|
---|
1. Aanguaye huanguliwa. |
2. Asiye sikia la mkuu, huvunjika guu. |
3. Abebwaye hujikaza. |
4. Adhabu ya kaburi aijuae maiti. |
5. Adui aangukapo, mnyanyue. |
6. Adui mpende. |
7. Adui wa mtu ni mtu. |
8. Afadhali ya Musa kuliko ya Firauna. |
9. Ahadi ni deni. |
10. Ajidhaniaye amesimama, aangalie asianguke. |
11. Akiba haiozi. |
12. Akili ni mali. |
13. Akili ni nywele kila mtu ana zake. |
14. Akili nyingi huondowa maarifa. |
15. Akutukanae hakuchagulii tusi. |
16. Akipenda chongo huita kengeza. |
17. Akufaae kwa dhiki, ndiye rafiki. |
18. Akufanyiaye ubaya, mlipe wema. |
19. Akupaye kisogo si mwenzio. |
20. Akutendaye mtende, mche asiyekutenda. |
21. Alisifuye jua, limeuangaza. |
22. Aliye juu msubiri chini. |
23. Aliye kando, haangukiwi na mti. |
24. Aliye kupa wewe kiti (kibao) ndiye aliye nipa mimi kumbi. |
25. Aliye kutwika, ndiye atakaye kutua. |
26. Akufukuzae hakwambii toka. |
27. Aliyekupa mkeka ndiye aliyenipa kumbesa. |
28. Amani haipatikani mpaka kwa ncha ya upanga. |
29. Ana hasira za mkizi. |
30. Anayekuja pasi na hodi, huondoka bila ya kuaga. |
31. Angurumapo simba, mcheza ni nani? |
32. Aninyimaye mbazi kanipunguzia mashuzi. |
33. Apewaye ndiye aongezwaye. |
34. Anaejipiga mwenyewe, halii. |
35. Asifuye mvuwa imemnyea. |
36. Asiye kubali kushindwa si mshindani. |
37. Asiye kujua, hakuthamini. |
38. Asiye kuwapo na lake halipo. |
39. Asiye lelewa na mamae hulelewa na ulimwengu. |
40. Asiye na mengi, ana machache. |
41. Asiye uliza, hanalo ajifunzalo. |
42. Asiyejua maana, haambiwi maana. |
43. Atangaye na jua hujuwa. |
44. Atangazaye mirimo, si mwana wa ruwari (Liwali). |
45. Atekaye maji mtoni hatukani mamba. |
46. Avumaye baharini papa kumbe wengi wapo. |
47. Baada ya dhiki faraja. |
48. Bahari hailindwi. |
49. Bamba na waume ni bamba, hakuna bamba la mume. |
50. Bandu bandu huisha gogo. |
51. Baniani mbaya, kiatu chake dawa. |
52. Bendera hufuata upepo. |
53. Biashara asubuhi. |
54. Bilisi wa mtu ni mtu. |
55. Bora kinga kuliko tiba. |
56. Bora lawama kuliko fedheha. |
57. Bora mchawi kuliko fitina. |
58. Biashara asubuhi. |
59. Bora nusu shari kuliko shari kamili. |
60. Bwawa limeingia ruba. |
61. Cha mtu mavi. |
62. Chaka la samba, halilali nguruwe. |
63. Chamlevi huliwa na mgema. |
64. Chanda chema huvikwa pete. |
65. Chelewa chelewa, utakuta mtoto si wako. |
66. Choko mchokoe pweza, binaadamu hutomuweza. |
67. Chombo cha kuzama hakina usukani. |
68. Chovya - chovya yamaliza buyu la asali. |
69. Chui hakumbatiwi. |
70. Chururu si ndo ndo ndo. |
71. Dalili ya mvua mawingu. |
72. Damu nzito kuliko maji. |
73. Daraja livuke ulifikapo. |
74. Dawa ya moto ni moto. |
75. Daraja ukilibomoa, ujue kuogelea. |
76. Dau la mnyonge haliendi joshi, likienda joshi ni matakwa ya Mungu. |
77. Dawa ya moto ni moto. |
78. Donda ndugu halina dawa. |
79. Dua ya kuku haimpati mwewe. |
80. Fadhila huna, hata hisani hukumbuki? |
81. Fadhila ya nyuki ni moto. |
