MTIHANI WA KUJIPIMA WA MADA

SAYANSI DARASA LA SITA

NISHATI YA UMEME

Sehemu A

  1. Kifaa gani kati ya hivi vifuatavyo huunganishwa na tarakilishi ili kulinda na umeme unaoongezeka?
  1. Ukinzani
  2. Kikata sakiti
  3. Kidhibiti nguvu ya umeme
  4. Kikingaradi
Choose Answer


  1. Umeme unapopita kwenye sakiti, mkondo wa umeme huwiana moja kwa moja na………..
  1. Kikinza
  2. Ampia
  3. Ohm
  4. Volteji
Choose Answer


  1. Kanuni ya Ohm huwasilishwa kwa…………..
  1. Volteji = mkondo wa umeme x ukinzani
  2. Volteji = mkondo wa umeme ÷ ukinzani
  3. Mkondo wa umeme = volteji x ukinzani
  4. Ukinzani = volteji x mkondo wa umeme
Choose Answer


4.Chunguza Kielelezo Na. 1 kisha jibu swali lifuatalo:

Kielelezo 1

Alama hii katika umeme huwakilisha:

  1. ukizani
  2. selikavu
  3. voltimita
  4. swichi
  5. glopu.
Choose Answer


5.Akyumuleta ni muungano wa seli zilizoungwa pamoja na hutumika kutoa umeme mkondo mnyoofu kwa matumizi ya:

  1. baiskeli, pasi na simu
  2. magari, matrekta na simu
  3. friji, pasi na feni
  4. baiskeli, friji na jiko la umeme.
  5. Seli kavu, jiko la mkaa na pasi
Choose Answer


6. Vyanzo asilia vya nishati katika maisha ya kila siku ni:

  1. kuni, moto na maji
  2. umeme, sumaku na gesi asili
  3. kuni, jua na upepo
  4. moto, upepo na sumaku
  5. umeme, upepo na maji
Choose Answer



7. Uhusiano kati ya sumaku na umeme ni................

  1. Chanzo cha sumaku ni nguvu ya atomiki
  2. Umeme huzuia mvutano wa sumaku.
  3. Popote penye usumaku pana umeme.
  4. Popote penye umeme pana usumaku.
  5. Sumaku huzuia umeme.
Choose Answer


8. Vifuatavyo ni vyanzo vya umemeisipokuwa

  1. betri
  2. seli kavu
  3. glopu
  4. jenereta
  5. sumaku
Choose Answer


9. Mzunguko kamili wa . . . . . .huitwa sakiti

  1. waya
  2. betri
  3. soketi
  4. umeme
Choose Answer


10. Mkondo wa umeme katika sakiti ni ampia 2. Kama nguvu ya umeme ni volti 4, ukinzani katika sakiti hiyo ni:

  1. omu 3.5
  2. omu 4
  3. omu 2
  4. omu 5
  5. omu 0.5.
Choose Answer


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256