MTIHANI WA MWISHO WA MADA

URAIA NA MAADILI LA SABA

KUAMINIKA KATIKA JAMII

MADA YA KUMI NA MBILI

Chagua jibu sahihi.

  1. Ni faida gani mwanafunzi hupata anapotimiza jukumu la kuhudhuria shuleni na kujifunza masomo yote darasani?
  1. Kutokuhudhuria baadhi ya vipindi darasani
  2. Kushirikiana na wenzake
  3. Kujifunza kikamilifu na kushiriki shughuli nyingine kama michezo
  4. Kuonesha wenzake njia kimasomo
Choose Answer


  1. Kujikinga na tabia hatarishi kama utumiaji wa dawa za kulevya na ngono huashiria nini kwa mwanafunzi?
  1. Anajituma
  2. Anawahi shuleni
  3. Ni kiongozi
  4. Anajitambua
Choose Answer


  1. Ipi ni mojawapo ya ishara ya kuheshimu sheria za shule?
  1. Kuchelewa shule
  2. Kuchonganisha wanafunzi wenzako
  3. Kufuata sheria za shule
  4. Kuheshimu wakubwa tu
Choose Answer


  1. Ipi kati ya vitendo vifuatavyo kinaonesha umuhimu wa kuheshimu Imani na itikadi za wengine?
  1. Kubeza Imani za wengine
  2. Kuchonganisha watu kwenye jamii
  3. Kuishi bila kubaguana kwa misingi ya kiimani na kiitikadi
  4. Kuishi kwa raha bila ykujali vurugu za kiitikadi
Choose Answer


ol start="5" type="1">
  • Kutunza mali za shule kunamaanisha nini?
    1. Mojawapo ya kitendo cha ujasiri
    2. Mojawapo ya vitendo vinavyoleta kuaminika shuleni na katika jamii
    3. Mojawapo ya vitendo vya umashuhuri shuleni
    4. Mojawapo ya vitendo vya kizalendo kwa familia kwa mwanafunzi
    Choose Answer


    Andika “kweli” kwa sentensi iliyo sahihi na “si kweli” kwa sentensi isiyo sahihi.

    1. Uaminifu ni nguzo muhimu inayokuwezesha kuishi na kukabilika kwa wenzako katika mazingira ya shule na jamii kwa ujumla………..
    2. View Answer


    3. Kutii sheria za shule humwezesha mwanafunzi kutokuaminika shuleni na katika jamii yake………………
    4. View Answer


    5. Kubeza Imani na itikadi za watu wengine ni namna ya kuheshimu wengine…………
    6. View Answer


    7. Faida mojawapo ya uchaguzi shuleni ni kusaidia wanafunzi kujifunza demokrasia kwa vitendo………..
    8. View Answer


    9. Mwanafunzi unapojitambua vyema hukusaidia kufikia malengo maalumu unayotaka kuyatimiza katika Maisha yako…………
    View Answer


    Download Learning
    Hub App

    For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256