MTIHANI WA KUJIPIMA WA MADA

SAYANSI DARASA LA SITA

USANISHAJI CHAKULA

Chagua Jibu Sahihi

1.  Mbegu za mimea uhifadhi chakula katika:

  1.  mizizi 
  2. majani      
  3. shina
  4. kotiledoni 
  5. tunda
Choose Answer



2. Gesi inayotumiwa na mimea kutengeneza protini ni:

  1. carbondayoksaidi
  2. haidrojen
  3. oksijen
  4. naitrojen
  5. gesi asilia
Choose Answer



3. Kukosekana kwa chanikiwiti katika mmea huweza kusababisha:

  1. mmea kukosa madini joto
  2. mmea kushindwa kusanisi chakula
  3. majani ya mmea kukauka
  4. majani ya mmea kuwa njano
  5. maj ani ya mmea kupukutika.
Choose Answer


4. Tendo Ia mimea kusafirisha maji kutoka kwenye mizizi hadi kwenye majani huitwa:

  1. osmosis
  2. difyusheni
  3. msukumo
  4. mgandamizo
  5. mjongeo
Choose Answer



5. Ni Vipi kati ya viumbe hai vifuatavyo hujitengenezea chakula chao kwa kutumia klorofili?

  1. Wadudu
  2. Mimea
  3. Wanyama
  4. Virusi
  5. Ndege
Choose Answer


6. Ili mimea iweze kuendelea kuishi katika mazingira yake inahitaji:

  1. hewa na udongo
  2. hewa na maji
  3. udongo na mbolea
  4. udongo na maji
  5. jotoridi na hewa
Choose Answer


7. Sehemu ya mmea inayofyonza maji inaitwa............

  1. shina
  2. tawi
  3. mzizi
  4. ua
  5. jani
Choose Answer


8. Mimea haiwezi kuendelea kukua bila hewa, maji na . . . . .

  1. Mwanga wa jua
  2. Upepo
  3. Baridi
  4. Barafu
Choose Answer


9. Muungano ufuatao ni muhimu kwenye utengenezaji wa kabohaidreti katika mimea:

  1. Oksijeni, klorofili na maji
  2. Kabondayoksaidi na maji
  3. Kabondayoksaidi, maji na mwanga wa jua
  4. Klorofili, maji na mwanga wa jua
  5. Klorofili, wanga na mwanga wa jua.
Choose Answer


10. Wakati wa kiangazi mimea hupukutisha majani kwa sababu ya:

  1. kuruhusu majani mapya yaote
  2. kukomaa sana
  3. kuongeza rutuba ardhini
  4. kuruhusu maua yaote
  5. kupunguza upotevu wa maji
Choose Answer


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256