MTIHANI WA MWISHO WA MADA

URAIA NA MAADILI LA SABA

KULINDA RASILIMALI KWA MASILAHI YA NCHI

MADA YA SITA

Chagua jibu sahihi.

  1. Kuendelea kwa tatizo la rushwa ni changamoto inayozikabili taasisi za Serikali na asasi zisizo za kiserikali kwa sababu gani?
  1. Wananchi wana Imani kwamba rushwa ni nzuri
  2. Wananchi wa Tanzania ni wakarimu
  3. Maadili na uadilifu unakosekana
  4. Watu wanataka kuwa na maendeleo binafsi na ya nchi
Choose Answer


  1. Taasisi zisizo za kiserikali zina wajibu gani katika jamii?
  1. Kuelimisha walioathiriwa na rushwa tu
  2. Kuwapa msaada wa kifedha walioathiriwa na matukio ya rushwa
  3. Kutoa elimu kwa umma juu ya madhara ya rushwa
  4. Kupambana na wanaotoa taarifa za rushwa kwenye jamii
Choose Answer


  1. Kuzuia na kupambana na rushwa nchini husaidia kukuza uchumi wa nchi na kuleta maendeleo katika uboreshaji wa jambo lipi katika Taifa?
  1. Miundombinu
  2. Masilahi ya watu wachache
  3. Watoa rushwa
  4. Afya za wapokea rushwa
Choose Answer


  1. Kwanini mitazamo tofauti ya madhara ya rushwa katika jamii hutokea?
  1. Utendaji duni wa kazi
  2. Elimu duni juu ya rushwa
  3. Ukosefu wa mipango
  4. Watoaji na wapokeaji wa rushwa kutoshitakiwa
Choose Answer


  1. Kipi kati ya yafuatayo si madhara ya rushwa kwa rasilimali za nchi?
  1. Kukosekana kwa mipango thabiti ya kulinda rasililimali
  2. Ukosefu wa huduma bora kwa wananchi
  3. Thamani halisi ya rasilimali kutojulikana
  4. Kuimarika kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na rushwa
Choose Answer


Andika “kweli” kwa sentensi iliyo sahihi na “si kweli” kwa sentensi isiyo sahihi.

  1. Asasi zisizo za kiserikali zina jukumu la kupambana na rushwa zote kasoro rushwa ya ngono…………
  2. View Answer


  3. Kukosekana kwa maadili na uadilifu katika jamii ni chanzo kikubwa cha kushamiri kwa rushwa nchini…………..
  4. View Answer


  5. Ufanisi katika ujenzi wa miundombinu katika nchi yetu ni ishara ya mafanikio katika mapambano dhidi ya rushwa……………
  6. View Answer


  7. Mapambano dhidi ya rushwa ni kazi ya Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa tu…………..
  8. View Answer


  9. Ukiukwaji wa haki za binadamu ni matokeo ya kushamiri kwa utoaji na upokeaji wa rushwa katika jamii…………
  10. View Answer


  11. Baadhi ya watumishi wa serikali hupoteza Ushahidi wa mienendo ya uchunguzi wa rushwa kwa masilahi ya nchi…………
  12. View Answer


  13. Ili taifa liweze kuendelea ni lazima rushwa ipigwe vita katika sehemu za kazi tu………….
  14. View Answer


  15. Asasi zisizo za serikali zinasaidia kutoa elimu dhidi ya rushwa kwa wananchi……….
  16. View Answer


  17. Mjadala ya wazi dhidi ya rushwa huwajengea wananchi uwezo wa kupambana na rushwa……….
  18. View Answer


  19. Mapambano dhidi ya rushwa katika kulinda rasilimali za nchi ni jukumu la serikali tu…………
View Answer


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256