82. Fadhila ya punda ni mateke (mashuz) |
83. Fahari ya macho haifilisi duka. |
84. Farasi hamuwawezi, tembo mtawalishani? |
85. Fata nyuki ule asali. |
86. Fimbo ya mbali haiui nyoka. |
87. Fumbo mfumbe mjinga, mwerevu huligangua. |
88. Funika kombe mwanakharamu apite. |
89. Ganda la mua la jana, chungu kaona kivuno. |
90. Gome la udi, si la mnuka uvundo. |
91. Haba na haba, hujaza kibaba. |
92. Haki ya mtu hailiki. |
93. Hakuna masika yaso mbu. |
94. Hakuna msiba usio na mwenziwe. |
95. Hakuna siri ya watu wawili. |
96. Hakuna ziada mbovu. |
97. Hala hala mti na macho. |
98. Hamadi ni ilio kibindoni, na silaha ni iliyo mkononi. |
99. Hapana marefu yasio na mwisho. |
100. Haraka haraka haina baraka. |
101. haraka haraka haina baraka. |
102. Haramu yako halali kwa mwenzio. |
103. Hasidi hasada. |
104. Hasidi mbaya. |
105. Hasira, hasara. |
106. Hatua ndefu hufupisha mwendo. |
107. Hauchi hauchi, unakucha. |
108. Hayawi hayawi, mara huwa. |
109. Heri kufa macho kuliko kufa moyo. |
110. Heri kujikwa kidole kuliko ulimi. |
111. Heri nitakula na nini?, kuliko nitakula nini? |
112. Heri ya marama kuliko kuzama. |
113. Hiari ya shinda utumwa. |
114. Hogo halihogoki mpaka kwa hogo jenziwe. |
115. Hucheka kovu asiye kuwa na jeraha. |
116. Ila ya kikwapa, kunuka pasipo kidonda. |
117. Yaliyoopita si ndwele, ganga yajayo. |
118. Iliyo jaa ndiyo ipunguzwayo. |
119. Imara ya jembe kaingojee shambani. |
120. Jambo usilolijua, usiku wa giza. |
121. Jina jema hungara gizani. |
122. Jini likujualo halikuli likakwisha. |
123. Jino la pembe si dawa ya pengo. |
124. Jitihada haiondoi kudura. |
125. Jitihadi haiondoi kudura. |
126. Jogoo la shamba haliwiki mjini. |
127. Jungu kuu, halikosi ukoko. |
128. Jununu fununu. |
129. Kafiri akufaaye, si muislamu asiye kufaa |
130. Kafiri akufaye si Isilamu asiyekufa. |
131. Kama hujui kufa,tazama kaburi. |
132. Kama wewe wasema cha nini, mwezio asema nitakipata lini. |
133. Kamba hukatika pabovu. |
134. Kanga hazai ugenini. |
135. Kawaida ni kama sheria. |
136. Kawia ufike. |
137. Kazi mbaya siyo mchezo mwema. |
138. Kelele za chura hazimzuwii ng'ombe kunywa maji. |
139. Kelele za mlango haziniwasi usingizi (Kelele za mlango hazimuudhi mwenye nyumba) |
140. Kenda karibu na kumi. |
141. Kesho kesho, kesho kiama. |
142. Kiburi si maungwana. |
143. Kibuzi na kibuzi hununua jahazi. |
144. Kichango kuchangizana. |
145. Kidole kimoja hakivunji chawa. |
146. Kikulacho ki nguoni mwako. |
147. Kikushindacho kukila usikitie ila. |
148. Kila chombo kwa wimblile. |
149. Kila mbwa hubwekea mlangoni kwao. |
150. Kila mlango na ufunguwo wake. |
151. Kila mtoto na koja lake. |
152. Kila mtu huzikwa na kaburi lake. |
153. Kila mtu na bahati yake. |
154. Kila mwamba ngoma ,ngozi huivuta kwake. |
155. Kila mtu hulilia mamae. |
156. Kila ndege huruka kwa ubawa wake. |
157. Kila shetani na mbuyu wake. |
158. Kilimia kikizama kwa jua, huzuka kwa mvua, na kikizama kwa mvua, huzuka kwa jua. |
