MTIHANI WA KUJIPIMA WA MADA
SAYANSI DARASA LA SABA
NISHATI YA UMEME
Chagua Jibu Sahihi
1. Tazama alama kwenye kielelezo kifuatacho kwa makini, kisha zipe majina kwa kuzingatia zilivyopangwa kutoka upande wa kushoto.
- Kapasita, dynamo, seli kavu, swichi, betri
- Swichi, glopu, kikinza, kapasita, seli kavu
- Glopu, kapasita, seli kavu, kikinza, betri
- Kikinza, glopu, swichi, seli kavu, kapasita
- Swichi, kikinza, glopu, seli kavu, kapasita.
Choose Answer
2. Kipi kati ya vifuatavyo hakipitishi mkondo wa umeme?
- Mpira
- Bati
- Shaba
- Chuma
- Zebaki
Choose Answer
3. Alama zifuatazo zinatumika katika sakiti ya umeme. Je, ni alama ipi inawakilisha kikinza?
Choose Answer
4. Chunguza sakiti ya umeme iliyooneshwa katika kielelezo Na 2 kisha jibu swali lifuatalo
Sakiti iliyooneshwa katika kielelezo Na 2 huitwa
- sakiti mfuatano
- sakiti sambamba
- sakiti kinzani
- sakiti pozo
- sakiti geu
Choose Answer
5. Mzunguko kamili wa . . . . . . huitwa sakiti
- waya
- betri
- soketi
- umeme
Choose Answer
6. Umeme unaotolewa katika seli kavu, chanzo chake ni nishati gani?
- Jua
- Kimakanika
- Sauti
- Sumaku
- Kikemikali
Choose Answer
7. Mkondo wa umeme katika sakiti ni ampia 2. Kama nguvu ya umeme ni volti 4, ukinzani katika sakiti hiyo ni:
- omu 3.5
- omu 4
- omu 2
- omu 5
- omu 0.5.
Choose Answer
8. Kitumi cha umeme kinachobadili mkondogeu wa umeme kuwa mkondo mnyofu huitwa:
- rektifaya
- transista
- amplifaya
- resista.
- transfoma
Choose Answer
9. Alama ifuatayo inawakilisha
- ukinzani
- taa ya umeme
- galvanomita
- amita
- kapasita
Choose Answer
Sehemu B
Andika KWELI kwa sentensi ya kweli na SI KWELI kwa sentensi isiyo ya kweli katika nafasi uliyopewa
- Nishati ya umeme huzalishwa kwa kutumia mafuta na gesivunde tu…………
View Answer
- Rasilimali za kuzalisha nishati jadidifu zinatokana na michakato ya asili…………
View Answer
- Mawimbi ya maji, maporomoko ya maji na jotoardhi ni baadhi ya vyanzo vya uzalishaji wa umeme……….
View Answer
- Gharama za kutengeneza na kufunga mitambo ya nishati jadidifu ni ndogo……..
View Answer
- Nishati ya umeme ityokanayoi na upepo haitegemei uwepo wa upepo wenye kasi kubwa…….
View Answer