MTIHANI WA MWISHO WA MADA

MADA: KUGAWANYWA KWA BARA LA AFRIKA

Chagua Jibu Sahihi

1.Ni Taifa lipi la kibepari liliitawala Tanganyika kuanzia mwaka 1891 hadi 1918?

  1. Ujerumani
  2. Uingereza
  3. China
  4. Ureno
  5. Ufaransa
Choose Answer


2. Kwa nini Berlin ni miongoni mwa miji maarufu katika historia?

  1. Ni Makao Makuu wa Umoja wa Mataifa
  2. Ni Makao Makuu wa Jumuiya ya Madola
  3. Ni mji uliokuwa kitovu cha biashara ya utumwa
  4. Ni mji wa Ufaransa ambao uliendesha utawala wa kulisha kasumba
  5. Ni mji ambao mgawanyo wa Bara la Afrika ulifanyika
Choose Answer


3.Mataifa makubwa ya kibepari yaliyogombania Bara la Afrika yalikuwa

  1. Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, Ubelgiji, Italia na Ureno
  2. Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, Uchina, Uhispania na Marekani
  3. Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, Japani, Uhispania na Ubelgiji
  4. Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, Urusi, Uchina na Japani
  5. Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, Ubelgiji, Italia na Uchina
Choose Answer


4. Mwanzilishi wa Kampuni wa Kibiashara ya Kiingereza ya Afrika Mashariki anaitwa

  1. David Livingstone
  2. Karl Peters
  3. Mungo Park
  4. William Mackinnon
  5. Seyyid Said
Choose Answer


5. Kwa nini vita vya Maji Maji vilitokea?..............

  1. Wareno waliwapeleka Watanganyika utumwani.
  2. Kinjekitile alikasirisha na uhasama wa Wajerumani na Waarabu.
  3. Watanganyika walipigwa mijeledi na Waingereza.
  4. Wajerumani waliwalazimisha watu kufanya kazi katika mashamba ya pamba.
  5. Sultani Seyyid Said aliwatesa na kuwatumikisha Waafrika.
Choose Answer


6. Mkataba wa 1890 uliogawanya Afrika Mashiriki kwa Wajerumani na Waingereli.ulijulikana kama:

  1. Mkataba wa Hamerton
  2. Mkataba wa Haligoland
  3. Mkataba wa Moresby
  4. Mkataba wa Afrika Mashariki
  5. Mkataba wa Frere
Choose Answer


7. Makoloni ya Kifaransa Afrika yalikuwa pamoja na:

  1. Togo na Morocco
  2. Senegal na Ghana
  3. Nigeria na Tunisia
  4. Senegal na Morocco
  5. Angola na Tunisia
Choose Answer


8. Ulinzi katika jamii ya Kimasai ulikuwa ni jukumu la:

  1. laiboni
  2. morani
  3. layoni
  4. mtemi
  5. kabaka
Choose Answer


9. Nchi ya kwanza kupata Uhuru katika Afrika Mashariki ilikuwa:

  1. Tanganyika
  2. Kenya
  3. Uganda
  4. Zanzibar
  5. Burundi
Choose Answer


10. Makoloni ya Ureno Kusini mwa Afrika yalikuwa yapi?

  1. Namibia na Angala
  2. Angola na Botswana
  3. Msumbuji
  4. Namibia na Zimbabwe
  5. Angola na Msumbiji
Choose Answer


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256