KISWAHILI 2010
SEHEMU A
SARUFI
Katika swali la 1-5 andika herufiya jibu lililo sahihi katika karatasiyakoya kujibia.
1. "Ukitaka cha mvunguni inama". Hii ni sentensi ya aina gani?
- ambatano
- changamano
- shurutia
- nyofu
- sahili
Chagua Jibu
2. Katika neno "hatutakamilisha", kiambishi kinachoonesha nafsi ni kipi?
- -ka-
- -ta-
- -ha-
- -sha-
- -tu-
Chagua Jibu
3. "Kampeni ya upandaji miti wilayani Kishapu ilifanikiwa sana na wananchi." Sentensi hii ipo katika kauli gani?
- kutendwa
- kutendewa
- kutenda
- kutendana
- kutendeka
Chagua Jibu
4. Kisawe cha neno "beseni" ni kipi?
- debe
- karai
- ndoo
- pipa
- chupa
Chagua Jibu
5. Wingi wa sentensi isemayo, "Ubao umetumika" ni ipi?
- Mbao itatumika
- mbao umetumika
- mbao zitatumika
- mbao imetumika
- mbao zimetumika
Chagua Jibu
6. Katika sentensi ifuatayo, ni neno lipi limetumika kama kiwakilishi? "Huu ni wa maziwa."
- ziwa
- huu
- Ni
- Wa
- Maziwa
Chagua Jibu
7. Ubegete ameshinda kondeni akiamia ndege. Kielezi katika sentensi hii ni kipi?
- Kondeni
- Akiamia
- Ameshinda
- Ndege
- Kondeni akiamia
Chagua Jibu
8. Mwalimu alikuwa anatunga mtihani. N eno "anatunga" limetumika kama aina ipi ya kitenzi?
- Kishirikishi
- Kitenzi Kikuu
- Kisaidizi
- Kitenzi kipungufu
- Kitenzi jina
Chagua Jibu
9. Alfajiri na mapema tuliondoka ukumbini. Mzizi katika neno lililopigiwa mstari ni upi?
- -ondo-
- -iondoka
- -ondok-
- ondoka
- -iondok-
Chagua Jibu
10. Kinyume cha neno "Tandika" ni kipi?
- Tandaza
- Tandua
- Tanzua
- Tanzia
- Tandiko
Chagua Jibu
11. Umoja wa sentensi "Machungwa mabichi yana ladha ya uchachu” ni...
- Chungwa bichi lina ladha ya uchachu
- Chungwa bichi lina ladha yake
- Chungwa bichi lina kaladha ka uchachu
- Chungwa bichi lina ladha kali
- Vichungwa vibichi vina ladha ya uchachu.
Chagua Jibu
12. Fundi atengenezaye herein, pete an mikufu huitwaje?
- Sofara
- Mfuaji
- Sonara
- Mnajimu
- Fundi
Chagua Jibu
13. "Zena amemnunulia mwanae kizibao” limetumika kwa maana ipi?
- Suti yenye mikono mirefu
- Jaketi kubwa
- Shati la mikono mifupi
- Koti fupi lisilo na mikono
- Koti lenye mikono mirefu
Chagua Jibu
14. Neno "kindumbwendumbwe” lina silabi ngapi?
- Saba
- Nne
- Tano
- Mbili
- Tisa
Chagua Jibu
15. Watalii wengi hufika Tanzania ili .mlima Kilimanjaro. Ni neno lipi linalokosekana kukamilisha sentensi hiyo?
- kuzuru
- kuthuru
- kudhuru
- kufuru
- kudhulu
Chagua Jibu
SEHEMU B
MSAMIATI
Katika swali la 16 - 25 andika herufiyajibu lililo sahihi katika karatasiyakoya kujibia.
16. Baada ya mshenga kutoa wageni waliondoka na kurudi makwao. Chagua neno sahihi kati ya maneno yafuatayo ili ukamilishe sentensi hiyo.
- fahari
- posa
- barua
- mahali
- mali
Chagua Jibu
17. Neno "msimu” lina maana gani?
- Majira
- Muda
- Mvua
- Kipupwe
- Masika
Chagua Jibu
18. Yule bwana amelima kwa bidii na amevuna . . mwingi sana.
- mipunga
- mchele
- mpunga
- wali
- michele
Chagua Jibu
19. Kisawe cha neno ”hitimisho” ni kipi?
- Hitima
- Tamati
- Mwanzo
- Katikati
- Tanguliza
Chagua Jibu
20. Katika vifungu vya maneno vifuatavyo ni kifungu kipi chenye maneno yanayoshabihiana?
- Kuku, chiriku, njiwa, mwewe.
- Almasi, dhahabu, kitok, chui
- Maembe, mapera, shaba, matopetope
- Shati, kiwiko, ukucha, kidole
- Tembo, nyani, kondoo, mtende
Chagua Jibu
BOFYA HAPA KUPAKUA APP YA LEANING HUB
ILI KUFUNGUA MTIHANI MZIMA
Try Another Test |