159. Kilio huanza mfiwa ndipo wa mbali wakaingia. |
160. Kimya kingi kina mshindo mkubwa. |
161. Kinga na kinga ndipo moto uwakapo. |
162. Kingiacho mjini si haramu. |
163. Kinyozi hajinyoi. |
164. Kinywa ni jumba la maneno. |
165. Kipendacho moyo dawa. |
166. Kipofu hasahau mkongojo wake. |
167. Kipya kinyemi ingawa kidonda. |
168. Kisebusebu na kiroho papo. |
169. Kisokula mlimwengu, sera nale. |
170. Kisokula mlimwengu,sera nale. |
171. Kisu kimenifika mfupani. |
172. Kitanda usicho kilalia hukijui kunguni wake. |
173. Kitumbua kimeingia mchanga. |
174. Kivuli cha fimbo hakimfichi mtu jua. |
175. Kiwi cha yule ni chema cha; hata ulimwengu uwishe. |
176. Kizuri chajiuza kibaya chajitembeza. |
177. Konzi ya maji, haifumbatiki. |
178. Konzo ya maji haifumbatiki. |
179. Kosa moja haliachi mke. |
180. Kozi mwandada, kulala na njaa kupenda. |
181. Kuagiza kufyekeza. |
182. Kuambizana kuko kusikilizana hapana. |
183. Kucha M'ngu si kilemba cheupe. |
184. Kuchamba kwingi, kuondoka na mavi. |
185. Kufa kufaana. |
186. Kufa kwa jamaa, harusi. |
187. Kufa kwa mdomo,mate hutawanyika. |
188. Kufanaya kosa sio kosa, kosa ni kurudia kosa. |
189. Kuishi kwingi, kuona mengi. |
190. Kujikwa si kuanguka,bali ni kwenda mbele. |
191. Kujikwaa si kuanguka, bali ni kwenda mbele. |
192. Kukopa harusi kulipa matanga. |
193. Kukopa harusi, kulipa matanga. |
194. Kuku havunji yai lake. |
195. Kuku mgeni hakosi kamba mguuni. |
196. Kula kutamu ,kulima mavune. |
197. Kulea mimba si kazi kazi kulea mwana. |
198. Kukopa harusi, kulipa matanga. |
199. Kumuashia taa kipofu ni kuharibu mafuta. |
200. Kunako matanga kume kufa mtu. |
201. Kunguru mwoga hukimbiza mbawa zake. |
202. Kupanda mchongoma, kushuka ndio ngoma. |
203. Kupata si werevu, na kukosa si ujinga. |
204. Kupoteya njia ndiyo kujua njia. |
205. Kurambaramba ndio kula, kunenepa kwake Mola. |
206. Kusikia si kuona. |
207. Kutangulia si kufika. |
208. Kutoa ni moyo usambe ni utajiri. |
209. Kutu kuu ni la mgeni. |
210. Kuugua sio kufa. |
211. Kuvuja kwa pakacha nafuu ya mchukuzi. |
212. Kuzima koleo si mwisho wa uhunzi. |
213. Kwa mwoga huenda kicheko na kwa shujaa huenda kilio. |
214. Kweli ilio chungu, si uongo ulio mtamu. |
215. Kwenda mbio siyo kufika. |
216. Kwenye miti hakuna wajenzi. |
217. La kuvunda halina rubani. |
218. La kuvunda halina ubani. |
219. Lake mtu halimtapishi bali humchefua. |
220. Leo kwako, kesho kwa mwenzio. |
221. Leo ni leo asemayo kesho ni mwongo. |
222. Liandikwalo ndiyo liwalo. |
223. Lila na fila hazitangamani. |
224. Lipitalo, hupishwa . |
225. Lisemwalo lipo,ikiwa halipo laja. |
226. Lisilo na mkoma, hujikoma lilo. |
227. Lisilokuwapo moyoni, halipo machoni. |
228. Maafuu hapatilizwi. |
229. Macho hayana pazia. |
230. Mafahali wawili hawakai zizi moja. |
231. Maiti haulizwi sanda. |
232. Maji hayapandi mlima. |
233. Maji hufuata mkondo. |
