MTIHANI WA KUJIPIMA WA MADA

MAARIFA YA JAMII DARASA LA SABA

MAJANGA YA ASILI

Jibu maswali yafuatayo

  1. Seti ya mambo yafuatayo husababisha kutokea kwa mlipuko wa volkano;
  1. mgandamizo, joto na lava
  2. nyufa, mgandamizo na magma
  3. nguvu ya msukumo, lava na hewa
  4. nguvu ya msukumo na mgandamizo wa hewa
Choose Answer


  1. Moja kati ya njia zifuatazo si njia ya kuzuia kutokea kwa janga la moto:
  1. kutumia vifaa vilivyothibitishwa kwa ubora
  2. matumizi ya mioto iliyo wazi
  3. elimu kwa umma
  4. kutumia moto wakati wa urinaji wa asali
Choose Answer


  1. Mmeguko wa ardhi kufuata mteremko mkali huitwa................
  1. Tetemeko la ardhi
  2. Mmomonyoko wa ardhi
  3. Maporomoko ya ardhi
  4. Kuchimbika kwa ardhi
Choose Answer


  1. Mambo yafuatayo husababisha kutokea kwa janga la tsunami isipokuwa
  1. Mlipuko wa volkano
  2. Kuanguka kwa vimondo baharini
  3. Tetemeko la ardhi
  4. Mafuriko
Choose Answer


  1. Moja kati ya mambo yafuatayo ni sababu ya asili ya kutokea kwa moto msituni;
  1. Kuchoma mkaa
  2. Umeme wa radi
  3. Urinaji wa asali
  4. Mila na desturi
Choose Answer


6. Wakati wa mvua kubwa inayoambatana na radi, watu hawaruhusiwi

  1. kuvaa nguo nyekundu.......
  2. kutumia miavuli
  3. kufungua milango na madirisha
  4. kujificha chini ya mti
  5. kufunga luninga na redio
Choose Answer


7. Janga la kimazingira linalosababishwa na nguvu za asili pekee linaitwa

  1. Ukame
  2. Tetemeko la ardhi
  3. Mmomonyoko wa udongo
  4. Njaa
  5. Uchafuzi wa mazingira
Choose Answer



8. Lipi kati ya majanga yafuatayo husababishwa na binadamu

  1. Vita
  2. Ukame
  3. Milipuko ya volkano
  4. Tetemeko la ardhi
  5. Kimbunga
Choose Answer


9. Moja ya majanga yanayoletwa na nguvu za asili na kazi za binadamu ni:

  1. miipuko wa volcano.
  2. tsunami.
  3. kitropiki.
  4. radi.
  5. mmomonyoko wa udongo.
Choose Answer


10. Chanzo kikuu cha wakimbizi Afrika Mashariki na Kati ni:

  1. uchochezi wa mataifa ya kijamaa yaliyosambaratika
  2. migogoro na vita vya wenyewe kwa wenyewe
  3. tamaa ya makundi yenye uwezo wa kupigana
  4. uvivu, njaa, ukame na kukosa demokrasia
  5. kuzaliana kwa wingi kwa kundi moja dhidi ya mengine
Choose Answer


Andika KWELI kwa sentensi ya kweli na SI KWELI kwa sentensi isiyo ya kweli.

  1. Mlipuko wa volkano husababisha kufanyika kwa udongo wenye rutuba.................
  2. View Answer


  3. Maporomoko ya ardhi yanaweza kukabiliwa kwa upandaji wa miti..............
  4. View Answer


  5. Oksijeni ni hewa ya asili ambayo ikikosekana moto hauwezi kuwaka..............
  6. View Answer


  7. Uchomaji wa mkaa ni chanzo pekee kinachosababisha janga la moto katika misitu........
  8. View Answer


  9. Kuongezeka kwa kiasi cha maji yaliyomo ardhini kutokana na mvua kubwa au kuyeyuka kwa barafu huchangia kutokea kwa mafuriko...............

View Answer


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256