KISWAHILI DARASA LA 4

SURA YA KWANZA.

UMAHIRI WA LUGHA

Katika sura hii utasoma habari kuhusu mahafali ya darasa Ia saba. Kutokana na habari hiyo utaweza kujifunza kuhusu maneno yenye maana za jumla. Pia, utajifunza maneno ya kundi moja na kuweza kuyatumia katika sentensi.

Ufahamu

Soma habari ifuatayo kisha jibu maswali.

Mahafali ya darasa Ia saba

Leo ni siku ya mahafali ya dada yangu Tunu. Amehitimu darasa la saba katika Shule ya Msingi Mtibwa. Jana mwalimu alitutangazia tuwahi shuleni kufanya usafi kabla wageni hawajafika.

Tulifika shuleni saa 12:30 asubuhi na tuligawana kazi kwa madarasa. Wanafunzi wa darasa Ia kwanza na la pili waliokota takataka eneo lute la shule. Wanafunzi wa darasa la tatu na la nne tulifagia madarasa na kupiga deki. Wanafunzi wa darasa la tano na la sita walikusanya kuni na kuchota maji. Wanafunzi wa darasa Ia saba hawakupangiwa kazi.

Wapishi waliandaa vyakula mbalimbali kwa ajili ya mahafali. Walipika pilau, wali, ndizi, nyama, njegere na maharage. Pia, walipika mboga za majani ambazo ni mchicha, kisamvu na majani ya kunde. Vilevile, waliandaa matunda kama mananasi, maembe na machungwa.

Jukwaa kubwa liliandaliwa kwa ajili ya wageni watakaokaa katika meta kuu. Pembeni mwa jukwaa hilo, kulikuwa na maturubai yaliyofungwa kwa ajili ya kivuli. Sehemu hiyo ilikuwa ni maalumu kwa wazazi na wageni waalikwa. Maeneo yote ya shule yalipambwa kwa maputo ya rangi ya bluu, kijani na nyekundu.

Ilipofika saa 3:00 asubuhi wazazi na wageni waalikwa walianza kuwasili. Tuliwakaribisha na kuwapeleka sehemu iliyoandaliwa kwa ajili yao. Wahitimu nao walikuwa tayari wameketi sehemu yao wakiwa wamevaa sare za shule.

Baada ya nusu saa Mgeni Rasmi aliwasili. Mwenyekiti wa kamati ya shule, mwalimu mkuu na wajumbe wa kamati ya shule walimpokea Mgeni Rasmi. Waliongozana naye hadi meza kuu. Wakati huo wote sisi sate tulisimama, tukipiga makofi, nderemo na vifijo vilisikika huku tukiimba wimbo ufuatao:

Karibuni wageni wetu, karibuni wageni x 2 Karibuni shule ya Mtibwa, karibuni wageni x2 Sisi ni nani jama, sisi wanafunzi x2

Taifa linatutegemea, wazazi wanatutegemea, Sisi wanafunzi.

Tuliimba wimbo huo hadi wageni walipokaa kwenye viti. Mshereheshaji alimkaribisha Mwalimu Mkuu kwa ajili ya kuwakaribisha na kuwatambulisha wageni. Baada ya utambulisho, vikundi mbalimbali vya burudani vilitumbuiza.Kulikuwa na nyimbo, maigizo, mashairi na ngonjera. Wageni waalikwa pamoja na wahitimu walifurahi sana.

Ilipofika saa 6:30 adhuhuri,Mgeni Rasmi alipewa nafasi ya kutoa nasaha kwa wahitimu. Aliwatahadharisha kuepukana na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI. Baada ya hapo alitoa zawadi. Zawadi zilitolewa kwa wahitimu waliofanya vizuri katika masomo, nidhamu, uongozi na michezo. Hatimaye aliwakabidhi wahitimu vyeti kisha akapiga picha pamoja nao.

Ilipofika saa 7:30 mchana, wageni pamoja na wahitimu walikwenda kupata chakula. Wanafunzi wengine tulikwenda kupata chakula katika madarasa yetu. Ilipofika saa 9:30 alasiriwageni waliondoka na wanafunzi tuliruhusiwa kurudi nyumbani.

