MTIHANI WA KUJIPIMA WA MADA

URAIA NA MAADILI A SITA

DEMOKRASIA

MADA YA NNE

  1. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huchaguliwa na:
  1. wananchi
  2. wabunge
  3. mawaziri
  4. madiwani
  5. Jaji Mkuu
Choose Answer


  1. Sababu kubwa ya kuruhusu mfumo wa vyama vingi Tanzania ni:
  1. kutekeleza matakwa ya wahisani
  2. kulinda haki za makundi maalumu katika jamii
  3. kuvutia wawekezaji wa nje
  4. kutekeleza maelekezo ya Umoja wa Mataifa
  5. kupanua demokrasia
Choose Answer


  1. Chombo chenye mamlaka ya kusimamia uchaguzi wa rais, wabunge na madiwani Tanzania ni:
  1. Jeshi la polisi
  2. Tume ya Taifa ya Uchaguzi
  3. Mahakama Kuu
  4. Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa
  5. Ofisi ya Waziri Mkuu
Choose Answer


  1. Uchaguzi wa Rais na Wabunge hapa Tanzania hufanyika kila baada ya
  1. miaka 10
  2. miaka 3
  3. miaka 4
  4. miaka 5
  5. miaka 6.
Choose Answer


  1. Jukumu mojawapo Ia Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni:
  1. kukosoa chama tawala
  2. kuchagua Wabunge
  3. kusajili vyama vya siasa
  4. kuteua Spika
  5. kusimamia kuhesabu kura
Choose Answer


  1. Kiongozi anayepatikana kwa njia ya kidemokrasia ana sifa zifuatazo, isipokuwa:
  1. Anafuata utawala wa sheria
  2. Anakubali kukosolewa
  3. Anaheshimu mawazo ya waliomchagua tu
  4. Anatumikia watu wote
Choose Answer


  1. Mfumo wa vyama vingi unamanufaa yafuatayo:
  1. Unaweza kuwagawa wananchi kwa itikadi
  2. Viongozi wa vyama wanaweza kuteua mgombea asiyekubalika
  3. Wananchi wana haki ya kujiunga na vyama wanavyovitaka
  4. Vyama vyote vinapata ruzuku
Choose Answer


  1. Zifuatazo ni haki za binadamu isipokuwa:
  1. Kuishi popote bila kubughudhiwa
  2. Kupata elimu
  3. Kufanya kampeni za uchaguzi
  4. Uhuru wa kuwa na familia
Choose Answer


  1. Mojawapo ni hatua ya kumpata rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  1. Kuteuliwa na wananchi wa jimbo lake
  2. Kupendekezwa na marafiki
  3. Kuteuliwa na chama chake
  4. Kupendekezwa na Bunge
Choose Answer


  1. Uvumilivu wa kisiasa ni msingi wa demokrasia kwa sababu:
  1. Unawapa watu ushindi wa kura bila kampeni
  2. Unasaidia kunyamazisha walioshindwa uchaguzi
  3. Unaleta kuelewana kwa pande zinazopingana kiitikadi
  4. Unafurahihsa wahisani
Choose Answer


  1. Andika Kweli kwa sentensi iliyo sahihi na Si kweli kwa sentensi isiyo shahihi
  1. Demokrasia ni utawala wa watu ambapo watawala hutawala kwa ridhaa ya watu............
  2. View Answer


  3. Wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huchaguliwa kwanza katika vyama kabla ya uchaguzu wa kitaifa kufanyika............................
  4. View Answer


  5. Kiongozi bora anapokea maagizo kutoka ngazi za juu za uongozi na kuyatekeleza pasipo wahusika kushirikishwa................................
  6. View Answer


  7. Katika demokrasia, mawazo ya wachache yanastahili kusikilizwa pia...................
  8. View Answer


  9. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kuchaguliwa huapishwa na Bunge...................
View Answer


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256