234. Maji ukiyavuliya nguo huna budi kuyaoga. |
235. Maji usiyoyafika hujui wingi wake. |
236. Maji ya kifuu, bahari ya chungu. |
237. Maji yakijaa hupwa. |
238. Maji yakimwagika hayazoleki. |
239. Maji yamenifika shingoni. |
240. Majuto ni mjukuu. |
241. Mali ya bahili huliwa na wadudu. |
242. Mama ni mama, hata kama ni rikwama. |
243. Mama nipe radhi kuishi na watu kazi. |
244. Mambo kunga. |
245. Manahodha wengi chombo huenda mrama. |
246. Maneno makali hayavunji mfupa. |
247. Maneno mazuri humtowa nyoka pangoni. |
248. Maneno si mkuki. |
249. Mapenzi ni kikohozi, hayawezi kufichika. |
250. Masikini akipata matako hulia mbwata. |
251. Masikini haokoti,akiokota huambiwa kaiba. |
252. Masikini na mwanawe tajiri na mali yake. |
253. Maskini hana kinyongo. |
254. Mavi usioyala, wayawingiani kuku? |
255. Mavi ya kale hayanuki. |
256. Mbinu hufuata mwendo. |
257. Mbio za sakafuni huishia ukingoni. |
258. Mbiu ya mgambo ikilia kuna jambo. |
259. Mchagua jembe si mkulima. |
260. Mchagua nazi hupata koroma. |
261. Mchagua nazi si mfuaji. |
262. Mchakacho ujao,halulengwi na jiwe. |
263. Mchama ago hanyeli,huenda akauya papo. |
264. Mchamba kwingi mara ujitia dole. |
265. Mcheka kilema hafi bila kumpata. |
266. Mchele mmoja mapishi mengi. |
267. Mchelea mwana kulia hulia yeye.. |
268. Mcheza hawi kiwete, ngoma yataka matao. |
269. Mcheza kwao hutuzwa. |
270. Mcheza na tope humrukia. |
271. Mchezea mavi, hayaachi kumnuka. |
272. Mchezea zuri, baya humfika. |
273. Mchimba kisima hungia mwenyewe. |
274. Mchonga mwiko hukimbiza mkono wake. |
275. Mchuma janga hula na wakwao. |
276. Mchumia juani,hulia kivulini. |
277. Mdharau biu, hubiuka yeye. |
278. Mdharau mwiba humchoma. |
279. Meno ya mbwa hayaumani. |
280. Mfa maji haachi kutapatapa. |
281. Mfa maji hukamata maji. |
282. Mficha uchi hazai. |
283. Mfinyazi hulia gaeni. |
284. Mfuata nyuki hakosi asali. |
285. Mfukuzwa kwao hana pakwenda. |
286. Mgaagaa na upwa hali ugari kande. |
287. Mganga hajigangi. |
288. Mgema akisifiwa tembo hulitia maji. |
289. Mgeni ni kuku mweupe. |
290. Mgeni njoo mwenyeji apone. |
291. Mgomba haushindwi na mkunguwe. |
292. Mgonjwa haulizwi uji. |
293. Miye nyumba ya udongo, sihimili vishindo. |
294. Mjinga akierevuka mwerevu yupo mashakani. |
295. Mjinga mpe kilemba utamuona mwendowe. |
296. Mjumbe hauawi. |
297. Mkaidi hafaidi mpaka siku ya idi. |
298. Mkamatwa na ngozi ndiye mwizi. |
299. Mkamia maji hayanywi. |
300. Mkamia maji hayanywi. |
301. Mkataa la mkuu huvunjika guu. |
302. Mkataa wengi ni mchawi. |
303. Mkataa ya Musa hupata ya Firauna. |
304. Mke ni nguo, mgomba kupalilia. |
305. Mkono moja hauchinji ng'ombe. |
306. Mkono moja haulei mwana. |
307. Mkono mtupu haulambwi. |
308. Mkono usioweza kuukata,ubusu. |
309. Mkosa kitoweo humangiria. |
310. Mkuki kwa nguruwe, kwa mwanadamu uchungu. |
311. Mkulima ni mmoja walaji ni wengi. |
312. Mla cha mwenziwe na chake huliwa. |
