MTIHANI WA KUJIPIMA WA MADA

MAARIFA YA JAMII DARASA LA SITA

RASILIMALI ZA TANZANIA

Chagua Jibu Sahihi

1. Vitu viwili vinavyopatikana katika mazingira ya nyumbani ni:

  1. vitanda na madawati
  2. madarasa na maktaba
  3. vitanda na vyombo vya jikoni
  4. mlingoti wa bendera na vitanda
  5. viwanja vya michezo na madarasa
Choose Answer


2.Watu wanaoishi kandokando mwa bahari na maziwa hujihusisha na shughuli za:

  1. kilimo
  2. uvuvi
  3. uvunaji magogo
  4. ufugaji
  5. usafirishaji
Choose Answer


3. Mbuga za wanyama zinazopatikana Tanzania ni:

  1. Serengeti, Ruaha na Mikumi
  2. Tarangire, Katavi na Ngorongoro
  3. Serengeti, Manyara na Ngorongoro
  4. Selous, Serengeti na Mikumi
  5. Mkomazi, Selous na Ngorongoro
Choose Answer


4. Uvuvi usio endeleevu waweza kusababisha yafuatayo kasoro:

  1. vifo vya watu
  2. vifo vya samaki
  3. uchafuzi wa maji
  4. umaskini
  5. utajiri
Choose Answer


5. Zao la mkonge hulimwa katika mikoa ipi Tanzania? ....... .

  1. Tanga na Mbeya.
  2. Morogoro na Pwani.
  3. Morogoro na Tanga.
  4. Kilimanjaro na Manyara.
  5. Mtwara na Singida
Choose Answer


6. TPC Moshi, Kagera, Mtibwa na Kilombero ni mfano wa viwanda vinavyozalisha:

  1. Saruji
  2. Sukari
  3. Sigara
  4. Mabati
  5. Kahawa
Choose Answer


7. Uoto unaopatikana katika eneo la ikweta ni

  1. uoto wa savana
  2. vichaka vyenye nyasi ndefu
  3. misitu minene
  4. misitu minene na nyasi fupi
  5. vichaka na nyasi fupi.
Choose Answer


8. Mikoa ipi ina mashamba makubwa ya Chai?

  1. Pwani, Njombe na Iringa
  2. Ruvuma na Morogoro
  3. Morogoro, Njombe na Iringa.
  4. Kilimanjaro na Mbeya
  5. Mbeya, Njombe na Iringa
Choose Answer


9. Mikoa inayolima zao la ndizi Tanzania ni:

  1. Kagera, Kilimanjaro na Mbeya
  2. Mbeya, Kagera na Lindi
  3. Kagera, Singida na Shinyanga
  4. Arusha, Morogoro na Shinyanga
  5. Singida, Lindi na Kagera
Choose Answer


10. Ranchi ni eno lililotengwa kwa:

  1. kilimo cha mazao
  2. machinjio ya ngombe
  3. ufugaji wa ngombe
  4. josho la ngombe
  5. kuotesha majani
Choose Answer


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256