MTIHANI WA KUJIPIMA WA MADA

MAARIFA YA JAMII DARASA LA SITA

UHUSIANO WA TANZANIA NA NCHI ZA AFRIKA

Chagua jibu lililo sahihi Zaidi na kisha kulijaza katika sehemu iliyo wazi.

  1. Baadhi ya viombo muhimu vinavyosaidia kuendesha Jumuiya ya Afrika Mashariki ni……….na………..
  1. Bunge na spika wa bunge
  2. Bunge na mahakama
  3. Mahakama na majaji
  4. Soko la Pamoja na ushuru wa forodha
Choose Answer


  1. Kufanya uchunguzi wa kina kabla ya kuanzisha uhusiano na nchi husaidia nini?
  1. Kufahamu utajiri wa nchi inayohusika ili kufaidika
  2. Kubaini usalama wa nchi inayohusika na tahadhari za kuchukua
  3. Kusaidia wananchi wanaopata shida
  4. Kutekeleza makubaliano
Choose Answer


  1. Nchi za kwanza kuanzisha uhusiano na Tanganyika wakati wa ukoloni ni……na……
  1. Kenya na Msumbiji
  2. Uganda na Rwanda
  3. China na Msumbiji
  4. Kenya na Uganda
Choose Answer


  1. Umoja wa Afrika (AU) uliundwa mwaka gani?
  1. 1964
  2. 2012
  3. 2002
  4. 1963
Choose Answer


  1. Wanachama waanzilishi wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) walikuwa:
  1.  nchi huru za Afrika ya Kati
  2.  nchi huru za Afrika          
  3. nchi huru za Afrika ya Kaskazini 
  4. nchi huru za Afrika ya Magharibi 
  5. nchi huru kusini mwa Afrika.
Choose Answer


  1. Umoja wa hiari wa nchi huru zilizowahi kutawaliwa na Uingereza hufahamika kama:
  1.  Jumuiya ya Madola         
  2. Umoja wa Mataifa
  3. Nchi zinazoendelea   
  4. Umoja wa Afrika
  5.  Shirikisho la Mataifa
Choose Answer


  1. Mojawapo ya udhaifu wa Umoja wa Mataifa ni:
  1.  kushindwa kuzuia kuenea kwa Utandawazi
  2.  Waafrika hawajawahi kupata nafasi katika uongozi wa juu katika Umoja wa Mataifa
  3.  baadhi ya watu tu ndio wenye kura ya turufu
  4.  kushindwa kupitisha maazimio ya haki za binadamu
  5.  kutokushirikishwa kwa Waafrika katika vikao vya baraza la usalama
Choose Answer


  1. Makao makuu ya Umoja wa Mataifa (UN) yapo:
  1.  New York 
  2.  San Francisco
  3.  San Diego         
  4.  Washington 
  5.  Los Angeles
Choose Answer


  1. Moja ya faida ya uhusiano wa kibiashara kati ya Tanganyika na jamii nyingine ilikuwa
  1. kukua kwa miji ya pwani ya Afrika Mashariki kama Kilwa na Lagos
  2. kukua kwa dola za Afrika Mashariki kama vile Buganda na Songhai
  3. kupatikana kwa bidhaa zilizokuwa hazizalishwi nchini
  4. kuingizwa kwa silaha Tanganyika
  5. kukomeshwa kwa biashara ya utumwa
Choose Answer


  1. Rais wa kwanza wa Bunge la Umoja wa Afrika lililoanzishwa Machi 2004 ni
  1. Dr. Salim Salim 
  2. Dr. Emek Anyauko
  3.  Mh. Getrude Mongela 
  4. William Erek 
  5. Peter Omu
Choose Answer


Andika “kweli” kwa sentensi ambayo ni sahihi na “si kweli” kwa sentensi ambayo siyo sahihi.

  1. Tanzania ina nchi marafiki ndani na nje ya Afrika………..
  2. View Answer


  3. Ushirikiano wa nchi za Afrika Mashariki ulianza mwaka 1967……….
  4. View Answer


  5. Lengo mojawapo la jumuiya ya zamani ya Afrika Mashariki ilikuwa  ni  kuzifanya nchi zote kuwa za kijamaa………..
  6. View Answer


  7. Kubadilishana wataalamu kati ya nchi na nchi kutasaidia nchi za Kiafrika kuwa na uchumi imara………….
  8. View Answer


  9. Kuboresha ushirikiano wa kiuchumi na kiteknolojia ni njia ya kuimarisha uhusiano wa kisiasa kati ya nchi na nchi………..
View Answer


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256