MTIHANI WA MWISHO WA MADA:

SURA YA TATU

1. Chagua kibu sahihi, kisha andika herufi ya jibu sahihi katika nafasi ulioyoachwa hapo chini.

 

  1. Serikali ya Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania imeundwa na serikali mbili nazo ni;
  1. Bunge na mahakama
  2. Serikali ya Tanganyika na ya Zanzibar
  3. Baraza la mawaziri na baraza la wawakilishi
  4. Serikali ya mtaa na serikali kuu
Choose Answer


  1. Ipi kati ya zifuatazo si kazi za bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?
  1. Kujadili na kuridhia mikataba
  2. Kutunga sheria na kupitisha bajeti
  3. Kutoa hukumu kwa wavunja sheria
  4. Kupitisha bajeti
Choose Answer


  1. Mahakama ni mhimili wa dola unaohusiana na kazi zifuataza, isipokuwa:
  1. Kupokea mashtaka
  2. Kutunga sheria
  3. Kusikiliza na kuamua kesi
  4. Kutafsiri sheria
Choose Answer


  1. Sheria hutungwa na huanza kutumika mara baada ya kutiwa saini na
  1. Spila wa bunge
  2. Rais
  3. Jaji mkuu wa Tanzania
  4. Jaji kiongozi wa Tanzania
Choose Answer


  1. Ni njia ipi hutumika kuwapata watumishi wa bunge la Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania  wasio wabunge?
  1. Kuajiriwa na serikali
  2. Kupigiwa kura na wananchi
  3. Kuteuliwa na waziri mkuu
  4. Kuteuliwa na mwanasheria mkuu wa serikali
Choose Answer


  1. Mahakama inayosikiliza na kuamua kesi zote zenye madai yasiozidi kiasi cha shilling milioni tatu ni
  1. Mahakama ya mwanzo
  2. Mahakama ya hakimu mkazi
  3. Mahakama ya wilaya
  4. Mahakama kuu ya Tanzania
Choose Answer


  1.                     Nani msimamizi na kiongozi wa shughuli zote za serikali Bungeni?
  1. Katibu wa bunge
  2. Spika wa bunge
  3. Waziri mkuu
  4. Naibu spika wa bunge
Choose Answer


  1.                   Upi sio mhimili mkuu wa serikali ya muungano ya Tanzania?
  1. Mahakama
  2. Serikali
  3. Bunge
  4. Polisi
Choose Answer


  1.  Mahakama ya ngazi ya juu kabisa ya kutatua mashauri Tanzania ni
  1. Mahakama kuu
  2. Mahakama ya mkazi
  3. Mahakama ya rufaa
  4. Mahakama ya jeshi
Choose Answer


  1. Uhudhuria mikutano ya baraza la mawaziri na kupewa haki zote za mjumbe lakini hana haki ya kupiga kura
  1. Katibu wa baraza la mawaziri
  2. Waziri mkuu
  3. Spika wa bunge
  4. Mwanasheria mkuu wa serikali
Choose Answer


 

 

2. Andika neno kweli au si kweli katika maswali yafuatayo.

  1. Mwenyekiti wa baraza na madiwani na kamati ya mipango ni kurugenzi za halmashauri
  2. View Answer


  3. Jukumu la Afisa elimu ni kupambana na magonjwa mfano ikimwi
  4. View Answer


  5. Mkuu wa mkoa huteuliwa na Raisi
  6. View Answer


  7. Mkuu wa Wilaya huapishwa na Mkuu wa Mkoa
  8. View Answer


  9. katibu tawala wa Wilaya ni mshauri mkuu wa Mkuu wa Wilaya
  10. View Answer


  11. Ofisa tarafa ana jukumu la kusimamia maofisa watendaji wa Kata, Vijiji na Vitongoji.
  12. View Answer


  13.   Katibu tawala wa Mkoa ni mratibu shughuli zote za kiutawala kimkoa.
  14. View Answer


  15. Mganga mfawidhi anasimamia manunuzi yote yanayofanywa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
  16. View Answer


  17. Ofisa maliasili Wilaya anasimamia na kubuni miradi ya biashara katika Wilaya yake.
  18. View Answer


  19. Mkuu wa Wilaya humsaidia Mkuu wa Mkoa katika kusimamia halmashauri zake.
View Answer


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256