p>MTIHANI WA KUJIPIMA WA MADA

SAYANSI DARASA LA SITA

BALEHE

Sehemu A

  1. Moja kati ya mabadiliko kwa msichana wakati wa balehe ni…………
  1. Ndoto nyevu
  2. Kuota nywele usoni
  3. Kupata hedhi
  4. Sauti kuwa nzito
Choose Answer


  1. Kwa kawaida mzunguko wa hedhi ni siku………….
  1. 20
  2. 30
  3. 28
  4. 40
Choose Answer


  1. Mabadiliko ya kiakili, kimaumbile, kitabia na kimaono huitwa………….
  1. Balehe
  2. Kukua
  3. Kujitambua
  4. Kujipenda
Choose Answer


  1. Dalili ya balehe kwa msichana na mvulana ni…………..
  1. Kukua na kutanuka matiti
  2. Kuota ndevu
  3. Kuota nywele kwapani
  4. Sauti kuwa nyororo
Choose Answer


  1. Njia mojawapo ya kukabiliana na changamoto za balehe ni……….
  1. Kuepuka matumizi ya vilevi
  2. Kulala siku nzima
  3. Kuangalia sinema
  4. Kufanya kazi bila kupumzika
Choose Answer


  1. Mojawapo ya mabadiliko ya kiakili ya mvulana wakati wa kubalehe ni
  1. Kutaka kuwa huru
  2. Uwezo wa kutambua mambo kuongezeka
  3. Kuongeza uwezo wa kuelewa mawazo
  4. Kuongeza uwezo wa kuelewa mawazo ya mtu mwingine
Choose Answer


  1. Moja wa mabadiliko ya kihusiano wakati wa balehe ni
  1. Kuanza kujitambua
  2. Kutaka kutambuliwa
  3. Kutaka kuwa huru
  4. Yote hapo juu
Choose Answer


  1. Lipi sio badiliko la kimaumbile kwa mvulana?
  1. Kukua kwa tezi za jasho
  2. Sauti kubadilika na kuwa nyororo
  3. Kupata ndoto nyevu
  4. Kupanuka kwa misuli sehemu ya kifuani na mikononi
Choose Answer


  1. Kwa kawaida mzunguko wa hedhi katika msichana huchukua siku ngapi?
  1. 30
  2. 14
  3. 28
  4. 21
Choose Answer


  1. Yai upevuka siku gani ya mzunguko wa hedhi?
  1. 10
  2. 21
  3. 14
  4. 28
Choose Answer


  1. Andika KWELI kwa sentensi sahihi na SI KWELI kwa sentensi isiyo sahihi.
  1. Mabadiliko wakati wa balehe yanasababishwa na homoni……………..
  2. View Answer


  3. Msichana anaweza kupata mimba kabla hajaanza kupata hedhi……………
  4. View Answer


  5. Wazazi na walezi wanatakiwa kuwasaidia vijana kukabiliana na changamoto za balehe……………
  6. View Answer


  7. Vijana wanatakiwa kuamua mambo yao yote wanapofika balehe……….
  8. View Answer


  9. Njia ya kumwongoza kijana wakati wa balehe ni adhabu kali…………..
  10. View Answer


  11. Hakuna njia ya kukabiliana na changamoto za balehe…………
  12. View Answer


  13. Kufanya mazoezi ni njia mojawapo ya kukabiliana na changamoto za balehe………..
  14. View Answer


  15. Wasichana wanaingia balehe mapema zaidi kuliko wavulana………….
View Answer


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256