KISWAHILI DARASA LA 4

SURA YA PILI

VITENDAWILI, NAHAU NA METHALI

Katika sura hii utajifunza namna ya kutega na kutegua vitendawili. Pia, kueleza maana ya nahau. Kisha, utaweza kukamilisha methali, kuelezea maana zake na kufafanua ujumbe uliomo. Vilevile, utaweza kueleza umuhimu wa vitendawili, nahau na methali.

Kuna tofauti gani kati ya Kiswahili na methali? Eleza kama hizi ni methali au kitendawili

  1. Pole pole ndio mwendo
  2. Athumani mfupi amesimama mlangoni
  3. Jogoo wa shamba hawiki mjini
  4. Kila mtu humwabudu apitapo

Ufahamu

Soma habari ifuatayo kisha jibu maswali.

Doto mshindi

Siku ya Jumamosi ni siku ya mapumziko. Mimi na wadogo zangu Ngwila na Aisha hatuendi shule. Tunafua nguo zetu za nyumbani na sare za shule. Pia tunawasaidia wazazi kazi za nyumbani.

Siku hiyo nilitembelewa na marafiki zangu Kulwa na Doto. Walipofika nyumbani kwetu walifurahia mazingira ya nyumba yetu.

Doto alisema, "Rafiki yangu Tumaini, nyumba yenu ni safi na inapendeza sana. Maua yamepandwa kwa mpangilio mzuri." Kulwa naye aliongeza, "Rangi mbalimbali zilizopakwa zinaifanya nyumba yenu ipendeze zaidi." Niliwaeleza kuwa siku za mapumziko tunawasaidia wazazi wetu kufanya usafi wa mazingira. Vilevile, tunamwagilia bustani ya maua. Doto naye alisema, "Kweli ninyi ni mfano bora wa kuigwa. Mazingira safi ni muhimu kwa afya zetu."

Siku hiyo baba alinunua matunda na mama alitupikia chakula kizuri. Baada ya chakula cha mchana tulikaa barazani na kutega vitendawili. Tulimkaribisha kaka iii aweze kusikiliza jinsi tunavyotega na kutegua vitendawili. Kaka alituambia yeye ataandika alama za kila mmoja wetu. Alitueleza kuwa atakayetega kitendawili na wengine wakashindwa kutegua, atakuwa amepata alama. Hivyo mshindi atakuwa ni yule aliyepata alama nyingi.

Mazungumzo yetu katika kutega vitendawili yalikuwa kama ifuatavyo:

Mimi: Kitendawili?

Wote: Tega.

Mimi: Ukoo wetu hauishiwi na safari.

Kulwa: Gari.

Mimi: Umekosa.

Aisha: Pikipiki.

Mimi: Umekosa. Nipeni mji.

Doto: Nenda Dodoma.

Mimi: Sawa naenda Dodoma nikirudi nitawaletea zabibu. Ukoo wetu hauishiwi na safari jibu lake ni siafu.

Kulwa: Sasa ni zamu yangu. Kitendawili?

Wote: Tega.

Kulwa: Ubwabwa wa mwana mtamu.

Aisha: Mahindi.

Kulwa Umekosa

Doto: Usingizi.

Kulwa: Umepata.

Tulishindana kutega vitendawili kwa saa moja. Mimi nilitegua kitendawili kimoja. Aisha alitegua vitendawili viwili na Doto aliweza kutegua vitendawili vitatu. Kaka alimtangaza Doto kuwa ndiye mshindi. Wote tulimpigia makofi ya kumsha' ngilia. Kaka alituambia, "Ninyi ni hodari wa kutega vitendawili." Baada ya kuona usiku umeingia, kaka aliwaambia Kulwa na Doto warudi nyumbani. Wote tulisimama na kuwasindikiza rafiki zetu.

Zoezi La Kwanza

Ufahamu.

  1. Tumaini alikuwa na wadogo zake wangapi?
  2. Doto alipofika nyumbani kwa akina tumaini alifurahia nini?
  3. Je una paswa kufanya nini siku za mapumziko?
  4. Tumaini aisha na rafiki zao walikua wakifanya nini barazani?
  5. Kwanini doto alishinda?

A. Tegua vitendawili vifuatavyo.

  1. Kiota changu kimezungushiwa boma la nyasi._______________
  1. Kila mtu humwabudu apitapo. _________________
  2. Kaa hapa nikae pale tumfinye mchawi.
  3. Kilemba chake haazimishi.

B. Tegua vitendawili vifuatavyo:

  1. Mjomba hataki tuonane.
  2. Watoto wa binamu wakiondoka hawarudi.
  3. Mtoto wangu ana mguu mmoja kila mtu anamwabudu.
  4. Hana miguu lakini huenda mbio sana.
  5. Kila niendapo hunifuata.

