MTIHANI WA KUJIPIMA WA MADA

SAYANSI DARASA LA SABA

MAJARIBIO YA KISAYANSI

Jibu maswali yote

Sehemu A

  1. Moto wa daraja gani hutokana na kuungua kwa vitu yabisi kama nguo na karatasi?
  1. Daraja D
  2. Daraja C
  3. Daraja A
  4. Daraja F
Choose Answer


  1. Tindikali ni dutu lenye kemikali ambayo hutumika kubadili karatasi ya litimasi………
  1. Nyekundu kuwa njano
  2. Bluu kuwa nyekunu
  3. Kijani kuwa bluu
  4. Nyekundu kuwa bluu
Choose Answer


  1. Ni kwa namna gani unaweza kuzuia vitu vya chuma visioate kutu?
  1. Kuviweka kwenye maji
  2. Kuvipaka majivu
  3. Kuviongeza oksijeni
  4. Kuvipaka rangi
Choose Answer


  1. Nyongo ina tabia mbili muhimu, ambazo ni…………
  1. Kubadili karatasi ya litimasi ya bluu kuwa  nyekundu na kuua vijidudu
  2. Kubadili karatasi ya litimasi bluu kuwa nyekundu na kuvunja mafuta mwilini
  3. Kubadili karatasi ya litimasi nyekundu kuwa bluu na kuvunja mafuta ya wanyama mwilini
  4. Kubadili karatasi ya litimasi ya bluu kuwa nyekundu na kukinga magonjwa
Choose Answer


  1. Ni gesi gani hutumika wakati wa kuzima moto?
  1. Kabonidayoksaidi
  2. Oksijeni
  3. Haidrojeni
  4. Naitrojeni
Choose Answer


6. Chembe ndogo kabisa za maada zinazounda elementi na zinazohusika katika kutengenezz bondi za kikemikali huitwa:

  1.  molekyuli      
  2.  elektroni      
  3.  protoni
  4.  atomi                                     
  5.  nyutroni
Choose Answer


7. Mwanga hupinda unapopita kutoka

  1.  Ncha ya Kaskazini kwenda Kusini      
  2.  media moja kwenda nyingine
  3.  Ncha ya Kaskazini kwenda Mashariki 
  4.  Magharibi kwenda Mashariki 
  5.  Kaskazini kwenda Magharibi
Choose Answer


8. Hewa ya kabonidaiyoksidi hutumika kuzima moto kwasababu:

  1.  haichochei uwakaji
  2.  ni nzito kuliko hewa
  3.  haiwaki
  4.  hunyonya joto
  5.  huungana na oksijeni
Choose Answer


9. Katika kurunzi, nishati ya umeme inayotoka kwenye betri hubadilishwa na kuwa:

  1.  nishati ya kikemikali  
  2.  nishati ya joto
  3.  nishati ya kimakaniki     
  4.  nishati ya mwanga 
  5.  Nishati ya moto
Choose Answer


10.Mojawapo ya hatua za kufuata unapoandaa jaribio la kisayansi ni: 

  1.  uchunguzi    
  2.  udadisi
  3.  utambuzi wa tatizo    
  4.  utatuzi wa tatizo
  5.  kuandaa ripoti
Choose Answer


11. Kiwango cha maji kinachopotezwa na mmea huathiriwa na hali za hewa zifuatazo...

  1.  joto na unyevu     
  2.  unyevu na mwanga
  3. upepo na mwanga wa jua               
  4.  mawingu na upepo
  5. unyevu na upepo
Choose Answer


 

  1. Andika KWELI kwa sentensi ya kweli na SI KWELI kwa sentensi isiyo ya kweli katika nafasi uliyopewa.
  1. Moto ni hali ya kuungua kwa vitu inayoambana na kuota joto na mwanga…….
  2. View Answer


  3. Fueli huwa katika hali ya yabisi tu…………
  4. View Answer


  5. Moto unaosababishwa na vimiminika kama dizeli, huzimwa kwa maji…………..
  6. View Answer


  7. Tindikali ni dutu ya kemikali ambayo ina ladha ya uchachu…………..
  8. View Answer


  9. Nyongo ni dutu ya kemikali ambayo ina ladha ya uchungu……….
View Answer


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256