SURA YA KWANZA

KUTAJA NENO MOJA LINALOBEBA MAANA YA JUMLA

Katika sura hii utasoma habari kuhusu mahafali ya darasa la saba. Kutokana na habari hiyo utaweza kujifunza kuhusu maneno yenye maana za jumla. Pia, utajifunza maneno ya kundi moja na kuweza kuyatumia katika sentensi.

Ufahamu

Soma habari ifuatayo kisha jibu maswali.

Mahafali ya darasa Ia saba

Leo ni siku ya mahafali ya dada yangu Tunu. Amehitimu darasa Ia saba katika Shule ya Msingi Mtibwa. Jana mwalimu alitutangazia tuwahi shuleni kufanya usafi kabla wageni hawajafika.

Tulifika shuleni saa 12:30 asubuhi na tuligawana kazi kwa madarasa. Wanafunzi wa darasa la kwanza na Ia pili waliokota takataka eneo lute la shule. Wanafunzi wa darasa Ia tatu na la nne tulifagia madarasa na kupiga deki. Wanafunzi wa darasa Ia tano na la sita walikusanya kuni na kuchota maji. Wanafu-= wa darasa Ia saba hawakupangiwa kazi.


Wapishi waliandaa vyakula mbalimbali kwa ajili ya mahafali. Walipika pilau, wall, ndizi, nyama, njegere na maharage. Pia, walipika mboga za majani ambazo ni mchicha, kisamvu na majani ya kunde. Vilevile, waliandaa matunda kama mananasi, maembe na machungwa.

Jukwaa kubwa liliandaliwa kwa ajili ya wageni watakaokaa katika meza kuu. Pembeni mwa Jukwaa hilo, kulikuwa na maturubai yaliyofungwa kwa ajili ya kivuli. Sehemu hiyo ilikuwa ni maalumu kwa wazazi na wageni waalikwa. Maeneo yote ya shule yalipambwa kwa maputo ya rangi ya bluu, kijani na nyekundu.

Ilipofika saa 3:00 asubuhi wazazi na wageni waalikwa walianza kuwasili. Tuliwakaribisha na kuwapeleka sehemu iliyoandaliwa kwa ajili yao. Wahitimu nao walikuwa tayari wameketi sehemu yao wakiwa wamevaa sare za shule.


Baada ya nusu saa Mgeni Rasmi aliwasili. Mwenyekiti wa kamati ya shule, mwalimu mkuu na wajumbe wa kamati ya shule walimpokea Mgeni Rasmi. Waliongozana naye hadi meza kuu. Wakati huo wote sisi sote tulisimama, tukipiga makofi, nderemo na vifijo vilisikika huku tukiimba wimbo ufuatao:

Karibuni wageni wetu, karibuni wageni x 2 Karibuni shule ya Mtibwa, karibuni wageni x2 Sisi ni nani fama, sisi wanafunzi x2

Taifa linatutegemea, wazazi wanatutegmea, Sisi wanafunzi.

Tuliimba wimbo huo hadi wageni walipokaa kwenye viti. Mshereheshaji alimkaribisha Mwalimu Mkuu kwa ajili ya kuwakaribisha na kuwatambulisha wageni. Baada ya utambulisho, vikundi mbalimbali vya burudani vilitumbuiza. Kulikuwa na nyimbo, maigizo, mashairi na ngonjera. Wageni waalikwa pamoja na wahitimu walifurahi sang.

Ilipofika saa 6:30 adhuhuri, Mgeni Rasmi alipewa nafasi ya kutoa nasaha kwa wahitimu. Aliwatahadharisha kuepukana na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI. Baada ya hapo alitoa zawadi. Zawadi zilitolewa kwa wahitimu waliofanya vizuri katika masomo, nidhamu, uongozi na michezo. Hatimaye aliwakabidhi wahitimu vyeti kisha akapiga picha pamoja nao.

Ilipofika saa 7:30 mchana, wageni pamoja na wahitimu walikwenda kupata chakula. Wanafunzi wengine tulikwenda kupata chakula katika madarasa yetu. Ilipofika saa 9:30 alasiri wageni waliondoka na wanafunzi tuliruhusiwa kurudi nyumbani.

1. Katika shule ya Mtibwa kulikuwa na tukio gani? Kazi gani walizifanya wanafunzi shuleni?


E. Cheza na wenzako mchezo ufuatao:

Simameni katika umbo Ia duara huku mkiwa mmeshikana mikono. Kisha kiongozi ataje maneno yaliyokolezwa rangi na ninyi mtajibu alichokisema kiongozi. Kiongozi atataja majina ya vitu mbalimbali vilivyo,kolezwa rangi. Endapo kilichosemwa ni sahihi mruke na kuitikia kwa kutaja jina la jumla Ia kitu alichokitaja. Kama si sahihi msiruke, mkae kimya. Atakayekosea atoke nje ya mduara. Mmoja atakayebaki mpaka mwisho ndiye mshindi.

Mnyama mnyama mnyama - mnyama

Ng'ombe mnyama

Mbuzi - mnyama

Gari (kimya)

Kondoo - mnyama

Tunda tunda tunda - tunda

Nanasi - tunda

Kijiko - (kimya)

Parachichi - tunda
Chungwa - tunda


Mti mti mti mti

Mfenesi - mti

Waridi - (kimya)

Mchungwa - mti

Mchongoma - mti

Ndege ndege ndege ndege

Kuku - ndege

Bata - ndege

Popo - (kimya)

Kasuku - ndege

Samaki samaki samaki - samaki

Sato - samaki

Kambare - samaki

Nyoka - (kimya)

Kibua - samaki

(ii) Taja majina ya jumla yaliyotajwa katika mchezo uliocheza.

