Katika swali la 1 — 20, weka kivuli katika herufiyajibu lililo sahihi.
1. "Ramadhani anacheza mpira uwanjani." Sentensi hii ikiwa katika hali ya mazoea itakuwa ipi kati ya hizi zifuatazo?.....
- Ramadhani hucheza mpira uwanjani.
- Ramadhani atacheza mpira uwanjani.
- Ramadhani alicheza mpira uwanjani.
- Ramadhani amecheza mpira uwanjani
- Ramadhani anacheza mpira uwanjani.
Chagua Jibu
2. "Bura yangu sibadili na rehani." Kitenzi "sibadili" kipo katika hali ipi?.......
- Mazoea
- Timilifu
- Ukanushi
- Kuendelea
- Shurutia
Chagua Jibu
3. "Babu alikuwa analima shambani." Neno "alikuwa" ni aina ipi ya kitenzi? .
- Kitenzi kikuu
- Kitenzi kitegemezi
- Kitenzi jina
- Kitenzi kishirikishi
- Kitenzi kisaidizi
Chagua Jibu
4. Katika sentensi zifuatazo ipi ina maana sahihi?..
- Sikuwa najua Halima ni dada yako.
- Sikujua kuwa Halima ni dada yako.
- Sikuwa ninajua Halima ni dada yako.
- Sikuwa ninajua kwamba Halima ni dada yako.
Chagua Jibu
5. Ni neno lipi kati ya yafuatayo ni kisawe cha neno "hifadhi"? .
- Weka
- Panga
- Tunza
- Ficha E.
- Funga
Chagua Jibu
6. Lahaula! Loo! La hasha! Masalale! Ni maneno ya aina gani?
- Vitenzi
- Vihisishi
- Viwakilishi
- Vivumishi
- Viunganishi
Chagua Jibu
7. "Ingawa walipata matatizo mengi safarini walifika salama." Neno lipi linakamilisha sentensi hiyo kwa usahihi?
- vilevile
- kwa hiyo
- halikadhalika D.
- hivyo
- hatimaye
Chagua Jibu
8. "Mjukuu wangu hupenda kuniamkia kila mara." Sentensi hiyo ipo katika kauli gani?
- Kutendwa
- Kutenda
- Kutendeka
- Kutendana
- Kutendewa
Chagua Jibu
9. "Wawili wameshindwa kupanda mlima Kilimanjaro." Kiwakilishi katika sentensi hiyo ni kipi?
- Mlima
- Kupanda
- Wameshindwa
- Kilimanjaro
- Wawili
Chagua Jibu
10. ”Vita ilipoanza nchini Kenya watu wote . . Kitenzi kipi kinakamilisha sentens hiyo?
- walitweta
- walitaharuki
- walitunukiwa
- walinusurika
- walitahamaki
Chagua Jibu
11. "Tulicheza ngoma na kuimba usiku kucha.” Katika sentensi hii watenda ni nafsi ipi?
- Ya tatu wingi
- Ya pili wingi
- Yapili umoja
- Ya tatu umoja
- Ya kwanza wingi.
Chagua Jibu
12. ”Utundu wake ulimfanya ajulikane shuleni.” Neno "Utundu” limetumika kama aina gani
neno?
- Kivumishi
- Nomino
- Kiwakilishi
- Kitenzi
- Kielezi.
Chagua Jibu
13. "Mwanamuziki hodari aliimba nyimbo vizuri.” Kielezi katika sentensi hii ni kipi? ........
- Hodari
- Aliimba
- Mwanamuziki
- Nyimbo
- Vizuri
Chagua Jibu
14. "Mgeni aliondoka alikofikia.............kuaga.” Kifungu kipi cha maneno kinachokamilishE sentensi hiyo kwa usahihi?
- licha ya
- pasi ya
- bila kwa
- bila ya
- bila na
Chagua Jibu
15. Neno moja linalojumuisha herufi "a, e, i, o na u” ni lipi?
- Silabi
- Konsonanti
- Mwambatano
- Kiambishi
- Irabu.
Chagua Jibu
16. "Kaka anapenda kujisomea chumbani mwake.” Katika sentensi hiyo kitenzi kisaidizi ni kipi? ........
- Anapenda
- . Chumbani
- Kujisomea
- Kaka
- Kwake.
Chagua Jibu
17. ”Mchezo mkali ni ule tuliocheza ......... ya Timu ya Majengo.” Neno lipi linakamilisha tungc hiyo kwa usahihi?
- zidi
- zaidi
- kabla
- thidi
- dhidi
Chagua Jibu
18. Mama Ntilie akiondoka, uondoke naye. Sentensi hii ipo katika wakati gani? ........
- Ujao
- Timilifu
- Shurutia
- Uliopo
- Mazoea.
Chagua Jibu
19. Mpira umegonga mwamba nusura goli liingie. Neno lipi linaonesha kitendwa? ........
- Nusura
- Goli C.
- Mpira D.
- Mwamba
- Liingie.
Chagua Jibu
20. Ni neno lipi kati ya haya yafuatayo ni tofauti na mengine? ........
- Sahibu
- Ajuza
- Msiri
- Mwandani
- Mwenzi
Chagua Jibu
BOFYA HAPA KUPAKUA APP YA LEANING HUB
ILI KUFUNGUA MTIHANI MZIMA
Try Another Test |