MTIHANI WA MWISHO WA MADA:

SURA YA KWANZA

 

1. Chagua jibu ambalo ni sahihi.

 

(i) Tunapaswa kuonesha upendo kwa watu

  1. Wenye mahitaji maalum
  2. Ndugu wa karibu
  3. Watu wanotupenda
  4. Watu wote bila ubaguzi.
Choose Answer


(ii) Wafuatao wana mahitaji maalum isipokuwa:

  1. Wazee
  2. Watoto
  3. Watu wenye ulemavu wa akili
  4. Yatima na maskini.
Choose Answer


(iii) Tofauti gani sio ya  kimaumbile kati ya mwanaume na mwanamke?

  1. Kupata hedhi
  2. Kupata mimba
  3. Uwezo wa kuzaa
  4. Kunyonyesha
Choose Answer


(iv) Tendo gani kati ya haya halionyeshi usawa wa kijinsia.

  1. Kutoa elimu sawa kwa mtoto wa kike na kiume
  2. Kutambua kuwa mwanaume na mwanamke wote ni binadamu
  3. Majukumu ya jikoni kuachiwa wasichana
  4. Kutobagua wasichana katika elimu
Choose Answer


(v) Moja ya mabadiliko ya wasichana wanapo balehe ni 

  1. Kuongezeka kwa kimo
  2. Kuonyesha heshima zaidi
  3. Kupata hedhi
  4. Kuwa na mpenzi wa jinsia tofauti.
Choose Answer


(vi) Wasichana wanaweza kujiepusha na mimba za mapema kwa;

  1. Kuwa na marafiki waaminifu
  2. Kwenda disko na jamaa zao
  3. Kupokea zawadi kutoka kwa wavulana
  4. Kuepuka matembezi yasiyo ya lazima usiku.
Choose Answer


(vii) Kwanini tunapaswa kuvaa mavazi yaliyo na staha?

  1. Yanaonyesha kujiheshimu
  2. Yanasaidia kuepuka magonjwa
  3. Ili tupendwe
  4. Ili tuvutie watu
Choose Answer


(viii) Kabila gani huvaa kaniki kwenye ngoma za asili?

  1. Maasai
  2. Wagogo
  3. Wanyasa
  4. Wasukuma
Choose Answer


(ix) Mabadiliko ya kimwili ya mtoto wa kiume na wa kike kuingia utu uzima huitwa

  1. Jinsia
  2. Kuvunja ungo
  3. Utu uzima
  4. Balehe
Choose Answer


(x) Ipi sio staha katka jamii

  1. Kuvalia nguo inayokustiri
  2. Kucheza na wavulana sehemu za uchochoro
  3. Kuwasalimia watu kwa heshima
  4. Kupenda watu wote
Choose Answer


2. Andika kweli au si kweli kwa matendo yafuatayo.

  1. Upendo halisi ni kujipenda mwenyewe_____________
  2. View Answer


  3. Watu wenye ulemavu wana mahitaji maalum_______________
  4. View Answer


  5. Moja ya mahitaji ya kwanza ya mtu ni upendo__________________
  6. View Answer


  7. Majukumu ya kujinsia hubadilika_______________
  8. View Answer


  9. Majukumu ya kijinsia hubadilika kutokana na mtazamo wa jamii  husika____________
  10. View Answer


  11. Watoto wa jinsia zote wanapaswa kujiheshimu na kuheshimiwa _____________
  12. View Answer


  13.   Wanaume wote hawashiriki kabisa kupika chakula cha nyumbani___________
  14. View Answer


  15. Mavazi ya heshima yanaonyesha tabia ya kupitwa na wakati na ushamba___________
  16. View Answer


  17.     Mavazi mengine huvaliwa na wanawake na wanaume_________________
  18. View Answer


  19.       Vazi la lubega huvaliwa na wamasai_______________
View Answer


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256