  1. Simulia sherehe uliyowahi kuhudhuria.
  2. Andika habari uliyoisimulia kWa kuzingatia mwongozo ufuatao.
  1. Kichwa cha habari.
  2. Nani walishiriki katika sherehe hiyo?
  3. Kitu gani kilifanyika kabla ya sherehe?
  4. Mambo gani yalifanyika wakati wa sherehe?
  5. Kitu gani kilikufurahisha katika sherehe hiyo?


Ufahamu

Soma na wenzako kisha muigize majigambo yafuatayo:

Tunda: Mimi ni tunda, tukiwa wengi tunaitwa matunda.

Matunda hayo yanaweza kuwa maembe, ndizi, mananasi au mapapai. Kazi yetu ni kuwapatia binadamu vitamin'. Binadamu akitumia matunda atajikinga na maradhi. Pia, ataongeza damu mwilini. Nani kama tunda?

Mti: Mimi ni mti, tukiwa wengi tunaitwa miti. Kuna miti

ya miembe, michungwa, mipera au miarobaini. Miti ina faida nyingi sang. Miti huzuia mmomonyoko wa udongo. Baadhi ya miti hutoa matunda. Majani, mizizi pamoja na magome ya miti hutumiwa na binadamu kutengeneza dawa. Miti hutoa hewa ya oksijeni na huleta mvua. Nani kama mti?

Mnyama: Mimi ni mnyama, tukiwa wengi tunaitwa wanyama. Kuna ng'ombe, mbuzi au kondoo. Huwapatia binadamu kitoweo, mbolea pamoja na maziwa. Ngozi yangu hutumika kutengenezea mikoba, viatu pamoja na mikanda. Nyama yangu husafirishwa nje ya nchi, hivyo husaidia kuinua uchumi wa nchi. Nani kama mnyama?

Mdudu: Mimi ni mdudu, tukiwa wengi tunaitwa wadudu.

Tunaweza kuwa nyuki, nzi, mbu, panzi, siafu, mende, nge au buibui. Miongoni mwetu wengine ni hatari na wengine si hatari. Tunamsaidia binadamu kupata majibu ya vitendawili vyake. Kama huamini tegua vitendawili vifuatavyo:

  1. Ana miguu ya msumeno.......................
  2. Anang'ata kwa mkia.........................
    Nani kama mdudu?

Zoezi la Ufahamu

Katika majigambo uliyosoma, kati ya tunda, mti, mnyama na mdudu unapenda kuwa nani? Kwa nini?

  • Eleza faida nyingine za miti ambazo hazikutajwa katika majigambo uliyosoma.
  • Katika majigambo uliyosoma mdudu anasema, "Miongoni mwetu wengine ni hatari na wengine si hatari." Taja wadudu ambao ni hatari na wasio hatari kwa binadamu.

Kanusha sentensi zifuatazo:

Mfano: Watoto wanacheza ngoma. Watoto hawachezi ngoma.

  1. Sisi tunakula nyama ya ng'ombe.
  2. Mama hupika chakula na mboga za majani.
  3. Sufuria, bakuli na vijiko hupatikana darasani.
  4. Samaki ni chakula chenye wanga.
  5. Mbwa anakula majani.
  6. Popo hutaga mayai.

Andika majigambo kwa kutumia vyombo viwili vya usafiri.

Mfano: Baiskeli: Mimi ni baiskeli.

Ni usafiri rahisi na wenye gharama nafuu.

Kila mtu anaweza kuninunua. Nani kama baiskeli?

Zoezi

Tunga sentensi kwa kutumia maneno yafuatayo:

  1. Mahafali
  2. Alfajiri
  3. Wasili
  4. Alasiri
  5. Adhuhuri
  6. Hitimu
  7. Mshereheshaji
  8. Kutumbuiza

Andika maneno manne yanayowakilishwa na neno la jumla. Namba tis ani mfano.

Namba

Neno la jumla

Maneno

nguo

Sketi, kaptura, shati, fulana

Rangi

Mboga

Wanyama

Vinywaji

Michezo

Matunda

Mikoa

Wadudu

Chakula

Pigia mstari neno lililo tofauti na maneno mengine katika kikundi

Mfano: kanga, mwewe, kalamu, njiwa .

  1. Sufuria, bakuli, kikombe, viatu.
  2. Nyumba, gari, pikipiki, baiskeli.
  3. Shati, suruali, taa, gauni.
  4. Ali, Juma, kunguru, Maria.
  5. Macho, pua, mboga, mdomo.
  6. Karoti, hoho, vitunguu, chupa.
  7. Baba, mama, ndama, mjomba.

Kanusha sentensi zifuatazo:

Mfano: Watoto wanacheza ngoma.

Watoto hawachezi ngoma.

  1. Sisi tunakula nyama ya ng’ombe.
  2. Mama hupika chakula na mboga za majani.
  3. Sufuria, bakuli na vijiko hupatikana darasani.
  4. Samaki ni chakula chenye wanga.
  5. Mbwa anakula majani.
  6. Popo hutaga mayai.

www.learninghubtz.co.tz

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256