MTIHANI WA KUJIPIMA WA MADA

MAARIFA YA JAMII DARASA LA SABA

MILA NA DESTURI ZA WATANZANIA

Chagua jibu sahihi

1. Ujumla wa taratibu za maisha ya kila siku ya mwanadamu huitwa:

  1. mila
  2. desturi
  3. sanaa
  4. utamaduni
  5. kazi za mikono
Choose Answer



2. Nini faida ya mgawanyo wa kazi katika familia?

  1. Hudhoofisha familia
  2. Huchochea utengano
  3. Huleta udikteta
  4. Huleta maendeleo
  5. Huleta mitafaruku
Choose Answer


3. Azimio la Arusha lililenga zaidi:

  1. uhuru na kazi
  2. siasa na kilimo
  3. elimu kwa wote
  4. ujamaa na kujitegemea
  5. mfumo wa vyama vingi
Choose Answer



4. Chanzo cha familia ni:

  1. ndugu na rafiki
  2. ukoo na kabila
  3. baba na mama
  4. watoto
  5. wazee na vijana
Choose Answer


5 . Familia inaweza kujikwamua kiuchumi iwapo .

  1. mama atajishughulisha na kazi za ndani.
  2. baba ataajiriwa.
  3. watoto watajishughulisha na masomo.
  4. wanafamilia watatimiza wajibu wao.
  5. wanafamilia watasali pamoja.
Choose Answer


6. Kabla ya ukoloni elimu ya jadi ilitolewa kwa njia ya .........

  1. sheria za serikali.
  2. jando na unyago.
  3. kwenda vitani.
  4. kusoma vitabu.
  5. shule za awali.
Choose Answer


7. Jukumu la ulinzi katika familia ni la nani?

  1. Baba na watoto.
  2. Baba, jamaa na marafiki.
  3. Watoto, mama na jirani
  4. Kila mtu katika familia
  5. Watoto, jamaa na marafiki
Choose Answer



8. Moja ya athari mbaya ya utandawazi kwa Tanzania ni ...

  1. kuongezeka kwa idadi ya wageni nchini
  2. kumomonyoka kwa maadili katika jamii
  3. kuongezeka kwa uhasama baina ya vyama vya siasa
  4. kuongezeka kwa uhuru wa vyombo vya habari
  5. ongezeko la matumizi ya teknolojia ya habari
Choose Answer


9. Wajibu wa serikali katika kujenga maadili ya viongozi ni....................

  1. Kuwakopesha magari viongozi wote
  2. Kuimarisha mfumo wa chama kimoja cha siasa
  3. Kusimamia sheria za utumishi wa umma
  4. Kuhamisha watumishi wasio waadilifu
  5. Kuajiri watumishi wenye elimu ya juu to
Choose Answer


10.Tofauti kati ya mila na desturi ni....

  1. Mila hubadilika mara kwa mara kuliko desturi
  2. Desturi hubadilika mara kwa mara kuliko mila
  3. Mila ni mazoea wakati desturi ni vitendo
  4. Mila ni mazoea na huweza kubadilika na kuwa desturi
  5. Desturi hubadilika mara kwa mara kuliko mazoea
Choose Answer


Andika KWELI kwa sentensi ya kweli na SI KWELI kwa sentensi isiyo ya kweli katika nafasi uliyopewa

  1. Wakoloni walikuja kuendeleza mila na desturi za jamii zetu……………..
  2. View Answer


  3. Wazazi na walezi wanaweza kusaidia kudumisha mila na desturi za jamii zetu kwa kizazi cha sasa……….
  4. View Answer


  5. Michezo na Sanaa katika jamii ni nyenzo muhimu katika kukuza na kuendeleza mila na desturi nchini………
  6. View Answer


  7. Matumizi ya dawa za kulevya, uasherati, ulevi na uvivu ni maendeleo ya mila na desturi nchini………..
  8. View Answer


  9. Kitendo cha kuiga tabia zote zinazoibuka katika jamii bila kujali madhara yake ni kuendana na wakati…………
View Answer


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256