MTIHANI WA KUJIPIMA WA MADA

URAIA NA MAADILI A TANO

KUSHIRIKIANA NA MATAIFA MENGINE

Chagua jibu sahihi

  1. Ipi sio manufaa ya ushirikiano wa Tanzania na Mataifa Mengine?
  1. Kupata masoko ya bidhaa
  2. Kuboresha usalama na amani
  3. Kupata mikopo
  4. Kupoteza utamaduni wake
Choose Answer


  1. Sera ya Tanzania ya Uhusiano wa kimataifa ilitungwa mwaka
  1. 1995
  2. 1977
  3. 2015
  4. 2005
Choose Answer


  1. Kipi hakipo kwenye sera ya Tanzania ya uhusiano wa kimataifa?
  1. Kulinda uhuru na usalama wa nchi
  2. Kuimarisha umoja wa mataifa na ushirikiano
  3. Kumaliza upinzani
  4. Kupigania uboreshaji wa umoja wa mataifa
Choose Answer


  1. Mojawapo ya changamoto za ushirikiano wa umoja wa mataifa ni;
  1. Mikopo yenye riba kubwa
  2. Migogoro ya mipaka
  3. Ujirani mwema
  4. Kukuza biashara
Choose Answer


5.Umoja wa hiari wa nchi huru zilizowahi kutawaliwa na Uingereza hufahamika kama:

  1. Jumuiya ya Madola
  2. Umoja wa Mataifa
  3. Nchi zinazoendelea
  4. Umoja wa Afrika
  5. Shirikisho la Mataifa
Choose Answer


6.Tanzania inapata faida gani kwa kuongeza biashara yake ya kimataifa?

  1. Kuongeza majengo
  2. Kupunguza wajasiriamali wa ndani
  3. Kuongeza deni
  4. Kupunguza mikataba ya kibiashara
  5. Kuongeza fedha za kigeni
Choose Answer


7.Mojawapo ya udhaifu wa Umoja wa Mataifa ni:

  1. kushindwa kuzuia kuenea kwa Utandawazi
  2. Waafrika hawajawahi kupata nafasi katika uongozi wa juu katika Umoja wa Mataifa
  3. baadhi ya watu tu ndio wenye kura ya turufu
  4. kushindwa kupitisha maazimio ya haki za binadamu
  5. kutokushirikishwa kwa Waafrika katika vikao vya baraza la usalama
Choose Answer


8.Ni chombo gani chenye jukumu la kumchagua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa?

  1. Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa.
  2. Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
  3. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
  4. Sekretarieti ya Umoja wa Mataifa.
  5. Mahakama Kuu ya Kimataifa.
Choose Answer


9. Makubaliano ya kuanzisha Umoja wa Mataifa yalifanyika

  1. New York
  2. San Francisco
  3. C. San Diego
  4. Washington
  5. Los Angeles
Choose Answer


10. Zipi kati ya nchi zifuatazo ni wanachama wa Jumuiya ya Madola?................

  1. Botswana na Burundi
  2. Botswana na Zambia
  3. Kenya na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
  4. Malawi na Burundi
  5. Zambia na Jamhuri ya Kidemkrasia ya Kongo
Choose Answer


Andika KWELI kwa sentensi iliyo sahihi na SI KWELI kwa sentensi isiyo sahihi.

  1. Ni marufuku kwa nchi iliyo na uchumi wa chini kujiunga na jumuiya ya Afrika Mashariki………..
  2. View Answer


  3. Mtanzania anatakiwa kufanya biashara zake hapa nchini tu……….
  4. View Answer


  5. Uhusiano wa Tanzania na Kenya umesaidia kuboresha uchumi wa nchi hizo mbili………..
  6. View Answer


  7. Umoja wa mataifa hutoa msaada wa kifedha kwa nchi wanachama kupitia jumuiya zake……..
  8. View Answer


  9. Tanzania hunufaika na uhusiano wa kibalozi na mataifa mengine kiutamaduni……..
View Answer


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256