313. Mla cha uchungu na tamu hakosi. |
314. Mla kuku wa mwenziwe miguu humwelekea. |
315. Mla mbuzi hulipa ngombe. |
316. Mla mla leo mla jana kala nini? |
317. Mla nawe hafi nawe ila mzaliwa nawe. |
318. Mlala na maiti haachi kulia lia. |
319. Mlenga jiwe kundini hajui limpataye. |
320. Mlimbua nchi ni mwananchi. |
321. Mnyamaa kadumbu. |
322. Mnywa maji kwa mkono mmoja,Kiu yake i pale pale. |
323. Moja shika, si kumi nenda urudi. |
324. Moto hauzai moto. |
325. Mpanda farasi wawili hupasuka msamba. |
326. Mpanda ngazi hushuka. |
327. Mpanda ovyo hula ovyo. |
328. Mpemba akipata gogo hanyii chini. |
329. Mpemba hakimbii mvua ndogo. |
330. Mpende akupendae asiyekupenda achana naye. |
331. Mpiga ngumi ukuta huumiza mkonowe. |
332. Mpofuka ukongweni,hapotewi na njia. |
333. Msafiri kafiri. |
334. Msafiri masikini ajapokuwa sultani. |
335. Msasi haogopi mwiba. |
336. Msema kweli hukimbiwa na rafiki zake. |
337. Msema pweke hakosi. |
338. Mshika kisu, hashiki makalini. |
339. Mshale kwenda msituni haukupotea. |
340. Mshoni hachagui nguo. |
341. Msi bahati, habahatishi. |
342. Msi mbele, hana nyuma. |
343. Msishukuru mja, hamshukuru Molawe. |
344. Msitukane wagema na ulevi ungalipo. |
345. Msitukane wakunga na uzazi ungalipo. |
346. Mstahimilivu hula mbivu. |
347. Mtaka cha mvunguni sharti ainame. |
348. Mtaka lake hasindwi. |
349. Mtaka nyingi nasaba hupata mwingi msiba. |
350. Mtaka unda haneni. |
351. Mtaka uzuri hudhurika. |
352. Mtaka yote hukosa yote. |
353. Mtegemea nundu haachi kunona. |
354. mtegemea nundu, haachi konona. |
355. Mtego bila ya chambo, haunasi. |
356. Mtembezi hula miguu yake. |
357. Mteuzi heshi tamaa. |
358. Mti hauwendi ila kwa nyenzo. |
359. Mtondoo haufi maji. |
360. Mtoto akililia wembe mpe. |
361. Mtoto umleyavyo ndivyo akuavyo. |
362. Mtoto wa nyoka ni nyoka. |
363. Mtu hakatai mwito,hukata aitwalo. |
364. Mtu hujikuna ajipatapo. |
365. Mtu huulizwa amevaani ,haulizwi amekulani. |
366. Mtumai cha ndugu hufa masikini. |
367. Mtumi wa kunga haambiwi maana. |
368. Mtumikie kafiri upate mradi wako. |
369. Mtupa jongoo hutupa na mti wake. |
370. Muhitaji khanithi walau kana rijaali. |
371. Muiba yai leo kesho hua mwizi wa ng'ombe. |
372. Mume wa mama ni baba. |
373. Mungu hamfichi mnafiki. |
374. Mungu si asumani. |
375. Muonja asali haonji mara moja. |
376. Muuza sanda, mauti kwake harusi. |
377. Mvua nguo, huchutama. |
378. Mvumbika changa hula mbovu. |
379. Mvumbika pevu hula mbivu na mvumbika changa hula mbovu. |
380. Mvungu mkeka. |
381. Mvunja nchi ni mwananchi. |
382. Mvuvi ajuwa pweza alipo. |
383. Mwacha asili ni mtumwa. |
384. Mwamba na wako hukutuma umwambiye. |
385. Mwamini Mungu si mtovu. |
386. Mwana maji wa kwale kufa maji mazowea. |
387. Mwana mkuwa nawe ni mwenzio kama wewe. |
388. Mwana simba ni simba.The child of lion is a lion. |
389. Mwana wa kuku hafunzwi kuchakura. |
390. Mwana wa mtu ni kizushi, akizuka, zuka naye. |
