STD VII KISWAHILI ONLINE SELF NECTA TEST FOR YEAR 2017
SEHEMU A: SARUFI Katika swali la 1 — 20, weka kivuli katika herufl ya jibu lililo sahihi katika karatasi yako ya kujibia
1. Neno lipi ni tofauti na maneno mengine kati ya haya
Chungwa
Embe
Ndizi
Nanasi
Mgomba
Chagua Jibu
2. Mto Ruvu umefurika mwaka huu. Katika sentensi hii, maneno "mwaka huu" ni ya aina gani?
Nomino
Vitenzi
Vivumishi
Vielezi
Viwakilishi
Chagua Jibu
3."Mimi sitakuja" Sentensi hii iko katika kauli gani?
Kanushi
Ombi
Swali
Taarifa
Halisi
Chagua Jibu
4.Mama mdogo amepika ugali mwingi". Maneno gani ni vivumishia sentensi hii?
Mdogo na mwingi
Mama na mdogo
Uglai na mwingi
Mdogo na amepika
Amepika na ugali
Chagua Jibu
5."Wakulima wamehamisha mizinga ya nyuki kutoka mashambani mwao. "Umoja wa sentensi hii ni upi?
Mkulima amehamisha mizinga ya nyuki kutoka shambani mwao.
Mkulima amehamisha mzinga wa nyuki kutoka shambani mwake
Mkulima amehamisha mizinga ya nyuki kutoka shambani mwake.
Mkulima amehamisha mzinga wa nyuki kutoka shambani mwao.
Mkulima amehamisha mzinga ya nyuki kutoka shambani mwake.
Chagua Jibu
6. "Mwajuma amemwibia Mwanahamisi kalamu yake". Katika sentensi hii."Mwajuma ni nani?
Mtendewa
Mtendana
Mtendeka
Mtenda
Mtendwa
Chagua Jibu
7.Kinyume cha neno "duwaa" ni kipi?
Shangaa
Staajabu
Bashasha
Pumbaa
Butwaa
Chagua Jibu
8. "Uvumilivu ulimfanya Pendo apate zawadi. "Uvumilivu ni aina gani ya neno?
Nomino
Kitenzi
Kivumishi
Kihisishi
Kiwakilishi
Chagua Jibu
9. Yupi kati ya wafuatao ni lazima awe mwanaume?
Mjomba
Binamu
Mjukuu
Ndugu
Mzee
Chagua Jibu
IO. "Walimu watafundisha masomo yao vizuri". Sentensi hii ipo katika wakati gani?
Uliopita
Ujao
Uliopo
Mazoea
Timilifu
Chagua Jibu
11. "Wanafunzi wenzake walimnyanyapaa. Neno walimnyanyapaa lina maana gani kati ya hizi zifuatazo?
Walimpenda
Walimhurumia
Walimtenga
Walimhusudu
Walimchekesha
Chagua Jibu
12. Neno nimerudi lipo katika nafsi ipi?
Pili umoja
Kwanza umoja
Kwanza wingi
Tatu umoja E.
Tatu wingi
Chagua Jibu
13. Kiwanda hutoa ajira kwa wananchi "kiwanda" ni aina gani ya neno?
Kivumishi
Kiwakilishi
Nomino
Kielezi
Kitenzi
Chagua Jibu
14. Mashine nyingi hupatikana" kiwandani" ni aina gani ya neno
Kivumishi.
Kiwakilishi
Nomino
Kielezi
Kitenzi.
Chagua Jibu
15.Kisawe cha neno "ndovu" ni kipi kati ya maneno yafuatayo?
Nyati
Faru
Nyumbu
Tembo
Mbogo.
Chagua Jibu
16, "Mlima meru unafuka moshi" Ukanusha wa sentensi hii ni upi?
Mlima meru unawaka moshi
Mlima meru unatoa moshi.
Mlima meru unafukiza moshi D.
Mlima meru haufuki moshi
Mlima meru hauwaki moshi.
Chagua Jibu
17.Panga maneno yafuatayo kwa kuanzia na neno ambalo katika familia hiyo linaonesha aliyetangulia kuzaliwa hadi wa mwisho kuzaliwa: Baba, kitukuu, babu, kilembwe,