MTIHANI WA KUJIPIMA WA MADA
MAARIFA YA JAMII DARASA LA SITA
MATUMIZI YA RAMANI
Chagua Jibu Sahihi
1. Ipi kati ya zifuatazo ni sifa ya ramani?
- Huonesha pande zote za kitu
- Urefu wa kitu huoneshwa
- Umbo la asili la kitu hubakia
- Rangi ya asili ya kitu huonekana
- Huonesha sura ya juu ya kitu.
Choose Answer
2.Sehemu ya muhimu ya ramani inayoelezea kuhusu alama zilizotumiwa katika ramani ni
- ufunguo
- fremu
- dira
- kipimio
- kichwa cha ramani
Choose Answer
3. Katika kuonesha mahali kwa kutumia mistari ya gridi katika ramani huanza kusomwa namba za mstari gani? .
- Ulalo halafu wima.
- Wima halafu ulalo.
- Kushoto halafu kulia.
- Kulia halafu juu.
- Kulia halafu kushoto.
Choose Answer
4. Iwapo umbali wa kilometa 25 kwenye ardhi unawakilishwa na urefu wa sentimeta 5 kwenye ramani. Kipimo cha ramani ni ...
- 1:20000
- 1:100000
- 1:50000
- 1:500000
- 1:10000
Choose Answer
5. Picha iliyopigwa katika uoto wa savanna huonesha ...
- misitu minene.
- nyasi ndefu.
- miti iliyochongoka juu.
- miti yenye umbile la mwavuli.
- nyasi fupi.
Choose Answer
6. Mambo muhimu katika ramani ni
- uoto, dira kipimio, mistari na jina la ramani.
- rangi, jina la ramani, kipimio, ufunguo na fremu.
- mistari, jina la ramani, dira, fremu na kipimio.
- jina la ramani, ufunguo, fremu, kipimio na dira.
- jina la ramani, ufunguo, kipimio, dira na mistari.
Choose Answer
7. Kipimo kidogo cha ramani hutumika kuchorea
- maeneo madogo
- maeneo makubwa
- maeneo ya kati tu
- maeneo madogo na ya kati
- maeneo madogo na makubwa
Choose Answer
8. Kitu muhimu katika ramani kinachotumika kuonesha uwiano wa umbali katika ramani na umbali halisi kwenye ardhi huitwa.
- Skeli
- Dira
- Ufunguo
- Fremu
- Jina la ramani
Choose Answer
9. Kipi kati ya vipimo vya ramani vifuatavyo kinawakilisha eneo dogo?................
- 1:50
- 1:500,000
- 1:50,000
- 1:5,000
- 1:500
Choose Answer
10. Matumizi sahihi ya mistari ya gridi kwenye ramani ni
- kuonesha mahali katika ramani
- kuonesha uelekeo wa Mashariki
- kuonesha umbali
- kupata muda
- kuonesha mwelekeo wa Kaskazini.
Choose Answer