6. Kamba yangu ndefu lakini haiwezi kufunga mzigo wa kuni.

  1. Bomu la machozi baridi.
  2. Nyumba yangu ina miango juu.

C. Andika vitendawili vyenye majibu yafuatayo:

Mfano: Macho Popoo mbili zavuka mto.

  1. Mhindi
  2. Mwiba
  3. Utelezi
  4. Konokono
  5. Ngoma

Zoezi la Tatu

Lugha.

Andika KWELI au SI KWELI.

  1. Watoto hawapaswi kujua vitendawili.
  2. Vitendawili ni maneno yanayoficha maana ya kitu iii kisijulikane kwa urahisi.
  3. Katika vitendawili mtu anapopewa mji anaweza kuukubali au kuukataa.
  4. Vitendawili husaidia kuhusisha vit0-vilivyomo katika mazingira yetu.
  5. Vitendawili havifikirishi.

ZOEZILA NNE

Tumia nahau zifuatazo kukamilisha maelezo uliyopewa.

Kwa mfano:

Sanga ni mkulima wa mahindi. Mafuriko yalipotokea mazao yake yote yalizolewa na maji. Baada ya mwezi mmoja mvua ilikatika. Sanga hakutaka tena kurudia kupanda mahindi. Je, Sanga alifanya nini? Sanga alikata tamaa.

Maelezo:

  1. Mwalimu Chapakazi aliwaambia wanafunzi warudi nyumbani. Wengine walimkwepa na kurudi tena kutazama mafuriko. Wanafunzi hao watakuwa wamemfanyia nini mwalimu wao?
  2. Bahati alipokaribia kuzama alijua ndio mwisho wa uhai wake. Maneno aliyoambiwa na wanafunzi wenzake yalimwezesha kuamini kuwa atatoka salama. Je, maneno ya wanafunzi hao yalimfanya nini Bahati?
  3. Kama Musa angezanya na kupoteza maisha wakati akimuokoa Bahati, angekuwa amefanya nini?
  4. Wanafunzi walipomuona Bahati anazama walipiga kelele. Wengine walifanya nini iii kumpa msaada?
  5. Mara baada ya kuzolewa na maji Bahati alijiona yuko hatarini. Alifanya nini iii kujiokoa.

A. Soma hadithi ifuatayo kisha andika methali zilizomo na maana zake.

Umoja ni nguvu

"Ama kweli kuishi kwingi, ni kuona mengi."Nilimsikia bibi

akiongea maneno hayo peke yake. Sikusita kumkaribia na kumuuliza, "Bibi unaongea na nani?" Bibi alijibu, "Nimekumbuka habari ya kijana aitwaye Besao. Ngoja nikusimulie mjukuu wangu."

Besao ni mtoto wa kwanza kuzaliwa katika familia yenye watoto wanne. Besao hakupenda kushirikiana na wadogo zake katika mambo mbalimbali. Alikuwa mbinafsi na alifanya kila kitu peke yake. Aliamini kuwa wingi si, hoja.Mama yake alimwambia kuwa, kidole kimoja, hakivunji chawa.

Siku moja Besao aliumia mguu. Ndugu zake walishirikiana kumuuguza hadi alipopona. Baada ya kupona mguu Besao aliona aibu sana. Aliwaomba radhi wazazi na wadogo zake.

Besao aliwaambia kwamba ameamini kuwa, umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu.Kuanzia hapo Besao alianza kushirikiana na wadogo zake.

B. Tumia methali zifuatazo kujaza nafasi zilizoachwa wazi katika maelezo uliyopewa 1 - 4.

Methali

  1. Umoja ni nguvu, na utengano ni udhaifu.
  2. Jungu kuu, halikosi ukoko.
  3. Akiba, haiozi.
  4. Kilema si, ugonjwa.

Maelezo

  1. Baraka ni miemavu wa mkono. Hufanya kazi kwa bidii kama watu wengine. Baraka hapendi ulemavu umfanye awe mvivu.
  1. Besao ni mtu' ambaye hapendi kushirikiana na wenzake. Muda mwingi hupenda kuwa peke yake na mambo yake mengi hayafanikiwi.
  2. Mawazo ni mwenyekiti wa kijiji. Ni mtu mwema na mwenye busara. Wanakijiji wanapotaka kutatua jambo hupenda kwenda kwake kwa ajili ya ushauri.
  3. Familia inatunza mazao waliovuna kwa ajili ya matumizi wakati wa njaa.

