MTIHANI WA KUJIPIMA WA MADA
SAYANSI DARASA LA SITA
HUDUMA YA KWANZA
Sehemu A
Chagua Jibu Sahihi
1. Hali ya mtu kuzimia hutokana na ukosefu wa damu katika .......
- Tumbo
- Figo
- Mapafu
- Moyo
- Ubongo
Choose Answer
2. Huduma ya kwanza anayopewa mtu aliyezimia ni:
- kumpa hewa ya oksijeni
- kumpa juisi ya nazi mbichi
- kumlaza juu chini na kumbonyeza tumbo
- kumpa maji yaliyochanganywa na glukosi
- kumpa juisi ya malimao, sukari na chumvi
Choose Answer
3. Huduma ya kwanza ni nini?
- Msaada wa dharura apewao mgonjwa na daktari.
- Msaadawa awali apewao mgonjwa kabla ya kupelekwa hospitali.
- Msaada kwa ajili ya mtu aliyeungua moto.
- Msaada kwa ajili ya mtu aliyeumwa na nyoka.
- Msaada kwa ajili ya mtu aliyevunjika mfupa.
Choose Answer
4. Mojawapo ya huduma ya huduma muhimu ya kumpa mtu aliye ungua moto ni;-
- kummwagia maji
- kumfunika nguo
- kumwagia asidi
- kumfunika blanketi
- kumpaka asali
Choose Answer
5. Mojawapo ya athari za kupaka mafuta kwenye jeraha la moto ni:
- kuongeza joto kwenye jeraha
- kuongeza maumivu kwenye jeraha
- kuruhusu hewa kupita kwenye jeraha
- kusababisha vijidudu kuingia kwenye jeraha
- kuongeza malengelenge.
Choose Answer
6. Huduma ya kwanza hutolewa kwa lengo gani?
- Kushusha gharama za matibabu
- Kuonesha umahiri wa kitabibu
- Kuokoa maisha ya wagonjwa
- Kurahisisha matibabu
- Kupunguza idadi ya madaktari.
Choose Answer
7. Huduma ipi ya kwanza kati ya zifuatazo hutolewa kwa mtu aliyekazwa na misuli?
- Kumfanyisha mazoezi ya viungo
- Kumpumzisha kitandani
- Kufunga misuli kwa bandeji
- Kumpa dawa ya kutuliza maumivu
- Kuchua polepole misuli husika
Choose Answer
8. Kifaa kifuatacho siyo muhimu kuwemo katika sanduku Ia huduma ya kwanza
- Wembe
- Pimajoto
- Mkasi
- Kijiko
- Kibanio
Choose Answer
9. Ipi kati ya sentensi zifuatazo inatoa maana ya huduma ya kwanza?.............
- Msaada wa haraka anaopewa mtu kabla ya kwenda hospitali.
- Msaada wa haraka anaopewa mtu baada ya kufika hospitali.
- Msaada wa haraka unaotolewa kwa mtu na mtaalamu wa afya.
- Msaada unaotolewa kwa mtu aliyezirai.
- Msaada unaotolewa kwa mtu aliyeumwa na nyoka.
Choose Answer
10. Je nini utakachokifanya ikiwa utaona nguo alizovaa rafiki yako zinaungua kwa moto?..........
- Kumpaka mafuta
- Kumweka maji kwenye jeraha
- Kumfunika kwa blanketi au nguo nzito
- Kumpulizia hewa ya oksijeni
- Kumvua nguo zilizokwisha ungua
Choose Answer
Andika NDIYO kwa sentensi iliyo sahihi na HAPANA kwa sentensi isiyo sahihi.
- Unatakiwa kuikata au kuichanjaa sehemu iliyoumwa na nyoka na kufyonza sumu………
View Answer
- Unatakiwa kugandamiza tumbo la mtu aliyezama kwenye maji akiwa amelala kifudifudi………..
View Answer
- Usijaribu kurudisha ndani mfupa uliovunjika wakati wa kutoa huduma ya kwanza…………..
View Answer
- Tangawizi na limau husaidia kuondoa kichefuchefu kwa mtu anayetapika………….
View Answer
- Msaidie mtu aliyezama kwenye maji kupumua kwa kupiliza pumzi kwa nguvu kwa kutumia mdomo kwa mdomo………..
View Answer