MTIHANI WA KUJIPIMA WA MADA

SAYANSI DARASA LA SABA

AFYA YA MWILI

Jibu maswali yote katika sehemu A, Bna C.

Sehemu A

Chagua herufi ya jibu sahihi.

  1. Yafuatayo ni  aina ya mazoezi ya mwili, isipokuwa……….
  1. Kutembea
  2. Kucheza mpira
  3. Kuruka Kamba
  4. Kusikiliza muziki
Choose Answer


  1. Mpira wa miguu ni mchezo unaofaa Zaidi kwa kundi la………..
  1. Wajawazito
  2. Watoto wachanga
  3. Wazee wa miaka 70
  4. Vijana
Choose Answer


  1. Mlo kamili ni chakula chenye………….
  1. Virutubisho vya mafuta, kabohaidreti na protini, wanga na hamirojo
  2. Virutubisho vya protini, kabohaidreti, mafuta, vitamini na madini
  3. Virutubisho vya vitamini, madini na protini, wanga na hamirojo
  4. Virutubisho vya vitamini, kalisi, potasiamu, chuma na zinki
Choose Answer


  1. Madini yafuatayo ni muhimu kwa ajili ya kuimarisha mifupa na meno………
  1. Madini ya chuma
  2. Madini ya magnesiamu
  3. Kalisi
  4. Potasiamu
Choose Answer


  1. Kazi kuu ya virutubisho vya vitamini ni kuuwezesha mwili…………..
  1. Kupata nguvu za kufanya kazi
  2. Kuwa na joto la kutosha
  3. Kukua na kuongezeka
  4. Kujilinda na magonjwa
Choose Answer


6. Hali ya mtu kuzimia hutokana na ukosefu wa damu katika .......

  1. Tumbo
  2. Figo
  3. Mapafu
  4. Moyo
  5. Ubongo
Choose Answer


7. Lipi kati ya magonjwa yafuatayo huambukizwa kwa njia ya kujamiiana?

  1.  Polio  
  2.  Kipindupindu         
  3.  Pepopunda
  4.  Kaswende                            
  5.  Tetekuwanga
Choose Answer


8. Lipi kati ya mafungu yafuatayo ya vyakula hulinda mwili?

  1.  Samaki na maziwa          
  2.  Ugali na ndizi
  3.  Maharagwe na karanga 
  4.  Mayai na kabichi 
  5.  Matunda na mboga za majani
Choose Answer


9. Tunaweza kujikinga na magonjwa ya moyo kwa kufanya yafuatayo: .......

  1. Kula chakula na kufanya mazoezi mara kwa mara
  2.  Kufanya mazoezi ya mwili, kuepuka kuvuta sigara na kuepuka kunywa pombe
  3.  Kula chakula chenye chumvi na kunywa pombe 
  4. Kufanya mazoezi ya mwili na kuvuta sigara 
  5. Kula vyakula vyenye mafuta na kunywa pombe
Choose Answer


10. Mtu anayetapika na kuharisha anapaswa kupewa:

  1.  asidi, maziwa na maji
  2.  maziwa, besi na sukari 
  3. maji, besi na maziwa
  4. chumvi, sukari na maji 
  5. sukari, asidi na besi
Choose Answer


Sehemu B

11. Andika KWELI kwa sentensi ya kweli na SI KWELI kwa sentensi isiyo ya kweli katika nafasi uliyopewa.

  1. Vyakula vyenye virutubisho vya madini husaidia kujenga mwili………..
  2. View Answer


  3. Kazi kuu ya virutubisho vya protini ni kulinda mwili usipatwe na magonjwa………..
  4. View Answer


  5. Kufanya mazoezi ya viungo husaidia mwili kuwa imara na kurekebisha uzito……….
  6. View Answer


  7. Kutofanya mazoezi ya viungo husababisha magonjwa kama shinikizo la damu, kupooza na kisukari…………
  8. View Answer


  9. Watu wanaofanya kazi za kutumia nguvu nyingi wanapaswa kula vyakula vya mafuta kwa wingi………..
  10. View Answer


  11. Inashauriwa kufanya mazoezi ya viungo kwa muda usiopungua dakika 30 kila siku ili kuwa na afya bora………………..
View Answer


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256