MTIHANI WA KUJIPIMA WA MADA

SAYANSI DARASA LA SABA

MFUMO WA FAHAMU

Jibu maswali yote katika sehemu A, B, C na D.

Sehemu A

Chagua herufi ya jibu sahihi.

  1. Zifuatazo ni kasoro za milango ya fahamu isipokuwa…………
  1. Uziwi
  2. Kutokuona mbali
  3. Anemia
  4. Kutokuona karibu
Choose Answer


  1. Mlango wa fahamu unaofanya kazi ya kuhisi baridi au joto ni………..
  1. Jicho
  2. Sikio
  3. Ulimi
  4. Ngozi
Choose Answer


  1. Kazi ya sikio la nje la binadamu ni………….
  1. Kukusanya mawimbi ya sauti
  2. Kutafsiri mawimbi ya sauti
  3. Kutawanya mawimbi ya sauti
  4. Kusisimua sikio la ndani
Choose Answer


  1. Mpangilio wa vifupa vitatu katika sikio la kati ni kama ufuatao………….
  1. Fuawe, nyundo, kikuku
  2. Kikuku, nyundo, fuawe
  3. Nyundo, kikuku, fuawe
  4. Nyundo, fuawe, kikuku
Choose Answer


  1. Ubongo umegawanyika katika sehemu tatu ambazo ni…………
  1. Serebramu, medula oblongata na ugwemgongo
  2. Serebelamu, ugwemgongo na medula oblongata
  3. Serebramu, serebelamu na medulla oblongata
  4. Medulla oblongata, serebramu na ugwemgongo
Choose Answer


  1. Neva inayopeleka taarifa kutoka kwenye pua kwenda kwenye ubongo inaitwa………..
  1. Neva ya olifaktori
  2. Neva ya optiki
  3. Neva ya akaustika
  4. Neva ya oditori
Choose Answer


  1. Neva inayotoa taarifa kutoka kwenye retina kwenda kwenye ubongo inaitwa……………
  1. Neva ya oditori
  2. Neva ya optiki
  3. Neva ya akaustika
  4. Neva ya olifaktori
Choose Answer


8. Kitu gani kitatokea endapo mfumo wa fahamu utasimama kufanya kazi?.............

  1. Mtu ataanza kutetemeka.
  2. Mtu ataanza kuhisi udhaifu.
  3. Mtu ataanza kuhisi maumivu makali mwilini.
  4. Kukosekana kwa mawasiliano ndani ya mwili.
  5. Mtu ataanza kupungua uzito.
Choose Answer



9. Vitu vinavyofanya mfumo wa damu ni pamoja na

  1. moyo, seli hai nyeupe na damu
  2. seli hai nyeupe, self hai nyekundu na mishipa ya damu
  3. moyo, mapafu na damu
  4. seli hai za damu, maji na moyo
  5.  moyo, mishipa ya damu na damu
Choose Answer


10. Homoni inayorekebisha uingiaji wa hewa ya oksijeni katika mfumo wa upumuaji katika mwili wa binadamu inaitwa.

  1. adrenalini 
  2. insulin 
  3. thairoksini 
  4. estrojeni 
  5. amilesi.
Choose Answer


Sehemu C

Andika KWELI kwa sentensi ya kweli na SI KWELI kwa sentensi isiyo ya kweli katika nafasi uliyopewa.

  1. Kazi ya pua ni kunusa tu……………..
  2. View Answer


  3. Ulimi hauna uwezo wa kutambua ladha ya limao………..
  4. View Answer


  5. Kazi ya lenzi ya jicho ni kuzuia miale ya mwanga isiingie kwenye jicho……………
  6. View Answer


  7. Lenzi mbonyeo hutumika kurekebisha kasoro ya kutokuona mbali……….
  8. View Answer


  9. Tabaka la juu la Ngozi limeundwa na neva nyingi Zaidi kuliko matabaka mengine…………
  10. View Answer


  11. Mtu anaweza kusikia vizuri sana hata kama ngoma ya sikio ikipasuka………..
  12. View Answer


  13. Koklea inahusika na msawazo wa mwili………..
View Answer


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256