KISWAHILI 2006
SEHEMU A
SARUFI
Katika swali la 1-15 andika herufi yajibu lililo sahihi katika karatasiya kujibia.
1. Huyu ......... mtoto aliyekuwa amepotea.
- ndio
- ndiyo
- ndiye
- ndiyo
- ndivyo
Chagua Jibu
2. Neno lipi ni kinyume cha neno 'Adili"? .
- wema
- uovu
- ujasiri
- ujanja
- ujinga
Chagua Jibu
3. "Ala kumbe! Ameondoka leo asubuhi”. Kihisishi ni kipi kati ya maneno haya?
- Ala kumbe
- leo
- Ala
- kumbe
- ameondoka
Chagua Jibu
4. Kisawe cha neno shaibu ni .
- barabara
- baneti
- buda
- ajuza
- kigori
Chagua Jibu
5. Neno "MBWA” lina silabi ngapi?
- nne
- mbili
- moja
- tatu
- sifuri
Chagua Jibu
6. Kipi kinyume cha neno aghalabu? ......
- mara nyingi
- mara kwa mara
- nadra
- muda wote
- kila wakati
Chagua Jibu
7. Kitoto hiki kinacheza kitQtQ. Neno lililopigiwa mstari limetumika kama ...
- Nomino
- Kitenzi
- Kielezi
- Kivumishi
- Kielelezi
Chagua Jibu
8. Shule ile imeendelea ingawa haina umeme. Sentensi hii iko katika aina ipi ya tungo?
- Tungo tegemezi
- Tungo sahihi
- Tungo shurutia
- Tungo ambatano
- Tungo huria
Chagua Jibu
9. Sikuweza kutambua ni nani amelala kitandani kwa sababu alijifunika shuka . . . . . . .
- Lote
- Gubigubi
- Zima
- Nzima
- Zama
Chagua Jibu
10.Neno "Vibaya” katika sentensi isemayo "Vibaya pia vinanunuliwa” limetumika kama aina ipi ya maneno?
- Kivumishi
- Kiwakilishi
- Kielezi
- Kisifa
- Nomino
Chagua Jibu
11. Mkutano kati ya Viongozi wa DECI na Serikali ulikuwa haujapatiwaNeno lipi linalokamilisha sentensi hii?
- Uchunguzi
- Ufumbuzi
- Ufunguzi
- Kutendwa
- Kutendea
Chagua Jibu
12. 'Salama na Samina wanapendana sana". Sentensi hii ipo katika kauli ipi?
- Kutendwa
- Kutendana
- Kutenda
- Kutendwa
- Kutendea
Chagua Jibu
13. Katika neno "tutakuja” kiambishi cha wakati ni .........
- tu-
- -ku
- -ja-
- u
- -ta-
Chagua Jibu
14. Neno ”MWALIMU” lipo katika upatanisho wa ngeli ya aina gani?
- A-WA
- I-ZI
- LI-YA
- U-YA
- U-ZI
Chagua Jibu
15. Wingi wa sentensi ifuatayo ni ipi? mti huu unaharibu mazingira
- Miti hizi zinaharibu mazingira
- Miti hiyo inaharibu mazingira
- Miti hii itaharibu mazingira
- Miti hii inaharibu mazingira
- Miti hii imeharibu mazingira
Chagua Jibu
SEHEMU B
MSAMIATI
16. Mzee Mwendapole aliwapa wanaemawaidha juu ya maisha ya baadaye. Neno lililopigiwa mstari lina maana gani?
- Hotuba
- Maonyo
- Urithi
- Mawazo
- Mahubiri
Chagua Jibu
17. Neno lenye maana sawa na "mawio” ni lipi kati ya yafuatayo?
- Asubuhi
- Maonyo
- Mawazo
- Urithi
- Mahubiri
Chagua Jibu
18. Mwl. Juma alinunua shati dukani. Neno lililopigiwa mstari lilmetumika kama aina gani ya maneno?
- Kivumishi
- Kiwakilishi
- Kielezi
- Kihisishi
Chagua Jibu
19. Mtu anayesimamia kazi za shambani anaitwaje?
- Kiongozi
- Msimamizi
- Mkuu
- Nokoa
- Mnyapara
Chagua Jibu
20. Jina analotumia mjomba kumwita mtoto wa dada yake ni:
- Mtoto
- Mjomba
- Binamu
- Shangazi
- Mpwa
Chagua Jibu
BOFYA HAPA KUPAKUA APP YA LEANING HUB
ILI KUFUNGUA MTIHANI MZIMA
Try Another Test |