C. Kamilisha methali zifuatazo.

  1. Kuku mgeni……………………………………………………………
  2. Kuvuja kwa pakacha …………………………………………………………..
  3. Jogoo wa shamba……………………………………………………………….
  4. Dau la mnyoge…………………………………………………………………….
  5. Leo ji leo………………………………………………………………………

D. Andika methali methali zitakazo tumika kuwaonya watu wenye tabia zifuatazo

  1. Mtu asiyetaka kushughulikia jambo dogo ambalo mwishowe umletea matatizo makubwa……………………………………………………………………………
  2. Mtu anayependa kuchagua sana na kushindwa kufanya uamuzi……………………….
  3. Malezi mabaya ya wazazi kwa watoto wao………………………………………
  4. Mtu ambaye ni mgeni mahali fulani na huonesha tabia zake tofauti na za wenyezi wake…………………………….
  5. Mtu anayependa kuuliza maswali hili kuelewa jambo……………………………..
  6. Mtu anayependa kutunza vitu kwa manufaa ya baadaye…………………………
  7. Mtu aliyeonywa na wazazi wake akashindikana ataonywa na jamii………………

ZOEZI LA SITA

MAZOEZI YA LUGHA.

A. Badili sentensi zifuatazo kuwa katika wakati ujao

  1. Bibi aliongea peke yake
  2. Bessao aliwaomba radhi ndugu zake
  3. Bibi anatusimulia hadith
  4. Wanafunzi walirudi shuleni mapema
  5. Wanafunzi wanaandika vizuri sana
  6. Dada anamwagilia bustani ya miti
  7. Wazazi waliwahi kwenye mkutano
  8. Sherehe ya watoto ilianza mapema

B. Andika sentensi zifuatazo katika hali timilifu

  1. Magugu yanaota bondeni
  2. Askari anabeba bunduki
  3. Mwalimu wetu anafundisha vizuri
  4. Sahani ilivunjika
  5. Mwalimu anafundisha somo la Kiswahili vizuri
  6. Maji yanamwagika
  7. Wanafunzi wanaimba wimbo wa taifa
  8. Jua linazama mapema
  9. Mapera yanadondoka
  10. Kaka anatupikia chakula kitamu

C. Oanisha methali zinazofanana kutoka sehemu ya A na B

Sehemu A

Sehemu B

  1. Kidole kimoja hakivunji chawa
  2. Mdharau mwiba mguu huota tende
  3. Mchagua jembe sii mkulima
  4. Samaki mkunje angali mbichi
  5. Polepole ndio mwendo
  6. Jembe halimtupi mkulima
  1. Usipoziba ufa utajenga ukuta
  2. Mchagua nazi huambulia koroma
  3. Mchumia juani ulia kivulini
  4. Haraka haraka haina Baraka
  5. Motto umleavyo ndivyo akuavyo
  6. Umoja ni nguvu utengano udhaifu

D. Andika sentensi zifuatazo katika hali ya ukanushi

  1. Kwasi alikua hodari katika masomo yake shuleni
  2. Rafiki yangu anapenda sana mchezo
  3. Kuku alitaga mayai mengi
  4. Tuliambiwa twende shuleni kumwagilia miti
  5. Juma ni mkarimu sana

E. Tegua vitendawili vifuatavyo tumia viteguzi ulivyopewa.

  1. Bikizee apepeta mafuta
  2. Shamba langu kubwa lakini mavuno hayajai ukufi
  3. Popoo mbili zavuka mto
  4. Mama nieleke!
  5. Parr! Hadi makka!
  6. Nyoka pangoni
  7. Popote niendapo unifuata
  8. Halo! Halo! Mpaka lamu
  9. Ni mgeni wa kila mtu lakini hapendwi
  10. Tik!Tik! kutwa kucha
  11. Nanywa supu, nyama natupa
  12. Nikimpiga mwanangu watu unicheka
  13. Njoo ukamwone umpendaye
  14. Mchaka mchaka chinja
  15. Nabii mwenye maneno mengi.

F. Tumia viteuzi hivi kutegua vitendawili vifuatavyo

  1. Nina mtoto wangu ambaye kila nikimwogesha hakauki
  2. Mvua inanyesha mlima unapanda
  3. Motto wangu nikimtumia anaconda nisipomtumia anasalia vile vile.
  4. Mtumishi wangu akitema mate hayafutiki yananipa ujumbe.
  5. Roda si dada yangu ni mimi
  6. Yumbayumba tuone
  7. Si mviringo si mviringo ah!
  8. Kenua kenua tupate mvua
  9. Subiri kidogo!
  10. Bingiri bingiri twende butere!

www.learninghubtz.co.tz

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256