KISWAHILI 2011
SEHEMU A
SARUFI
Katika swali la (1 - 20) andika herufi ya jibu sahihi katika karatasi yako ya kujibia.
1. Neno "jenga" likinyumbulishwa katika kauli ya kutendeka litakuwa neno lipi?
- Jengwa
- Jengea
- Jengeka
- Jengesha
- Jengewa
Chagua Jibu
2. Neno "wamewalisha" linadokeza hali gani ya kitenzi?
- Kuendelea
- Mazoea
- Masharti
- Matarajio
- Timilisho
Chagua Jibu
3. "Yeye hupenda sana kusoma Kiswahili". Katika sentensi hii ni neno lipi limetumika kama kiwakilishi?
- Hupenda
- Kiswahili
- Sana
- Yeye
- Kusoma
Chagua Jibu
4. Katika sentensi zifuatazo ni ipi ipo katika hali ya mazoea
- Roda alisoma gazeti la Mtanzania.
- Roda atasoma gazeti la Mtanzania.
- Roda husoma gazeti la Mtanzania.
- Roda amesoma gazeti la Mtanzania.
- Roda anasoma gazeti la Mtanzania.
Chagua Jibu
3. Sara alimwambia Heri kwamba hakusafiri bali alikuwepo pale pale. Kauli halisi itakuwa ipi?
- Sara alimwambia Heri, "Sikusafiri nipo hapa hapa".
- Sara alimwambia Heri, "Sitasafiri nipo hapa hapa".
- Sara alimwambia Heri, "Sisafirinipo hapa hapa".
- Sara alimwambia Heri, "Hajasafiri yupo hapa hapa".
- Sara alimwambia Heri, "hakusafiri yupo hapa hapa".
Chagua Jibu
6. "Alikuwa anajibu kihuni". Neno "kihuni" limetumika kama aina gani ya neno?
- Kielezi
- Kiwakilishi
- Kivumishi
- Kitenzi
- Kihisishi
Chagua Jibu
7. "Mtu anayetaka msaada wa aina nitampa". Neno linalofaa kukamilisha tungo hiyo ni lipi?
- wowote
- yoyote
- yeyote
- vyovyote
- lolote
Chagua Jibu
8. "Wanafunzi wanaendelea kusoma Kiswahili ingawa hawana mwalimu". Neno "wanaendelea" limetumika kama aina gani ya kitenzi?
- Kikuu
- Kishirikishi
- Jina
- Kisaidizi
- Kitegemezi
Chagua Jibu
9. Mahali pale panatisha. Neno "pale" ni aina gani ya neno
- Kivumishi
- Kiwakilishi
- Kiunganishi
- kihisishi
- Kielezi
Chagua Jibu
10. "Kinyonga anatembea". Ukanushi wa sentensi hii ni upi?
- Kinyonga hakitembei
- Kinyonga hakutembea
- Kinyonga hajatembea
- Kinyonga haternbei
- Kinyonga hatatembea
Chagua Jibu
11. "Mama anapika lakini baba abapangamawe". Neno lakini limetumika kama aina gani ya neno?
- Kivumishi
- Kiwakilishi
- Kielezi
- Kitenzi
- Kiunganishi
Chagua Jibu
12. "Kiburi si maungwana". Neno "si" limetumika kama aina gani ya kitenzi
- Kikuu
- Kishirikishi
- Jina
- Kisaidizi
- Kitegemezi
Chagua Jibu
13. "Baba yangu ni mwenyekiti wa lopp". Neno "mwenyekiti ni nomino ya aina gani?
- Dhahania
- Kawaida
- Pekee
- Jumla
- Mguso
Chagua Jibu
14. Wingi wa neno chuma ni upi kati ya maneno yafuatayo?
- Machuma
- Mavyuma
- Vichuma
- Vyuma
- Michuma
Chagua Jibu
15. "Wanafunzi walitumiana salamu". Sentensi hii ipo katika kauli gani?
- Kutendeana
- Kutendana
- Kutendewa
- Kutendea
- Kutendeka
Chagua Jibu
16. Kinyume cha neno "elea" ni kipi?
- [buka
- Ibukia
- Zamia
- Zama
- Zamisha
Chagua Jibu
17. "Huyu mwanangu mpendwa". Neno lipi ni sahihi iii kukamilisha sentensi hiyo.
- ndiye
- ndio
- ndiyo
- ndie
- ndiwe
Chagua Jibu
18. "Mbwa ameonekana". Neno lipi ni sahihi kukamilisha tungo hiyo?
- aliyepotea
- aliopotea
- alipotea
- amepotea
- alivyopotea
Chagua Jibu
19. Hall ya kuwa na fedha au mall nyingi huitwaje?
- Ukachero
- Ukapa
- Ukata
- Ubahili
- Ukwasi
Chagua Jibu
20. Ni sentensi ipi inawakilisha kauli ya kutendwa?
- Nyumba imeharibiwa na mvua.
- Nyumba imeharibishwa na mvua.
- Nyumba imeharibika na mvua.
- Nyumba imeharibika kwa mvua.
- Nyumba imeharibiwa kwa mvua.
Chagua Jibu
BOFYA HAPA KUPAKUA APP YA LEANING HUB
ILI KUFUNGUA MTIHANI MZIMA
Try Another Test |