MTIHANI WA KUJIPIMA WA MADA

MAARIFA YA JAMII DARASA LA SITA

MAJANGA YATOKANAYO NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA

Chagua Jibu Sahihi

1. Ipi kati ya majanga yafuatayo husababishwa na mwanadamu na pia nguvu za asili?

 1.  Kimbunga      
 2. Mlipuko wa volkano
 3. Milipuko wa mabomu 
 4. Moto 
 5. Vita
Choose Answer


2.      Maji ya mvua yanaweza kukingwa na kuhifadhiwa kwa matumizi ya baadaye kwa kutumia:

 1.  Ndoo na mabomba     
 2.  Chupa na majaba
 3. Visima na chupa    
 4. Visima na mapipa 
 5.  Ndoo na chupa
Choose Answer


3.  Ili kupunguza/kuondoa ongezeko la joto la dunia tunapaswa ......... 

 1. tuongeze utoaji wa hewa ya kabonidayoksaidi
 2. tuongeze hewa ya kabonidayoksaidi inayotolewa na wanyama
 3. tutumie vyanzo vya nishati vilivyo rafiki kwa mazingira
 4. tuchome vichaka, misitu na nyasi
 5.  tukate miti ili kupata eneo la kilimo
Choose Answer


4. Athari kuu za viwanda katika mazingira ni .....

 1.  kuchafua maji, hewa na harufu mbaya.
 2.  kutoa moshi na matumizi makubwa ya nguvu ya nishati. 
 3. uchafuzi wa hewa, udongo na harufu mbaya. 
 4. kumwaga kemikali na kutoa moshi. 
 5. uchafuzi wa hewa, maji na ardhi.
Choose Answer


5. Ipi kati ya zifuatazo ni njia ya kuzuia mafuriko? 

 1.  Kujenga nyumba imara.  
 2.  Kupanda miti.
 3.  Kukata miti.                           
 4.  Kuchoma misitu.
 5.  Kujenga nyumba mabondeni.
Choose Answer


6. Chanzo kikuu cha uharibifu wa mazingira barani Afrika ni

 1.  ongezeko la watu 
 2.  silaha za nyuklia
 3.  kilimo cha mazao ya chakula 
 4.  kilimo cha mazao ya biashara 
 5.  kilimo cha matuta kwenye miinuko
Choose Answer


7. Ongezeko Ia joto duniani, ukame, mafuriko na vimbunga ni matokeo ya athari zitokanazona

 1.  uharibifu wa mazingira
 2.  tsunami iliyotoka Asia
 3.  ongezeko kubwa Ia watu katika nchi za Ulaya
 4.  matumizi ya mabomu ya nyuklia
 5.  Mvua nyingi
Choose Answer


8. Wakati wa mvua kubwa inayoambatana na radi, watu hawaruhusiwi

 1.  kuvaa nguo nyekundu.......
 2.  kutumia miavuli 
 3.  kufungua milango na madirisha
 4.  kujificha chini ya mti 
 5.  kufunga luninga na redio
Choose Answer


9. Janga la kimazingira linalosababishwa na nguvu za asili pekee linaitwa

 1.  Ukame 
 2.  Tetemeko la ardhi
 3.  Mmomonyoko wa udongo 
 4.  Njaa
 5.  Uchafuzi wa mazingira
Choose Answer


10. Uchafuzi wa hewa katika maeneo ya makazi unaweza kuthibitiwa kwa: 

 1.  matumizi ya vyoo 
 2.  kuchoma takataka
 3.  kumwaga maji taka mitaani 
 4. kuchemsha maji ya kunywa
 5.  kupunguza matumizi ya mifuko ya plastiki
Choose Answer


Andika “kweli” kwa sentensi ambazo ni sahihi na “si kweli” kwa sentensi ambazo si sahihi

 1. Majanga husababishwa na shughuli za upandaji miti ya kutosha………
 2. View Answer


 3. Shughuli za binadamu zinazozalisha gesijoto ndio chanzo kikuu cha ongezeko la joto duniani………
 4. View Answer


 5. Matumizi ya nishati mbadala yanaweza kupunguza kasi ya uharibifu wa mazingira yetu…….
 6. View Answer


 7. Ujenzi holela huchochea mafuriko……….
 8. View Answer


 9. Uchimbaji wa mifereji na mitaro inayopeleka maji sehemu za mbali kunaweza kupunguza athari za mafuriko katika mazingira yetu……….
View Answer


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256