SURA YA PILI

VITENDAWILI, NAHAU NA METHALI

Katika sura hii utajifunza namna ya kutega na kutegua vitendawili. Pia, kueleza maana ya nahau. Kisha, utaweza kukamiFsha methali, kuelezea maana zake na kufafanua ujumbe uliomo, Vilevile, utaweza kueleza umuhimu wa vitendawili, nahau na methali.

Chunguza kila sentensi kisha taja sentensi hiyo ni kitendawili au methali?

  • Polepole, ndio mwendo.
  • Athumani mfupi kasimama miangoni.
  • Jogoo wa shamba, hawiki mjini.
    Kila mtu humwabudu apitapo.

Ufahamu

Soma habari ifuatayo kisha jibu maswali.

Doto mshindi

Siku ya Jumamosi ni siku ya mapumziko. Mimi na wadogo zangu Ngwila na Aisha hatuendi shule. Tunafua nguo zetu za nyumbani na sare za shule. Pia tunawasaidia wazazi kazi za nyumbani.

Siku hiyo nilitembelewa na marafiki zangu Kulwa na Doto. Walipofika nyumbani kwetu walifurahia mazingira ya nyumba yetu.


Doto alisema, "Rafiki yangu Tumaini, nyumba yenu ni safi na inapendeza sana. Maua yamepandwa kwa mpangilio mzuri." Kulwa naye aliongeza, "Rangi mbalimbali zilizopakwa zinaifanya nyumba yenu ipendeze zaidi." Niliwaeleza kuwa siku za mapumziko tunawasaidia wazazi wetu kufanya usafi wa mazingira. Vilevile, tunamwagilia bustani ya maua. Doto naye alisema, "Kweli ninyi ni mfano bora wa kuigwa. Mazingira safi ni muhimu kwa afya zetu."

Siku hiyo baba alinunua matunda na mama alitupikia chakula kizuri. Baada ya chakula cha mchana tulikaa barazani na kutega vitendawili. Tulimkaribisha kaka ili aweze kusikiliza jinsi tunavyotega na kutegua vitendawili. Kaka alituambia yeye ataandika alama za kila mmoja wetu. Alitueleza kuwa atakayetega kitendawili na wengine wakashindwa kutegua, atakuwa amepata alama. Hivyo mshindi atakuwa ni yule aliyepata alama nyingi.

Mazungumzo yetu katika kutega vitendawili yalikuwa kama ifuatavyo:

Mimi: Kitendawili?

Wote: Tega.

Mimi: Ukoo wetu hauishiwi na safari.

Kulwa: Gari.

Mimi: Umekosa.

Aisha: Pikipiki.

Mimi: Umekosa. Nipeni mji.

Doto: Nenda Dodoma.

Mimi: Sawa naenda Dodoma nikirudi nitawaletea zabibu. Ukoo wetu hauishiwi na safari jibu lake ni siafu.

Kuiwa: Sasa ni zamu yangu. Kitendawili?

Wote: Tega.

Kuiwa: Ubwabwa wa mwana mtamu.

Aisha: Mahindi.

Kuiwa: Umekosa

Doto: Usingizi.

Kulwa: Umepata.

Zoezi

Tulishindana kutega vitendawili kwa saa moja. Mimi nilitegua kitendawili kimoja. Aisha alitegua vitendawili viwili na Doto aliweza kutegua vitendawili vitatu. Kaka alimtangaza Doto kuwa ndiye mshindi. Wote tulimpigia makofi ya kumshangilia. Kaka alituambia, "Ninyi ni hodari wa kutega vitendawili." Baada ya kuona usiku umeingia, kaka aliwaambia Kulwa na Doto warudi nyumbani. Wote tulisimama na kuwasindikiza rafiki zetu.

Maswali

  1. Tumaini alikuwa na wadogo zake wangapi?
  2. Doto alipofika nyumbani kwa akina Tumaini alifurahia nini?
  3. Je, tunapaswa kufanya nini siku za mapumziko?
  4. Tumaini, Aisha na rafiki zao walikuwa wakifanya nini barazani?
  5. Kwa nini Doto alishinda?


  1. Kiota changu kimezungushiwa boma la nyasi.____________
  2. Kila mtu humwabudu apitapo._______________
  3. Kaa hapa nikae pale tumfinye mchawi. _______________
  4. Kilemba chake haazimishi.


Zoezi la pili

Tumia nahau zifuatazo kukamilisha maelezo uliyopewa.

tia moyo kufa kishujaa piga chenga piga yowe

piga mbizi kata tamaa piga marufuku

Kwa mfano:

Sanga ni mkulima wa mahindi. Mafuriko yalipotokea mazao yake yote yalizolewa na maji. Baada ya mwezi mmoja mvua ilikatika. Sanga hakutaka tena kurudia kupanda mahindi. Je, Sanga alifanya nini? Sanga alikata tamaa.

Maelezo:

  1. Mwalimu Chapakazi aliwaambia wanafunzi warudi nyumbani.
    Wengine walimkwepa na kurudi tena kutazama mafuriko.
    Wanafunzi hao watakuwa wamemfanyia nini mwalimu wao?
  1. Bahati alipokaribia kuzama alijua ndio mwisho wa uhai wake. Maneno aliyoambiwa na wanafunzi wenzake yalimwezesha kuamini kuwa atatoka salama. Je, maneno ya wanafunzi hao yalimfanya nini Bahati?
  2. Kama Musa angezam,a na kupoteza maisha wakati akimuokoa Bahati, angekuwa amefanya nini?
  3. Wanafunzi walipomuona Bahati anazama walipiga kelele. Wengine walifanya nini iii kumpa msaada?
  4. Mara baada ya kuzolewa na maji Bahati alijiona yuko hatarini. Alifanya nini iii kujiokoa?

