KISWAHILI-2012
SEHEMU A
SARUFI
Chagua herufiyajibu lililo sahihi kisha andika katika karatasiyakoya kujibia.
1. Katika maneno yafuatayo ni lipi ambalo ni nomino dhahania?
- Unakuja
- Umeenea
- Utalima
- Uelewa
- Ulisoma
Chagua Jibu
2. Wingi wa neno "paka" ni upi?
- Mipaka
- Paka
- Mapaka
- Vipaka
- Wapaka
Chagua Jibu
3."Akiondoka Sulubu kazi zote zitalala." Neno "sulubu" ni la aina ipi?
- Kielezi
- Kivumishi
- Kiwakilishi
- Nomino
- Kiunganishi
Chagua Jibu
4."Ili tuendelee.... ..... kufanya kazi kvva bidii." Neno lipi limekosekana kukamilisha sentensi hiyo?
- ni budi
- hatuna budi
- tuna budi
- kuna budi
- Hapana budi
Chagua Jibu
5."Mvua ilinyesha jana usiku kucha. " Katika sentensi hiyo kikundi kielezi ni kipi?
- Mvua ilinyesha jana
- Usiku kucha
- Ilinyesha jana
- Mvua ilinyesha
- Jana usiku kucha
Chagua Jibu
6."Baba alilimiwa shamba." Sentensi hii ipo katika kauli gani?
- Kutenda
- Kutendewa
- Kutendwa
- Kutendeka E. Kutendea
Chagua Jibu
7."Adili alikuwa anaimba tangu ujana wake." Neno "alikuwa" ni aina gani ya kitenzi?
- Kisaidizi
- Jina
- Kishirikishi
- Kitegemezi
- Kikuu
Chagua Jibu
8."Mchungaji alivaa suti maridadi sana."Katika sentensi hii neno lipi limetumika kama kivumishi?
- Suti
- Alivaa
- Maridadi
- Mchungaji
- Sana
Chagua Jibu
9.Kitenzi " anapigwa" kipo katika kauli gani?
- Kutenda
- Kutendewa
- Kutendwa
- Kutendeka
- Kutendesha
Chagua Jibu
10.Kisawe cha neno "bahati" ni kipi kati ya maneno yafuatayo?
- Tunu
- Sudi
- Shani
- Hiba
- Hidaya
Chagua Jibu
11."Maandishi yanasomeka vizuri." Sentensi hii ipo katika wakati gani?
- Ujao
- Uliopita
- Mazoea
- Uliopo
- Timilifu
Chagua Jibu
12. "Makubi ni mtoto wa mjukuu wangu." Makubi ni nani kwangu?
- Kilembwekeza
- Kijukuu
- Kilembwe
- Kitukuu
- Mtukuu
Chagua Jibu
13."Sipendi uongo." Sentensi hii ipo katika nafsi ipi?
- Nafsi ya kwanza wingi
- Nafsi ya tatu umoja
- Nafsi ya kwanza umoja
- Nafsi ya tatu wingi
- Nafsi ya pili umoja.
Chagua Jibu
14.Neno "poni" lina maana sawa na neno lipi kati ya maneno?
- Posho
- Rahani
- Mali
- Mkopo
- Pesa
Chagua Jibu
15. "Shuleni kwetu kuna upungufuwa . Ni neno lipi hukamilisha tungo hiyo kwa usahihi?
- thamani
- thamini
- dhamini
- zamani
- samani
Chagua Jibu
16. "Mtoto ametengeneza toroli Ia mti." Wingi wa sentensi hii ni upi?
- Watoto wametengeneza toroli za miti
- Watoto wametengeneza matoroli ya mti
- Watoto ametengeneza matoroli ya miti
- Watoto wametengeneza toroli za mti
- Watoto wametengeneza matoroli ya miti
Chagua Jibu
17. "Muda mfupi atakuwa anaingia uwanjani." Sentensi hii ipo katika wakati gani?
- Uliopo
- Uliopita
- Wa mazoea
- Ujao
- Timilifu
Chagua Jibu
18.
Ni neno lipi kati ya haya yafuatayo halilandani na mengine?
- Fikiria
- Dodosa
- Uliza
- Hoji
- Saili
Chagua Jibu
19. Juma aliondoka hivi punde. Maneno "hivi punde" yana maana ipi?
- Haraka
- Muda mrefu
- Karibuni
- Kwa pupa
- Kwa haraka
Chagua Jibu
20. Neno lipi ni kisawe cha neno adili?
- Ujinga
- Wema
- Uovu
- Ujasiri
- Ukatili
Chagua Jibu
BOFYA HAPA KUPAKUA APP YA LEANING HUB
ILI KUFUNGUA MTIHANI MZIMA
Try Another Test |