MTIHANI WA KUJIPIMA WA MADA

SAYANSI DARASA LA NNE

KINGA YA MWILI

Chagua Jibu Sahihi

1. Ni ugonjwa upi unaotokana na ukosefu wa madini joto (ayodini) mwilini?

  1. Surua
  2. Goita
  3. UKIMWI
  4. Matege
Choose Answer



2. Ni kundi lipi linalowakilisha vyakula vinavyoupa mwili nguvu na joto......

  1. Mkate, maziwa na mboga za majani
  2. Maembe, karoti na mboga za majani
  3. Mihogo, viazi mviringo na mahindi
  4. Nyama, mahindi na maharagwe
Choose Answer


3. Nywele chafu huwa ni makazi ya

  1. chawa
  2. inzi
  3. kunguni
  4. kupe
Choose Answer



4. Ugonjwa wa hatari zaidi unaosababishwa kwa kufaya ngono zembe ni

  1. kaswende
  2. UKIMWI
  3. kisonono
  4. Ebola
Choose Answer


5. Ni sehemu gani ya damu inatumiwa kulinda mwili?

  1. Plasma
  2. Chembe hai nyekundu
  3. Chembe hai nyeupe
  4. Ngozi
Choose Answer


6. Kinga ya mwili inaweza kuimarishwa kwa:

  1. Kupata chanjo
  2. Kupumzika
  3. Kutofanya mazoezi
  4. Kuimba
Choose Answer


7. Chakula gani kinasaidia kuongeza kinga ya mwili?

  1. Madini
  2. Vitamini
  3. Protini
  4. Wanga.
Choose Answer


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256