MTIHANI WA KUJIPIMA WA MADA

URAIA NA MAADILI A SITA

KUJIFUNZA MAMBO KIYAKINIFU

MADA YA KUMI NA TATU

 

Chagua Jibu Lilosahihi

  1. Tunaweza kujifunza mambo katika mazingira yetu kwa njia ifuatazo isipokuwa:
  1. Kusoma magazeti na vitabu
  2. Kusikiliza redio na kuangalia runinga
  3. Kupitia ndoto zetu
  4. Mahubiri kanisani na msikitini
Choose Answer


  1. Kwa nini tunajaribu nadharia mbalimbali kwa vitendo?
  1. Kuthibitisha ukweli wake
  2. Kuzitofautisha
  3. Kuzifanya ziweze kukubalika kimataifa
  4. Kubaini zisizofaa
Choose Answer


  1. Tunawezaje kudhibitisha mambo tuliyojifunza?
  1. Iwapo tutafaulu katika mitihani
  2. Iwapo tutaeleza wengine
  3. Iwapo tutayatumia katika maisha yetu
  4. Iwapo tutayakiri
Choose Answer


  1. Tunapojifunza na wenzetu tunapata faida zifuatazo isipokuwa:
  1. Kujenga kumbukumbu ya muda mrefu
  2. Kujenga tabia ya uvumilivu
  3. Kupendelea wengine
  4. Kujenga urafiki
Choose Answer


  1. Unawezaje kuongeza ufanisi katika kujifunza?
  1. Kubeba vitabu vingi
  2. Kusoma kwa vikundi
  3. Kucheza na wenzako
  4. Kufanya mtihani
Choose Answer


Andika KWELI kwa sentensi iliyo sahihi na SI KWELI kwa sentensi isiyo sahihi.

  1. Kusoma kwa ratiba huongeza ufanisi katika kujifunza.............
  2. View Answer


  3. Kujifunza na watu wengine hujenga kumbukumbu ya muda mrefu.................
  4. View Answer


  5. Nadharia ni wazo linalotumika kuthibitisha ukweli wa jambo fulani...............
  6. View Answer


  7. Unaweza kuthibitisha ukweli wa dhana kwa kuuliza wenzako...............
  8. View Answer


  9. Kujenga tabia ya uvumilivu hutokana na kutoshirikiana na wengine..........
View Answer


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256