391. Mwanga mpe mtoto kulea. |
392. Mwangaza mbili moja humponyoka. |
393. Mwanzo kokochi mwisho nazi. |
394. Mwanzo wa chanzo ni chane mbili. |
395. Mwanzo wa ngoma ni lele. |
396. Mwapiza la nje hupata la ndani. |
397. Mwekaji kisasi haambiwi mwerevu. |
398. Mwenda bure si mkaa bure,huenda akaokota. |
399. Mwenda mbio hujikwa kidole. |
400. Mwenda omo na tezi marejeo ni ngamani. |
401. Mwenda pole hajikwai. |
402. Mwenda wazimu hapewi panga. |
403. Mwenda wazimu hapoi, bali hupata nafuu. |
404. Mwenye haja hwenda chooni. |
405. Mwenye kelele hana neno. |
406. Mwenye kovu usidhani kapowa. |
407. Mwenye kubebwa hujikaza. |
408. Mwenye kuchinja hachelei kuchuna. |
409. Mwenye kuumwa na nyoka akiona jani hushtuka. |
410. Mwenye macho haambiwi tazama. |
411. Mwenye mdomo hapotei. |
412. Mwenye nguvu mpishe. |
413. Mwenye njaa hana miko. |
414. Mwenye pupa hadiriki kula tamu. |
415. Mwenye shibe hamjui mwenye njaa. |
416. Mwenye shoka hakosi kuni. |
417. Mwenye tumbo ni tumbole, angafunga mkaja. |
418. Mwenzako akinyolewa wewe tia maji. |
419. Mwibaji na watwana, mlifi ni mwungwana. |
420. Mwili wa mwenzio ni kando ya mwilio. |
421. Mwizi hushikwa na mwizi mwenziwe. |
422. Mwomba chumvi huombea chunguche. |
423. Mwosha hadhuru maiti. |
424. Mwosha huoshwa. |
425. Mwosha husitiri maiti. |
426. Mzaha,mzaha, mara hutumbuka usaha. |
427. Mzazi haachi ujusi. |
428. Mzigo usiouweza unaubebea nini? |
429. Mzigo Wa mwenzio ni kanda Ia usufi. |
430. Mzika pembe ndiye mzua pembe. |
431. Mzowea kutwaa, kutoa ni vita. |
432. Mzowea vya kunyonga, vya kuchinja haviwezi. |
433. Mzungu Wa kula hafundishwi mwana. |
434. Nahodha wengi, chombo huenda mrama. |
435. Nani kama mama? |
436. Natuone ndipo twambe, kusikia Si kuona. |
437. Nazi haishindani na jiwe. |
438. Nazi mbovu harabu ya nzima. |
439. Ndege mjanja hunaswa na tundu bovu. |
440. Ndege mwigo hana mazowea. |
441. Ndevu sio shani, hata beberu anazo. |
442. Ndugu chungu, jirani mkungu. |
443. Ndugu mwui afadhali kuwa naye. |
444. Ndugu wakigombana, chukua jembe ukalime, wakipatana chukua kikapu ukavune. |
445. Ngoja! ngoja? huumiza matumbo. |
446. Ngoma ivumayo haidumu. |
447. Ngoma ivumayo haikawii kupasuka. |
448. Ngoma ya kitoto, haikeshi. |
449. Ng'ombe avunjikapo guu hurejea zizini. |
450. Ng'ombe haelemewi na nunduye. |
451. Ngombe wa Maskini hazai. |
452. Ngozi ivute ili maji. ( Udongo upate uli maji ) |
453. Nguo ya kuazima, Haistiri matako. |
454. Nia njema ni tabibu, nia mbaya huharibu. |
455. Nifae na mvua nikufae na jua. |
456. Nimekula asali udogoni, utamu ungali gegoni. |
457. Nimekupaka wanja, wewe wanipaka pilipili. |
458. Nimerejesha kikombe na kisahani chake. |
459. Njia ya muongo fupi. |
460. Njia ya mwongo ni fupi. |
461. Njia ya siku zote haina alama. |
462. Nta Si asali; nalikuwa nazo Si uchunga. |
463. Nyani haoni kundule, huliona la mwenziwe. |
464. Nyani haoni kundule. |
465. Nyimbo mbaya haibembelezewi mtoto. |
