MTIHANI WA KUJIPIMA WA MADA

SAYANSI DARASA LA SITA

MFUMO WA UZAZI

Jibu maswali yafuatayo

Sehemu A

  1. Kuna njia kuu……….za uzazi wa mpango.
  1. Nne
  2. Tatu
  3. Nyingi
  4. Mbili
Choose Answer


  1. …………….huzalisha gameti ume.
  1. Ovari
  2. Korodani
  3. Tezidume
  4. Falopio
Choose Answer


  1. Njia salama na isiyo na athari ya uzazi wa mpango ni……………
  1. Kutofanya ngono
  2. Kufanya ngono
  3. Njia za kisasa za uzazi wa mpango
  4. Njia zote za uzazi wa mpango
Choose Answer


  1. …………..ni kasoro katika mfumo wa uzazi.
  1. Pacha
  2. Ugumba
  3. Vvu na ukimwi
  4. Magonjwa ya ngono
Choose Answer



5. Njia za uzazi wa mpango ambazo ni salama kwa afya ya mama ni.............

  1. kitanzi na sindano 
  2. njia ya asili
  3. sindano na vidonge 
  4. vidonge na kondomu
  5.  kondomu na sindano
Choose Answer



6. Uzazi wa mpango una umuhimu gani kwa familia?

  1. Huwezesha familia kumiliki nyumba
  2. Huongeza idadi ya watoto
  3. Huwezesha familia kumudu safari za pamoja
  4. Huwafanya wanafamilia kuwa na furaha
  5. Huwezesha familia kupata chakula cha kutosha.
View Answer


7. Magonjwa ya zinaa huambukizwa kwa njia ya:

  1. kugusana 
  2. kupeana damu
  3. kucheza pamoja 
  4. kuchangia vikombe
  5. kujamiiana
View Answer


8. Sehemu zifuatazo hufanya kazi sawa ya kuhifadhi gamete za uzazi kwa binadamu:

  1. mirija ya falopio na mirija ya manii
  2. uume na uke
  3. korodani na uterasi
  4. ovari na uume
  5. ovari na korodani
View Answer



9. Ipi ni njia bora ya asili ya uzazi wa mpango?

  1. Kutumia kondomu wakati wa kujamiiana
  2. Kutumia njia ya kitanzi
  3. Kutumia sindano
  4. Kutumia vidonge vya uzazi wa majira
  5. Kutojamiiana katika kipindi cha hatari
View Answer


10. Baada ya utungisho, kitoto chura huitwa:

  1. lava 
  2. buu 
  3. tunutu 
  4. tedipoli
  5. yai
View Answer


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256