KISWAHILI 2007
SEHEMU A
SARUFI
Katika swali Ia 1-15 andika herufiyajibu lililo sahihi katika karatasiyakoya kujibia.
1. Mvutano kati ya wanakijiji na viongozi wao ulikuwa haujapatiwa neno lipi linakamilisha sentensi hii?
- Ugunduzi
- Ufunguzi
- Ufumbuzi
- Uvumbuzi
- Uchunguzi
Chagua Jibu
2. Maneno "mrefu, mweusi, mwerevu na mpole" yakitumika pamoja na majina hufanya kazi gani?
- Kivumishi
- Kielezi
- Kitenzi
- Nomino
- Kiswahili
Chagua Jibu
3. Sentensi ipi kati ya zifuatazo ni umoja wa sentensi "Bakari amehamisha mizinga ya nyuki kutoka shambani mwake"?
- Bakari amehamisha mizinga ya nyuki shambani
- Bakari amehamisha mzinga wa nyuki shambani mwake
- Alihamisha kimzinga cha nyuki shambani mwake
- Amehamisha kamzinga ka shambani mwake
- Bakari ameamishia mzinga wa nyuki shambani mwake
Chagua Jibu
4. Katika sentensi ifuatayo ni neno lipi limetumika kama kiwakilishi "Yule ni mnene kupita kiasi".
- Yule
- Ni
- Mnene
- Kupita
- Kiasi
Chagua Jibu
5. Kinyume cha neno ughaibuni ni kipi?
- Nchi jirani
- Magharibi
- Nchi za mbali
- Mashariki
- Nyumbani
Chagua Jibu
6. Sentensi ipi kati ya hizi zifuatazo ipo katika kauli taarifa?
- Rafiki yetu yule kachoka kusubiri
- Amechoka kusubiri rafiki yetu yule
- Rafiki yetu amesema kwamba amechoka kusubiri
- Rafiki yetu vipi, umesema umechoka kusubiri?
- Amesema hajachoka kusubiri
Chagua Jibu
7. Kipi ni kinyume cha neno gwiji?
- Mwerevu
- Asiye hodari
- Mwanamuziki
- Mwimbaji
- Hodari
Chagua Jibu
8. Katika neno "sitakuwepo" kiambishi kinachoonyesha ni kipi?
- -ta-
- -we-
- -ku-
- -po-
- -si-
Chagua Jibu
9. "Mvvanafunzi aliyefaulu vizuri atapewa tuzo". Kishazi tegemezi katika sentensi hii ni kipi?
- Atapewa tunzo
- Aliyefaulu tunzo
- Mwanafunzi aliyefaulu vizuri
- Mwanafunzi vizuri atapewa
- Aliyefaulu vizuri atapewa
Chagua Jibu
10. Neno lipi limekosekana kuikamilisha sentensi ifuatayo kwa usahihi? "Mtoto haandiki . . . . . . . . . . . hasomi".
- Ila
- bali
- kama
- wala
- hata
Chagua Jibu
11. "Ukifanya vizuri utapongezwa". Sentensi hii ni ya aina gani?
- Sahili
- Shurutia
- Changamano
- Tegemezi
- Ambatano
Chagua Jibu
12. "Nyumba ya Amini imejengeka vizuri". Sentensi hiyo ipo katika kauli gani?
- Kutenda
- Shurutia
- Kutendeka
- Kutendeana
- Kutendwa
Chagua Jibu
13. Unaponyumbulisha neno apiza unapata nomino ipi?
- Apizo
- Pizo
- Apizika
- Waapizo
- Apizana
Chagua Jibu
14. Neno lipi ni tofauti na maneno mengine kati ya yafuatayo?
- Senge'nge
- Wigo
- Barabara
- Ukuta
- Ukingo
Chagua Jibu
15. "Uji huu una sukari na maziwa". Ukanushi wa kauli hii ni upi?
- Uji huo hauna sukari ila maziwa
- Uji huu hauna sukari wala maziwa
- Uji huo hauna sukari bila maziwa
- Uji huu sukari bila maziwa
- Uji huu hauna lakini una maziwa
Chagua Jibu
SEHEMU B
MSAMIATI
Katika swali 16 - 25, andika herufiya jibu lililo sahihi katika karatasiyakoya kujibia.
16. Neno lenye maana sawa na neno "mawio" ni lipi kati ya yafuatayo?
- Macheo
- Magharibi
- Mchana
- Jioni
- Machweo
Chagua Jibu
17. Watu waliokusanyika kwa pamoja ili kuabudu huitwaje?
- Wafuasi
- Waabudu
- Waumini
- Waswalishwa
- Wakereketwa
Chagua Jibu
18. Selina alitumwa sokoni kununua mbuzi ya kukuna nazi. Neno "mbuzi" limetumika kwa maana ipi?
- Mnyama anayekuna nazi
- Kinu cha kutwangia nazi
- Kibao chenye kipande cha chuma cha kukunia nazi
- Kitu cha kukalia ambacho hutumika kukunia nazi
- Kitu chenye kibao cha kukunia nazi
Chagua Jibu
19. Neno lipi kati ya maneno yafuatayo lina maana sawa na neno "shaghalabaghala"?
- Mpangilio
- Ovyo ovyo
- Vizuri
- Viovu
- Faragha
Chagua Jibu
20. Neno lipi kati ya maneno yafuatayo halilandani na mengine?
- Kuona
- Kunusa
- Kuonja
- Kusikia
- Kutoa jasho
Chagua Jibu
BOFYA HAPA KUPAKUA APP YA LEANING HUB
ILI KUFUNGUA MTIHANI MZIMA
Try Another Test |