STD VII KISWAHILI ONLINE SELF NECTA TEST FOR YEAR 2013
11. Sentensi ipi kati ya hizi ipo katika hali timilifu?
Mheshimiwa Rais anahutubia mkutano
Mheshimiwa Rais alihutubia mkutano
Mheshimiwa Rais atahutubia mkutamo
Mheshimiwa Rais amehutubua mkutano
Mheshimiwa Rais alikuwa anahutubia mkutano.
Chagua Jibu
12.Neno lipi ni tofauti na maneno mengine kati ya yafuatayo?
Maji
Maziwa
Soda
Juisi
Samli
Chagua Jibu
13. "Kitabu chako ni kizuri, ukienda dukani nami uninunulie ... ......” Ni kifungu kipi cha maneno hukamilisha sentensi hiyo?
kama hivyo
kama hiko
kama icho
mfano wa iko
kama hicho
Chagua Jibu
14. Tunda huachwa mpaka likauke." Setensi hiyo ikiwa katika hali ya ukanushi itakuwa ipi kati ya zifuatazo?
Tunda haliachwi mpaka likauke
Tunda haliachi mpaka likauke
Tunda halikuachwa mpaka likauke
Tunda halitaachwa mpaka likauke
Tunda halijaachwa mpaka likauke
Chagua Jibu
15. Mkutano haukufanyika kwa sababu mwenyekiti na katibu hawakufika. Kifungu kipi cha maneno kati ya vifuatavyo kinasadifu sentensi hiyo?
Mkutano uliairisha
Mkutano uliahirishwa
Mkutano ulihairishwa
Mkutano uliharishwa
Mkutano ulihairisha
Chagua Jibu
16. Mlinzi wa mlangoni huitwaje?
Boharia
Baharia
Bawaba
Banati
Bawabu
Chagua Jibu
17. Joshua yuko jikoni anapaa samaki. Neno "anapaa” kama lilivyotumika katika sentensi hii lina maana ipi?
Kuwapaka samaki chumvi
Kuondoa magamba ya samaki
Kuondoa mifupa katika samaki
Kukausha samaki kwa moto
.Kuwakata samaki vipande vipande.
Chagua Jibu
18. "Mtoto wa ngombe anaitwa ndama, watoto wa kuku, bata, kanga wanaitwa vifaranga, kimatu ni mtoto wa nani?
Nzige
Nyuki
Inzi
Kipepeo
Buibi
Chagua Jibu
19. Kisawe cha neno ”eupe” ni kipi?
Chokaa
Angavu
Theluji
Ukungu
Angaza
Chagua Jibu
20. Siku ya nne baada ya leo huitwaje?
Mtondo
Mtondo kutwa
Mtondogoo
Kesho kutwa
Mtondogoo kutwa
Chagua Jibu
SEHEMU C
UFAHAMU
Soma kifungu cha habari na kishajibu maswaliyanayofuata:
Maji ni moja kati ya vitu vitatu muhimu sana vinavyotuwezesha kuishi. Vitu vingine ni hewa na chakula. Hewa ndiyo yenye umuhimu wa kwanza, ikifuatiwa na chakula. Kusingelikuwa na maji maisha ya binadamu na ya viumbe wengine yasingewezekana. Kila mtu anaelewa umuhimu wa maji katika maisha. Maji yanatawala maisha kwa kiasi kikubwa sana. Baadhi ya viumbe kama vile samaki, mamba, kasa, konokono, nyangumi na wengineo maskani yao ni majini, hivyo maji yakikosekana viumbe hao huweza kuaga dunia.
Binadamu anatumia maji kwa shughuli mbalimbali. Shughuli hizo ni pamoja na kupikia, kufulia, kusafishia vyombo, kuoga na kunywa. Katika sehemu nyingi za nchi yetu watu hutumia maji kwa kumwagilia bustani za mboga, maua na miti. Katika maeneo yenye mito mikubwa na maziwa maji yake hutumika kwa kumwagilia mashamba kama yale ya mpunga na mahindi. Kilimo cha umwagiliaji kinafaa kwa sababu mkulima anakuwa na uhakika wa kuvuna.
Maji ya mvua huwezesha watu kulima na kupanda mazao ya chakula na ya biashara. Hivyo zipo sehemu ambazo wakulima hulima kilimo cha umwagiliaji lakini sehemu kubwa ya wakulima hutegemea kilimo cha mvua.
Kwa ujumla maji yawe ya mvua au yanayotokana na mito au maziwa yana umuhimu mkubwa mno kwa binadamu kama walivyosema wahenga maji ni uhai, hivyo inashauriwa kwamba ni muhimu kwa kila mtu kunyvva maji safi na salama ili kulinda siha zetu.
MASWALI
31.Vitu vitatu muhimu vinavyomwezesha binadamu kuishi ni vipi?
Hewa, chakula na nyumba
Hewa, maji ma chakula
Maji ushauri na hewa
Maji, hewa na mvua
Chakula, mvua na hewa
Chagua Jibu
32.Wakulima wengi kama ilivyoelezwa katika habari hii hulima kilimo kinachotegemea nini?
Mito
Umwagiliaji
Mvua
Mabwawa
Maziwa
Chagua Jibu
33. Kiumbe yupi kati ya wafuatao halandani na wenzie?
Kima
Mamba
Nyangumi
Kasa
Samaki
Chagua Jibu
34.Kilimo cha umwagiliaji kina sifa gani kubwa?
Uvunaji upo dhahiri
Kinatumia maji ya maziwa makubwa
Kinatumia maji yaliyohifadhiwa
Mazao hayapati magonjwa
Kinalimika majira yoyote
Chagua Jibu
35.Neno "siha" kama lilivyotumika katika kifungu hiki cha habari lina maana gani?
Afya njeme
Sifa njema
Maisha mema
Tabia njema
Kinywa safi
Chagua Jibu
36. "Kuaga dunia" ni msemo wenye maana gani?
Kuzirai
Kuzimu
Kulala fofofo
Kufariki
Kufia mbali
Chagua Jibu
37. Ni kwanini mtunzi wa habari hii anashauri watu kunywa maji safi na salama?
Ili kuondokana na kiu
Ili kulinda vinywa vyetu
Ili kuburudisha mwili
Ili kuondokana na kichocho
Ili kulinda afya zetu
Chagua Jibu
38.Neno "maskani" kama lilivyotumika katika kifungu cha habari lina maana gani?
Nyumba
Makao
Maisha
Mahitaji
Shughuli
Chagua Jibu
39.Kichwa cha habari kinachofaa kwa kifungu hiki ni kipi?
Hewa ni muhimu
Maji ni uhai
Maji salama
Hewa na chakula
Siha bora
Chagua Jibu
39.Kichwa cha habari kinachofaa kwa kifungu hiki ni kipi?