Umoja ni nguvu

"Ama kweli kuishi kwingi, ni kuona mengi." Nilimsikia bibi

akiongea maneno hayo peke yake. Sikusita kumkaribia na kumuuliza, "Bibi unaongea na nani?" Bibi alijibu, "Nimekumbuka habari ya kijana aitwaye Besao. Ngoja nikusimulie mjukuu wangu."

Besao ni mtoto wa kwanza kuzaliwa katika familia yenye watoto wanne. Besao hakupenda kushirikiana na wadogo zake katika mambo mbalimbali. Alikuwa mbinafsi na alifanya kila kitu peke yake. Aliamini kuwa wingi si, hoja. Mama yake alimwambia kuwa, kidole kimoja, hakivunji chawa.

Siku moja Besao aliumia mguu. Ndugu zake walishirikiana kumuuguza hadi alipopona. Baada ya kupona mguu Besao aliona aibu sana. Aliwaomba radhi wazazi na wadogo zake.

Besao aliwaambia kwamba ameamini kuwa, umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu. Kuanzia hapo Besao alianza kushirikiana na wadogo zake.

B. Tumia methali zifuatazo kujaza nafasi zilizoachwa wazi katika maelezo uliyopewa 1 - 4.

Methali

  1. Umoja ni nguvu, na utengano ni udhaifu.
  2. Jungu kuu, halikosi ukoko.
  3. Akiba, haiozi.
  4. Kilema si, ugonjwa.

Maelezo

Baraka ni miemavu wa mkono. Hufanya kazi kwa bidii kama watu wengine. Baraka hapendi ulemavu umfanye awe mvivu.

Besao ni mtu ambaye hapendi kushirikiana na wenzake.. Muda mwingi hupenda kuwa peke yake na mambo yake mengi hayafanikiwi.

Zoezi

Tegua vitendawilivifuatavyo:

  1. Mjombahatakituonane……………………
  2. Watoto wabinamuwakiondokahawarudi……………..
  3. Mtotowangu ana mguummojakilamtuanamwabudu……………
  4. Hana miguulakinihuendambiosana…………
  5. Kila niendapohunifuata………………..
  6. Kamba yangundefulakinihaiwezikufungamzigowakuni……………
  7. Bomu la machozibaridi………………
  8. Nyumbayanguinamlangojuu………….

Andikavitendawilivyenyemajibuyafuatayo:

Mfano: machopopoombilizavukamto.

  1. Mhindi ………………………………
  2. Mwiba ……………………………
  3. Utelezi …………………………….
  4. Konokono ………………………..
  5. Ngoma …………………………….

Andika KWELI au SI KWELI.

  1. Watoto hawapaswikujuavitendawili……………….
  2. Vitendawilinimanenoyanayofichamaanayakituilikisijulikanekwaurahisi…………………
  3. Katikavitendawilimtuanapopewamjianawezakuukubali au kuukataa…………………..
  4. Vitendawilihusaidiakuhusishavituvilivyomokatikamazingirayetu……………………..
  5. Vitendawilihavifikirishi…………………….

Kamilishamethalizifuatazo:

  1. Kuku mgeni, …………………..
  2. Kivunjakwapakacha, …………………..
  3. Jogoowa shamba, ……………………….
  4. Dau la mnyonge, …………………………
  5. Leo nileo, ……………………………….

Andikamethalizitakazotumikakuwaonyawatuwenye tabia zifuatazo:

Mfano:mtuasiyesikilizaushaurianaopewanawakubwazake.

Asiyesikia la mkuu, huvunjikaguu.

  1. Mtuasiyetakakushughulikiajambodogoambalomwishowehumleteamatatizomakubwa.

……………………………………………….

  1. Mtuanayependakuchaguasananakushindwakufanyauamuzi …………………………………………………………..
  2. Malezimabayayawazazikwa Watoto wao

…………………………………………….

  1. Mtuambayenimgenimahali Fulani nahuonesha tabia zaketofautina za wenyeji wake ………………………………….
  2. Mtuanayependakuulizamaswalisanailikuelewajambo …………………………………………………………………...
  3. Mtuanayependakutunzavitukwamanufaayabaadaye

……………………………………………..

  1. Mtualiyeonywanawazazi wake akashindikanaataonywanajamii.

………………………………………………

Badilisentensizifuatazokuwakatikawakatiujao.

  1. Bibi aliongea peke yake
  2. Besaoaliwaombaradhinduguzake
  3. Bibi anatusimuliahadithi
  4. Wanafunziwalirudishulenimapema
  5. Wanafunziwanaandikavizurisana
  6. Dada anamwagiliabustaniyamiti
  7. Wazaziwaliwahikwenyemkutano
  8. Shereheya Watoto ilianzamapema

Andikasentensizifuatazokatikahalitimilifu.

  1. Maguguyanaotabondeni
  2. Askari anabebabunduki
  3. Mwalimuwetuanatufundishavizuri
  4. Sahaniilivunjika
  5. Mwalimuanafundishasomo la Kiswahili vizuri
  6. Maji yanamwagika
  7. Wanafunziwanaimbawimbowataifa
  8. Jualinazamamapema
  9. Maperayanadondoka
  10. Kaka anatupikiachakulakitamu

Andikasentensizifuatazokatikahaliyaukanushi.

  1. Kwasi alikuwa Hodari katikamasomoyakeshuleni
  2. Rafiki yangualipendasanamichezo
  3. Kuku alitagamayaimengi
  4. Tuliambiwatwendeshulenikumwagiliamiti
  5. Jumanimkarimusana

www.learninghubtz.co.tz

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256