ZOEZI LA KWANZA.

UFAHAMU.

 1. Katika shule ya mtibwa kulikua na tukio gani?
 2. Kkazi gani walifanya wanafunzi shuleni?
 3. Kwanini wanafunzi wa darasa la saba hawakupangiwa kazi?
 4. Wapishi walipika nini?
 5. Mgeni rasm aliwaasa nini wahitimu?
 6. Umejifunza nini kutokana na habari ulioisoma?

ZOEZI LA PILI

Tunga sentensi ukitumia maneno yafuatayo;

 1. Mahafali
 2. Alfajiri
 3. Wasili
 4. Alasiri
 5. Adhuhuri
 6. Hitimu
 7. Mshereheshaji
 8. Kutuimbuiza

ZOEZI LA TATU

MAZOEZI YA LUGHA.

A. Andika sentensi hizi kwa lugha sanifu na hati nadhifu

 1. Mkono yangu ilichafuka nikaosha
 2. Motto yake ana miguu mbili
 3. Kitabu hii nzuri ni ya nani?
 4. Chakula yangu ilikua tamu
 5. Mpira ndogo imeanguka
 6. Maji ilimwagika yote
 7. Nyumba letu ni nzuri
 8. Kuku hizi ni za mjomba yangu
 9. Maembe mangu mameiva
 10. Kifuli cha mlango ule kimepotea.

B. Andika maneno manne yanayowakilishwa na neon la jumla namba (i) ni mfano.

Na.

Neno la jumla

Maneno

1

Nguo

Sketi, kaptura, shati, fulana

2

Rangi

3

Mboga

4

Wanyama

5

Vinywaji

6

Mchezo

7

Matunda

8

Mikoa

9

Wadudu

10

Chakula

C. Pigia mstari neon lililo tofauti na maneno mengine katika kundi.

 1. Sufuria, bakuli, kikombe, viatu
 2. Nyumba, gari, pikipiki, baiskeli
 3. Shati, suruali, taa, gauni
 4. Ali, juma, kunguru, maria
 5. Macho, pua, mboga, mdomo
 6. Karoti, hoho, vitunguu, chupa.
 7. Baba, mama, ndama, mjomba

D. Andika na ukamilishe methali hizi kwa kimalizio sahii

 1. Pole pole ndio………………………………
 2. Njia ya mwongo ni……………………………
 3. Teke la kuku halimuumizi………………………..
 4. Harahaka haina……………………………………………
 5. Mtaka yoye hukosa………………………………
 6. Adui……………………………………………….
 7. Kawia…………………………………………
 8. Umoja ni………………………………………..
 9. Kuuliza si…………………………………………..
 10. Bendera hufuata………………………………….

E. Andika kwa wingi.

 1. Jina limeandikwa
 2. Swali litaulizwa
 3. Godoro linapendeza
 4. Goti linauma
 5. Dawati limefungwa
 6. Jiko linawaka
 7. Jino litaota
 8. Kufulu limeanguka
 9. Gurudumu limetoboka
 10. Jani linapendeza

F. Jibu maswali haya kwa ufasaha.

 1. Mtoto wa mwanagu nitamwita…………………………………
 2. Kitukuu ni mtoto wa……………………………………………..
 3. Dada anamtoto anayeitwa Rukia, mimi nitamwita Rukia…………………..
 4. Mama mdogo ambaye ambaye ni mke wa baba nitamwita…………………….
 5. Baba wa mama yangu ni………………………………..
 6. Kaka ya baba yangu ni……………………………………….
 7. Dada wa baba yangu ni………………………………………
 8. Mtoto wa mjomba utamwita………………………………………….
 9. Mama wa nyanya yangu ni………………………………………
 10. Sauda ni mtoto wa kike wa mama, kwa hivyo nitamwita……………

G. Kanusha sentensi zifuatazo

 1. Sisi tunakula nyama ya ng’ombe
 2. Mama hupika chakula na mboga za majani
 3. Sufuria, bakuri, na vijiko hupatikana darasani
 4. Samaki ni chakula chenye wanga
 5. Mbwa anakula majani
 6. Popo hutaga mayai

www.learninghubtz.co.tz

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256