MTIHANI WA KUJIPIMA WA MADA

MAARIFA YA JAMII DARASA LA SABA

IDADI YA WATU NA MAKAZI

Chagua jibu sahihi.

  1. Ipi ni njia sahihi ya kupata idadi ya watu katika eneo fulani?
  1. Kufanya mkutano
  2. Kuwaandikisha watu katika vyama vya siasa
  3. Kufanya sense ya watu na makazi
  4. Kusajili idadi ya watoto wanaozaliwa nchini
Choose Answer


  1. Makazi ya watu ni...........
  1. Uwapo nyumbani
  2. Sehemu ambapo binadamu huishi
  3. Eneo tupu
  4. Umbo au mwonekano wa mji
Choose Answer


  1. Idadi ndogo ya watu ni...............
  1. Hali ya watu kuwa wengi hivyo kutumia rasilimali ipasavyo
  2. Hali ya watu kuwa wa kutosha katika eneo
  3. Hali ya watu kuwa wachache hivyo kushindwa kutumia rasilimali ipasavyo
  4. Hali ya watu kupungua
Choose Answer


4. Uchafuzi wa hewa katika maeneo ya makazi unaweza kuthibitiwa kwa:

  1. matumizi ya vyoo
  2. kuchoma takataka
  3. kumwaga maji taka mitaani
  4. kuchemsha maji ya kunywa
  5. kupunguza matumizi ya mifuko ya plastiki
Choose Answer


5. Kuhama kwa watu na bidhaa kutoka sehemu moja kwenda nyingine inaitwa:

  1. Usafirishaji
  2. Utalii
  3. Biashara
  4. Mawasiliano
  5. Uhamiaji.
Choose Answer


6. Sababu kubwa zinazochangia idadi ya vifo barani Africa ni pamoja na

  1. maisha ya starehe na michezo ya hatari
  2. njaa, maradhi na milipuko ya vita
  3. ukeketaji na mimba za utotoni
  4. mila potofu na makazi yasiyo na uhakika
  5. Rushwa, udikteta na ukuaji wa miti.
Choose Answer


7. Ipi kati ya zifuatazo sio miongoni mwa sababu za uchafuzi wa mazingira?

  1. Teknolojia duni
  2. Kuwepo kwa watu wengi
  3. Kutokuwa na Elimu
  4. Kutumia mbolea za asili zaidi katika kilimo
  5. Utaratibu mbaya wa kutupa takataka
Choose Answer


8. Moja ya majanga yanayoletwa na nguvu za asili na kazi za binadamu ni:

  1. miipuko wa volcano.
  2. tsunami.
  3. kitropiki.
  4. radi.
  5. mmomonyoko wa udongo.
Choose Answer


9. Kiutaratibu wa viwanda vinatakiwa vijengwe mbali na makazi ya watu kwa sababu

  1. serikali imeamua utaratibu huo
  2. ya kuepuka uchafuzi wa mazingira
  3. malighafi hazipatikani kwenye makazi ya watu
  4. ya kuepukana na wezi
  5. ya kudhibiti matumizi ya maji na umeme
Choose Answer


10. Watu wengi wamehamia mjini kutoka vijijini kwa sababu gani?

  1. vijijini hakuna barabara za lami
  2. mijini kuna burudani
  3. vijijini kuna mashamba
  4. mijini hakuna umaskini
  5. mijini kuna ajira na huduma za jamii
Choose Answer


Andika KWELI kwa sentensi ya kweli na SI KWELI kwa sentensi isiyo ya kweli katika nafasi uliyopewa.

  1. Idadi kubwa ya Watanzania huishi mjini...........
  2. View Answer


  3. Vifo katika eneo ni kisababishi cha ongezeko la watu.................
  4. View Answer


  5. Kuzuia mimba za utotoni ni njia mojawapo ya kudhibiti ongezeko kasi la watu.............
  6. View Answer


  7. Idadi ya watu ni jumla ya watu wanaoishi katika maeneo mbalimbali............
View Answer


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256