MTIHANI WA KUJIPIMA WA MADA

URAIA NA MAADILI A TANO

KUWA MWADILIFU

 

Chagua jibu sahihi

  1. Kanuni zinazowekwa shuleni na nyumbani husaidia nini?
  1. Kufuata utaratibu na kudhibiti nidhamu
  2. Ukiukaji wa haki za mtoto
  3. Ubabe wa wazazi au walezi
  4. Kuleta fujo
Choose Answer


  1. Lipi kati ya haya yaliyoorodheshwa ni tendo la kutetea haki zako na za Watoto wenzako:
  1. Kukosekana utawala bora
  2. Kutii sheria na kutozitumia
  3. Kusaidia kutoa taarifa kwenye mamlaka zinazohusika
  4. Kulia kwa uchungu
Choose Answer


  1. Ipi kati ya tabia zilizoorodheshwa inaonesha uvunjifu wa sheria za shule?
  1. Kuwahi sana shuleni
  2. Kusoma kwa bidi
  3. Utoro na kupigana
  4. Kujisomea nyumbani baada ya masomo
Choose Answer


  1. Unafiki ni nini?
  1. Hali ya ukweli na uwazi
  2. Kujenga hali ya uwajibikaji
  3. Uongo na uzembe
  4. Kujifanya rafiki wakati ni adui
Choose Answer


  1. Yafuatayo ni madhara ya kutokuwa muwazi:
  1. Kusifiwa na kuharibu
  2. Kuleta migongano
  3. Uzembe na uhalifu
  4. Mshikamano na uvivu
Choose Answer


  1. Kipi kati ya vifuatavyo ni chombo cha kisheria kinachohusika na kusimamia haki?
  1. Polisi
  2. Bunge
  3. Shule
  4. Mahakama
Choose Answer


  1. Ipi kati ya zifuatazo ni sababu za ongezeko la matendo ya ukiukwaji wa haki za binadamu?
  1. Kulipa kodi stahiki
  2. Watoto kutopelekwa shule za bweni
  3. Watu kujichukulia sheria mkononi
  4. Upendo kwa watu wenye mahitaji maalumu
Choose Answer


  1. Hali ya kuficha au kutoonesha uhalisia wa ukweli katika jambo fulani huitwa:
  1. Uwongo
  2. Unafiki
  3. Umahiri
  4. Ujanja
Choose Answer


  1. Hali au tabia ya kuzungumza bila kificho huitwa?
  1. Unafiki
  2. Lofa
  3. Uwazi
  4. Uzabinazabina
Choose Answer


 

Jibu KWELI au SI KWELI katika sentensi hizi

  1. Taarifa zote za mitandaoni zinazingatia maadili…………
  2. View Answer


  3. Ukitumia vizuri mitandao unaweza kujenga ujuzi na maarifa………….
  4. View Answer


  5. Ukitumia vibaya mitandao unaweza kushtakiwa kwa mujibu wa sheria…………
  6. View Answer


  7. Sheria ni kanuni au utaratibu uliotungwa na chombo chenye mamlaka ili kutosimamia taratibu za mahali Fulani………..

 

View Answer


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256