466. Nyimbo ya kufunzwa haikeshi ngoma. |
467. Nyongeza huenda kwenye chungu. |
468. Nyota njema huonekana asubuhi. |
469. Nyumba usiyolala ndani huijui ila yake. |
470. Nyumba ya udongo haihimili vishindo. |
471. Nzi kufa juu ya kidonda Si haramu. (Jihadi ya nzi, kufa kidondani) |
472. Ondoa dari uwezeke paa. |
473. Pabaya pako Si pema pa mwenzako. |
474. Padogo pako Si pakubwa pa mwenzako. |
475. Painamapo ndipo painukapo. |
476. Paka akiondoka, panya hutawala. |
477. Paka hakubali kulala chali. |
478. Paka hashibi kwa wali, matilabaye ni panya. |
479. Paka wa nyumba haingwa. |
480. Panapo wengi hapaharibiki neno. |
481. Papo kwa papo kamba hukata jiwe. |
482. Pele hupewa msi kucha. |
483. Pema usijapo pema; ukipema Si pema tena. |
484. Penye kuku wengi usimwage mtama. |
485. Penye mafundi, hapakosi wanafunzi. |
486. Penye mbaya wako, hapakosi mwema wako/na mwema wako hakosi. |
487. Penye miti hakuna wajenzi. |
488. Penye nia pana njia. |
489. Penye urembo ndipo penye urimbo. |
490. Penye wazee haliharibiki neno. |
491. Penye wengi pana mengi. |
492. Penye wengi pana Mungu. |
493. Pilipili usoila, wewe inakuwashia nini? |
494. Pole pole ndio mwendo. |
495. Pwagu hupata pwaguzi. |
496. Radhi ni bora kuliko mali . |
497. Radhi za wazee, ni fimbo. |
498. Sahani iliyofunikwa, kilichomo kimesitirika. |
499. Sahau ni dawa ya Waja. |
500. Samaki mmoja akioza, huoza wote. |
501. Samaki mpinde angali mbichi. |
502. Shida haina hodi. |
503. Shida huzaa maarifa. |
504. Shika! Shika! na mwenyewe uwe nyuma. |
505. Shimo Ia ulimi mkono haufutiki. |
506. Shoka lisilo mpini halichanji kuni. |
507. Si kila king'aacho ni dhahabu. |
508. Si kila mwenye makucha huwa simba. |
509. Si Mungu mtupu na mkono wa mtu. |
510. Sikio halilali na njaa. |
511. Sikio halipwani kichwa. (Sikio halipiti kichwa). |
512. Sikio Ia kufa halisikii dawa. |
513. Siri ya mtungi aijuaye ni kata. |
514. Sitaacha kula mkate kwa kuogopa kiungulia. |
515. Siku njema huonekana asubuhi. |
516. Siku utakayokwenda uchi, ndiyo siku utakayokutana na mkweo. |
517. Siku ya kufa nyani, miti yote huteleza. |
518. Siku za mwizi, arubaini. |
519. Simba mwenda kimya (pole) ndiye mla nyama. |
520. Simbiko haisimbuki ila kwa msukosuko. |
521. Sio shehe bali ni shehena. |
522. Siri ya maiti aijuaye muosha. |
523. Sitafuga ndwele na waganga tele. |
524. Sitapiki nyongo harudi haramba. |
525. Subira ni ufunguo Wa faraja. |
526. Sumu mpe paka, mbuzi utamdhulumu. |
527. Sumu ya neno ni neno. |
528. Tabia ni ngozi ya mwili. |
529. Tamaa mbele, mauti nyuma. |
530. Taratibu ndio mwendo. |
531. Tawi kavu kuanguka si ajabu. |
532. Teke Ia kuku halimuumizi mwanawe |
533. Tonga si tuwi |
534. Tunda jema halikawii mtini. |
535. Ucheshi wa mtoto ni anga Ia nyumba. |
536. Ujuzi hauzeeki. |
537. Uchungu wa mwana, aujue mzazi. |
538. Udongo uwahi ungali maji (Udongo upate uli maji) |
539. Udugu wa nazi hukutania chunguni (Udugu wa nazi hukutana pakachani) |
