MTIHANI WA KUJIPIMA WA MADA

SAYANSI DARASA LA SITA

UKIMWI NA MAGONJWA YA NGONO

Chagua jibu sahihi

1.Mtandao wa watu wenye virusi vya UKIMWI unatanuka kwa kuwa

  1. matumizi ya kondom na simu za mkononi yameongezeka
  2. matangazo kuhusu UKIMWI yameboreshwa
  3. kuna ongezeko la mahusiano ya kingono yasiyo salama
  4. elimu ya UKIMWI inatolewa kwa watu wachache
  5. watu wenye UKIMWI wanazingatia kanuni za kujikinga na UKIMWI
Choose Answer


2.UKIMWI husambazwa kwa kupitia:

  1. kusalimiana kwa kushikana mikono na mgonjwa wa UKIMWI
  2. kulala chumba kimoja na mgonjwa wa UKIMWI
  3. kuongea na mwathirika wa UKIMWI
  4. kuwekewa damu
  5. kuosha nguo za mwathirika wa UKIMWI.
Choose Answer


3. Ili kuepuka kupata maambukizi mapya ya UKIMWI tunashauriwa:

  1. kumeza dawa na kufanya mazoezi
  2. kuwa mwaminifu na kuepuka ngono zembe
  3. kuepuka kushirikiana na waathirika
  4. kuepuka kula pamoja na kubadilishana nguo na waathirika
  5. kupata chanjo ya UKIMWI na Kifua Kikuu.
Choose Answer


4.Lipi kati ya yafuatayo linapaswa kuzingatiwa kabla ya kumhudumia mgonjwa wa UKIMWI?

  1. Vaa nguo safi
  2. Nawa kwa sabuni
  3. Vaa glovu
  4. Sali
  5. Mruhusu apumzike
Choose Answer


5. Ni hoja ipi kati ya zifuatazo iko sahihi kuhusu VVU na UKIMWI?

  1. Kuwa na VVU ni sawa na kuwa na UKIMWI
  2. Chanzo cha VVU na UKIMWI ni magonjwa ya zinaa.
  3. Ni rahisi kujikinga na UKIMWI kuliko VVU.
  4. Ukiepuka maambukizi ya VVU pia umeepuka UKIMWI.
  5. Mtu mwenye WU hana chembe nyeupe za damu.
Choose Answer



6. Kipi kati ya vifuatavyo ni maarufu kwa kuchangia maambukizi ya WU katika jamii?

  1. Uchangiaji wa sindano, miswaki, damu na ngono zembe.
  2. Kanda za video, nyimbo, muziki na maigizo.
  3. Televisheni, magazeti na vipeperushi kuhusu WU.
  4. Kondomu, wataalamu wa afya, semina na taasisi za UKIMWI.
  5. Tohara kwa wanaume na wanawake.
Choose Answer



7. Virusi Vya Ukimwi hushambulia aina gani ya chembe hai katika damu?

  1. chembe sahani
  2. chembe hai nyeupe
  3. Chembe hai nyekundu
  4. Hemoglobini
  5. Plazima
Choose Answer



8. Mgonjwa wa UKIMWI anastahili kupata mlo maalumu ili

  1. aweze kupona haraka
  2. asiambukize watu VVU
  3. awe na nguvu ya kufanya kazi
  4. mwili upambane na maradhi
  5. VVU viangamie kabisa
Choose Answer



9. Dalili mojawapo ya ugonjwa wa UKIMWI ni

  1. kupungua uzito kwa haraka
  2. kuwashwa sehemu za siri
  3. kuvimba miguu na tumbo
  4. kupoteza uwezo wa kuona
  5. kuwa na hasira
Choose Answer


10.Ipi kati ya zifuatazo siyo dalili ya UKIMWI?

  1. Kuvimba kwa matezi
  2. Kupoteza uzito
  3. Kuharisha kusikokoma
  4. Kikohozi cha muda mrefu kisicho cha kawaida.
  5. Kutoa jasho kusiko kwa kawaida wakati wa usiku.
Choose Answer


  1. Andika KWELI kwa sentensi iliyo sahihi na SI KWELI kwa sentensi isiyo sahihi.
  1. Magonjwa ya ngono ni kundi la magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya hewa………..
  2. View Answer


  3. Magonjwa ya ngono isipokuwa UKIMWI hayana tiba…………
  4. View Answer


  5. Huwezi kutambua mtu anayeishi na VVU kwa kumuangalia………
  6. View Answer


  7. Unashauriwa kutumia mipira ya kuvaa mikononi unapomhudumia mtu anayetokwa na damu ili kujikinga na VVU…………
  8. View Answer


  9. Wanaoishi na VVU wanashauriwa kuzingatia ushauri wa daktari ili kutowaambukiza wengine……..
  10. View Answer


  11. Baadhi ya magonjwa ya ngono husababisha kuziba kwa njia ya mkojo kwa wanaume…….
  12. View Answer


  13. Hakuna uhusiano kati ya magonjwa ya ngono na VVU na UKIMWI…………
  14. View Answer


  15. Mtu anayeishi na VVU na mwenye UKIMWI anatakiwa kuzingatia usafi………..
  16. View Answer


  17. Si rahisi kwa VVU kupenya kupitia vidonda……..
View Answer


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256