STD VII KISWAHILI ONLINE SELF NECTA TEST FOR YEAR 2009
KISWAHILI 2009
SEHEMU A
SARUFI
Etika swali la 1 - 15 andika herufi yajibu lililo sahihi katika karatasiyakoya kujibia.
1. Angeliamka mapema asingeliachwa na ndege. Kiambishi cha masharti katika sentensi hiyo ni kipi?
-a-
-nge-
-ngeli-
angeli-
-ili-
Chagua Jibu
2. Neno lipi kati ya haya yafuatayo halina uhusiano na mengine?
Masika
Mavunde
Kipupwe
Kiangazi
Kifuku
Chagua Jibu
3. Alisema hajisikii vizuri. Kauli halisi ya sentensi hii ni ipi?
"Hajisikii vizuri”
"Anajisikia vizuri”
"Najisikia vizuri”
"Nilijisikia vizuri”
"Sijisikii vizuri”
Chagua Jibu
4. Neno lipi linakamilisha sentensi ifuatayo:
Kama kazi hii ingalifanywa na mtu mmoJa ... ... ... kumaliza.
asingeweza
asingaliweza
angaliweza
asingeliweza
asingeweza
Chagua Jibu
5. Chakula hiki si kibayahakina viungo. Neno linalokosekana katika sentensi hii ni lipi?
kama
ila
wala
alimurudia
kwa kuwa
Chagua Jibu
6. "Shule imefunguliwa” ukanushi wa sentensi hii ni ipi?
Shule haitafunguliwa
Shule aijafunguliwa
Shule haijafunguliwa
Shule haikufunguliwa
Shule aikufunguliwa
Chagua Jibu
7. Kiranja mkuu wa shule . . . . . . . . mawazo ya wanafunzi wenzake katika kikao cha uongozi wa shule. Neno lipi linakamilisha sentensi hiyo?
aliwakilisha
ariwasilisha
aliwasirisha
aliwasilisha
ariwasirisha
Chagua Jibu
8. Wingi wa neno "kuku” ni upi?
Kuku
Vikuku
Makuku
Makuku
Vijikuku
Chagua Jibu
9. Kayumba na Neema wanaosha vyombo. Neno "vyombo” limetumika kama aina gani ya neno?
Kitenzi
Nomino
Kivumishi
Kielezi
Kiwakilishi
Chagua Jibu
10. "Padri Joni anapenda sana kucheza mpira wa kikapu." Sentensi hii ipo katika nafasi ipi?
Nafsi ya kwanza - umoja
Nafsi ya tatu - wingi
Nafsi ya pili - umoja
Nafsi ya tatu - umoja
Nafsi ya kwanza — wingi
Chagua Jibu
11. Sentensi ipi kati ya zifuatazo ipo katika kauli taarifa?
Anakwenda mjini, Joti alisema
Joti alisema, ninakwenda mjini
Joti alisema, nitakwenda mjini
Joti alitaka kujua kama atakwenda mjini
Joti alisema kuwa amekwenda mjini
Chagua Jibu
12. Buibui, inzi, mbu, papasi na tandu kwa neno moja huwa wanaitwaje?
Wanyama
Warukao
Wadudu
Ndege
Viroboto
Chagua Jibu
13. "Mzee Masanja amempa binti yake mume." Sentensi hii ina maana ipi?
Mzee Masanja amemwolesha binti yake
Mzee Masanja ameozesheana na binti yake
Mzee Masanja amemwozesha binti yake
Mzee Masanja amemwoza binti yake
Mzee Masanja amemchukua mume na kumpa binti yake
Chagua Jibu
14. Katika sentensi zifuatazo ni ipi iliyo sahihi kimuundo?
Nilikwenda kituo cha afya nilimkuta daktari hayupo
Nilikwenda kituo cha afya lakini nilimkuta daftari hayupo
Nilikwenda kituo cha afya lakini sikumkuta daktari
Nilipokwenda kituo cha afya nikamkuta daktari hayupo
Nilipokwenda nikamkuta hayupo
Chagua Jibu
15. Ni kipi kinyume cha neno "kaditama?"
Kati
Mwanzo
China
Juu
Mwisho
Chagua Jibu
SEHEMU B
MSAMIATI
Katika swali la 16 - 25 andika herufiyajibu lililo sahihi latika karatasiyakoya kujibia.
16. Wakati akiendesha baiskeli yake, magurudumu yalimrushia tope kwa kuwa hayajakuwz na . . . . . . la kuzuia. Sentensi hii inakamilishwa na neno lipi?
mbago
zuio
bati
jiwe
bano
Chagua Jibu
17. Mtu mwenye elimu ya mienendo ya nyota anaitwaje?
Mnadhimu
Mnajimu
Mnandi
Mwananyota
Shauku
Chagua Jibu
18. "Mnyamavu" ni neno lenye maana sawa na kifungu kipi cha maneno kati ya vifuatavyo?
Mwenye kupenda wanyama
Mwenye kuchukia wanyama
Mwenye tabia ya kuongea sana
Mwenye tabia ya kukaa kimya
Mwenye tabia ya ucheshi
Chagua Jibu
19. Kifungu cha maneno chenye maana sawa na neno "mwafaka" ni kipi?
Mapatano baina ya watu
Mafarakano baina ya watu
Utengano baina ya watu
Matatizo baina ya watu
Ushirikiano baina ya watu
Chagua Jibu
20. Wanakijiji wa Songambele walifanya kazi zao kikoa. Neno "kikoa" lina maana gani?