540. Uji hajauonja, tayari ushamuunguza |
541. Ukenda kwa wenye chongo, fumba lako jicho. |
542. Ukimpa shubiri huchukua pima. |
543. Ukimuiga tembo kunya, utapasuka mkundu. |
544. Ukimwamsha alolala utalala weye. |
545. Ukinyofoa mnofu, ukumbuke kuguguna mfupa. |
546. Ukiona kwako kunaungua kwa mwenzako kunateketea. |
21 |
547. Ukiona moshi, chini kuna moto. |
548. Ukiona neno, usiposema neno, hutapatikana na neno. |
549. Ukiona vinaelea, vimeundwa. |
550. Ukiona zinduna, na ambari iko nyuma. |
551. Ukistahi mke ndugu, huzai nae. |
552. Ukitaja nyoka, shika fimbo mkononi. |
553. Ukitaka kula nguruwe, chagua aliye nona. |
554. Ukitaka salama ya dunia, zuia ulimi wako. |
555. Ukiujua wa mbele, nina ujua wa nyuma. |
556. Ukupigao ndio ukufunzao. |
557. Ukuukuu wa kamba Si upya wa ukambaa. |
558. Ulimi hauna mfupa. |
559. Ulimi unauma kuliko meno. |
560. Ulipendalo hupati, hupata ujaaliwalo. |
561. Ulivyoligema, utalinywa. |
562. Umeadimika kama la jogoo. |
563. Umegeuka mung'unye waharibika ukubwani. |
564. Umejigeuza pweza, unajipalia makaa? |
565. Umekuwa bata akili kwa watoto? |
566. Umekuwa nguva, huhimili kishindo? |
567. Umeruka mkojo unakanyaga mavi. |
568. Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu. |
569. Unajenga kwa mwenzio na kwako kunaporomoka!! |
570. Unakuja juu kama moto wa kifuu. |
571. Unamlaumu mwewe, kipanga yuwesha kuku. |
572. Ungalijua alacho nyuki, usingalionja asali. |
573. Ushikwapo shikamana (Ukibebwa usijiachie). |
574. Usiache kunanua kwa kutega. |
575. Usiache mbachao kwa msala upitao. |
576. Usiache tawi kabla ya kushika tawi. |
577. Usiandikie mate na wino ungalipo |
578. Usicheze na simba, ukamtia mkono kinywani. |
579. Usijifanye kuku mweupe. |
580. Usikaange mbuyu ukawaachia wenye meno |
581. Usile na kipofu ukamgusa rnkono. |
582. Usimgombe mkwezi, nazi imeliwa na mwezi. |
583. Usiniache njia panda. |
584. Usinikumbushe kilio matangani. |
585. Usinipake mafuta kwa nyuma ya chupa. |
586. Usinivishe kilemba cha ukoka. |
587. Usione simba kapigwa na mvua. |
588. Usipoziba ufa utajenga ukuta. |
589. Usisafirie nyota ya mwenzio. |
590. Usisahau ubaharia kwa sababu ya unahodha. |
591. Usishindane na Kari; Kari ni mja wa Mungu. |
592. Usitukane wagema na ulevi ungalipo. |
593. Usitukane wakunga na uzazi 'ungalipo. |
594. Utakosa mtoto na maji ya moto. |
595. Usiyavuke maji usiyoweza kuyaoga. |
596. Utaula na chua kwa uvivu wa kuchagua. |
597. Vita havina macho. |
598. Vita si lele mama. |
599. Vita vya panzi, neema ya kunguru |
600. Waarabu wa pemba, hujuana kwa vilemba |
601. Wache waseme. |
602. Wafadhilaka wapundaka. |
603. Wagombanao ndio wapatanao. |
604. Watu wanahisabu nazi, wewe unahisabu makoroma. |
605. Wapiganapo tembo wawili ziumiazo ni nyasi. |
606. Watetea ndizi, mgomba si wao. |
607. Wazuri haweshi. |
608. Wema hauozi.. |
609. wengi wape. |
610. Zinguo la mtukufu, ni ufito. |