2014: KISWAHILI
SEHEMU A: SARUFI
Katika swali la 1 - 20, andika herufi ya jibu lililo sahihi katika karatasi yaka ya kujibia.
1. "Yeye amefaulu mitihani yake vizuri." katika sentensi hii neno lipi limetumika kama kielezi?
- amefaulu
- yeye
- vizuri
- mitihani
- yake
Chagua Jibu
2. "Dada ameandika barua kwa baba." Sentensi hii iko katika kauli gani?
- kutendea
- kutenda
- kutendwa
- kutendeana
- kutendeka
Chagua Jibu
3. Katika sentensi zifuatazo ipi ni sahihi?
- Nimekuja hapa tangia asubuhi
- Nimekuja hapa tangiapo asubuhi
- Nimekuja hapa tanguapo asubuhi
- Nimekuja hapa tangu asubuhi
- Nimekuja hapa tangiepo asubuhi
Chagua Jibu
4. Neno lipi ni tofauti na maneno mengine kati ya maneno yafuatayo?
- viwakilishi
- vivumishi
- vielezi
- vitenzi
- visaidizi
Chagua Jibu
5. "Tunu angalisoma ..... mtihani wake." Neno lipi linakamilisha sentensi hiyo kwa usahihi?
- angefaulu
- angalifaulu
- asingefeli
- angelifaulu
- asingalifaulu
Chagua Jibu
6. "Mnyama mkali amekamatwa leo." Katika sentensi hii neno "mkali" limetumika kama aina gani ya neno?
- kielezi
- kiwakilishi
- kitenzi
- kivumishi
- kiunganishi
Chagua Jibu
7. "juma amefika na hatacheza mpira" Kitenzi "hatacheza" kipo katika half gani?
- Ukanushi
- Titnilifu
- Mazoea
- Ujao
- Shurutia
Chagua Jibu
8. "Alisema hanywi dawa tena." Kauli halisi ya sentensi hii ni ipi?
- "Hanywi dawa"
- "Hatakunywa dawa"
- "Sinywi dawa"
- "Sitakunywa tena dawa"
- ."Sinywi tena"
Chagua Jibu
9. "Walikotoka kuna mvua." Sentensi hii ipo katika wakati gani?
- Mazoea
- Shurutia
- Uliopo
- UliopitaE.Ujao
Chagua Jibu
10. "Hamisa na Hanifa ni mapacha walioungana." Katika sentensi hii neno "na" limetumikakama aina gani ya neno?
- Kihisishi
- Kiunganishi
- Kimilikishi
- Kivumishi
- Kiwakilishi
Chagua Jibu
11. Panya huyu anakula unga wangu. Wingi wa sentensi hii ni upi?
- Panya hawa wanakula unga wangu.
- Mapanya hawa wanakula unga wetu.
- Panya hizi zinakula unga wangu.
- Panya hizi zinakula unga wetu.
- Panya hawa wanakula unga wetu.
Chagua Jibu
12. Siku ile ya maandamano kulikuwa na...........wa pikipiki. Ni neno lipi linakamilisha sentensi hii?
- msururu
- msuluru
- msurulu
- Msululu
- musururu
Chagua Jibu
13. "Mpira wetu umechanika vibaya" Sentensi hii ipo katika kauli gani?
- Kutenda
- Kutendeka
- Kutendeana
- Kutendwa
- Kutendewa
Chagua Jibu
14. Neno mchwa lina silabi ngapi?
- Mbili
- Tana
- Moja
- Nne
- Tatu
Chagua Jibu
15. "Hapa ...............alipoishi chifu Mirambo." Ni neno lipi linakamilisha sentensi hii kwa usahihi?
- ndiko
- ndimo
- ndiyo
- ndipo
- ndio
Chagua Jibu
16. Atakapomnyonyoa yule hata ......... kwenye moto. Kitenzi kipi kinakamilisha tungo hii?
- atambanika
- anambanika
- humbanika
- amembanika
- alimbanika
Chagua Jibu
17. "Kitabu changu ni cheusi, chako ni cheupe." Neno "chako" ni aina gani ya neno?
- Kivumishi
- Kiwakilishi
- Kielezi
- Kihusishi
- Kiunganishi
Chagua Jibu
18. Yeye ni kijana mdogo. Neno "yeye" lipo katika nafsi gani?
- Ya kwanza umoja
- Ya tatu umoja
- Ya pill umoja
- Ya tatu wingi
- Ya pill wingi
Chagua Jibu
19. Kinyume cha kitenzi "paa" ni kipi?
- Toweka
- Potea
- Elea
- Shuka
- Tua
Chagua Jibu
20. Mwalimu J. K. Nyerere ni mwasisi wa chama cha TANU. Neno "ni" limetumika kama ainaipi ya kitenzi?
- Kitenzi kikuu
- Kitenzi kisaidizi
- Kitenzi kishirikishi
- Kitenzi kikamilifu
- Kitenzi kitegemezi
Chagua Jibu
BOFYA HAPA KUPAKUA APP YA LEANING HUB
ILI KUFUNGUA MTIHANI MZIMA
Try Another Test |