STD VII KISWAHILI ONLINE SELF NECTA TEST FOR YEAR 2021
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI
01 KISWAHILI
Muda: Saa 1:40 Mwaka: 2021
Maelekezo
l . Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali arobaini na tano (45).
2. Jibu maswali yote katika kila sehemu.
3. Soma maelekezo yote yaliyoko katika fomu maalum ya kujibia (OMR).
4. Jaza taarifa zote katika fomu ya OMR.
5. Andika Namba yako ya Mtihani kisha weka kivuli kwenye tarakimu za namba hiyo mahali panapohusika kwenye karatasi yako ya kujibia.
6. Weka kivuli kwenye herufi ya jibu lililo sahihi kwa swali 1 — 40. Kwa mfano, kama jibu sahihi ni A weka kivuli kama ifuatavyo:
7. Ukigundua kuwa herufi uliyowekea kivuli si jibu sahihi futa kivuli hicho kwa umakini kwa kutumia kifutio safi kabla ya kuweka kivuli katika herufi mpya.
8. Tumia penseli ya HB tu katika kujibu swali la 1— 40; na kalamu ya Wino wa bluu au mweusi kwa swali la 41 hadi 45.
9. Simu za mkononi na Vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi ndani ya chumba cha mtihani.
SEHEMU A (Alama 35)
Sikiliza kwa makini hadithi utakayosomewa na msimamizi, kisha jibu swali la 1 - 5, kwa kuweka katika herufi ya jibu lililo sahihi katika fomu yako ya kujibia.
Bofya Hapa Kusikiliza Hadithi
Maswali
1. Malkia wa nyuki alikuwa analindwa na nani?
Vibaraka
Askari hodari
Wanakijiji
Nyuki Hohehahe
Wafanyakazi.
Chagua Jibu
2. Ni kitu gani ambacho malkia wa nyuki hakukipenda?
Wanakijiji hohehahe
Mafundi wa masega
Ushirikiano wa nyuki
Vibaraka wa malkia
Kuwalipa vibarua
Chagua Jibu
3. Nani alijishughulisha kutafuta nekta kwenye maua?
Nyaki wote
Vibarua
Wafanyakazi
Vibaraka
Wanakijiji
Chagua Jibu
4. Utajiri katika kijiji cha nyuki ulitokana na nini?
Kuuza asali
Kuuza nta
Kuuza masega
Kuuza maua
Kuuza mizinga
Chagua Jibu
5. Nani walitumika kupeleka habari mbalimbali katika vijiji vya jirani?
Vibarua
Wafanyakazi
Vibaraka
Wanakijiji
Nyuki
Chagua Jibu
Katika swali la 6 - 35, weka kivuli katika herufi ya jibu lililo sahihi katika fomu yako ya kujibia.
6. Wanakijiji walifanya juu Chini ili kuleta maendeleo katika kijiji Chao. Nahau "fanya juu chini" inafafanuliwa na kifungu kipi cha maneno kati ya vifuatavyo?
Walijitahidi kwa kila njia.
Walishirikiana kwa pamoja.
Walijituma kwa ujasiri.
Walijituma kwa uzalendo.
Walitumia nguvu.
Chagua Jibu
7. Nahau ipi yenye maana ya "kunywa pombe?"
Piga mbizi
Piga chenga
Piga yowe
Piga soga
Piga maji
Chagua Jibu
8. Katika sentensi "Dada alimwambia kuwa atakapopata muda atakuja nyumbani ," mzungumzaji ametumia nafsi gani kati ya hizi?
Nafsi ya pili wingi
Nafsi ya tatu wingi
Nafsi ya tatu umoja
Nafsi ya pili umoja
Nafsi ya kwanza wingi
Chagua Jibu
6. "Sisi ni wanafunzi hodari wa somo la kiswahili". Kauli hiyo inawakilisha nafsi ipi kati ya hizi zifuatazo?
Nafsi ya kwanza umoja
Nafsi ya tatu wingi
Nafsi ya tatu umoja
Nafsi ya kwanza wingi
Nafsi ya pili wingi
Chagua Jibu
10. Daktati alisema kwamba mgojwa wetu amepata ahueni" Hiyo ni aina gani ya kauli kati ya zifuatazo?
Tata
Mazoea
Halisi
Taarifa
Kutenda
Chagua Jibu
11. Masumbuko aliwaambia kuwa, hataingia darasani tena. Kauli halisi ya sentesi hii ni ipi kati ya zifuatazo??
12. "Nyamante alikata shauri na kuwaambia wenzake, kweli elimu ndiyo mkombozi wa mtoto wa kike." Nahau "kata shauri" katika sentensi hii ina maana ipi kati ya zifuatazo?
Kuamua
Kuwatahadharisha
Kuwaasa
Kuonya
Kufundisha
Chagua Jibu
13. Chekacheka anapenda watoto wake wawe na tabia njema hadi ukubwani. Methali ipi kati ya zifuatazo inahimiza tabia ya aina hiyo?
Zimwi likujualo halikuli likakwisha.
Asiyesikia la mkuu huvujika guu.
Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.
Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu.
Tabia hupamba kuliko libasi.
Chagua Jibu
14. "Nikitembea walio wafu huamka na walio hai hukaa kimya." Jibu la kitendawili hiki ni lipi kati ya yafuatayo?
Nyuki ndani na nje ya mzinga
Yai na kifaranga chake
Majani makavu na mabichi
Kulala usingizi na kuamka
Tumbo na chakula
Chagua Jibu
15, Ni methali ipi kati ya zifuatazo inamaana sawa na methali "akufaaye kwa dhiki ndio rafiki"?
Baniani mbaya kiatu chake dawa,
Damu nzito kuliko maji,
Undugu kufaana si kufanana,
Shukrnni ya punda njateke,
Sikio la kufa halisikii dawa,
Chagua Jibu
16. Neno lipi kati ya yafuatayo ni jumuishi kwa maneno haya "nyanya, vitunguu, pilipili na tangawizi'?"
Nafaka
Matunda
Vinywaji
Vitoweo
Viungo
Chagua Jibu
17. Mwaka 1985 Mwalimu Julius Kambaragc Nyerere aliamua kung'atuka madarakaní na kumwachia Mheshimiwa, Ali Hassan Mwinyi, Kitcndo cha Mwalimu Julias Kambarage Nyerere kung'atuka kinamaanisha nini?
Kuaga wafanyakazi
Kuwaachia wafanyakazí
Kustaafu kazi
Kujiuzulu madaraka
Kupumzika kazi kidogo
Chagua Jibu
18. Neno lipi kati ya yafuatayo ni jumuishi kwa maneno haya "almasí, dhahabu, Tanzanaiti na lulu" ?
Shaba
Vyuma
Marumaru
Mgodi
Madini
Chagua Jibu
19. Katika neno "ninakula" kiambishi cha wakati uliopo ni kipi kati ya vifuatavyo?
-ni-
-ku-
-na-
-la-
-kul-
Chagua Jibu
20. "Muda ulipowadia wanafunzi wote tulisimama foleni.' Neno "wadia" linashabihiana na neno lipi kati ya yafuatayo?