MTIHANI WA KUJIPIMA WA MADA

MAARIFA YA JAMII DARASA LA SABA

MATUMIZI YA RAMANI

Chagua jibu sahihi

  1. Mji upi utashuhudia mawio ya jua mapema kabla ya miji miingine?
  1. Mji uliopo 40° Mashariki
  2. Mji uliopo 45° Magharibi
  3. Mji uliopo 45° Mashariki
  4. Mji uliopo 40° Magharibi
Choose Answer


  1. Eneo gani litashuhudia machweo ya jua mapema kabla ya maeneo mengine?
  1. Kasese 30° Mashariki
  2. Tanga 39° Mashariki
  3. Kisumu 35° Mashariki
  4. Bujumbura 29° Mashariki
Choose Answer


  1. Moja ya mambo yafuatayo siyo matumizi ya longitudo:
  1. Kuonesha mahali katika ramani
  2. Kuonesha njia za safari za anga na baharini
  3. Kukokotoa muda wa mahali
  4. Kuonesha umbali wa maeneo katika ramani
Choose Answer


4. Ipi kati ya zifuatazo ni sifa ya ramani?

  1. Huonesha pande zote za kitu
  2. Urefu wa kitu huoneshwa
  3. Umbo la asili la kitu hubakia
  4. Rangi ya asili ya kitu huonekana
  5. Huonesha sura ya juu ya kitu.
Choose Answer


5. Soma ramani ifuatayo kwa umakini kisha jibu maswali yafuatayo:


Tafuta eneo Ia sehemu iliyotiwa kivuli katika kilometa kwa kutumia kipimio cha 1: 100000

  1. km2 10.5
  2. km 2 20.05
  3. km2 15
  4. km2 15.5
  5. km 2 20.5
Choose Answer


6. Soma ramani ya kontua ifuatayo kisha jibu maswali yafuatayo:


Eneo lenye herufi A huitwa .........

  1. Korongo
  2. Uwanda
  3. Bonde
  4. Kilele
  5. Pitio
Choose Answer


7. Kipimo kidogo cha ramani hutumika kuchorea

  1. maeneo madogo
  2. maeneo makubwa
  3. maeneo ya kati tu
  4. maeneo madogo na ya kati
  5. maeneo madogo na makubwa
Choose Answer


8. Kipi kati ya vipimo vya ramani vifuatavyo kinawakilisha eneo dogo?................

  1. 1:50
  2. 1:500,000
  3. 1:50,000
  4. 1:5,000
  5. 1:500
Choose Answer



9. Kipi kati ya vipimio vya ramani vifuatavyo ni kidogo kuliko vyote?

  1. 1:10000
  2. 1:50000.
  3. 1:125000.
  4. 1:500000.
  5. 1:100000.
Choose Answer


Andika KWELI kwa sentensi ya kweli na SI KWELI kwa sentensi isiyo ya kweli katika nafasi uliyopewa.

  1. Nchi zilizo upande wa Mashariki mwa Meridiani Kuu muda wake uko mbele kuliko nchi zilizoko upande wa Magharibi mwa Meridiani Kuu..................
  2. View Answer


  3. longitudo kuu huitwa Ikweta...............
  4. View Answer


  5. Dunia hutumia zaidi ya saa 24 kukamilisha mzunguko mmoja wa 360°...............
  6. View Answer


  7. Mistaridunia ya latitudo na longitudo hutumika kuonesha mahali katika picha...........
  8. View Answer


  9. Mtari wa Ikweta unaigawa dunia katika vipande viwili vikuu ambavyo ni kizio cha Mashariki na kizio cha Magharibi.................
View Answer


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256