Katika swali la 1 — 20, weka kivuli katika herufiyajibu lililo sahihi.
1. "Wachache wamehamia Boro". Katika sentensi hiyo "Wachache" limetumika kama aina gani ya neno?
- Kivumishi
- Kielezi
- Kiwakilishi
- Kitenzi
- Kiunganishi
Chagua Jibu
2. Alimwita nyumbani kwake kwa dhamira ya kumpa karo ya shule. Neno "dhamira" lina maana ipi?
- Dhamana
- Madhumuni
- Thumuni
- Dhumuni
- Dhamini
Chagua Jibu
3. Kauli ipi inaonesha hali ya kutendewa?
- Tumechimba visima vyetu.
- Tunachimbisha kisima chetu.
- Tulichimbiwa kisima chetu.
- Tumechimba kisima chetu.
- Tutachimba kisima chetu.
Chagua Jibu
4. Katika vifungu vya maneno vifuatavyo, kifungu kipi kipo katika kauli taarifa?
- Unataka kuondoka lini?
- Alitaka kukuuliza unaondoka lini.
- Ni lini wewe utaondoka?
- Aliuliza, utaondoka lini?
- Aliuliza kuwa ataondoka lini?
Chagua Jibu
5. Mwenyekiti hakufika mkutanoni leo. Kitenzi "hakufika" kipo katika hali gani?
- Mazoea
- Kuendelea
- Timilifu
- Matarajio
- Kanushi
Chagua Jibu
6. "Wapiganaji wetu walipowasili visiwa vya Comoro walishangiliwa kwa Ni neno lipi linakamilisha sentensi hiyo?
- hofu
- mzaha
- shangwe
- mayowe
- dhihaka
Chagua Jibu
7. Mawaziri wote wa Baraza la Mapinduzi waliapishwa. Neno "wote" limetumika kama aina gani ya neno?
- Nomino
- Kiwakilishi
- Kitenzi
- Kivumishi
- Kiunganishi
Chagua Jibu
8. Babu amemhamishia yule mbuguma kwenye zizi kubwa. Neno "mbuguma" lina maana
- Mbuzi dume anayelima
- Ngombe dume anayelima
- Kondoo jike aliyezaa
- BWombe jike anayelima
- Ngombe jike anayeendelea kuzaa
Chagua Jibu
9. "Chama kimeteka nyara sera ya serikali." Wingi wa sentensi hiyo ni upi?
- Vyama vimeteka nyara masera ya serikali.
- Vyama vimeteka nyara sera ya serikali.
- Vyama vimeteka nyara serikali.
- Vyama vimeteka sera za serikali.
- Vyama vimeteka nyara visera vya serikali.
Chagua Jibu
10. Nyumba ya ndege huitwaje?
- Mzinga
- Kiota
- Korongo
- Banda
- Shimo
Chagua Jibu
11. "Wanafunzi hodari watapewa zawadi". Sentensi hiyo ipo katika wakati gani?
- Ujao
- Timilifu
- Uliopita
- Mazoea
- Uliopo
Chagua Jibu
12. Maji yamejaa "pomoni" Neno "pomoni" ni aina ipi ya neno?
- Nomino
- Kiwakilishi
- Kielezi
- Kihisishi
- Kivumishi
Chagua Jibu
13. Kati ya maneno "Sherehi, Sherehe, Shamrashamra, Hafla, Tafrija" neno lipi halihusiani na mengine?
- Sherehi
- Sherehe
- Shamrashamra
- Hafia
- Tafrija
Chagua Jibu
14. Neno lipi kati ya maneno yafuatayo lina maana sawa na "thubutu"?
- Ufidhuli
- Ujasiri
- Umahiri
- Ukakamavu
- Utashi
Chagua Jibu
15."Kuzua kizaazaa" ni msemo wenye maana gani?
- Ushabiki
- Upendeleo
- Malumbano
- Masikitiko
- Majungu
Chagua Jibu
16. Mtu anayetafuta kujua jambo fulani kwa kuuliza maswali huitwaje?
- Mawazo
- Mbeya
- Mfitini
- Mdadisi
- Mjuaji
Chagua Jibu
17. Neno Mchakato lina maana ya mfululizo wa................
- Mawazo
- maoni
- shughuli
- safari
- fikra
Chagua Jibu
18. Neno lipi kati ya yafuatayo lina maana sawa na neno shehena
- roda
- furushi
- mizigo
- bidhaa
- robota
Chagua Jibu
19. Mtu aliyezaliwa na wazazi wa rangi mbalimbali huitwaje?
- Albino
- Mkimbizi
- mhamiaji
- chotara
- mzawa
Chagua Jibu
20. Baada ya miaka minne Kalunde ... ...... mafunzo yake ya udaktari. Ni neno lipi linakamilisha sentensi hiyo?
- aliitimu
- alihimidi
- aliitimisha
- alihitimu
- halihitimu
Chagua Jibu
BOFYA HAPA KUPAKUA APP YA LEANING HUB
ILI KUFUNGUA MTIHANI MZIMA
Try Another Test |