MTIHANI WA MWISHO WA MADA

URAIA NA MAADILI LA SABA

KUJIJALI NA KUWAJALI WENZETU

MADA YA NNE

Chagua jibu sahihi.

  1. Lipi kati ya yafuatayo si lengo sahihi la elimu ya afya ya uzazi?
  1. Kusaidia kuondoa mila potofu zinazoathiri afya ya uzazi
  2. Kupunguza idadi ya watu wasio na ajira duniani
  3. Kuepusha mimba za utotoni
  4. Kuwajengea vijana uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya mwili katika makuzi
Choose Answer


  1. Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania lilianzishwa mwaka gani?
  1. 1975
  2. 1993
  3. 2005
  4. 2007
Choose Answer


  1. Ipi ni hatua ya hadhari ya kuchukua kabla ya janga la moto kutokea?
  1. Kuziba mdomo na blanketi
  2. Kuwapa majeruhi matibabu
  3. Kujenga nyumba zenye milango na madirisha ya mbele
  4. Kujenga nyumba zenye milango na madirisha ya dharura
Choose Answer


  1. Ni jaribio lipi hatari Zaidi linaloweza kuleta na kusababisha mlipuko wa moto katika maeneo yetu?
  1. Matumizi ya mkaa wa kisasa
  2. Kutumia jiko la mafuta ya taa kwa uangalifu
  3. Kuwasha jiko la gesi bila kuzingatia taratibu za kiusalama
  4. Majibu a, b na c yote ni sahihi
Choose Answer


Andika “kweli” kwa sentensi iliyo sahihi na “si kweli” kwa sentensi isiyo sahihi.

  1. Unapoona janga la moto kwenye nyumba unapoishi haraka kimbilia chumbani ukachomoe redio kwenye swichi ya umeme ili kuokoa isiungue………..
  2. View Answer


  3. Ili kuharakisha shughuli ya kujiokoa na kuwaokoa wenzako walio ghorofani ni vizuri ukatumia lifti kama nyenzo ya kujiokoa kwa haraka Zaidi………….
  4. View Answer


  5. Elimu ya zimamoto na uokoaji hutolewa madarasani tu kwa kuwa ndipo walipo wanafunzi wengi……….
  6. View Answer


  7. Elimu ya afya ya uzazi husaidia kuepusha mimba za utotoni…………
  8. View Answer


  9. Blanketi si kifaa muhimu cha uokoaji katika majanga ya moto…………
View Answer


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256