MTIHANI WA MWISHO WA MADA

URAIA NA MAADILI LA SABA

KUTEKELEZA MAJUKUMU KATIKA JAMII

MADA YA SABA

Chagua jibu sahihi.

  1. Kulisha mifugo bila kuathiri mazingira ni mojawapo ya namna mwanafunzi anavyoweza kushiriki katika kutoa huduma gani?
  1. Huduma binafsi
  2. Huduma za shule
  3. Huduma za jamii
  4. Huduma za serikali
Choose Answer


  1. Mwanafunzi anawezaje kushiriki kazi ya ujenzi wa miundombinu ya barabara?
  1. Kuendesha mitambo ya kujenga barabara
  2. Kulima barabara na kufukia mashimo katikati ya barabara
  3. Kukagua na kubaini mashimo ya barabara tu
  4. Kuwaelimisha mafundi ujenzi namna ya kujenga barabara
Choose Answer


  1. Kutunza vyanzo vya maji kama mito, maziwa na bahari huleta faida gani katika jamii?
  1. Husaidia wasiojiweza kupata huduma za maji
  2. Kufanya maji yaishe haraka ili kutafuta vyanzo vingine
  3. Kuongeza wigo wa upatikanaji wa maji ya uhakika
  4. Hupunguza upatikanaji wa maji na shughuli za uzalishaji mali
Choose Answer


  1. Ipi kati ya zifuatazo si faida ya kushiriki kutekeleza majukumu katika jamii?
  1. Kujenga ari ya kujitolea
  2. Kujenga maarifa na ujuzi mpya
  3. Kuongeza utengano katika jamii
  4. Kujenga tabia ya kutumia muda ipasavyo
Choose Answer


  1. Ipi kati ya yafuatayo siyo matumizi sahihi ya fedha kwa mwanafunzi kutekeleza majukumu yake katika jamii?
  1. Kutumia fedha kwa ajili ya matembezi na kula vyakula vizuri
  2. Kuanzisha shughuli mbalimbali za uzalishaji mali kama kilimo
  3. Kununua vifaa kwa ajili ya kutekeleza shughuli za kilimo
  4. Kutumia fedha kujifunza mafunzo ya ujasiriamali ili kupata maarifa ya uwekezaji
Choose Answer


Andika “kweli” kwa sentensi iliyo sahihi na “si kweli” kwa sentensi isiyo sahihi.

  1. Mwanafunzi anatakiwa ahudhurie shule na kushiriki katika kutekeleza majukumu katika jamii anamoishi……….
  2. View Answer


  3. Kitendo cha mwanafunzi kusaidia kazi shuleni ni namna mojawapo ya kushiriki katika kutekeleza majukumu katika jamii yake………..
  4. View Answer


  5. Kushiriki katika shughuli za ujenzi wa miundombinu ya shule ni kupoteza muda wa masomo…………
  6. View Answer


  7. Kushiriki katika kufundisha wanajamii kusoma, kuandika na kuhesabu ni jukumu la mwanafunzi tu………….
  8. View Answer


  9. Fedha, muda, watu, mifugo na vyombo vya usafiri ni rasilimali………….
View Answer


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256