MTIHANI WA KUJIPIMA WA MADA

MAARIFA YA JAMII DARASA LA SITA

UTUNZAJI WA KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA

Chagua jibu lililo sahihi Zaidi

  1. ……..huonesha michoro na utamaduni wa watu wa kale.
  1. Sehemu zenye masalia ya kale
  2. Makumbusho ya Taifa
  3. Akiolojia
  4. Ofisi za Nyaraka
Choose Answer


  1. ……….ni sehemu katika tanzania lilipovumbuliwa fuvu la binadamu wa kale.
  1. Isimila (Iringa)
  2. Kondoa (Dodoma)
  3. Kaole (Pwani)
  4. Bonde la Olduvai (Arusha)
Choose Answer


  1. Waliovumbua fuvu la binadamu wa kwanza hapa Tanzania ni………na……….
  1. Dkt Mary George na Dkt George Lincolin
  2. Dkt Louis Leakey na Dkt Mary Leakey
  3. Dkt Gorge Louis na Dkt Mary Leakey
  4. Dkt Majid Said na Dkt Braghash Said
Choose Answer


4. Michoro ya mapangoni iliyoko Kondoa Irangi inasadikiwa kuchorwa wakati wa zama za

  1. mwanzo za mawe
  2. Kati za mawe
  3. Mwisho za mawe
  4. Chuma
  5. Ugunduzi wa moto
Choose Answer


5. Mtaalamu wa mambo wa kale aliyevumbua fuvu la binadamu wa kwanza Olduvai aliitwa

  1.  Charles Darwin 
  2.  Zinjathropus
  3.  Homo Habilis 
  4.  David Livingstone 
  5.  Louis Leakey
Choose Answer


6. Mojawapo wa faida ya utunzaji wa kumbukumbu kwa maandishi ni:

  1. Huduma kwa muda mfupi
  2. Taarifa hupotoshwa
  3. Huleta urahisi wa kupata taarifa
  4. Ni vigumu kutafsiri taarifa
Choose Answer


7. Mojawapo ya changamoto za kumbukumbu kwa njia ya maandishi ni

  1. Huharibika haraka
  2. Unahitaji masharti magumu
  3. Uandishi huchukua muda mrefu
  4. Ni rahisi kufanyia marekebisho
Choose Answer


8. maandiko ya kitaaluma yanayotokana na kufanya tafiti huitwa?

  1. Tovuti
  2. Wavuti
  3. Taaluma
  4. Tasnifu
Choose Answer


9. Ipi sio faida ya utunzaji kumbukumbu kutumia nakala laini?

  1. Kumbukumbu hupatikana katika uhalisia wake
  2. Huifadhi taarifa nyingi
  3. Ni rahisi kusambaza taarifa
  4. Ni rahisi kutunza
Choose Answer


10. ipi sio faida ya kutumia sehemu zenye masalia ya kale kama chanzo cha taarifa za kihistoria?

  1. Kutoa ajira
  2. Kuvutia watalii
  3. Kuleta utamaduni wa kigeni
  4. Kutoa taarifa za kihistoria kwa watafiti wa mambo ya kale
Choose Answer


Andika “kweli” kwa sentensi ambazo ni sahihi na “si kweli” kwa sentensi ambazo siyo sahihi

  1. Akiolojia ni sehemu za kuhifadhi kumbukumbu na zana zilizotumika wakati wa kale………..
  2. View Answer


  3. Upo uwezekano wa msimuliaji wa matukio ya kihistoria kupitia mazungumzo ya mdomo kuongeza au kupunguza maudhui kutokana na matakwa yake……..
  4. View Answer


  5. Ofisi za kutunza nyaraka za serikali zinahitaji wataalamu wabobezi ili utunzaji wa nyaraka hizo uwe endelevu…….
  6. View Answer


  7. Maendeleo ya sayansi na teknolojia yamesababisha njia za zamani za kutunza kumbukumbu za matukio ya kale kupitwa na wakati, hivyo kutotumika………
  8. View Answer


  9. Utunzaji wa kumbukumbu kwa njia ya kielekitroniki ni bora Zaidi kuliko kutumia nakala ngumu…….
View Answer


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256