wa harusi ya Sekelo
  4. taarifa ya matatizo ya Mzee Musa 
  5. taarifa ya janga kijijini Tongoni


37. Anayeolewa tarehe 10/10/2005 ana uhusiano upi na mwandishi wa barua hii?

  1. Mwanakijiji mwenzake 
  2. Jirani yake
  3. Rafiki yake 
  4. Shangazi yake 
  5. Binadamu


38. Maradhi ya Mzee Musa yametokana na sababu ipi?

  1. Msituko wa kuibiwa ng'ombe sita wa maziwa
  2. Majeraha aliyoyapata kutoka kwa wezi
  3. Hali ya hewa iliyonyausha mazao shambani
  4. Msituko wa moyo kutokana na janga la njaa
  5. Msituko wa moyo kwa kuuza mbuzi kwa bei duni


39. Neno "nyonda" kwa mujibu wa barua hii lina maana ipi?

  1. Kukonda sana 
  2. Shinikizo la damu
  3. Maradhi
  4. Unyonge 
  5. Kid onda


40. Ni tarehe ipi ya mwezi Oktoba 2005 ambayo Hawa na mama yake watawasili Tongoni?

  1. 6
  2. 8
  3. 13
  4. 7
  5. 14


41. Hawa na mama yake watakwenda kijijini na mizigo mingi kwa sababu ipi?

  1. Nguo za bibi harusi 
  2. Mazao ya biashara
  3. Chakula cha harusini 
  4. Nyama kwa ajili ya kitoweo
  5. Bidhaa za maonesho harusini


42. Kwa nini mwandishi anasema . njaa inavyowanyemelea bila kuikaribisha”?

  1. Juhudi ya kulima imefanywa ila ukame umewaathiri
  2. Juhudi ya kulima imefanywa lakini masika yamewaathiri
  3. Wananchi hawakulima kwa utaalamu 
  4. Wananchi wamekata tama
  5. Mvua za masika hazikunyesha kabisa


43. Methali inayoeleza hali ya ukame na matokeo yake ni ipi?

  1. Mchagua jembe si mkulima 
  2. Hakuna masika yasiyokuwa na mbu
  3. Mtangatanga na jua hujua 
  4. Mgaagaa na upwa hali wali mkavu 
  5. Kufa kufaana


44. Kwa nini familia ya Mzee Musa haikuathirika kwa njaa?

  1. Walikuwa na fedha ya kununulia chakula
  2. Mazao yao yalihimili ukame
  3. Ni wakulima hodari
  4. Wana shamba kubwa 
  5. Wana shamba la bonde


45. Hawa ana maana ipi asemapo ”Tongoni sasa kumekucha”?

  1. Watu wa Tongoni sasa wajanja
  2. Tongoni ya sasa ina maendeleo
  3. Watu wa Tongoni sasa hawana tongotongo 
  4. Tongoni sasa kuna njaa
  5. Tongoni ya sasa ni duni.


SEHEMU E

UTUNCAJI

Umepewa insha yenye sentensi tano (5) zilizoandikwa bila mtiririko sahihi wa mawazo. Zipange sentensi hizo ili ziwe na mtririko wenye mantinki kwa kuzipa herufi A, B, C, D na E ili ujibu maswali 46-50.

46. ”Tusipopanda misitu mipya tutaishiwa na miti kabisa.” Bwana Miti alijibu.



47. Alipomaliza kusema hayo, Mzee Komba akauliza: ”Kwa nini tupande miti ilihali inaota kwa uwezo wa Mungu?”



48. Bwana Miti akajibu tena, ”Yatupasa kupanda miti kwa sababu matumizi yake yameongezeka sana siku hizi.”



49. Mkutano ulipomalizika, kila mtu alirejea nyumbani kwake, akiwa na dhamiri ya kupanda miti.



50.  "Tena tutafanana na mtu anayekula chakula chote alichonacho kabla ya kuzalisha kingine". Bwana Miti alihitimisha.



Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256

   Click Here To Access You Scheme(ONLY IF YOU A HAVE CODE)