MTIHANI WA MWISHO WA MADA

URAIA NA MAADILI LA SABA

KUIPENDA NA KUJIVUNIA NCHI YAKO

MADA YA TATU

Chagua jibu sahihi.

  1. Lipi kati ya yafuatayo ni kitendo kisicho cha kudumisha amani katika jamii?
  1. Kutii sheria bila shuruti
  2. Kukemea vitendo viovu
  3. Kulinda mipaka ya nchi
  4. Kutotumia mitandao ya kijamii kulingana na sheria
Choose Answer


  1. Kati ya vitendo vifuatavyo kimojawapo si kitendo cha kusaidia kuhamasisha amani kwenye jamii
  1. Kubishana na majirani zako
  2. Kutumia mitandao ya kijamii kupinga ubaguzi
  3. Kutumia mikutano na semina kujadili umoja
  4. Kuandaa kisamafunzo na ngonjera kuhamasisha upendo katika jamii
Choose Answer


  1. Kujisitiri na kuwasitiri wengine vinasaidiaje jamii?
  1. Kuhamasisha amani katika jamii
  2. Kuthamini utu
  3. Kutokujipenda sana
  4. Kujipenda kwanza na wengine baadaye
Choose Answer


  1. Kutenda haki husaidia kulinda uhuru na umoja wa taifa kwa sababu gani?
  1. Viongozi wa nchi hutoa maagizo
  2. Watu huwa na uhuru wa kufanya lolote walipendalo
  3. Raia huwa huru kufanya ugaidi
  4. Wananchi huipenda nchi yao
Choose Answer


  1. Jukumu la kulinda uhuru na umoja wa taifa letu ni jukumu la nani?
  1. Usalama wa Taifa tu
  2. Polisi tu
  3. Idara ya uhamiaji tu
  4. Kila mwananchi
Choose Answer


Andika “kweli” kwa sentensi iliyo sahihi na “si kweli” kwa sentensi isiyo sahihi.

  1. Amani ni hali ya uhasama baina ya mtu na mtu au jamii na jamii nyingine……………
  2. Choose Answer


  3. Kutii sheria bila shuruti ni mojawapo ya vitendo vya kudumisha amani katika jamii……….
Choose Answer


  • Mitandao ya kijamii inaweza kutumika kama njia mojawapo ya kuhamasisha amani katika jamii………….
  • Choose Answer


  • Kuthamini utu ni hali ya kutoheshimu mtu mwingine………..
  • Choose Answer


    1. Kutenda haki ni mojawapo ya vitendo vya kuthamini utu…………
    2. Choose Answer


    Download Learning
    Hub App

    For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256